KUKUA NA KUENEA KWA LUGHA YA KISWAHILI AFRIKA MASHARIKI

Kiswahili ni lugha ambayo ilikuwa ikitumiwa na wakazi wa maeneo ya pwani ya Afrika Mashariki hata kabla ya ukoloni. Lugha hii ilitumika katika kufanyia mawasiliano na ilitumika kuwaunganisha watu kwa kuwa waliweza kuelewana na kuongea kwa mshikamano wa watu wengi.

Lugha ya Kiswahili iliweza kukua sana na kuenea katika nchi ya Tanzania kuliko Kenya na Uganda kutokana na sababu zifuatazo.

  • Kuteuliwa kwa lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya taifa: baada ya kupata uhuru mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliteua lugha ya Kiswahili itumike kama lugha kuu.
  • Hii ilipelekea sana kuenea kwa lugha ya Kiswahili Tanzania kuliko nchi za Kenya na Uganda pamoja na kuanzisha vyama mbalimbali kama BAKITA, BAMITA na vingine ambavyo vilisaidia kukua kwa lugha ya Kiswahili kwa kuongeza misamiati ambayo ilifanya lugha ya Kiswahili kuendelea kukua.
  • Vyombo vya habari kama vile televisheni, redio na hata magazeti ambavyo vilizungumza na kuchapisha majalada mbalimbali kwa kutumia lugha ya Kiswahili.
  • Kutumika kwa Kiswahili kama lugha ya kufundishia: lugha ya Kiswahili ilitumika kufundishia katika shule za msingi mpaka vyuoni kwa hiyo hili lilipelekea kuelea na kuenea kwa lugha ya Kiswahili Tanzania kuliko Kenya na Uganda. Mnamo mwaka 2009 taasisi hiyo ilibadilishiwa jina baada ya kuungana na idara ya Kiswahili chuo kikuu cha Dar es Salaam na kujulikana kwa jina la Taasisi za Taaluma za Kiswahili (TATAKI) ikawa imejiongezea dhima nyingine ya kufundisha taaluma mbalimbali za Kiswahili. Dhima hizo ni:
  • Kufanya utafiti wa kuiendeleza na kuikuza lugha ya Kiswahili
  • Kuendeleza uchapishaji wa jarida la Kiswahili
  • Kutoa machapisho mengine yatakayoonekana kuwa na manufaa
  • Kukusanya taarifa zote za sasa zilizopo ulimwenguni
  • Kufanya miradi ya utafiti ya muda mrefu
  • Kutafsiri maandishi yafanyayo katika Kiswahili
  • Vyombo vya habari
  • Tangu kupata uhuru hadi hivi sasa kumekuwepo na ongezeko kubwa la vyombo vya habari nchini. Vyombo hivi ni kama:
  • Magazeti: kuna magazeti mengi yanayochapishwa kwa lugha ya Kiswahili; mfano wa magazeti hayo ni Uhuru, Mzalendo, Mwananchi, Nipashe, Mtanzania na kadhalika. Magazeti yanayochapishwa kwa lugha ya Kiswahili yamekuza Kiswahili kwa njia kuu mbili:
  • Mfumo wake wa kuchapisha habari kwa kutumia Kiswahili
  • Kuwa na safu maalumu zinazohusiana na taaluma ya Kiswahili, mathalani uhakiki wa vitabu, mashairi na hadithi. Kutokana na kusoma magazeti hayo watu wengi wameweza kukijua Kiswahili kuliko hapo awali
  • Redio na televisheni; kumekuwa na ongezeko kubwa la vituo vya redio na televisheni baada ya uhuru. Kwa upande wa redio baadhi ya vituo hivyo ni TBC taifa, Redio one, Redio Free Afrika, Sauti ya Tanzania Zanzibari na kwa televisheni kuna ITV na vinginevyo.
  • Uenezi wa Kiswahili na magazeti kama vile; Daima – Tanzania, Zanzibar, Taifa Leo, Un Nuur, Jamvi ya Habari, Mwananchi, Habari Leo, Majira, Nipashe, Raia, Moja, Mwanahalisi, Upendo, Uhuru, Michezo, Maendeleo.

