WANYAMA NA VIKEMBE VYAO-KIDATO CHA KWANZA

Wanyama, Ndege na Wadudu (Animals, Birds and Insects)

Duniani Kuna wanyama wa aina mbili, yaani;

1. Wanyama wa nyumbani.

2. Wanyama wa porini.

Wanyama nyumbani:

Wanyama wa nyumbani Ni wale wanyama wanaofugiwa nyumbani na binadamu.

Wanyama wa nyumbani au wanyama au mifugo ya nyumbani ni wale wanyama ambao huishi katika mazingira ambayo mwanadamu anaishi na hawawezi kumuathiri kwa kiasi kikubwa.

Wanyama Hawa wanafungwa kwa malengo matatu; kwa ajili ya urafiki, chakula na wengine kwa ajili ya kufanya kazi za binadamu.

Wanyama hao wanatunzwa kwa uangalizi wa binadamu kwa ajili ya ulinzimichezokazipambo na majaribio ya maabara.

Wanyama wanaofugwa kwa ajili ya urafiki Ni pamoja na; mbwa(dog) na Paka(cat) wanyama Hawa kijadi walikuwa wanaofugwa kwa ajili ya urafiki tu, lakini ukuaji wa populesheni na tekinolojia umewafanya baadhi ya Watu kubadilisha urafiki kuwa uadui kwa kuanza kuwala Hawa wanyama 😂

Wanyama wanaofugwa kwa ajili ya chakula Ni pamoja na; kondoo (sheep), nguruwe (pig), ng’ombe (cow), batamzinga (turkey) n.k.

Halafu wanyama wanaofugwa kwa ajili ya kuwafanyia binadamu kazi Ni pamoja na; farasi(horse), punda (donkey), ngamia(camel) n.k.

Wanyama wa nyumbani kwa ujumla Ni pamoja na;

1. Mbuzi (goat)

Ng’ombe (cow)

Nguruwe (pig)

Batamzinga (turkey)

Kuku (chicken)

Kondoo (sheep)

Kanga (Guinea fowl)

Kanga wa nyumbani.

sungura(rabbit)

Sungura wa nyumbani. Anafugwa Sana kwa ajili ya chakula.

Ngamia (camel)

Ngamia wa nyumbani: Anafugwa Sana kwa ajili ya kumsaidia kufanya kazi.

Farasi (horse)

Watu wanamtumia kwa ajili ya usafiri.

Mbwa (dog)

Mbwa anasaidia kukimbiza wezi nyumbani.

Paka(cat)

Wanyama wa porini:

Wanyama wa porini Ni wale ambao hawana uhusiano wa karibu na binadamu. Wanyama Hawa huishi msituni.

Wao wanakuwa maadui wa binadamu wakati mwingine.

Wanyama wa porini Ni pamoja na;

Wanyama hawa, ikiwa hawajafugwa, wote wanachukuliwa kuwa wanyama wa porini.

Orodha ya Wanyama wa Porini;

Tumbili (monkey)

Tumbili huwa na sifa karibu na za binadamu.

Pundamilia (zebra)

Chui (leopard)

mbwaMwitu (wolf)

Mbwamwitu anafanana na mbwa tofauti Ni kuwa yeye ansishi msituni.

Twiga ( Giraffe)

Twiga huwa na shingo ndefu ambayo inamsaidia kupata chakula kutoka miti mirefu.

Ngamia (camel)

Mamba (crocodile)

Mamba ansishi katika maziwa makuu.

Bundi (owl)

Sokwe (chimpanzee)

Simba (lion)

Tembo (elephant)

Nyoka (snake)

Kangaruu ( kangaroo)

Kiboko (hippopotamus)


Mbweha (Fox)


Popo (bat)

Chura (Frog)

Panya (Rat)

Mjusi (lizard)

FAIDA ZA WANYAMA:


1. Mbwa husaidia hasa katika suala la ulinzi katika mazingira yanayomzunguka mwanadamu.


3. Mbuzi huwapatia watu nyama, maziwa na pia ngozi yake hutumika kutengenezea vitu kama vile ngoma, mikanda na viatu hasa katika jamii za Afrika.


4. Kware ni ndege mdogo; mayai yake ni madogo sana yana faida kubwa katika mwili wa mwanadamu kwa sababu yanasemekena kutibu baadhi ya magonjwa katika miili yetu.

6. Mifugo hutupatia pesa kwa kuuza nyamamaziwangozikwatombolea na hata wanyama wenyewe. Tunapata pesa nyingi baada ya kuuza wanyama Hawa.

7. Tunapata maziwa kutoka wanyama Hawa kamavile kondoo, mbuzi na ng’ombe.

8. Tunapata chakula kitamu ambacho Ni nyama kutoka wanyama Hawa.

9. Ngozi ya ng’ombe hutumika kutengenezea vitu kama vile ngomaviatumikandanguoVitu vinavyotengenezwa kwa kutumia ngozi ni imara na pia hudumu kwa muda mrefu.

