NADHARIA NA MBINU ZA UJIFUNZAJI NA UAMILIAJI LUGHA YA PILI

Lugha ya pili ni lugha ambayo mtu anajifunza baada ya kujifunza lugha ya kwanza. Mbinu za ufundishaji au ujifunzaji wa lugha ya pili ni tofauti kabisa na za lugha ya kwanza.Tofauti ni kuwa ili kujifunza lugha ya pili, ni lazima ifanywe kuonekana kukaribiana na lugha ya kwanza kama iwezekanavyo.


Kwa mujibu wa Krashen (1987), kuna njia mbili za kuwa na umilisi lugha: yaani Kupata na Kujifunza lugha.

Kupata lugha ni kupata ufahamu wa lugha katika mazingira asilia bila kufunzwa, kufuata mpangilio maalum wala kupewa mazoezi. Kupata lugha hutokea kwa kuirithi kutoka kwa wazawa wa lugha hiyo. Zaidi ya hayo, kuipata lugha hutokea bila ya mtu kutarajia katika mazingira ya kawaida kama vile mtoto mdogo anapoipokea L2, mtu mzima anapoipokea L2 katika nchi nyingine anakohamia kwa sababu tofauti. Kwa kuingiliana au kutangamana na wenyeji kimazungumzo, mtu hupata umilisi lugha.

Kwa upande mwingine, kujifunza lugha ni kupata ufahamu wa lugha katika mazingira rasmi kwa kufuata utaratibu wa silabasi na kupewa mazoezi. Mazingira rasmi yanaweza kuwa darasa au maabara ambapo mwanafunzi hufunzwa na mwalimu akiongozwa na utaratibu wa silabasi na kumpa mwanafunzi mazoezi, mijarabu na mitihani ya kukadiria uelewa wa mafunzo kutegemea malengo ya silabasi.

Hivyo basi, mbinu za utafiti katika ujifunzaji lugha ya pili zinaweza kuwa za kitaamuli na kiwingiidadi.

Katika mbinu za Kitaamuli, Mtaalam Jeff sauro (2015) alipendekeza na kuunga mkono mbinu zifuatazo za utafiti;

Ethnografia; Utafiti wa kiethnografia labda ni aina ya kawaida na inayofaa ya njia ya ubora kwa wataalamu wengi.

Katika ethnografia, unajiingiza katika mazingira ya washiriki lengwa kuelewa malengo, tamaduni, changamoto, motisha, na mada zinazojitokeza.

Ethnografia ina mizizi yake katika anthropolojia ya kitamaduni ambapo watafiti huzama ndani ya utamaduni, mara nyingi kwa miaka! Badala ya kutegemea mahojiano au tafiti, unapata mazingira mwenyewe, na wakati mwingine kama “mwangalizi mshiriki.”

Utafiti Simulizi; Huduma za simulizi husonga mlolongo wa vitendo, kawaida kutoka kwa mtu mmoja au wawili kuunda hadithi inayoshikamana. Unafanya mahojiano ya kina, unasoma nyaraka, na unatafuta mada; kwa maneno mengine, hadithi ya mtu binafsi inaonyeshaje athari kubwa za maisha ambazo ziliiunda. Mara nyingi mahojiano hufanywa kwa wiki, miezi, au hata miaka.

Kwa mfano, njia moja ya kufunua mahitaji yasiyotimizwa ya wanaojifunza lugha ni “kuwafuata nyumbani” na kuyazingatia maisha na matumizi yao ya lugha ukiwa mshiriki. Baada ya kuangalia makosa, halafu jukumu la kurekebisha linakubakia kama mfunza lugha hiyo ama mtafiti.

Utafiti wa kiukweli. (phenomenological);Wakati unataka kuelezea hafla, shughuli, au ukweli, Uchunguzi wa Kiukweli uliopewa jina ni njia inayofaa ya ubora. Katika utafiti huu, unatumia njia kadhaa, kama vile kufanya mahojiano, kusoma nyaraka, kutazama video, au kutembelea maeneo na hafla, kuelewa maana washiriki wanaweka juu ya chochote kinachochunguzwa.

Unategemea mitazamo ya washiriki ili kutoa ufahamu juu ya motisha zao.

Kama njia zingine za kitaamuli, huanzi na nadharia tete iliyoundwa vizuri. Katika utafiti wa kiuhalisia, mara nyingi hufanya mahojiano mengi, kawaida kati ya 5 na 25 kwa mada za kawaida, kujenga daftari ya kutosha kutafuta mada zinazoibuka na kutumia washiriki wengine kudhibitisha matokeo yako.

Kwa mfano, wajifunzaji lugha watoe kauli na wazoee.

Utafiti wa Kiuhalisia utakusudia kuelewa vizuri uzoefu wa wanafunzi na jinsi hiyo inaweza kuathiri ufahamu wa lugha ya pili.

Nadharia ya kimsingi; Wakati utafiti wa kiukweli unaonekana kuelezea kiini cha shughuli au tukio, nadharia ya kimsingi inaonekana kutoa ufafanuzi au nadharia nyuma ya matukio. Unatumia mahojiano haswa na hati zilizopo kujenga nadharia kulingana na data.

Nadharia iliyo na msingi inaweza kusaidia kuarifu maamuzi ya muundo kwa kuelewa vizuri jinsi jamii ya watumiaji lugha ya pili sasa hutekeleza majukumu.

Kwa mfano, utafiti wa nadharia ya kimsingi unaweza kuhusisha kuelewa jinsi watoto au watu wazima wanavyojifunza lugha na kuwasiliana na wenzao.

Uchunguzi kifani; Imefanywa maarufu na Shule ya Biashara ya Harvard, hata watafiti wa kiwingiidadi wanaweza kuelezea thamani ya utafiti huo kuelezea shirika, taasisi, kampuni, au hafla. Uchunguzi kifani unahusisha uelewa wa kina kupitia aina anuwai za vyanzo vya data. Uchunguzi kifani unaweza kuwa wa kuelezea, uchunguzi, au kuelezea tukio.(tafsiri yangu)

Kuna mbinu nyingine ambazo zinajitokeza ndani ya pendekezo la Jeff anbazo ni;

Kuna mbinu ya Hojaji;

Kwa mujibu wa Kothari C.R, (2004), uk 100, anafasili neno hojaji kuwa ni maswali yanayoandikwa katika karatasi ili yaulizwe kwa mtafitiwa kwa lengo la kupata taarifa za tatizo la utafiti.

Nayo Kamusi ya Kiswahili sanifu (2004) TUKI uk 116, inasema kwamba hojaji ni karatasi yenye maswali ya uchunguzi.