Ghanem (2005) anaeleza kwamba lugha ya Kiswahili ni miongoni mwa lugha kubwa barani Afrika.

Ukubwa wake inafaa kabisa kuwa lugha ya kidiplomasia .Matumizi ya lugha katika masuala ya kidiplomasia yatakifanya Kiswahili kuenea kwa kiasi kikubwa Zaidi ya kupata wazungmzaji wengi kuliko sasa.

Mohamed (2006) anataja lugha kubwa barani Afrika kuwa Kihausa, kifulani, kizulu, kilingala, kiarabu na Kiswahili. Hata hivyo, Kiswahili kinazishinda lugha za kihausa na kifulani katika kuruka mipaka na kutumiwa katika shemu kubwa ya bara la Afrika ikilinganishwa na lugha hizo. Lugha za kihausa na kifulani huzungmzwa katika nchi za Nigeria na karibu nchi zote za magharibi. Kiswahili kinazungmzwa katika nchi zote za Afrika mashariki yaani Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi, na Uganda.

Pia, kinazungmzwa Afrika ya kati hasa katika Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo, Zambia, Malawi, msumbiji, Somalia, na sehemu mbalimbali za Afrika na nje (Amir; 1994, sherrif; 1994, na ohwida; 2006). Kiswahili kuwa lugha kubwa duniani kumekifanya kitumike katika maendeleo ya maisha ya mwanadamu ya kila siku.

Mohamed (2006) anaeleza kuwa Kiswahili nchini Kenya, Tanzania, na Uganda kimetangazwa kama lugha ya taifa kwa maana ya kutumika katika shughuli za kila siku za kiserikali, kisiasa, kidini, na kijamii.

Katika kukienzi na kukikuza Kiswahili, mifano ya nchini Tanzania kinafundishwa kama somo kuanzia ngazi ya elimu ya msingi mpaka vyuo vikuu. Vile vile, kinatumika kama lugha ya kufundisha elimu ya msingi.

Katika nchi za Kenya, Rwanda, Burundi na Uganda Kiswahili kinafundishwa kama ngazi ya elimu ya msingi hadi vyuo vikuu.

Pia, Mohamed (2006) anaeleza kwamba hivi sasa Kiswahili kinafundishwa kama somo katika viwango mbalimbali vya elimu katika nchi za lybia, Afrika ya kusini, Nigeria, Ghana, sudani, marekani, uingereza, china, japan, korea ya kusini, oman, mexico, nakadhalika. Hali hii huifanya lugha ya Kiswahili kukua na kuenea Zaidi katika sehemu mbalimbali kote duniani.

Mohamed (2006) anaongeza kusema kwamba kwa sasa ipo mikakati ya kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya umoja wa nchi za Afrika. Dalili za kufanikiwa kwa mikakati hiyo zimeishaanza kuonekana kutokana na lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha maalumu zinazotumiwa katika mikutano ya umoja wa nchi za Afrika.

Rais mstaafu wa Msumbiji bwana Chisano na rais wa Tanzania dkt Jakaya Kikwete ni miongoni mwa viongozi wakubwa wanaotumia lugha ya Kiswahili katika vikao vya mataifa ya Afrika.

Mohamed (2006) anashadidia kwamba kiongozi wa Lybia kanali Mohamed Al-Qaddafi (kwa sasa ni marehemu) alionyesha dhamira ya dhati kabisa kukifanya Kiswahili kuwa ndyo lugha kuu barani Afrika.

