UNAAMINI KATIKA MIZIMU?

Kisha ilikuwa chaguo rahisi kwa wachache yaani kama elfu nyakati hizo. “Hili lilikuwa limefungwa kwa miaka mingapi kweli?” Rafiki yangu Kawaida aliuliza. “Inakaribia mia au labda mia moja na mitano”. Nilimjibu. Kutegemea vile jumba lilikuwa linaonekana, tulikuta tetesi kwamba lilikuwa la wakubwa majenerali katika serikali kutoka sehemu fulani waliopigana vita vya ukombozi msituni. Palikuwepo Watoto wachanga hivi wa miaka kama minne mitano. Tulichukua jukumu la kuwauliza mmiliki wa jengo. Watoto hawakusita wote kwa Pamoja “ni Musaba”. Sisi kama watu wazima hatukuwa na uhakika wala tulijaribu kuchunguza kauli ya Watoto wachanga hawa, tulikubaliana kwamba huenda wenye nyadhifa na mamlaka ndio wanamiliki kila chenye mali humu nchini. Sisi wataalamu chipukizi na waliotamani sana kuandika na kuchunguza kuhusu mafanikio ya serikali, tuligundua kwamba Subira huvuta kheri.

Bado katika jengo la ajabu hilo, kwa miaka mia moja na mitano, jengo lilipaswa kuvutwa na wengi lakini mtu fulani mwenye mamlaka aliliweka kwenye orodha ya urithi na hilo likalifikisha mwisho wake kwasababu hapakuwa na wa kulinunua lakini pia wangekuwa wa kwao wamiliki hela.

Kawaida alikuwa mhakiki na mpenda historia sana. Alitumia mwezi mmoja kuangalia ndani ya jengo hilo, akitafuta mipango ya ujenzi, mawasiliano ya awali na wakati wa ujenzi. Mbinu za ujenzi alisema, ambazo hazipo kwa sasa lakini zilikuwa nzuri sana za aina yake kwa kipindi hicho.

Ilikuwa ni sababu ya sisi kusimama katika mlango mkuu sasa. Tulijifanya wahandisi chipukizi wa ujenzi kwamba na chuo kikuu kiliweza kuandaa ziara kwa hatari yetu wenyewe. Ili tuweze kuwasawishi wanaoishi hapo kutukubali kuingia kumbe sisi ni walimu wa somo la kisanaa yaani Kiswahili. Angalau tungekuwa wa sayansi, tungekubaliwa papohapo kwasababu hata na kiongozi mkuu aliyekuwa anasukuma Gurudumu la nchi kwa takribani miongo minne alikuwa anashabiki wa sayansi. Halikutukatiza kuendelea na utafiti wetu huku tukijifanya wa sayansi. Ndugu yangu Kawaida mnena mengi alianza shughuli zake za kupokonya urembo na uzuri wa jengo hata kabla ya kukubaliwa rasmi kuingia. Nilisimama kando nikimuona akinung’unia huku akijisemesha mwenyewe, “ hawa waliweka mamilioni hapa, watu wanakufa njaa, hizi hela za kujenga jumba hili likabaki bila faida kwa nchi zingepewa watu wa Karamoja waweze kupata chakula” Kawaida alisema huku akitizama jengo sehemu zote kaskazi, mashariki, magharibi na kusini. Miwani yake alitoa ili achunguze kwa makini. Na wakati huo nilipomkaribia nikamwambia tuone njia ya kuingia katika jengo hili.

 Aliyejifanya mmiliki wa jengo alikuwa amehakikisha kuwa tumetia saini katika waraka wa afya na usalama kabla ya kutoa idhini. Saini hizi ziliwekwa ili tukifia ndani asilaumiwe na serikali kwa lile lililotokea.

Kwakuwa watu wote walikuwa na hofu kuingia jengo hilo, mlinzi alitupeleka tu hadi kwenye mlango wa mbele. Alitupa namba yake ya simu ili tumpigie tukimaliza. Tulipomuuliza kwa nini hataki kuingia nasi, hakusema lakini ilikuwa wazi kwangu alikuwa anaogopa kitu. Ndugu yetu Edson tuliyekuwa naye akauliza, “ je mbona giza totoro humu, tutawezaje jamani?” Nilimjibu kwa kumuuliza, je simu yako iko na betri inayotosha? Jibu lake lilikuwa inachukuwa masaa Matano. Basi bila wasiwasi nikamwambia hatutaweza kumaliza masaa hayo yote ndani humu. Kawaida alikuwa kando akijaribu kusafisha miwani yake ili aweze kuingia na kutazama vizuri huku moyo wake ukitiwa na hofu pia juu ya lililokuwa likidhaniwa kuwa ndani.

Lakini hakuna hata mmoja wetu aliyeamini katika mizimu. “Unaweza kuona mambo ya makanisa katika maeneo machafu na wachungaji waongo, Unaweza kugeuza nafasi hii kuwa kanisa kwa urahisi na sote tukawa mapasta tukaanza kuhubiri injiri.” Edson alisema. Simon papohapo alileta mzaha kuhusu mchungaji katika wilaya moja nchini aliyewapiga viboko watumishi wa kanisa na kuwatema mate vinywani mwao ili washike miujiza. Papo nikamkumbuka rais wa nchi Jirani aliyepitisha sheria kuwa kila pasta lazima awe na digrii ya theolojia ili apewe leseni ya kuhubiri injiri nchini humo. Tukatamani hii sheria ingetumika kwetu, basi maskini kondoo wangekuwa na akili timamu sio hadi kuamini mtu akuteme mate kinywani ili uweze kuona miujiza. 

 Nilikuwa nimeleta kipimajoto pamoja nami, na ndani tulipokuwa tumesimama palikuwa na halijoto bora ya kuhifadhi mvinyo. Nyuma ya vizimba vya kutolea fedha kulikuwa na milango minne mikubwa ya chuma kwenye vyumba hivyo. Zilikuwa kubwa na mara moja zilikuwa na kiasi kikubwa cha fedha, dhahabu, na chochote kingine kilichoonekana kuwa cha thamani. Zote zilikuwa tupu sasa, rafu na sakafu zilikuwa zimetawanyika vipande vya vifaa vya benki na kwenye kona, masanduku kadhaa ya kadibodi, yamefunikwa na vumbi zaidi. Nyuma ya kabati hizo kulikuwa na ofisi, zenye urefu wa nusu na vigawanya vioo, madawati na viti vikiwa bado vipo, na vingine vikiwa na droo za kabati za kuhifadhia karatasi za mbao zikiwa wazi nusu. Wengine walikuwa na benchi na moja iliyowekwa kwenye kona kubwa sana, na ilionekana kama ofisi ya meneja.

Tofauti na ofisi nyingine iliyokuwa na vigae vya plastiki, hii ilikuwa na kapeti. Pembeni kulikuwa na kabati kubwa la kioo lililokuwa limeegemezwa likiwa na chupa kadhaa zilizokuwa nusu tupu. “Inaongeza maana mpya kabisa kwa whisky iliyozeeka, usifikirie.” Edson aliitazama lakini hakuipokea. “Nashangaa kwa nini waliiacha,” nilinong’ona.

Mahali hapo palikuwa na hisia Pamoja na dalili za kuwa huenda paliachwa kwa haraka, bila kuchukua kila kitu pamoja nao. Nilitetemeka, lakini haikutokana na baridi……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..inaendelea….

4 thoughts on “UNAAMINI KATIKA MIZIMU?

Leave a reply to ATUHE BONEFENCE Cancel reply