Ni seti ya maswali mengi apewayo mtu/watu kwa lengo la kupata taarifa juu ya jambo fulani (Macmillan Dictionary) [1]

Kutokana na fasili hizo hapo juu tunaweza kusema kuwa, hojaji ni maswali yanayoandaliwa na mtafiti kwa lengo la kukusanya data kutoka kwa watafitiwa.

Hojaji hizo mtafiti anaweza kupeleka mwenyewe kwa mtafitiwa kwa njia ya mkono au kwa njia ya posta ikiwa na kimbatanisho cha kumwomba mtafitiwa asome na kuelewa maswali kisha ajibu maswali katika nafasi zilizoachwa wazi kwa matumizi tu ya hojaji kisha kuyarudisha kwa mtafiti.

Hojaji zinazopelekwa kwa njia ya mkono husambazwa kwa haraka zaidi, na huwafikia watu wengi hususani wale wanaomzunguka mtafiti.

Hojaji zimegawanyika katika makundi makubwa mawili; kwanza hojaji funge na hojaji za wazi (zisizo funge).

Hojaji funge maswali yake yako wazi na yanaeleweka kwa watafitiwa. Maswali yanayoulizwa yanakuwa sawa kwa watafitiwa wote, yanalenga kutoa jibu moja tu.

Mfano ndiyo au hapana, au ya kuchagua a,b,c,d…. hayaruhusu mtafitiwa kuweka hisia zake. Muundo wa maswali waweza kuwa funge. Kwa mfano; andika “n” kama jibu ni ndiyo na “h” kama jibu ni hapana. au chagua herufi ya jibu sahii tu.

Hojaji isiyo funge ni hojaji ambayo inamruhusu mtafitiwa kutoa maelezo/kujieleza/au kutoa maoni ya ziada (kutoa ufanuzi zaidi kadri ya uelewa wake kulingana na jinsi alivyoulizwa)

Zifuatazo ni faida za mbinu ya hojaji katika ujifunzaji lugha ya pili;

Ni rahisi kukusanya data na inampa mwanafunzi/mjifunzaji lugha fursa ya kusoma maswali na kuyaelewa vilivyo,

Zinachukua muda mfupi yaani sio kama mahojiano yanayohitaji muda wa kukaa na wahojiwa,

Vile vile gharama zake ni ndogo kwani ni kutuma tu maswali na kujazwa na wanaojifunza lugha ya pili,

Faida ya kutumia njia ya posta ni pamoja na kutumia gharama ndogo na husambazwa katika eneo kubwa kwa muda mfupi.

Mtafitiwa/mfunzwa ana muda wa kutosha wa kuweza kutoa majibu kadri maswali yalivyoulizwa.

Mtafitiwa/mfunzwa ambaye hawezi kuingiliwa kwa urahisi hii inaweza kuwa njia nzuri ya kutumia.

Licha ya njia hiyo kuwa na faida pia zina hasara kama zifuatazo;

Udhaifu hasa wa mbinu hii ni kwamba haitilii mkazo juu ya matamshi sahihi pamoja na stadi za kimawasiliano. Inasisitiza sana ujuzi wa sheria za kisarufi bila kupatia wanafunzi nafasi ya kutosha kujieleza kutokana na nafsi zao

Matokeo ya kujishughulisha sana na mbinu hii ni kwamba waalimu huishia kwa kufundisha wanafunzi lugha ya ulimwengu wa vitabu, lugha isiyokuwa na uhai, na ambayo mara nyingi haina manufaa katika ufanikishaji wa mawasiliano ya kawaida.  

Utumiaji wa mbinu hii unalifanya somo la ujifunzaji lugha kukosa ubunifu unaotakikana. Wanafunzi hawapati nafasi ya kutumia lugha kama chombo wanachoweza kukitegemea kutekeleza mahitaji yao ya kimawasiliano. Wanalolifanya ni kujaza tu makaratasi.

Kwanza mara nyingi hojaji zinazorudi zikiwa zimejazwa ni chache. Hii ni kutokana na mtafitiwa/mfunzwa kutokuona umuhimu wa hojaji au kusongwa na majukumu au maswali kutokueleweka hatimaye kutatiza mchakato wa kujifunza lugha ya pili.

Pili inabagua maana inahitaji watu wanaojua kusoma na kuandika yaani wasiojua kusoma na kuandika itawawia vigumu kujifunza lugha ya pili ikiwa ndio njia pekee inayotumiwa.

Hojaji zinaweza kupotea zinapokuwa zinatumwa au kurudishwa na hivyo kutatiza mchakato wa ujifunzaji kwani matokeo hayatajulikana wazi.

Ni vigumu kuelewa kama majibu yatolewayo ni ya kwa kweli au ya uongo.

Hata hivyo njia hii ni ya taratibu mno kuliko njia zingine katika ukusanyaji wa data.

Mbinu nyingiine ni Mahojiano; Mahojiano yanajulikana kama mazungumzo kati ya watu wawili au zaidi ambao wako katika jukumu la mhoji na aliyehojiwa, ili yule wa zamani apate habari juu ya jambo fulani kutoka kwa yule mwingine. 

Cohen na wenzake (2000), wanasema, mahojiano ni mbinu ya ukusanyaji data kwa njia ya mazungumzo ya ana kwa ana baina ya mtafiti na mtafitiwa.

Kothari (2004) anasema, mahojianoni njia ya ukusanyaji data ambayo inahusisha maswali na majibu yanayoendesha mazungumzo ya ana kwa ana au simu baina ya mtafiti na mtafitiwa.

Mazungumzo kati ya watu wawili kwa lengo la kukusanya habari muhimu kwa kusudi la utafiti.

Kuna aina tofauti za mahojiano;

Mahojiano ya Kibinafsi: (structured)

Ni majibizano ya ana kwa ana (au ya simu, kidijitali/barua pepe), kati ya watu wawili au zaidi kwa lengo la kukusanya taarifa au maoni kuhusu suala fulani la kiutafiti lililoainishwa.

Ni mawasiliano ya  Ana kwa ana kati ya mhoji(mfunza lugha) na mhojiwa (mjifunzaji lugha).

Ujumla wa aina hii ya mahojiano hufanywa kwa njia iliyopangwa na inajulikana kama ‘mahojiano yaliyopangwa’.

Hii inaweza kufanywa kwa aina nyingi k.v. mlango kwa mlango au kama mkutano uliopangwa rasmi wa watendaji.

Mahojiano funge (structured interviews) aina hii hujikita katika jedwali/ hojaji zilizotayarishwa kabla. Hufaa kama maswali mengi yasiyohitaji mjadala mkubwa yataulizwa.

Mahojiano nusu-funge (semi-structured) -jedwali hutumika, lakini huacha mwanya kwa maswali mengine.

Mahojiano huru (unstructured) Haya ni mahojiano ya kina zaidi, na huhitaji ujuzi na umakinifu katika kumwongoza mhojiwa kutoa taarifa zinazohitajika.

