Wanyama, Ndege na Wadudu (Animals, Birds and Insects)
Duniani Kuna wanyama wa aina mbili, yaani;
1. Wanyama wa nyumbani.
2. Wanyama wa porini.
Wanyama nyumbani:
Wanyama wa nyumbani Ni wale wanyama wanaofugiwa nyumbani na binadamu.
Wanyama wa nyumbani au wanyama au mifugo ya nyumbani ni wale wanyama ambao huishi katika mazingira ambayo mwanadamu anaishi na hawawezi kumuathiri kwa kiasi kikubwa.
Wanyama Hawa wanafungwa kwa malengo matatu; kwa ajili ya urafiki, chakula na wengine kwa ajili ya kufanya kazi za binadamu.
Wanyama hao wanatunzwa kwa uangalizi wa binadamu kwa ajili ya ulinzi, michezo, kazi, pambo na majaribio ya maabara.
Wanyama wanaofugwa kwa ajili ya urafiki Ni pamoja na; mbwa(dog) na Paka(cat) wanyama Hawa kijadi walikuwa wanaofugwa kwa ajili ya urafiki tu, lakini ukuaji wa populesheni na tekinolojia umewafanya baadhi ya Watu kubadilisha urafiki kuwa uadui kwa kuanza kuwala Hawa wanyama 😂
Wanyama wanaofugwa kwa ajili ya chakula Ni pamoja na; kondoo (sheep), nguruwe (pig), ng’ombe (cow), batamzinga (turkey) n.k.
Halafu wanyama wanaofugwa kwa ajili ya kuwafanyia binadamu kazi Ni pamoja na; farasi(horse), punda (donkey), ngamia(camel) n.k.
Wanyama wa nyumbani kwa ujumla Ni pamoja na;
1. Mbuzi (goat)

Ng’ombe (cow)

Nguruwe (pig)

Batamzinga (turkey)

Kuku (chicken)

Kondoo (sheep)

Kanga (Guinea fowl)

sungura(rabbit)

Ngamia (camel)

Farasi (horse)

Mbwa (dog)

Paka(cat)

Wanyama wa porini:
Wanyama wa porini Ni wale ambao hawana uhusiano wa karibu na binadamu. Wanyama Hawa huishi msituni.
Wao wanakuwa maadui wa binadamu wakati mwingine.
Wanyama wa porini Ni pamoja na;
Wanyama hawa, ikiwa hawajafugwa, wote wanachukuliwa kuwa wanyama wa porini.
Orodha ya Wanyama wa Porini;
Tumbili (monkey)

Pundamilia (zebra)

Chui (leopard)

mbwaMwitu (wolf)

Twiga ( Giraffe)

Ngamia (camel)

Mamba (crocodile)

Bundi (owl)

Sokwe (chimpanzee)

Simba (lion)

Tembo (elephant)

Nyoka (snake)

Kangaruu ( kangaroo)

Kiboko (hippopotamus)

Mbweha (Fox)

Popo (bat)

Chura (Frog)

Panya (Rat)

Mjusi (lizard)

FAIDA ZA WANYAMA:
1. Mbwa husaidia hasa katika suala la ulinzi katika mazingira yanayomzunguka mwanadamu.
3. Mbuzi huwapatia watu nyama, maziwa na pia ngozi yake hutumika kutengenezea vitu kama vile ngoma, mikanda na viatu hasa katika jamii za Afrika.
4. Kware ni ndege mdogo; mayai yake ni madogo sana yana faida kubwa katika mwili wa mwanadamu kwa sababu yanasemekena kutibu baadhi ya magonjwa katika miili yetu.
6. Mifugo hutupatia pesa kwa kuuza nyama, maziwa, ngozi, kwato, mbolea na hata wanyama wenyewe. Tunapata pesa nyingi baada ya kuuza wanyama Hawa.
7. Tunapata maziwa kutoka wanyama Hawa kamavile kondoo, mbuzi na ng’ombe.
8. Tunapata chakula kitamu ambacho Ni nyama kutoka wanyama Hawa.
9. Ngozi ya ng’ombe hutumika kutengenezea vitu kama vile ngoma, viatu, mikanda, nguoVitu vinavyotengenezwa kwa kutumia ngozi ni imara na pia hudumu kwa muda mrefu.
10. Mavi ya wanyama hutumika kama mbolea ambayo huwezesha mazao kukua haraka na kustawi vizuri.
11. Wanyama hawa huondoa upweke kwa watu wasiokuwa na marafiki au mahusiano ya kijamii kama wazee, watoto na wajawazito.
Hivyobasi, wanyama hawa inafaa tuwatunze vizuri kwani tunawategemea katika shughuli mbalimbali za kijamii na za kiuchumi.
Hivyo hawatakiwi kupigwa ovyo. Wanatakiwa waangaliwe afya zao na kupata mahitaji yao.
WANYAMA NA VIKEMBE VYAO.
Vikembe pia huitwa vizawa.
Vikembe ni wana wa viumbe mbalimbali.
Ng’ombe………………….Ndama

