Kongamano la Kiswahili Shule ya Upili Uganda Martyrs Namugongo 29 JUNI 2025

Kongamano la Kiswahili Shule ya Upili Uganda Martyrs Namugongo

Tarehe: 29 Juni 2025

Shule ya Upili Uganda Martyrs Namugongo inajivunia kuandaa na kukukaribisha kwa kongamano la Kiswahili tarehe 29 Juni 2025. Kongamano hili limeandaliwa kwa lengo la kusaidia wanafunzi na walimu kuboresha mbinu za ufundishaji na utathmini wa Kiswahili pamoja na kuongeza ujuzi hasa kwa watahiniwa wetu mwaka huu 2025.

Malengo ya Semina

Kongamano hili lina malengo makuu matatu muhimu:

  1. Kutambua changamoto za watahiniwa wa Kiswahili wa mwaka jana:
    Tutachambua makosa yanayojirudia mara kwa mara katika mtihani wa Kiswahili na kutoa mikakati bora ya kuwasaidia wanafunzi kuboresha ujuzi wao, kuongeza kujiamini na kupata matokeo mazuri zaidi.
  2. Kuimarisha uelewa wa sarufi na uandishi wa insha:
    Tutafundisha wanafunzi miundo muhimu ya kisarufi na kuwasaidia jinsi ya kuandika insha kwa njia rahisi na yenye ubora, jambo ambalo ni msingi muhimu katika mtihani wa Kiswahili.
  3. Kuboresha uwezo wa wanafunzi katika fasihi:
    Tutawasaidia wanafunzi kuchambua na kufasiri kazi za fasihi kwa urahisi. Pia, tutaelekeza namna bora ya kujibu maswali ya fasihi katika mtihani, kwa njia ambayo itawasaidia kupata alama nzuri.

Kongamano linamlenga nani?

  • Wanafunzi: Wanafunzi wa Kiswahili hasa kidato cha tatu na nne ili waweze kupata faida kubwa kwa kushiriki semina hii.
  • Walimu wa Kiswahili: Walimu wataweza kupata fursa ya kuelekezwa jinsi ya kutunga maswali na kuboresha mbinu za kufundishia Kiswahili na kuleta mabadiliko chanya katika darasani.
  • Wadau wa Elimu: Watu wote wanaopenda na kuhamasisha matumizi ya Kiswahili nchini, na hasa wale wanaoshirikiana na shule katika kukuza lugha hii muhimu.

Mwongozo wa Kongamano

  • Kongamano litafanyika kwa siku moja, tarehe 29 Juni 2025, shuleni Uganda Martyrs SS Namugongo.
  • Kila kipindi cha semina kitashughulikia mojawapo ya malengo yaliyotajwa hapo juu.
  • Kutakuwa na mafunzo ya vitendo, mijadala na maswali na majibu ili kuhakikisha kila mshiriki anapata uelewa wa kina.
  • Kutakuwa na miongozo ya karatasi zote mbili yaani 336/1 na 336/2 ambayo itasaidia walimu na wanafunzi kujipangia mitihani ya mwaka huu.
  • Mwisho wa kongamano kutakuwa na tathmini ndogo ya mwelekeo wa matokeo na mapendekezo ya hatua za kuendelea kuboresha kutoka kwa walimu na wanafunzi.

Kongamano hili ni fursa nzuri kwa kila mwanafunzi na mwalimu wa Kiswahili kujifunza mbinu za kuongeza ufaulu na kuendeleza lugha yetu ya Kiswahili. Tunawahimiza nyote kushiriki kikamilifu ili kupata mafanikio makubwa katika mtihani wa Kiswahili wa mwaka huu. KISWAHILI LEO KISWAHILI KESHO NYUMA HATURUDI

JOHNPAUL ARIGUMAHO 0778514179

MUKAMA CHRISPUS 0702745415

3 thoughts on “Kongamano la Kiswahili Shule ya Upili Uganda Martyrs Namugongo 29 JUNI 2025

  1. Shikamoo kaka , tutahudhuria bila shaka

    On Wed, May 28, 2025, 10:39 AM Jifunze Kiswahili na mwalimu Johnpaul

    Like

Leave a reply to Glorious Anyorekire Cancel reply