Mahojiano huweza kuwa sanifu au huru. Njia itakayoteuliwa kutumika itategemea lengo.

Zifuatazo ni faida za mbinu ya mahojiano katika ujifunzaji lugha ya pili;

Mahojiano Humruhusu mfunza lugha kuuliza maswali ya papo kwa papo na kufahamiana na mhojiwa/mfunzwa lugha na hili husaidia kutambua makosa ya kisarufi na kimatamshi hatimaye kufungua mwanya wa kuyarekebisha na kusanifisha mchakato wa ujifunzaji lugha ya pili.

Mahojiano pia Husaidia wanafunzi kutafakari na kugandisha (weka pamoja mawazo) huku wakitambua dhana muhimu. Hili hufanyika ana kwa ana na kuruhus kudurusu na kumakini luha vilivyo.

Isitoshe, mahojiano humruhusu mfunza lugha kuuliza mhojiwa maswali ya binafsi na ya ikirari (factual) – yeye ni nani? anafikiria nini?, ana maoni gani?, anahisi nini?, n.k. hili husaidia kutambua makosa ya kimatamshi na kisarufi halafu kufungua fursa ya kuyarekebisha.

Mahojiano pia hukusanya tabasuri na tafsili za wahusika kuhusu matukio ya ujifunzaji lugha.

Mahojiano huwaruhusu wahojiwa kuelezea misukumo na sababu za mienendo yao, hili humpa mfunzwa kuuliza maswali asiyoyaelewa na hatimaye kufanikisha mchakato wa ujifunzaji lugha.

Mahojiano hukubali fursa ya kuuliza maswali tokezi au ya nyongeza.

Hasara/mipaka ya mbinu ya mahojiano;

Udhaifu mkubwa ni kwamba mbinu hii huhitaji muda mrefu sana ambao ni nadra kupatikana katika harakati za ujifunzaji wa lugha ya pili.

Taarifa inayopatikana kwa kawaida huelemea upande mmoja.

Wahojiwa wengine hushindwa kujieleza kutokana na haya au sababu nyinginezo.

Wanafunzi wasioelewa lugha inayofunzwa vyema huchukizwa na maswali ya mahojiano kwasababu inawahitaji kutumia lugha yao hiyo mbovu huku wakichekwa na wenzao. Kwa hivyo wanafunzi wandani (introverts) na wasiofurahia lugha hiyo huenda wasishiriki vilivyo.

Njia hii hutegemea uhusiano unaojengeka kati ya mtafiti na mhojiwa; muulizaji mbaya huibua muulizwa mbaya.

Njia hii hutawaliwa na muktadha mahsusi amabo siyo rahisi kujengeka.

Mbinu nyingiiine ni Ushuhudiaji;

Kushuhudia ni mbinu ya kuangalia tukio linapotendeka na kukusanya taarifa zake. Katika ujifunzaji lugha ya pili, mtafiti/mfunza hushuhudia umilisi wa wanafuzi wake kwa kuangalia vipengele kama usemi, maandishi, kusoma uelewa wa wanafunzi wake.

Namna za ushuhudiaji ni kama;

Uchunguzi na upimaji (k.m. katika jiografia, muziki) Mtafiti/mfunza awe na vifaa vinavyohitajika kwa kazi hiyo tepu rekoda na vifaa vya kurikodi sauti na matendo ya wanafunzi katika ujifunzaji lugha.

Ushuhudiaji fungemno (highly structured observation) – kwa kutumia mandhari yaliyodhibitiwa – kwa kutumia majedwali yaliyosanifiwa. Hapa jedwali la sauti za lugha huweza kutumiwa na kuchorwa wakati mtafiti/mfunza akishuhudia na kurekodi umilisi wao katika lugha hiyo ya pili.

Ushuhudiaji funge (structured observation) – unatoa uhuru zaidi – huchanganya majedwali na mahojiano – mtafiti si mshiriki, lakini huangalia na kukusanya taarifa waziwazi – taarifa za ushuhudiaji husaidiana na taarifa za mahojiano na vidadisi. Hapa taarifa za ujifunzaji lugha ya pili hukusanywa kwa namna ya mahojiano wakati wajifunzaji lugha ya pili wakiulizwa maswali na kuyajibu wakayi mwalimu au mfunza akirekodi taarifa ana umilisi wao.

Ushuhudiaji lengani (focused observation) – mtafiti huangalia tukio/tendo katika mazingira yake asilia bila majedwali. Taarifa hupatikana kutokana na kuzoeana na kuwa na mawasiliano ya muda mrefu na watafitiwa.

Ushuhudiaji huru/ usiofunge (unstructured observation) – hufanywa kwa siri na mtafiti bila mtafitiwa kufahamu na bila mpangilio wa wazi.

Faida za mbinu ya ushuhudiaji katika ujifunzaji lugha ya pili na kama zifuatazo;

Ushuhudiaji humwezesha mtafiti kukusanya taarifa kwa mpangilio mzuri isio tatizwa na wasiwasi.

Mshuhudiaji hutaamali matendo na matukio ya kijamii moja kwa moja yanapotokea kwamfano mfunza huelewa kiwango cha uelewa wa wajifunzaji lugha barabara bila changamoto.

Mfunza lugha huchunguza duru za shughuli au tabia katika mazingira yake asilia ya kijamii kama vile makosa ya kimatamshi hutambulika wakati jamii Fulani inapoongea na tofauti na jamii nyingiine.

Ushuhudiaji huchunguza namna watu wanavyoishi na kufanya kazi bila kuingilia shughuli zao yaani hamu ya kujifunza lugha hutambulika wazi.

Ushuhudiaji hukusanya taarifa ambazo haziwezi kupatikana kwa njia ya mahojiano au mazungumzo – ni njia inyomwezesha mtafiti kupata taarifa nyingi kwa gharama ndogo.

 Mipaka/upungufu wa mbinu ya ushuhudiaji ni kama;

Baadhi ya shughuli au matukio yanayochunguzwa hayawezi kufikiwa au kuonekana na mtafiti kama vile changamoto za asili ya kifamilia katika ujifunzaji lugha ya pili ni suala ambalo haliwezi likashuhudiwa mara kwa mara.

Wakati mwingine, kuwepo kwa mshuhudiaji huweza kupotosha au kuathiri shughuli inayohusika yani kama ni uimbaji au mazungmzo kati ya wanafunzi ilikususdi kuelewa umilisi wao katika lugha, basi kuwepo kwa mshuhudiaji kutaleta hofu na changamoto katika mazungmzo ya wanafunzi/wajifunzaji lugha hao.

Njia hii hufaa zaidi kwa matukio ya wakati uliopo; haifai kutumika kuchunguza matukio yaliyopita/ya zamani halafu huchanganya katika kuchunguza asili ya uamiliaji lugha.

