“Itabidi utoe mimba hiyo. Siko tayari kwa jukumu hilo kwa sasa! Tafadhali, nitagharamia kila kitu katika zoezi zima la utoaji mimba.
Chochote kitakachohitajika, niko tayari kulipa. Nitakupa pesa, nenda tu kliniki utoe mimba hiyo!. Ninataka zoezi hili lifanyike ndani ya masaa 24.” Ali alimwambia Namakula. Walikuwa kwenye hoteli kuu ya Moonlight ambako Ali alikuwa ameenda kukutana naye ili waongee ana kwa ana kuhusu hali hiyo.
“Kwa nini unataka kukatisha maisha ya mtoto asiye na hatia? Kwanini hutaki mtoto? watu wengi wanatafuta watoto na sisi sasa tuna wetu dhahabu na unataka niitoe mimba? Sidhani kama nitafanya hivyo. Sitoi mimba!.” Namakula alisema bila kupepesa macho huku Ali akionekana kuwa na wasiwasi.
“Namakula, huelewi ninachosema. Ukweli ni kwamba habari hizi zikisambaa na watu wakajua kuwa nimekupa mimba, zitaharibu maisha yangu. Angalia, kilichotokea kati yetu kilikuwa ni bahati mbaya tu, hakukuwa na kitu zaidi. Kwa kweli, ilikuwa ni makosa na nilikuwa nimelewa usiku ule. Sikuwa na fahamu zangu kamili. Tafadhali, uondoe mimba hiyo.” Ali alisema huku sauti yake ikiishilia.
Hali ilizidi kuwa tete.
“Sina hakika naweza kufanya hivo!. Tafadhali, fikiria juu yake. Je, nikifa katika mchakato huo? Utoaji mimba ni hatari. Hebu tupate mtoto. Ni jambo jema. Hata kama hautanioa, chukua jukumu la kumlea mtoto, sijali. Nitamtunza mtoto na huo ndio uamuzi wangu wa mwisho.” Namakula aliapa. Baadhi ya wateja walianza kupiga kelele za kuhudumiwa kwani walikuwa wamesubiri kwa muda mrefu, hivyo Namakula alitaka kuachana na mazungumzo hayo na kwenda kuwahudumia. Alisimama ili kuondoka lakini Ali alimshika mgongo. Alilazimika kuketi tena.
“Inaonekana yote ninayosema hayaingii masikioni mwako. Je, una maji masikioni au una tatizo la kusikia? Nimesema siwezi kuwa na mtoto. Ukweli ni kwamba nimeoa.” Hatimaye Ali aliamua kufunguka.
Namakula alinyamaza kwa muda kana kwamba hakusikia alichokisema. Alimsikia vizuri sana, lakini alikuwa akijaribu tu kufikiria vizuri amemanisha nini juu ya kuoa
“Unasema?” Namakula aliuliza huku akiwa na mikunjo ya maumivu na hasira usoni mwake.
“Nimesema nimeoa tayari. Ukweli ni kwamba, usiku nilipolala kwako nilikuwa hotelini na mke wangu. Huo ulikuwa usiku wa harusi yetu na tulikuwa pale kwa honeymoon yetu. Tulibishana kidogo tu ndio maana niliangukia mikononi mwako. Tafadhali, toa mimba hii ikiwa hutaki kuharibu maisha na ndoa yangu.” Ali alisema huku akipeperusha pete yake usoni mwa Namakula ili kuthibitisha kwamba ashachukuliwa tayari.
Alikuwa amekuja katika bar na begi dogo lenye milioni 1, Kwa haraka akaidondosha mezani kwa Namakula.
“Katika begi hili, kuna milioni 1 kwa ajili yako. Tafadhali, itumie kutoa mimba. Na tafadhali, usithubutu kunipigia simu tena. Ninapoondoka kwenye hoteli hii, ninafuta nambari yako ya simu na sitaki kukuona tena maishani mwangu. Hatukuwahi kuwa na mahusiano, lililotokea kati yetu lilikuwa bahati mbaya. Ichukulie tu kana kwamba hatukuwahi kukutana na hukumjua mtu yeyote anayeitwa Ali. Nimeoa na nina furaha na ndoa yangu” aliongea huku akisimama na kuiacha ile bar kisha akatoka nje ya hoteli hiyo akiwa ndani ya gari lake aina ya Subaru.
Namakula alipatwa na kiwewe na kuvunjika moyo kupita maelezo.. Ana umri wa miaka ishirini na tatu na Ali alikuwa mwanaume wa kwanza kuwahi kulala naye. Alianza kujilaumu.
“Nimetunza mwili wangu kwa miaka mingi ili tu nimpe mwanaume ambaye hatauthamini mwili wangu?!. Mimi ndiye mjinga!. Sijui pia nilikuwa mlevi au vipi? Kwa nini nililala na mwanaume niliyekutana naye hivi punde?” Namakula alijiuliza kwa huzuni. Aliisimama kutoka kwenye kiti cha plastiki alichokuwa amekalia na kukimbilia kwenye baa. Alichukua begi lake la mkono, akatoa kalamu na karatasi, akaandika barua yake ya kujiuzulu na kuondoka hotelini, asirudi tena.
wakati huo huo, nyumbani kwa Ali, ilikuwa ni mwezi mmoja sasa baada ya Ali na Catherine kuoana na mambo yaliendelea kuwa mabaya kati yao chumbani. Kwa mwezi mmoja, Catherine alikataa kumruhusu Ali kufanya naye mapenzi.
