MCHANGO WA INNOCENT AGUME KATIKA TASNIA YA UANDISHI NCHINI UGANDA

Agume Innocent ni mzaliwa wa kijiji cha Nyamunuka Wilayani Ntungamo Magharibi mwa Uganda. Ni mwana wa pili kutoka mwisho katika familia ya watoto nane.

Kusoma kwake hakukuwa kunyoofu kwa sababu mbalimbali hasa uhaba wa karo pamoja na vifaa vingine vya matumizi shuleni. Kwake maisha yalikuwa kutazamia mbali mkate hata ingawa akiwa na nia ya kuupata. Hata, hivyo anamhimidi na kumshukuru Mungu kwa kwa maisha alimopitia na uhai wake wa hadi siku ya Leo.

Alisoma shule ya Msingi ya Kishariro. Alipomaliza masomo ya Msingi, alijiunga na shule ya upili ya Kagamba alikosoma sekondari ya daraja la chini na la juu na huko ndiko alikoanzia kusoma Kiswahili katika kidato Cha kwanza hadi Cha sita. Walikuwa wanafunzi wawili tu katika kidato Cha Tano na Cha sita waliosoma na kukalia mtihani wa Kiswahili.

Mnamo 2007, alijiunga na chuo cha taifa cha ualimu cha Kabale alikofuzu stashahada ya ualimu katika mafunzo ya Kiswahili na kisha akajiunga na chuo kikuu cha Kyambogo alikosomea na kufuzu shahada ya kwanza katika mafunzo ya Kiswahili mnamo 2015.

Katika mwaka 2019, alijiunga na chuo kikuu cha Moi nchini Kenya na Kusoma shahada ya uzamili katika mafunzo ya Kiswahili pia na akahitimu vizuri.

Amefundisha Kiswahili katika shule za Msingi (Greenhill Academy Primary) alikoanzisha Kiswahili katika darasa la kwanza hadi la sita. Amefunza pia shule za sekondari mbalimbali mkiwemo (Kampala Secondary pamoja na Greenhill Academy Secondary School), amefundisha katika vyuo vya walimu wa shule za Msingi mfano (Buloba PTC) kwa miaka minne, vyuo vya ufundi hasa (Spear Motors Vocational training center) huku pia akiwa mwanajopo katika ofisi za magalacha wa Kiswahili katika Kituo cha Taifa cha Ukuzaji Mitaala nchini Uganda.

Amejitolea katika Kufundisha Kiswahili Kwa watu wazima katika mashirika mbalimbali (mfano, wafanyakazi- NCDC staff – 2015 na Staff ya Wizara ya Utumishi wa umma – (ministry of public service- 2017.)

Kwa Sasa, ni mhadhiri kabambe wa lugha ya Kiswahili katika chuo kikuu Cha Kabale kusini magharibi mwa Uganda. (Kabaale University)

Jitihada zake za kuanza kuandika vitabu zilianza Mwaka wa 2012, aliposhiriki katika zabuni ya serikari ya uandishi na utoaji wa vitabu vya Kiswahili kwa shule za Msingi. Aliandika kitabu Cha mwanafunzi pamoja na mwongozo wa Mwalimu kwa darasa la tano, la sita, na la Saba, na vyote hivyo vitabu sita havikufaulu. Viliangushwa vyote! Kwa hivyo, aliambulia patupu katika mradi huo mzima.

Kwa kuwa kujikwaa siyo kuanguka, alishirikiana na wenzake watano mkiwemo Lubuuka Yunusu, (Mhadhiri wa Kiswahili Chuo Kikuu Cha Kyambogo) Arinaitwe Annensia (Mhadhiri wa Kiswahili Chuo Kikuu Cha Makerere pamoja na wengine, wakaandika kitabu Cha Kiswahili Cha darasa la nne Kwa shule za Msingi Cha Msingi Bora 4.

Tajriba ilipokolea, akaandika vitabu vya hadithi fupi za watoto ambavyo vilitumika sana hasa kwa watoto wa shule alizofundisha. Vitabu hivi ni kama; Fanya Adabu , Michezo shuleni na Rangi zetu . Hivi viliandikwa mwaka 2015.

Zabuni ya uandishi wa vitabu kwa vyuo vya walimu wa shule za Msingi ilijitokeza. Hapa alishirikiana na Dkt Yerindabo Innocent, wakaandika vitabu viwili vya Msingi Imara wa Kufundisha Kiswahili kitabu Cha kwanza na Cha pili vya Mwaka wa kwanza na wa pili mtawalia, hivyo vyote viwili vilipita ushindani na vikasambazwa katika Kila chuo Cha walimu na wizara ya elimu na Michezo.

Suala hili lilichangia motisha na tangu wakati huo, hajasitisha kuchangia katika tasnia ya uandishi. Ameshiriki pia na Dkt. Asiimwe Caroline pamoja na Dkt. Yerindabo Innocent wakaandika vitabu vya shule za upili Kwa kuegemea mtaala mpya vya Msingi wa Umilisi 1, 2, 3, na 4 huku wakiandaa pia miongozi ya walimu. Kwa Sasa anahesabu vitabu vya Kiswahili kumi na vitano na ushei.

Amejitoa pia Kwa ubia na TaRL Afrika, na kuandika hadithi fupi nyingi kwa ajili ya kuwashirikisha watoto katika Kambi za wakimbizi hasa Kambi ya wakimbizi ya Nakivaale.

Falsafa yake ya kimaisha ni kwamba, binadamu anafaa kutenda mema, na Mwenyezi Mungu ndiye atakayemtunuku. Ni ukweli wakati mwingine Mungu anaweza kuchelewa, lakini hawezi kukusahau. Mungu hasahau waja wake! Falsafa yake hii aliichora sana zaidi katika tamthilia yake ya hivi juzi ya Chema Chajiuza alimchora Mhusika mkuu Kwatampora (mtenda mema) analipwa na Mungu hata yasiyo matarajio yake. Anapendekeza kila mtu kuongozwa na kauli hii pamoja na mihimili yake hiyo;

Tenda linalostahili katika wakati stahilivu na usubiri neema na Baraka za bwana. Mungu atakubariki na utashangaa katika maisha yako yote.

Mchango wake unatambulika sana katika harakati za kukuza lugha ya Kiswahili Nchini Uganda hasa kupitia tasnia ya uandishi.

20 thoughts on “MCHANGO WA INNOCENT AGUME KATIKA TASNIA YA UANDISHI NCHINI UGANDA

  1. Nimependa sana juhudi Zake. Hongera sana Mwalimu Innocent.
    Mimi Mwalimu Bassu kutoka Tanzania nakupongeza.
    Mwenyezi Mungu akulinde uendelee kuifanya kazi yake kwa juhudi daima.

    Like

  2. Vilevile nilifanya utafiti kumhusu jinsi alivyosoma ndilo ambalo likanihimiza kuwa taabu si mauti, nina dada yangu aliyesoma naye kaniambia kuhusu maisha yake nikaona kuwa mtu hafai kukata tamaa ukiwa unaishi

    Liked by 1 person

  3. Mradi huu ni mema sana endelea kufanya kazi vizuri kama kawaida, mimi natokea kazkazini mwa Uganda wilaya ya Gulu ila mimi najua kuongea lugha hii adhimu tayari, asante sana.

    Like

  4. Ni mpenda lugha na pia mcha Mungu!
    Ndiyo Bwana Agume Innocent alisadiwa na jitihada zake za mchwa kuanzia chini mpaka juu. Namwita mwanangu Mimi!
    Asante Sana !

    Like

Leave a reply to ninsiimaalfred Cancel reply