Mbinu hii haifai kwa kukusanya taarifa kuhusu mikabala, maoni, nia, maana, n.k.

Mbinu hii haifai kwa kuchunguza makundi makubwa ya watu – huweza kuchukua muda sana, na haifai kwa kuchunguza mwenendo au mchakato kwa muda mrefu sana.

Mbinu nyingiine ni Utafiti kwa kushiriki, Utafiti huu unahusu kwenda kuishi na kushiriki katika shughuli za wale unaowatafiti/ unazozitafiti.

Hapa mfunza lugha hujishughulisha katika mchakato wa ujifunzaji kama mshiriki yani ikiwa ni kuimba nyimbo, huenda atakuwa kiongozi wakati anatafiti kiwango cha uelewa na umilisi wao.

Manufaa ya njia hi ni kama;

Hukuwezesha kuwafahamu vizuri watu na shughuli unazotaka kuzitafiti, na pengine kukubaliwa na hao unaowatafiti/wajifunzaji lugha.

Kutokana na tajiriba unayoipata kwa kuangalia na kushiriki, unapata ufahamu wa undani wa yale unayoyatafiti.

Udhaifu wa mbinu ya ushiriki na kama;

Utafiti wa kushiriki huweza kuhitaji muda mrefu zaidi kuliko ule alio nao mtafiti na huenda linalokusudiwa halitatimiwa.

Si mara zote unaweza kushiriki katika shughuli unayoitafiti: Mifano – katika shughuli ya siri au mwiko, shughuli haramu/ya kuvunja sheria, shughuli isiyokubalika kijamii, shughuli ya hatari, shughuli inyodai sifa za kipekee kutoka kwa mtafiti (ambazo hana), mtafiti-mshiriki huweza kuona ugumu kukaa kando na kuichunguza shughuli inayohusika kwa uhuru bila kuelemea upande Fulani.

Mikakati ya mawasiliano katika ujifunzaji lugha ya pili;

Msingi  wa  mbinu  hii  ni  imani  kwamba  kazi  kuu  ya  lugha  ni  kufanikishamaingiliano pamoja   na   mawasiliano   katika   jamii.   Lugha ni chombo ambacho kinamwezesha binadamu kushirikiana na watu wengine na pia kutekeleza mahitaji ya maisha yake.

Kwa hivyo, kulingana na waasisi wa mbinu hii, lengo kuu la kufundisha lugha  ni  kuwezesha  mwanafunzi  kuwa  na  uwezo  wa  kuwasilian akitumia  lugha inayohusika.

Mbinu hii iliibuka katika miaka ya 1980 na iliendelea kukubalika katika nchi nyingi duniani kama njia bora ya kufundishia lugha ya pili.

Kuibuka kwake kulichochewa na hali ya kutegemeana miongoni mwa nchi za bara la ulaya hasa kiuchumi na soko la dunia kati ya nchi hizo, kama taaluma mbinu hii chimbuko lake lilitokea siku nyingi hata kabla ya 1980, wapo wanaisimu waamirifu kama vile Firth 1968, Halliday 1973 na mwanaisimu jamii Hyrmes 1972, walikuwa na mawazo kuwa lugha ni mawasiliano, wanasema “msingi wa mbinu hii ni mwanafunzi ndilo eneo la mafunzo na kwamba kujifunza lugha ni kujifunza kuwasiliana.

Hawa wanatofautiana na Noam chomsky kuwa anayedai kuwa kujua lugha ni kujua umilisi wa mfumo na kanuni na hivyo kuitumia sahihi.

Hivyo tangu siku ya kwanza jitihada za mawasiliano lazima zifanyike katika ujifunzaji na ufundishaji, madhumuni ya mbinu hii ni kukuza stadi zote za lugha ambazo hutumika katika mawasiliano.

Maana ya mbinu ya kimawasiliano:-

Ni mbinu iliyokitwa kwa mwanafunzi, hutoa mwanya kwa mwanafunzi si katika umilisi wa sarufi bali pia katika stadi za jamii yaani nini cha kusemanamna ya kusemalini aseme na wapi aseme ili kuridhika na kile anachohitaji kila siku.

Lengo kuu la mbinu hii ni kumfanya mwanafunzi apate umilisi wa mawasiliano na mwalimu kazi yake ni kumwezesha mwanafunzi kupata umilisi wa mawasiliano.

Njia moja ya kuhakikisha kuwa mwanafunzi anakuwa na uwezo wa kuwasiliana ni, kwanza, kumpa fursa ya kushiriki kama mhusika mpokezi.

Mwanafunzi anapata fursa ya kupanua upeo wake wa lugha kupitia kusikiliza na kusoma. Baada ya kushiriki katika matumizi ya lugha akiwa mhusika mpokezi mwanafunzi anashirikishwa kama mhusika mwanzilishi wa mawasiliano.

Kulingana na waasisi wa mbinu ya mawasiliano, lugha ambayo ni ya maana / manufaa kwa wanafunzi inatilia nguvu juhudi za kujifunza. Kwa hivyo ni muhimu kwa walimu kuhakikisha kwamba wanapochagua kazi ya wanafunzi wanatilia  maanani uwezo wa kazi hiyo wa kuwashirikisha katika  matumizi  ya  lugha yenye maana na uhalisi.

Je, jukumu hasa la mwalimu ni nini? Kwa  mujibu  wa  waasisi  wa  mbinu  hii, jukumu la mwalimu ni kuhamasisha wanafunzi na kutoa kwao nafasi ya kujieleza katika lugha inayohusika. Ana  wajibu  wa  kuhamasisha  wanafunzi  kutumia  lugha  kwa  njia mbalimbali. Anapaswa pia kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anapata fursa ya kujieleza.

Pamoja na hayo, mwalimu ana wajibu kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa vizuri kwa nini wanafundishwa kile wanachofundishwa. Hivi ndivyo watakavyoweza kushiriki kwa njia ya maana na  manufaa  kwao. 

Vilevile ni  lazima  mwalimu  ahakikishe  kuwa wanafunzi wake wanahusika zaidi kuliko vile anavyohusika mwenyewe.

Aidha, mwalimu  anashauriwa  kushirikisha  wanafunzi katika vitendo ambavyo vinaweza kuwalazimisha kuwasiliana kwa kutumia lugha inayofaa kulingana na mkutadha. Kwa maneno mengine, mwalimu anapaswa kubuni hali na mazingira ambamowanafunzi hawawezi kukidhi mahitaji na matarajio yao bila kuwasiliana

Misingi ya mbinu ya ufundishaji lugha kimawasiliano,

Asili ya mbinu ya kimawasiliano ni imani inayoshikilia kwamba:

Lugha ni mfumo wa kueleza maana.

Jukumu kuu la lugha ni kufanikisha maingiliano na mawasiliano baina ya watu.