10. Mavi ya wanyama hutumika kama mbolea ambayo huwezesha mazao kukua haraka na kustawi vizuri.

11. Wanyama hawa huondoa upweke kwa watu wasiokuwa na marafiki au mahusiano ya kijamii kama wazee, watoto na wajawazito.

Hivyobasi, wanyama hawa inafaa tuwatunze vizuri kwani tunawategemea katika shughuli mbalimbali za kijamii na za kiuchumi.

Hivyo hawatakiwi kupigwa ovyo. Wanatakiwa waangaliwe afya zao na kupata mahitaji yao.

WANYAMA NA VIKEMBE VYAO.

Vikembe pia huitwa vizawa.

Vikembe ni wana wa viumbe mbalimbali.

Ng’ombe………………….Ndama

Ndama watoto wa ng’ombe.

Nzige…………….kimatu/maige/tunutu/matumatu/funutu

Kimatu mtoto wa nzige.

Ndege……………………..Kinda

Kinda watoto wa ndege

Kipepeo/nondo…………kiwavi

Kiwavi mtoto wa kipepeo.

Nzi…………………………Buu

Buu Ni mtoto wa nzi.

Farasi……………………..Kitekli

Kitekli mtoto wa farasi.

Mamba………………….. Kigwena

Nyangumi…………. Kinyangunya

Fisi…………..,………….. Kikuto.

Ngamia………………….. Nirigi/nirihi

Paka…………..kinyaunyau/kipusi

Ndovu……………………. Kidanga

Mbweha……………….. Nyamawa

Nyani…………………….. Kigunge

Kondoo………………….. Kibebe/katama

Mbuzi…….Kibui/kibuli/kimeme

Farasi na punda………. Nyumbu

Punda……… Kiongwe/kihongwe

Kihongwe mtoto wa punda

Mbu………………………kiluwiluwi

Chura…………………. kiluwiluwi

Kiluwiluwi mtoto wa chura.

Kuku…………………….. Kifaranga

Vifaranga watoto wa kuku

Papa…………………….. Kinengwe

Nyuki……………………. Jana

Simba…………………… Shibli

Shibli mtoto wa Simba.

Sungura………………..,.Kitungule

Vitungule watoto wa sungura.

Samaki……….. Chengo/kichengo

Chui……………… Chongole/kisui

Mbwa……….Kilebu/kidue/kibwa

Kilebu mtoto wa mbwa.

Nyoka………………… Kinyemere

Njiwa……………………Kipura

Paka na Panya kwa Ushirikiano

Paka na panya walitaka kuishi pamoja katika nyumba moja kwa ushirikiano.

Walijitayarisha kwa ajili ya misimu mikali ya ukosefu wa chakula kwa kununua chungu kizima Cha chakula kwasababu hawakuwa na sehemu salama zaidi kwa ajili ya kukiweka, walikiweka kanisani hadi wakati ambapo wangekihitaji.

Hata hivyo, siku moja paka alichukua hamu kwa ajili yake, na akakaribia panya.

Paka kamwambia panya “Sikiliza, panya mdogo, binamu yangu ameniita kutumika kama baba wa kidini wa mtoto wake. Amejifungua mtoto mdogo wa rangi ya kahawia na nyeupae, na natakiwa kumsindikiza hadi ubatizo wake.

Je, ni sawa mimi kukuacha hapa nyumbani peke yako na kazi za nyumbani leo halafu nikamsindikiza binamu yangu?

Nenda mbele,” panya alisema, “na ikiwa watakuhudumia chakula kizuri, nifikirie tu ndugu yangu.

Hakika paka alikwenda moja kwa moja kanisani na kula chakula walichokihifadhi kwa misimu mikali kisha akaenda kuzunguka-zunguka mjini na hakurudi nyumbani hadi jioni.

Nyakati za saa kumi na mbili, paka alionekana akitembea mwendo wa kobe tumbo mbele yake Kama mawaziri wa Uganda.

“Lazima ulikuwa na wakati mzuri,” panya alisema. “Walimpa mtoto jina gani?”

Shiba,” paka akajibu.

Shiba! Hilo ni jina gani, ambalo bado sijalisikia.” Au Kama wewe umeshiba?

Muda mfupi baadaye paka alichukua hamu nyingine, akaenda kwa panya, na kusema, “Nimeombwa kutumika kama baba wa kidini kwa mara nyingine tena.

Mtoto ana pete nyeupe kuzunguka mwili wake. Siwezi kusema hapana. Utakuwa na kunifanyia upendeleo na kutunza nyumba peke yako leo.”

Panya alikubali, na paka akaenda na kula nusu ya mafuta. Aliporudi nyumbani, panya aliuliza, “Je! Mtoto huyu wa mungu alipokea jina gani?.

12 thoughts on “WANYAMA NA VIKEMBE VYAO-KIDATO CHA KWANZA

  1. Asante sana mkeleketwa WA lugha kwa juhudi zako za utafiti lakini tulisoma pamoja hapo Stuart kwa hayo mashule kwani usinitafutie kazi nikaachana na kijiji. Asante

    Like

Leave a reply to Brian nyaga Cancel reply