Nia yake njema bwana kanali Mohamed Al-Quddafi juu ya kukifanya Kiswahili kionekane pale serikali yake ilipoamua kutoa fedha za kuwasomesha wanafunzi wa Lybia, lugha ya Kiswahili ngazi mabalimbali ili wapatikane walybia ambao ni walimu wa lugha ya Kiswahili (Ghanem; 2005,

Mohamed; 2006, ohwida; 2006). Wanafunzi hao kutoka lybia wanasomea katika vyuo mbalimbali ndani na Nje ya Lybia, mfano wapo wanafunzi toka Lybia wanasomea Tanzania, Kenya na nchi nyingiine za Afrika. Hata baada ya mapinduzi ya Lybia, sera ya kukieneza Kiswahili bado imeshikiliwa na viongozi wapya wa serikali.

Lugha ya Kiswahili inatambuliwa kama lugha ya kimataifa kwa sababu inatumika katika shughuli za kiuchumi, kidini na kisiasa katika ngazi za kimataifa. Vyuo vingi barani Afrika, Ulaya, Asia na Marekani vinafundisha somo la Kiswahili.

Vituo vingi vya redio hurusha matangazo yao kwa lugha ya Kiswahili pia. Kiswahili ni miongoni mwa lugha zilizotafitiwa sana na kuandikiwa vitabu vingi na makamusi. Maandishi mengi ya Kiswahili yamechapishwa na kusambazwayakiwemo majarida, vitabu vya dini, riwaya, tamthilia, mashairi na nyimbo zinazoimbwa pamoja na vitabu vya hadithi fupi. Kazi nyingi pia zimetafsiriwa kwa Kiswahili. Wazungumzaji wa Kiswahili wanakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 140, ( (R.M, 1998) Chimerah 1998; Lewis na wenzake 2013) katika makala ya Ethnologue Toleo la 17

Kwa mujibu wa (Nkwera, 2003) waarabu walifika pwani ya Afrika mashariki karne ya kumi. Walipofika hapa waliwakuta wenyeji wanazungmza Kiswahili na kutokana na nia ya kueneza biashara yao hususan ile ya watumwa, walishirikiana sana na watumwa katika dini, biashara na kuoana. Waarabu walitumia lugha ya Kiswahili kila walipopita kufanya biashara yao. Lugha ilikuwa ya muhimu sana katika mawasiliano ya kila jambo walilolifanya waarabu kati yao na wenyeji hususan kwa kuwatumia watumwa wao. Kwa kufanya hivyo, walijikuta tayari wanaeneza Kiswahili.

Katika kuhakikisha kuwa lugha hii inafundishwa vyema na biashara inaendelea bila tatizo, waarabu walianzisha vituo maalumu kwa ajili ya biashara na huo huo kufundisha dini ya kiislamu. Vituo vya kibiashara kamavile Tabora, Ujiji, vilikuwa na umuhimu mkubwa sana katika kueneza dini ya kiislamu na lugha ya Kiswahili.

Wamishenari na dini yao ya kikristo walifika pwani afrika mashariki kabla ya utawala wa wakoloni. Mashirika mbalimbali ya kidini yaliingia afrika mashariki katika nyakati tofauti tofauti. Mashirika haya ni roho mtakatifu toka ufaransa mwaka wa (1868), white fathers toka ufaransa mwaka wa (1878), church missionary society ambalo liliongozwa na J.C krapf kutoka ujerumani. Shirika hili mwaka wa (1876) liliandika sarufi ya kwanza ya Kiswahili cha kimvita katika kitabu kilichoitwa ‘’OUTLINES OF THE ELEMENTS OF KISWAHILI LANGUAGE’’ amabyo ilikuwa na marejeo mahususi ya lahaja ya kinika. (Tafsiri yangu)

Pia, mwaka wa (1845) orodha pana ya maneno (muhtasari) wa sarufi pamoja na tafsiri ya injili ya luka na yohana ili kuwasaidia wamishenari wengiine ambao walikuwa wakiletwa Afrika ya mashariki. Mwaka wa (1905) misioni ya Magila walitoa kijitabu juu ya historia ya wasambaa na kilichoitwa ‘’habari za Wakilindi’’ Makao makuu ya shirika hili yalikuwa Mombasa.