Shughuli  ambazo  zinachangia  kufanikisha  ufahamu  wa  lugha  ni zile ambazo  zinatoa  kwa  wanafunzi  nafasi  ya  kushiriki  katika  mawasiliano halisi (real communication).

Vitendo  vinavyohusisha  matumizi  ya  lugha  ili  kutekeleza  shughuliza maana (meaningful tasks) husaidia kufanikisha ujuzi wa lugha.

Lugha yenye maana kwa wanafunzi inaimarisha hali ya kujifunza.

Mawasiliano hufanyika ikiwa wale wanaohusika wana hamu (motisha) ya kuwasiliana.

Uamiliaji asilia wa lugha kuwa mwanafunzi ajifunze lugha katika muktadha halisi na wenye uasilia.

Ufundishaji uhusishwe na hali halisi ya maisha, ili mwanafunzi aelewe uasilia wa maisha.

Lugha ifindishwe kama stadi, lugha isifundishwe kama somo, katika mbinu hii mwalimu awafanye wanafunzi wake wazungumze ili kujua hali halisi. Hivyoikubalike kuwa lugha ni stadi

Ukuzaji uwezo wa kuwasiliana, katika mawasiliano kuna stadi ndogo 4 ambazo zinapaswa kukuzwa kwa mwanafunzi ili aweze kuwasiliana ambazo ni; Kuzungumza, Kusikiliza, Kusoma, na Kuandika

Mikakati ya mawasiliano katika ujifunzaji lugha ya pili ni lazima yazingatie hatua zifuatazo;

Kwa ufupi, mwalimu anaweza kusaidia kuendeleza uwezo wa wanafunzi wa kuwasiliana wakitumia lugha kwa kuzingatia mfuatano wa hatua zifuatazo: Mapokezi ya lugha, Ufafanuzi / Maelezo, Majaribio ya matumizi ya lugha na Mawasiliano huru.

Hatua ya mapokezi; Katika hatua ya mapokezi wanafunzi wanashiriki kama wahusika wapokezi.

Kazi yao katika hatua hii ni kupokea ujumbe unaowasilishwa na watu wengine na kupata maana ya ujumbe unaowasilishwa. Wanaweza kutekeleza jambo  hili  kupitia  zoezi  la kusikiliza au kusoma.

Zoezi la kusikiliza husaidia wanafunzi kupata nafasi ya kupanua upeo wa lugha.

Kupitia zoezi hili wanaweza kujifunza msamiati mpya na miundo mbalimbali ya kisarufi. 

Vilevile wanafunzi wanaimarisha ujuzi wao wa yale ambayo wamejifunza tayari.

Hatua ya ufafanuzi; Kwa upande mwingine, katika hatua ya ufafanuzi (maelezo) mwalimu anaweza kudondoa madondoo fulani ya lugha ambayo wanafunzi wamewahi kukumbana nayo, katika zoezi la kusikia na kusoma.

Kisha anatoa maelezo kuhusu madondoo hayo ili wanafunzi wayatilie maanani Zaidi kuliko mengine kwa wakati huo.  

Baada   ya kuhakikisha kwamba wanafunzi wanafahamu kiini cha somo, mwalimu anawapa wanafunzi nafasi ya kujaribu kutumia madondoo hayo katika vielelezo vya sentensi wakizingatia maagizo yaliyotolewa.

Hatua ya mawasiliano huru; Katika hatua ya mawasiliano huru wanafunzi wanapata fursa zaidi ya kujieleza bila kufuata maagizo ya mwalimu. Wanaweza kujieleza kwa njia halisi kulingana na mahitaji ya mawasiliano katika mkutadha unaohusika. 

Wanafunzi watateua lugha kulingana na hali halisi inayowakabili wakati huo.

Mawasiliano huru huwapa wanafunzi fursa ya kutambua kuwa lugha siyo somo ambalo linajikita katika mipaka ya mazingira ya darasani tu, lakini pia ni chombo cha mawasiliano nje ya mipaka ya darasa.

Mawasiliano huru huwapa wanafunzi nafasi ya kutumia lugha kwa njia ya ubunifu katika miktadha tofauti tofauti ya kijamii. Wanatumia lugha bila usimamizi wa mwalimu, lakini kulingana na hali halisi katika mazingira ya mawasiliano. Huwa wajitegemea wao wenyewe.

Kadiri wanavyoshiriki katika mikutadha tofauti ya mawasiliano na kushuhudia jinsi lugha inavyotumiwa, ndivyo wanavyoendelea kukuza na kuimarisha uwezo wao wa kimawasiliano (communicative competence).

Uwezo huu ni muhimu kwa mwanafunzi kwa sababu akiwa nao anaweza kufasiri lugha kwa njia iliyo sahihi akizingatia mkutadha unaohusika.  Na akifanya hivyo anaweza kuitikia kama inavyotarajiwa.

Kwamfano mwalimu akiingia darasani ambamo mna joto jingi na agundue kuwa madirisha yamefungwa, anaweza akasema: “Mbona joto limezidi sana humu ndani”. Mwanafunzi mwenye uwezo wa kimawasiliano atatambua kuwa mwalimu angetaka madirisha yafunguliwe, na ataitikia kwa kuyafungua.

Yule asiyekuwa na uwezo huo atachukulia usemi wa mwalimu kama kauli ya kawaida tu.

Mahitimisho; Sifa kuu ya mbinu ya mawasiliano, inasisitiza mawasiliano lugha inatumika kwa mawasiliano, hivyo mbinu hii husisitiza mawasiliano katika kufundisha lugha. Husisitiza hali halisi ya maisha na mawasiliano katika muktadha hivyo ujumbe unaoelezwa katika mawasiliano huwa katika muundo wa kidhima.

Kwahivyo, kiukweli mukatadha wa mawasiliano ndiyo mbinu mwafaka katika ujifunzaji lugha ya pili kwasababu inatilia manani katika umilisi wa usemi na utendaji. Kila lugha huwa ni chombo cha mawasiliano, isipowekwa katika muktadha wa mawsiliano itabaki tu na unasibu bila rejeleo la uhalisia wa maisha, hivyo basi naunga mkono watalamu Firth 1968, Halliday 1973 na mwanaisimu jamii Hyrmes 1972, ambao walikuwa na mawazo kuwa lugha ni mawasiliano, wanasema “msingi wa lugha ni mawasiliano. Mwanafunzi ndilo eneo la mafunzo na kwamba kujifunza lugha ni kujifunza kuwasiliana. Kwahivyo, lugha ni chombo cha mawasiliano.

Sipingi wala kuyapa jicho chafu mawazo ya Noam Chomsky yanayoshikilia lugha na umilisi na kuwa kujua lugha ni kujua umilisi wa mfumo na kanuni na hivyo kuitumia sahihi. Basi kanuni zieleweke na zifafanuliwe katika muktadha wa mawasiliano.

