Imeandikwa na: Mwalimu Arigumaho Johnpaul
Tarehe: 5 Agosti 2025
Kitengo: Kiswahili | Afrika Mashariki Fest
π Baada ya mafanikio makubwa ya Kongamano la Kimataifa la Kiswahili lililofanyika Kololo, Uganda, Afrika Mashariki Fest inakualika katika safari ya pili ya kihistoria: Twende Zetu Kuhiji Butiama 2025!
π₯ Tunapanga kusafiri na majina haya maalum kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki ili kuendelea kuhamasisha, kusherehekea na kuonyesha umuhimu wa umoja na mshikamano wa Afrika Mashariki, tukilenga Kiswahili kama lugha ya kutuunganisha pamoja, kutufafanua kama Waafrika na kutupeleka mbele kama jamii moja yenye ndoto moja.
π Tutakaoafiri nao na waliokaribishwa ni pamoja na:
KENYA
- Prof. PLO Lumumba β Mwanasheria maarufu, mwanamapinduzi na sauti ya Uafrika
- Prof. Wallah Bin Wallah β Mshairi hodari, mwalimu wa Kiswahili, na mtaalamu wa fasihi mashuhuri
- Dr. Kimani Njogu β Mwandishi na mchambuzi wa masuala ya lugha
- Prof. Clara Momanyi β Mtaalamu wa Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Kenyatta
- Eric Omondi β Mchekeshaji na balozi wa vijana barani Afrika
TANZANIA
- Prof. Mutembei β Mtafiti na mhadhiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
- Dr. Ahmad Sovu β Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere
- Joram Nkumbi β Balozi wa BAKITA na mlumbi wa lugha
- Vanessa Mdee β Msanii na mhamasishaji wa vijana kupitia Kiswahili
UGANDA
- H.E. Hon. Col (Rtd) Fred Mwesigye β Balozi wa Uganda nchini Tanzania
- Brig. Gen. Henry Isoke β Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Ufisadi, Ikulu
- Mwalimu Arigumaho Johnpaul β Mwandishi, mtafiti na mtetezi wa Kiswahili Uganda
- Mwalimu Abraham Kubakurungi β Mhadhiri na mtafiti, Bishop Stuart University
- Dr. Kisembo Ronex β Mkurugenzi wa Afrika Mashariki Fest na mwanaharakati wa Kiswahili
- Jose Chameleone β Msanii maarufu wa Uganda ambaye ameimba nyimbo za Kiswahili zilizotapakaa kote Afrika Mashariki, akiwakilisha utamaduni na umoja wa kikanda kupitia muziki
RWANDA
- Dr. Charles Murigande β Mwanadiplomasia na msomi
- Marie Claire Ingabire β Mwalimu na mwanaharakati wa Kiswahili nchini Rwanda
- Bruce Melodie β Msanii anayejihusisha na lugha ya Kiswahili miongoni mwa vijana
BURUNDI
- Dr. DΓ©ogratias Niyonzima β Mtafiti wa lugha na utamaduni
- Aline Umutoni β Msanii na muigizaji wa tamthilia za Kiswahili
SUDAN KUSINI
- Hon. Albino Aboug β Mbunge wa Sudan Kusini na mtetezi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
ποΈ Tarehe na Mahali:
π Butiama, Mkoa wa Mara, Tanzania
π
Septemba 26 β 30, 2025
π Yatakayojiri:
- Ziara ya Jumba la Makumbusho la Mwalimu Nyerere, Mwitongo
- Misa Maalum ya Kumuombea Mwalimu Nyerere
- Midahalo ya Kiswahili, Uongozi na Maadili ya Kiafrika
- Usiku wa Mashairi, Filamu, Hadithi na Moto wa umoja
- Ziara ya Mbuga ya Wanyama ya Serengeti β tukihisi uhai wa Afrika
π° Gharama:
UGX 650,000 / USD 170
(Inajumuisha: usafiri, milo, malazi ya starehe, na shughuli zote)
π Jisajili Sasa:
π Tembelea: www.afrikamasharikikwetu.org
π¦ Benki: UBA Bank β Tawi la Jinja Road
- Akaunti ya UGX: 0153007291
- Akaunti ya USD: 0153007307
- Jina: BUTIAMA PILGRIMAGE SAFARIS
π Mawasiliano:
WhatsApp / Simu: 0772963625 / 0704611062
Email: info@afrikamasharikikwetu.org
π£οΈ Kaulimbiu Rasmi ya 2025:
“Kuhimiza Urathi na Maadili ya Mwalimu Julius Nyerere: Kuimarisha Jumuiya kwa Kukubali na Kuitumia Lugha ya Kiswahili.”

Hujambo kaka.
Zangu ni shukrani kwako kwa bidii zako za kuendelea kukieneza Kiswahili. Isingekuwa kwamba nitakuwa nimerudi Ughaibuni kwa sababu za kikazi, ningeandamana nanyi kwenda BUTIAMA. Kila la heri katika safari yenu.
LikeLike
Ndugu yangu,
Asante sana kwa maneno yako na kututia moyo. Ingawa uko mbali, roho yako iko nasi. Nakutakia mafanikio mema huko ughaibuni.
Tutaendelea kueneza mwanga wa Kiswahili popote tulipo. πβπΏ
Tuwasiliane kupitia +256778514179.
#TwendeZetuButiama #KiswahiliMoja
LikeLike