Kwa kweli, mambo yalikuwa mabaya zaidi kwa sababu muda si muda waliacha kulala katika chumba kimoja. ilikuwa ni kama pepo linampagawisha Catherine na hangemruhusu mume wake aone hata uchi wake.
Mwanzoni mwa mwezi wa pili baada ya ndoa yao, Ali alikumbwa na msononeko wa mawazo na huzuni. Alijiuliza kama amefanya makosa kumuoa Catherine.
“Kwa nini nisifanye mapenzi na mwanamke ambaye nimemuoa? Kwa nini sitakiwi hata kugusa na kuhisi mwili wa mke ambaye nililipa mahari kwa pesa yangu mwenyewe?. Mwanamke niliyemuoa siku thelathini zilizopita amenikataa na kuuweka mbali kabisa mwili wake kwangu. Anakataa kuvua nguo mbele yangu. Anakataa kuniruhusu niuone uchi wake.” Ali alisema jioni moja alipoenda kupata chupa moja ili apunguze mawazo . Kichwa chake kilikuwa kikizunguka na alikuwa akitafakari kwa kina.
“Ananificha nini? Je, mimi si mume wake? hata biblia inasema wawili watakuwa mwili mmoja na hawataona haya. Au yeye si mwanamke? Je, hana lile tunda muhimu la kunifurahisha chumbani? Jambo baya zaidi ni kwamba sijawahi hata kuona uchi wake katika miaka sita iliyopita. Je, nina uhakika gani kuwa yeye ni mwanamke? Mungu wangu, nimejiingiza katika chaka gani hili? Lakini hili lina mwisho; .” Ali alitamka kwa umakini.
Licha ya yote hayo, hakuwahi kumwambia mtu yeyote kile kilichokuwa kikiendelea. Hajui angewezaje kufunua mdomo wake na kusema kwa masikio ya watu kwamba mkewe alikataa kuguswa kwa siku thelathini baada ya harusi.
Usiku huo, Ali alienda nyumbani, akiwa amedhamiria kufanya mapenzi na mke wake kwa namna yoyote ile, iwe kheri au shari. Alipofika nyumbani saa mbili usiku, mkewe, Catherine alikuwa tayari amelala. Basi akaingia chumbani, akamvua gauni lake na kuanza kumshikashika.
Alikuwa tayari kabisa kumlazimisha ikiwa atakataa. Mwanzoni, hakusogea huku akilegea mwili wake kana kwamba alikuwa akifurahia mguso wa Ali. Hata alimrudishia busu lake na pia akamgusa kwa njia iliyooneshaa mwanamke ambaye yuko tayari kwa malavidavi na upendo. Lakini mwili wa Ali ulipopata joto na alipotaka kufikia chungu cha asali, alimsukumia mbali.
“Mpenzi tafadhali acha. Siwezi kufanya hivi. Mwili wangu hauko tayari. Siko tayari, kufanya mapenzi na wewe bado. Tafadhali niruhusu nilale.” Catherine akamwambia mumewe.
“Hii ni kauli ile ile ambayo umekuwa ukiitoa kila siku mwezi mmoja umepita sasa. Kauli hiyohiyo nimekuwa nikiisikia tangu nilipokutana nawe. Catherine una miaka ishirini na saba Je, wewe ni mtoto? Mwili wako utakuwa tayari lini?” Ali aliuliza kwa sauti ya hasira iliyojaa mfadhaiko na kukosa msaada.
“Ni mwili wangu. Nina haki ya kusema sitalala na mume wangu. Ni mimi tu najua nitakapotaka. Nikitaka nitakujulisha. Wewe ni mume wangu tu na humiliki mwili wangu. Mimi nina umiliki kamili wa mwili wangu na utauonja tu nitakapotaka.” Catherine alisema huku akiufunika mwili wake kwa nguo.
Ali alihuzunika. Alijiona kana kwamba si mwanaume tena. Utu wake wa kiume ulichubuka. Maumivu yalikuwa mengi sana kwake .Alimrukia Catherine na kuanza kumlazimisha kulala naye. Alirarua nguo zake zote, huku wakihangaika kitandani kama watoto wadogo wanaogombana.
Catherine alipiga kelele na majirani walikuwa wakizisikia. Ali hakufanikiwa kwani licha ya kurarua gauni lake la kulalia Catherine alibana mapaja yake Ikabidi asimame na kwa hasira alienda kulala chumba kingine.
Asubuhi iliyofuata, Catherine alimripoti mumewe polisi kwa shitaka la ubakaji. Ali alikamatwa na kuwekwa ndani….
Je, unashabiki tendo la Catherine?

Kazi bora
On Mon, Oct 30, 2023, 9:18 AM Jifunze Kiswahili na mwalimu Johnpaul
LikeLike
Umesoma?
LikeLike