NADHARIA ZA AWALI ZA UAMILIAJI/UJIFUNZAJI LUGHA YA PILI.

Utangulizi.

Sinclair(1995)anaeleza nadharia kama wazo au mfumo wa mawazo maalum unaolenga kufafanua suala fulani.

Isitoshe Pearshall na Trumble(1982) wanaelezanadharia kuwa ni mfumo wa mawazo wa kueleza jambo fulani; hasa ule ulio na misingi yake katika kanuni za kijumla zisizo na uhusiano wa jambo linalofafanuliwa. Hata hivyo, nadharia ni mawazo yanayoelezea kitu au jambofulani na kuchukuliwa kuwa sahihi.

TUKI (2004) inaeleza ufunzaji kama namna yakufundisha au kuelekeza mtu kufanya jambo ili alifahamu

Kazi hii ni muhtasari wa, Nadharia za Awali katika Uamiliaji wa Lugha ya Pili (UALU2 kuanzia sasa).

USULI WA NADHARIA ZA UJIFUNZAJI LUGHA YA PILI.

Kabla ya miaka ya 1990 ufafanuzi wa uamiliaji wa lugha ya pili

(UALU2) uliangukia katika vipindi viwili vya msingi kinadharia.

Kwanza, kipindi kilichotumia nadharia ya utabia iliyochukuliwa kutoka katika taaluma ya saikolojia katika kueleza masuala ya uamiliaji wa L1 na L2.

Pili, utumizi wa mikabala ya kimuundo katika taaluma ya lugha. Baada ya tafiti jaribizi kuhusu uamiliaji wa L1 na L2 kudhihirisha matatizo kadhaa katika mikabala hiyo ya wanautabia-muundo, nadharia nyingi ziliibuka kujaribu kueleza

UALU2. Wakati huo, kulitokea pia ushindani katika kushughulikia na kufafanua vipengele mbalimbali vya UALU2.

Baadhi ya nadharia ziliendelea kukua taratibu na kubaki maarufu na nyingine zilififia.

Nadharia iliyokuwa inatawala katika kipindi hiki na imebakia kuwa maarufu hadi leo hii ni nadharia Elekezi ya Stephen Krashen.

Hivyo basi, hapa tutachunguza mkabala wa Wanautabia-muundo na nadharia Elekezi zote kwa pamoja zimekuwa na athari ya kudumu katika UALU2 hususani ufundishaji darasani.

Nadharia ya Utabia na Isimu-Muundo.

Nadharia ya utabia kulingana na nakalala taifaleo.nation.co.ke/?p 27291 na Mary Wangari akishughulikia UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI anasema kwamba mwasisi wa nadharia hii ni B.Watson. Anaendelea kusema kuwa wataalamu wengineo wanaoafikiana na nadharia hii ni pamoja na Leornard Bloomfield, B.FSkinner na A.W Staats. Kwa mujibu wa wataalamu hawa wanaeleza kuwa mtu kujifunza lugha ni mwigo kwa maana ya kwamba anaiga kile kinachosemwa na watu wanaomzunguka.

Kulingana na Nyandiba C. (2012) katika modula ya mbinu za Ufundishaji wa kiswahili anasema kuwa, wafuasi wa nadharia hii walidhamiria kueleza namna tabia inavyojengwa.Waliamini kuwa tabia itadumu, itaigwa, itarudiwarudiwa na kutuzwa. Lakini tabia isiyorudiwa na isiyotuzwa hufifia. Kwa hivyo, walisisitiza ujifunzaji wa lugha ni sawa na ujifunzaji wa tabia yoyote ile ya binadamu kamavile kuendesha baiskeli, kuogelea nakadhalika

Nadharia hii ilitumika sana katika miaka ya hamsini (1950) hadi miaka ya sitini (1960) kule Marekani. Baadhi ya vipengele vya nadharia hii vingali vinatumika mpaka leo

Uwanja wa UALU2 tangu uanze ulikuwa ukichukua mawazo ya kinadharia kutoka katika nyanja nyingine za kitaaluma na kabla ya kuanzishwa kwa nadharia na utafiti kuhusu UALU2, suala la kwa vipi watu huamilia/hujifunza lugha ya pili lilifungamanishwa kwa ukaribu na masuala yanayohusu ufundishaji.

Kwa kiasi fulani uliegemea mbinu mbalimbali kutoka katika saikolojia-tabia na kwa kiasi kikubwa kutoka katika isimu muundo.

Ingawa nyanja hizi mbili ziliibuka kwa nyakati tofauti, zilikuja kuwa na uhusiano baadaye katika kipindi hiki.

 Nadharia ya utabia na mihimili yake.

Utabia ni nadharia inayohusu tabia za wanyama na binadamu.

Nadharia hii hueleza tabia bila kuhusisha matukio ya kiakili na michakato ya ndani kwenye ubongo bali huelezwa kwa kuhusishwa na sababu za nje za kimazingira (rejelea majaribio ya pavlov na mbwa wake na mengineyo katika VanPatten na Williams 2015:18).

Kwa mujibu wa nadharia hii, inaonyesha kuwa kurudiarudia ni muhimu katika kujifunza jambo. Aidha, wanautabia walidai kuwa katika kijifunza, mchakato wa kiakili hauhusishwi.

Hawa Wanaona kuwa kujifunza ni tokeo la uhusisho wa matukio, mwitiko wa kichocheo katika mazingira na uimarisho chanya au uimarisho hasi.

Uimarisho chanya huhamasisha mwendelezo wa mwitiko, wakati uimarisho hasi hufifisha au kuzuia mwitikio usiendelee.

Katika nadharia hii fikira, hisia na dhamira si lazima kuhusishwa katika tabia za binadamu kama ilivyo kwa tabia za wanyama, iliyoonekana kama seti ya mwitikio katika vichocheo vya nje.

Katika nadharia hii, ujifunzaji wowote ukiwemo ujifunzaji wa lugha ulionekana kama uamiliaji wa tabia mpya.

Nadharia hii inatambua nafasi ya mazingira katika uamiliaji na ujifunzaji wa lugha ya pili.

Hapa izingatiwe kuwa mazingira yanatumika kwa maana pana zaidi kwa kuhusisha maswala ya utamaduni wa jamii ambayo hutumia lugha hiyo.

Ujifunzaji wa lugha ni sawa na ujifunzaji mwingine wowote kutokana na kuiga modeli katika ingizo kufanya mazoezi ya hiyo tabia mpya na kutoa mrejesho sahihi. Kwa mfano, mjifunzaji kujifunza jinsi watu wengine wanavyotamka sauti au maneno fulani naye anaiga na kufanya mazoezi ya utamkaji kutoka kwa wasemaji wazawa na hatimaye anaweza kutamka kwa usahii.