Shirika la misioni ya vyuo vikuu katika Afrika ya kati (UMCA) (UINGEREZA) iliingia mwaka wa (1875). Shirika hili lilijishugulisha kukiweka kiunguja katika maandishi mwaka wa (1870). Askofu Edward steere alichapisha toleo la kwanza la sarufi ya Kiswahili cha kiungujalililoitwa ‘’A HANDBOOK OF THE KISWAHILI LANGUAGE’’ iliyozungmzwa nchini unguja. Pia walichapisha vitabu vya nyimbo na kamusi za Kiswahili na kingereza-kiswahili.

Kazi ya awali ya kuziandaa kamusi hizo ni ya Edward Steere lakini ilikamilishwa na A. Madan na badaaye kurudiwa na F. Johnson aliyeandaa kamusi mbili ‘’A STANDARD ENGLISH-SWAHILI DICTIONARY’’ ambazo zilitolewa mwaka wa (1939).

UMCA pia walichapisha magazeti ya msimulizi (1888), Habari za mwezi (1876) pwani na bara (1910).

Kwa ujumla, wamisheni walijishughulisha sana na kiswahili kwasababu walikihitaji katika shughuli zao za kidini na kwakufanya hivyo walijikuta wanakikuza na kukieneza Kiswahili kwa kiasi kikubwa kufuatana na uongezekaji wa vituo vyao.

Baadhi ya vituo hivyo Bagamoya (1868), Magila (1864), mpwapwa (1876), ujiji (1877), Masai (1876), Zanzibar (1860), na ziwa nyasa (1881).

Tunafahamishwa na Nkwera (2003) kwamba wajerumani wameitawala Tanganyika kwa miaka thelathini (28) yaani (1885-1916) kwa jina la ‘’DEUSTCH UST AFRIKA’’ (Afrika mashariki). Wajerumani walipoingia Tanzania walikuta tayari kuna misingi mizuri ya lugha ya Kiswahili.

Wamisheni walikuwa tayari wameandaa mfumo wa elimu na dini uliokuwa unatumia lugha ya Kiswahili. Kutokana na misingi hiyo, utawala wa kijerumani ulipoanzishwa nchini tayari Kiswahili kilikuwa kimeimarika. Kwahiyo, wajerumani walikiona kama chombo muhimu sana kwa kuwasiliana na wananchi.

Kama inavyofahamika, chimbuko la Kiswahili ni upwa wote wa Afrika Mashariki. Hata hivyo lugha hii haikubaki tu katika eneo la pwani bali ilienea katika sehemu kubwa ya Afrika Mashariki. Sababu za kuenea katika sehemu mbalimbali za Afrika Mashariki kulisababishwa na mambo mengi. Yako mambo yaliyosababisha kuenea kwa Kiswahili kutoka pwani hadi bara. Mambo hayo ni shughuli za biashara, dini, ukoloni na hatimaye harakati za kupata uhuru.

Mbali na biashara, (Mwaro, 2002) anaeleza kuwa wamishenari nao walipofika hapa Afrika Mashariki walisaidia sana katika kufanikisha maenezi ya Kiswahili.

Kwa kuanzia wamisionari waliandika vitabu na hata kuchapisha magazeti kwa kutumia Kiswahili. Mwaro (2002) anaeleza kuwa shughuli za utangazaji pia zimechangia katika kukisambaza Kiswahili ulimwenguni kote na hivyo kukifanya kuwa lugha ya Kimataifa. Idhaa maarufu za utangazaji duniani kama vile B.B.C, V.O.A, Dutche Welle, Radio China na Radio Moscow huwa na vipindi vya matangazo kwa Kiswahili.

Idhaa hizi basi huchangia katika kuikuza lugha ya Kiswahili kama lugha ya kimataifa. Tunayo magazeti yaliyochapishwa na yalisaidia sana kukieneza Kiswahili, kwa mfano, Habari za mwezi -1988, Pwani na bara – 1910, Barazani – 1910, Rafiki yangu, Habari za Wakilindi 1903, Gazeti la Msimulizi, Kitabu cha Wakilindi.n.k.