Nzige…………….kimatu/maige/tunutu/matumatu/funutu

Ndege……………………..Kinda

Kipepeo/nondo…………kiwavi

Nzi…………………………Buu

Farasi……………………..Kitekli

Mamba………………….. Kigwena
Nyangumi…………. Kinyangunya
Fisi…………..,………….. Kikuto.
Ngamia………………….. Nirigi/nirihi
Paka…………..kinyaunyau/kipusi
Ndovu……………………. Kidanga
Mbweha……………….. Nyamawa
Nyani…………………….. Kigunge
Kondoo………………….. Kibebe/katama
Mbuzi…….Kibui/kibuli/kimeme
Farasi na punda………. Nyumbu
Punda……… Kiongwe/kihongwe

Mbu………………………kiluwiluwi
Chura…………………. kiluwiluwi

Kuku…………………….. Kifaranga

Papa…………………….. Kinengwe
Nyuki……………………. Jana
Simba…………………… Shibli

Sungura………………..,.Kitungule

Samaki……….. Chengo/kichengo
Chui……………… Chongole/kisui
Mbwa……….Kilebu/kidue/kibwa

Nyoka………………… Kinyemere
Njiwa……………………Kipura
Paka na Panya kwa Ushirikiano
Paka na panya walitaka kuishi pamoja katika nyumba moja kwa ushirikiano.
Walijitayarisha kwa ajili ya misimu mikali ya ukosefu wa chakula kwa kununua chungu kizima Cha chakula kwasababu hawakuwa na sehemu salama zaidi kwa ajili ya kukiweka, walikiweka kanisani hadi wakati ambapo wangekihitaji.
Hata hivyo, siku moja paka alichukua hamu kwa ajili yake, na akakaribia panya.
Paka kamwambia panya “Sikiliza, panya mdogo, binamu yangu ameniita kutumika kama baba wa kidini wa mtoto wake. Amejifungua mtoto mdogo wa rangi ya kahawia na nyeupae, na natakiwa kumsindikiza hadi ubatizo wake.
Je, ni sawa mimi kukuacha hapa nyumbani peke yako na kazi za nyumbani leo halafu nikamsindikiza binamu yangu?
Nenda mbele,” panya alisema, “na ikiwa watakuhudumia chakula kizuri, nifikirie tu ndugu yangu.
Hakika paka alikwenda moja kwa moja kanisani na kula chakula walichokihifadhi kwa misimu mikali kisha akaenda kuzunguka-zunguka mjini na hakurudi nyumbani hadi jioni.
Nyakati za saa kumi na mbili, paka alionekana akitembea mwendo wa kobe tumbo mbele yake Kama mawaziri wa Uganda.
“Lazima ulikuwa na wakati mzuri,” panya alisema. “Walimpa mtoto jina gani?”
Shiba,” paka akajibu.
Shiba! Hilo ni jina gani, ambalo bado sijalisikia.” Au Kama wewe umeshiba?
Muda mfupi baadaye paka alichukua hamu nyingine, akaenda kwa panya, na kusema, “Nimeombwa kutumika kama baba wa kidini kwa mara nyingine tena.
Mtoto ana pete nyeupe kuzunguka mwili wake. Siwezi kusema hapana. Utakuwa na kunifanyia upendeleo na kutunza nyumba peke yako leo.”
Panya alikubali, na paka akaenda na kula nusu ya mafuta. Aliporudi nyumbani, panya aliuliza, “Je! Mtoto huyu wa mungu alipokea jina gani?.

Usaidizi went ni wa umuhimu kwetu
LikeLike
Nashukuru sana
LikeLike
Nilikuumiza Mambo ya mapabazuko utanjibu
LikeLike
Sijakuelewa vizuri ndugu yangu
LikeLike
Hiyo kiswahili ikosawa hata nimejifunza mkafulahi Asante
LikeLike
Asante sana kifuatilia
LikeLike
Asante sana mkeleketwa WA lugha kwa juhudi zako za utafiti lakini tulisoma pamoja hapo Stuart kwa hayo mashule kwani usinitafutie kazi nikaachana na kijiji. Asante
LikeLike
Hujambo mwalimu. Huu mtando ni WA kuelimisha. Basi fikia inbox yangu. Asante
LikeLike
Swali mwalimu
LikeLike
Asante sana mwalimu kwa kazi nzuri yakupendeza ,,,hasa michoro itasaidia wanafunzi kuelewa zaidi
LikeLike
Nashukuru
LikeLike
jifunzekiswahiliart.wordpress.com
LikeLike