Kulingana na nadharia hii, uimarisho chanya na ingizo sahihi na pakiwa na ukosoaji wa kile ambacho si sahihi huwezesha mchakato wa ujifunzaji kufanikiwa.

Vitu vya msingi kuzingatia katika mchakatowa ujifunzaji wa lugha ya pili ni pamoja na tabia lengwa, ushiriki wa mwanafunzi na tokeo. Hii ina maana kwamba lazima mwanafunzi afanye mazoezi ya kuzungumza bila kufanya hivyo tokeo la kuweza kuzungumza na kuwasiliana halitaonekana.

Kwa mujibu wa nadharia hii, mjifunzaji wa L2, tayari anakuwa na misingi ya lugha ya kwanza ambapo humsaidia kuhawilisha maarifa ya L1 kwenye L2. Kama kuna ufanano kati ya L1 na L2, uhawilishaji unaweza kumsaidia kujifunza lugha ya pili au kumpotosha kama lugha hizo hazifanani.

 Kwa ujumla nadharia hii ina mihimili mitatu ambayo ni uzoeshi, uimarisho chanya na uimarisho hasi.

Uthibitisho wa ushahidi wa nadharia ya utabia.

Ukichunguza kwa makini maelezo ya wanautabia utagundua kuwa hakuna ushahidi jaribizi wa kutosha kutoa maelezo katika nadharia ikiwa na maana kuwa hakuna ushahidi wa kisayansi wa kutosha kuthibitisha madai yao.

Tafiti zilizofanywa na wanautabia zililenga kufafanua kile kilichokuwa kinaonekana moja kwa moja na siyo kueleza michakato (ya ndani ya ubongo) iliyofungamana na matendo hayo.

Hata hivyo, ushahidi wa msingi uliotolewa na watafiti kuhusu lugha ya kwanza haukuwa wa moja kwa moja. Kwa mfano, umuhimu wa L1 kwa L2 ulionekana dhahiri kwa mtu yeyote kwamba makosa anayoyafanya mjifunzaji wa L2 yanaweza kufuatiliwa kutoka katika lugha ya kwanza. Kwa mfano, makosa ya kimuundo yanayofanyika mara kwa mara katika Kingereza yanaweza kuwa yanatokana na lugha ya kinyankore kama L1 kwa wanyankore wanaojifunza Kingereza kama lugha ya pili. Kinyankore kina muundo wa kivumishi kufuata nomino na Kingereza ni kinyume chake. Iwapo mjifunzaji wa Kingereza atafanya ujumuishi basi atakuwa anafanya makosa ya kimuundo kila mara kama vile badala ya kusema kusema “Good girl” atasema *”girl good”.

Kwa namna gani nadharia hueleza mambo yaliyojidhihirisha katika uchunguaji wakati wa UALU2.?

Mikabala ya wanautabia inaweza kutumika kueleza yafuatayo kutokana na uchunguaji:

  1. Ingizo la vipengele vya lugha kwa misingi ya kujua maana katika UALU2 ni muhimu.

Mazingira yanaoneshwa kuwa ni kipengele kinachotawala ujifunzaji wa aina yoyote ile. Pamoja na kwamba mchakato wa kujifunza unaonekana ni wa kuiga na kurudiarudia kile anachokisikia, mchakato huo hauwezi kuendelea bila ingizo lolote la lugha lengwa kama kichocheo cha kujifunza.

  • Vipengele vingine katika UALU2 mtu hujifunza bila kujua wakati wakati mchakato wa kujifunza unaendelea. Wanautabia hudai kuwa ujifunzaji unatokea nje ung‟amuzi tambuzi, hakuna michakato ya akili inayohusika bali vichocheo vya nje kutokana na mwingiliano na mazingira ya mjifunzaji.
  • Ujifunzaji wa lugha ya pili ni geugeu katika matokeo yake.

Muktadha wa ujifunzaji huathiri matokeo ya UALU2 kwa namna mbili:

Kwanza, wajifunzaji wenye L1 tofauti watakuwa na matokeo tofauti kwa sababu ya utofauti wa L1 na L2. Kwa mfano, tukilinganisha Muhindi na Mswahili katika kujifunza Kingereza, Muhindi atajua haraka kingereza kuliko Mswahili.

 Au kama Mmarekani na Mganda katika kujifunza Kiswahili ambayo ni lugha ya Kibantu, Mganda atajifunza haraka kuliko Mmarekani kwa kuwa L1 na L2 kwake ni tofauti sana.

Lakini izingatiwe kuwa, wakati mwingine ujifunzaji unategemea umri, malengo, mbinu, uwezo wa akili, motisha, mazingira n.k.

Pili, wajifunzaji wanaotofautiana vichocheo vya mazingira mwishoni watakuwa na viwango tofauti vya tokeo. Hoja hii ni sahihi. Vichocheo au motisha au malengo yanaweza kuwa na athari hasi au chanya katika kujifunza kutegemea mjifunzaji kama mfano uliotolewa hapo juu.

Tafiti kubwa jaribizi zilizofanyika juu ya uamilaji wa lugha ya pili katika miaka ya 1970, matokeo yake hayakukubaliana na mawazo ya wanautabia.

 Matokeo ya utafiti yalibainisha kuwa:

  • Ukosoaji katika ukoseaji haukuboresha matokeo katikaujifunzaji.
  • Si wakati wote ufundishaji unapelekea ujifunzaji wa lugha.
  • Makosa mengi yaliyotabiriwa na uchanganuzi linganishi hayakutokea.
  • Makosa mengi yaliyojitokeza hayawezi kuelezwa kwa uwepo wa athari ya L1.

Kwa kuhitimisha sehemu hii, tunaweza kusema kuwa, pamoja na udhaifu huo unaojitokeza katika nadharia hii ya wanautabia, haina maana kuwa tuachane kabisa na hiyo nadharia. Kuna vipengele vingine vya msingi ambavyo ni muhimu sana kama vile utoaji wa mazoezi, kufundisha kwa kuzingatia mazingira na wakati mwingine mazoezi ya kurudiarudia inapobidi.

Mjadala kuhusu UALU2 kwa kutambua au kutotambua.

Mjadala kuhusu UALU2 kwa kujitambua au kutojitambua haukuwepo katika nadharia ya wanautabia kwa kuwa kwao mchakato wa kujifunza unaathiriwa na vichocheo vya nje.

 Changamoto katika tafiti za UALU ya L1 na L2.

Katika miaka ya 1960 na 1970 nyanja kubwa kama vile saikolojia na isimu ziliacha kutumia mkabala wa utabia na muundo katika kujifunza na kusasanyua lugha.