Baada ya nchi za Afrika Mashariki kupata uhuru (Tanganyika 1961, Uganda 1962, Kenya 1963 na Zanzibar 1964 baada ya Mapinduzi, kila nchi ikawa na kipaumbele chake katika sera ya lugha. Nchini Tanganyika na Kenya, Kiswahili kilitumika kujenga umoja na kilifanywa kuwa ni lugha ya taifa kwa nchi hizi mbili.

Kwa upande wa Tanganyika, Kiswahili kilifanywa kuwa ni lugha ya kufundishia masomo yote katika shule za msingi na pia kama somo kuanzia darasa la kwanza hadi la nane/saba. Kwa upande wa sekondari, Kiswahili kinatumika kama somo kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne na kwa kidato cha tano na sita ilikuwa ni somo la upendeleo na si la lazima.

Hatua zilizochukuliwa na Serikali ya Tanganyika katika kukiendeleza na kukikuza Kiswahili ni kwa kuanzisha asasi kadhaa kama:

Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Idara ya Kiswahili kwa ajili ya kufundisha fasihi na isimu baada ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuundwa kwa Sheria ya Bunge, 1970.Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima 1975, Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita) 1976

Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni (TAKILUKI), Zanzibar kwa ajili ya kufundisha, kukuza na kuendeleza Kiswahili na pia lugha za kigeni kama Kiarabu, Kifaransa, Kireno, Kijerumani na Kiingereza. Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA)

(Muaka, 2011) anaeleza kuwa hata ingawa lugha ya Kiswahili ni lugha ya kiasili nchini Kenya, lugha hii imekuwa na kusambaa kimatumizi hadi kuwa lugha ya taifa na lugha rasmi nchini Kenya mbali na kuwa lugha ya Kimataifa. Kufikia karne ya 13, lugha ya Kiswahili ilikuwa imeanza kukua na kuenea hadi kufikia kiwango hiki chake cha sasa wakati ilipoanza kutumiwa kama lugha ya kibiashara kati ya wageni wa awali wa pwani ya Afrika Mashariki kama vile Wareno na Waarabu na wenyeji wa Kiafrika wa pwani ya Afrika Mashariki.

Nchini Kenya Kiswahili kilipata msukumo mkubwa baada ya Rais wa Kenya Mzee Jomo Kenyetta kutoa kauli kuwa Kiswahili kinafaa kuwa lugha rasmi kwa nchi ya Kenya na kuwa hapo baadaye kingekuwa ni lugha ya mawasiliano katika Bunge. Mwaka 1975 Kiswahili kilianza kutumika katika Bunge la Kenya. Ili kufanikisha azma hii, Ofisi ya Bunge la Kenya ilimtuma mtaalamu wake kuja Tanzania kuonana na viongozi wa Bakita ili kushauriana kuhusu istilahi zilizosanifiwa na kukubaliwa kuwa ni istilahi rasmi za Bakita na kulinganisha orodha hiyo na ya Kenya.

Inafahamika kuwa vyuo vikuu vyote vya serikali nchini Kenya vilivyoanzishwa miaka ya 1980 vinafundisha somo la Kiswahili kwa kutumia Kiswahili. Mifano hai ni Chuo Kikuu cha Nairobi, baadaye Chuo Kikuu cha Kenyatta na cha Moi. Kwa utaratibu huu idadi ya wahitimu wa Kiswahili wa kiwango cha digrii ya kwanza nchini Kenya ni kubwa ikilinganishwa na idadi ya wahitimu wa Kiswahili kutoka Tanzania.

Kiko chama nchini Kenya kinachojulikana kama Kenya Kiswahili Association (KKA) ambacho wanachama wake ni walimu pamoja na wakuza mitalaa ya Kiswahili katika shule za sekondari. Pia wako wanafunzi wa Kiswahili walioungana na wenzao wa Tanzania na kuanzisha chama cha kukuza Kiswahili kinachojulikana kama CHAWAKAMA. (Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili vyuo vikuu Afrika Mashariki). Chama hiki kinawaunganisha wanafunzi wote wa Kiswahili wanaosoma katika vyuo vikuu vya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Huandaa semina na warsha za Kiswahili kila mwaka na hukutana kwa nchi wanachama kwa mzunguko ili kushughulikia masuala ya ukuaji na uendelezaji wa lugha ya Kiswahili.

Suala linalotokana na mfumo wa elimu ya Kenya wa 8-4-4 unawalazimisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuchukua somo la Kiswahili kama somo la lazima. Hatua hii itawafanya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini Kenya kuona umuhimu wa lugha ya Kiswahili.

Lugha ya Kiswahili ni lugha muhimu katika masuala ya siasa, elimu, uchumi, biashara na utamaduni. Kwa maana hiyo, Kiswahili kina nafasi kubwa kwa maendeleo ya Afrika Mashariki. Tumeona kuwa lugha ya Kiswahili inawaunganisha watu na kuwaletea umoja. Hakuna lugha nyingine ambayo imeenea sehemu kubwa ya Afrika Mashariki kama Kiswahili.

Kwa mfumo huu ndiyo lugha inayoweza kuleta maelewano katika masuala ya kisiasa kwa wananchi wote.

Katika masuala ya kiuchumi, Kiswahili kinatumika kama lugha ya mawasilano. Kwa upande wa biashara, Watu wote toka nchi za Afrika mashariki wanaweza kwenda sehemu yoyote ya vijijini katika nchi nyingiine na kufanya biashara bila shida. Sehemu nyingine wanazoweza kutumia Kiswahili katika biashara ni Mashariki mwa Kongo na kwa kiasi fulani Rwanda na Burundi.

CHANGAMOTO ZILIZOKUMBA UKUZAJI NA UENDELEZAJI WA KISWAHILI NCHINI UGANDA

Pamoja na mafanikio hayo, zimekuwapo changamoto kadhaa zinazoathiri maendeleo ya Kiswahili. Baadhi ya changamoto hizo ni:

Upotoshwaji wa lugha ya Kiswahili

Upotwashwaji wa Kiswahili hutokea kwa namna kadhaa kwamfano,) anatufahamisha kwamba lugha ya maandishi ya Kiswahili chini uganda ilianza kutumika katika Baraza la Kifalme la Buganda na Bunyoro, hata kabla ya ukoloni (1862). Nchini Uganda Kiswahili kilitumika katika shughuli za biashara, dini na mila.

Wakoloni walipofika walikuta lugha hii inatumika, ingawa sio kwa kiwango kikubwa. Wakoloni walikitumia katika maswala ya kiserikali na kidini. Lakini maendeleo ya Kiswahili nchini Uganda yalikuwa duni sana ukilinganisha na Tanganyika na Kenya.

Maganga, (1997) anaeleza kuwa Sababu zilizokifanya Kiswahili nchini Uganda kuwa duni sana ukilinganisha na Tanganyika na Kenya ni kama ifuatavyo:

(a) Waganda walikiona Kiswahili kwamba ni lugha ya ki-Islamu, na Waislamu ni maadui wa dini

ya Kikristo, na kwa hiyo, Waislamu ni maadui wa Wakristo. Hivi ndivyo ilivyoaminika wakati ule

huko Uganda.Kwa mantiki hiyo, kukipenda Kiswahili waliona ni kuwakaribisha Waislamu ambao nimaadui wakubwa wa Wakristo, kwani Kiswahili kilimaanisha Uislamu.

(b) Katika kufundishia elimu, mkazo zaidi ulikuwa katika matumizi ya Kiingereza na lugha yaBuganda. Kiswahili kilitumika katika sehemu chache tu kwa upande wa Elimu, kama vile Jimbo laMashariki (isipokuwa Busoga), sehemu za Kaskazini na Magharibi ya Nile.Kwa msingi huo,Bunyoro, Toro, Ankole na Buganda hazikufundishwa lugha ya Kiswahili.

  • Watawala na viongozi pia walipinga kuenezwa kwa Kiswahili nchini Uganda. Kabaka Daudi na Maaskofu wa Uganda walipinga kuenezwa kwa Kiswahili nchini Uganda; badala yakewalipendelea lugha ya Buganda iwe lugha rasmi ya Uganda.Kutokana na hatua hii, Kiswahili kilitengwa kuhusishwa katika shughuli au mipango ya maendeleo ya Uganda.
  • Kiswahili kilididimizwa zaidi na Tume ya Kifalme ya Afrika Mashariki ambayo ilizuia kutumika kwa Kiswahili na Vyombo vya Serikali, Kiingereza peke yake ndicho kilichopewa kipaumbele badala ya Kiswahili.
  • Nchini Uganda Kiswahili kilifikiriwa kwamba ni lugha ya watumwa. Na kwa kuwa Kiswahili kilitumiwa zaidi na Polisi na Wanajeshi ambao, kwa bahati mbaya mara nyingi walikosa nidhamu, wananchi wengi waliichukia lugha hii kwa kuinasibisha na utumwa.Kwa msingi huo, Waganda kwa ujumla wao hawakuwa tayari kukipokea Kiswahili.
  • (Mnamo, 1960) na (Maganga, 1997) Serikali ya Uganda iliporuhusu na kulazimisha Kiswahili kitumike nchini Uganda; Kiingereza na lugha za kikabila zilikuwa tayari zinatawala mawasiliano Uganda nzima.
  • Kwa ujumla wakati wa ukoloni, matumizi ya Kiswahili nchini Uganda yalibakia sehemu za Kaskazini tu, tena mapolisi, wanajeshi na madereva wa taksi tu, ndio waliotumia Kiswahili; na watumishi hotelini waliongea Kiswahili cha kibiashara.
  • Uchanganyaji wa Kiswahili na kingereza na pia kutumia Kiswahili kwa maneno yasio sanifu na pia utumizi wa Kiswahili ulioathiriwa na sarufi ya lugha za kikabila hususan kimatamshi na kimuundo.

Athari za lugha za kigeni

Tatizo la kutokithamini Kiswahili miongoni mwa wanajamii ni changamoto ya kuathiriwa na kasumba za ukoloni ambapo wanajamii huthamini Zaidi lugha za kigeni hususan kingereza.

Kutokuwepo uwiano wa kimatumizi

Hii ni changamoto nyengine ambapo Kiswahili hakina uwiano wa kimatumizi katika nchi nzima, tofauti hizi zipo kutokana na jamii moja na nyingine kuathiriwa na lugha mama.

Utofauti wa sera, malengo na mipango ya vyombo vya ukuzaji Kiswahili

Juhudi za ukuzaji Kiswahili zinaonekana hazina mashiko kutokana na kuwepo idadi kubwa ya vyombo vya ukuzaji Kiswahili ambayo havina mshikamano wa pamoja kwani kila chombo kina malengo, sera, na mipango ya yake ya uendeshaji wa Kiswahili.

Uhaba wa wataalamu

Uhaba wa wataalamu katika vyombo vya ukuzaji wa Kiswahili husababisha vyombo kutofanya na kutekeleza malengo kwa ufanisi.

Kutokwepo mipango ya kukitumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia

Ni tatizo jengine linalokwamisha maendeleo ya Kiswahili kwa kutotekelezwa kwa mpango wa kukitumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia katika ngazi zote za elimu nchini, na hivyo kutoa nafasi hasa kwa lugha za kigeni kama vile kingereza kustawi zaidi na hivyo kuathiri nafasi ya Kiswahili katika jamii.

Maandishi kuhusu dhima ya ukuzaji na uendelezaji wa Kiswahili

Mipango iliyokuza Kiswahili Nchini Uganda

(Mulokozi, 2000) anatambua kwamba lugha ni nyenzo kuu ya utambulisho. (Nsibambi, 2000). Hii na kwa maana kwamba, nchi nyingi za Afrika ambazo zinatumia lugha za kigeni hazijihisi vizuri katika kujitambua kiutamaduni na badaaye wako tayari kupokea lugha asili ambayo inaweza ikawatatua kutoka misha hayo.

Whiteley (1969) anaripoti kuwa Kiswahili kiliendelea kutumiwa na polisi, sehemu za Kaskazini kuwasiliana na watu ambao hawajui Kiingereza na Luganda. Vilevile Wanilotiki wa Uganda walitumia sana Kiswahili kuwasiliana na makabila mengine. Kiswahili kilitumika pia kwenye mipira, na sehemu nyingine ambazo Kiingereza na Luganda havikuhitajika au havikuwezekana kutumika.

Kingine, kuja kwa wote wasome ya shule za msingi (UPE), serikali inalaumiwa kwamba wote wanaoacha kusoma shuleni ni kwa ajili ya kutojua kingereza katika shule za misingi (1981, December 2oo4) .Hata hivyo, kwa urahisi wanaweza wakazungmza katika Kiswahili.

Kiswahili ni lugha inayotumiwa katika vyombo vya habari. Sasa hizi televiseni ambazo zinakuja zinaendelea kutumia Kiswahili kamaRadio FM OPG, Mbale FM,Uganda Radio zinachangia katika kukuza Kiswahili katika nchi nzima ya Uganda. Hata hivyo Uganda inakaribia kuanzisha magazeti yanayotumia Kiswahili. Hivi vyote vitasaidia katika kuelimisha watu na kuwaangazia kuhusu masuala yanayowakabili. Mfano thabiti ni kwamba wakati ugonjwa wa ebola ilipokuwa inasambaa katika Uganda ya kaskazini, wakati huo Kiswahili kilikuwa kinatumika kuelimisha watu kuhusu jinsi ya kujiokoa na kuelewa usafi wa watu binafsi.

Katika siasa, wanajeshi wanatumia Kiswahili kuendeleza umoja na kukomesha ukabila. Katika Uganda ya kaskazini, Kiswahili ndiyo lugha inayotumiwa kupigania uhalifu na ukosefu wa usalama inayoletwa na uasi. Kupitia njia hiyo, Kiswahili ni kifaa cha kuleta umoja wa makabila inayotamaniwa leo.

Sasa, wanasiasa wanaowakilisha Uganda katika bunge la afrika masahriki wanatumia lugha ya Kiswahili. Hata nyumbani, wagombea viti vya ubunge kutoka kaskazini, mashariki, na magharibi wanatumia lugha ya Kiswahili katika kampeni zao. Juu ya yote, mbio uraisi haiwezi ikakamilika bila wagombezi kutumia Kiswahili. Hii ni maanakwamba hivi karibuni lugha ya Kiswahili itachukua jukumu la kuleta demokrasia kati ya wanaUganda na hatimaye itachukuliwa kiraia kutumika katika elimu kama ilivyo Kenya na Tanzania.

Katika biashara, jukumu la Kiswahili linaweza kukaguliwa. Inabidi kieleweke kwamba lugha hii iliingia Uganda hasa juu ya Biashara na imechangia sana kitaifa na kimataifa. Juu ya hayo yote, lugha hii ni lugha muhimu katika kuleta umoja. Inatumiwa katika thieta na barabarani na wakomedia kubrudisha watu.

5 thoughts on “KUKUA NA KUENEA KWA LUGHA YA KISWAHILI AFRIKA MASHARIKI

  1. Shukrani kwa kazi nzuri unayofanya juu ya uenezaji wa lugha ya kiswahili nchini UGANDA. Nchi ya uganda na Wizara la Elimu inahitaji kuleta lugha hata katika mashule ya msingi.

    Like

Leave a reply to Anyorekire Cancel reply