Utafiti wa kwanza katika miaka ya 1960 ulibainisha kuwa watoto hawawezi kuchakata mfumo wa isimu kwa kuwa ni changamani.

Watafiti walianza kuhoji kuwa watoto wanaonyesha ushahidi wa kutumia miundo ambayo siyo ya kuiga, hivyo watoto wanatumia uwezo wa kihulka wa kujifunza lugha katika uamiliaji wa lugha ya pili.

Uwezo wa kihulka haikuathiriwa na uzoeshi wa namna yoyote ile kama iliyopendekezwa na wanautabia.

Kwa mfano, watoto wanaweza kutoa uneni ambao hawajawahi kusikia katika igizo. Aidha, watoto huweza kujifunza miundo changamani ambayo hawaigizi kama vile kutafsiri swali, kuuliza maswali ya kwa nini, nani, nini n.k.

Lakini jambo la kujiuliza ni je, tuna uhakika gani kuwa mtoto huyo au watoto hawajawahi kusikia miundo hiyo kutoka kwa wazazi, walezi au watu wengine. Je, mtoto akiwekwa katika mazingira ambayo hayana wazungumzaji anaweza kuzungumza?

Pia watoto walionekana kutumia sarufi changamani katika mtiririko unaofanana na ambao haubadiliki kutoka kwa mtoto mmoja kwenda kwa mwingine kulingana na mazingira, muktadha, mlezi au athari za kitu chochote cha nje kama madai ya wanautabia yalivyotabiri.

Mwisho, matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa si utabia wala

usasanyuzi linganishi unaweza kutabiri kwa asilimia zote au kueleza kasoro za ujifunzaji.

Pia walipendekeza kuwa wajifunzaji wa L2 hujifunza miundo mingi ya kisarufi kwa utaratibu maalumu na kuwa kasoro zinazojitokeza zilikuwa sawa na zile zinazojitokeza kwa watoto wanaojifunza lugha mama.

Walihitimisha kuwa, uamiliaji wa lugha zote ni mchakato wa ndani ya ubongo na UALU2 hauathiriwi na L1 kwa kiasi kikubwa.

Hivyo UALU2 unafanana na uamiliaji wa lugha ya kwanza. Mawazo haya yanarejelewa kama nadharia tete ya Uundaji bunifu (Dulax & Burt

1975) ambayo hudai kuwa ujifunzaji wa lugha ni mchakato wa ubunifu ambao mjifunzaji hufanya bila ung‟amuzi–tambuzi katika misingi ya ingizo, mchakato ambao huthibitiwa na nguvu ya uhulka kama ilivyo kwenye lugha ya kwanza. Wazo hili ndilo lililounda msingi wa nadharia Elekezi.

NADHARIA ELEKEZI.

Hii ni nadharia ambayo inafahamika zaidi katika UALU2 na kwa walimu. Nadharia hii iliyoanzishwa na Stephen Krashen miaka ya 1970 na mwanzoni mwa miaka ya 1980.

Ni nadharia ya kwanza kuanzishwa mahususi kwa ajili ya UALU2.

Nadharia Elekezi na mihimili yake

Nadharia Elekezi ni nadharia ambayo ilichukua mawanda mapana na kujaribu kuhusisha na kueleza mambo mbalimbali katika ujifunzaji lugha, kuanzia athari za umri katika uamiliji lugha ya pili mpaka kwenye athari zinazotokana na ufundishaji tofauti na utabia.

Nadharia hii ilipendekeza modeli mahsusi ya ujifunzaji lugha ingawa mchakato halisi utakaohusika katika ujifunzaji haukubainishwa katika maandishi ya Krashen.

Nadharia yake inaonekana kuhusiana na nadharia ya lugha ya Chomsky inayosema kuwa binadamu amejaliwa kipekee kuwa kifaa cha uamiliaji lugha (KIULU) katika ubongo.

Hivyo, mtoto anakuwa tayari na kiwango kikubwa cha vipengele vya lugha, kinachotakiwa ni kuchokonoa data ingizi za lugha katika kuamilia lugha ya pili.

Katika nadharia hii, mhimili katika uamiliaji wa aina yoyote ni maana ya ingizo na kuwasiliana yaani utumizi wa lugha.

Nadharia Elekezi inaweza kueleza kwa nini kinachofundishwa si mara zote mjifunzaji awe amejifunza; kwani mjifunzaji anachojifunza inawezekana sicho alichofundishwa na kwa nini tofauti katika wajifunzaji, muktadha na kujifunza huhusiana na tokeo geugeu la UALU2.

Nadhariatete za nadharia Elekezi.

(i) Nadhariatete ya uamiliaji na ujifunzaji wa lugha ya pili

Nadhariatete hii inadai kuwa kuna mifumo miwili tofauti katika utendaji lugha. Kwanza, kuna mfumo wa uamiliaji na pili kuna mfumo wa ujifunzaji.

Uamiliaji hufanyika kiasili bila kujua na hivyo UALU2 ni kama kujifunza lugha ya kwanza.

Ujifunzaji huusisha kupata maarifa ya lugha kama vile kanuni, ruwaza kwa kutambua au kwa kuelekezwa, hapa kuna ung‟amuzi tambuzi na jitihada za makusudi.

Kwa mtazamo wa Krashen, mfumo wa ujifunzaji lugha siyo muhimu sana kama ule wa uamiliaji.

(ii) Nadhariatete Elekezi

Nadhariatete hii inazungumzia uhusiano uliopo baina ya uamiliaji na ujifunzaji na kuonesha athari za mwanzo kuwa katika utumizi wa lugha kwa sasa.

Elekezi ni kazi ya utendaji wa sarufi iliyojifunza wakati fulani. Krashen anadai kuwa mfumo wa uamiliaji ni mwanzo wa uneni, wakati mfumo wa ujifunzaji hutekeleza maelekezo au uhariri.

Uelekezi hutendwa katika kupanga, kuhariri na kusahihisha.

Kwa kuzingatia hayo, mjifunzaji lazima awe na muda wa kujifunza kwa kujikita katika usahihi wa tungo na kujua kanuni za lugha husika.

(iii) Nadhariatete ya Mfuatano Asili

Nadhariatete hii inadai kuwa uamiliaji wa miundo mahsusi ya sarufi hufuata mipangilio asilia ambao hutabirika. Inaonekana kuwa wajifunzaji hupitia hatua zinazotabirika katika kuamili miundo ya kisarufi kama kuuliza maswali kwa mfano, (nini, kwa nini n.k), ukanushi (sikuji, siji) na baadae vishazi rejeshi.

Lakini izingatiwe kuwa mpangilio huweza kutegemea umri, usuli wa lugha ya kwanza na mazingira.

Pia lengo la kujifunza liwe ni kuamili na siyo kujifunza sarufi tu kwa sababu kuna utumizi mwingine wa lugha ambao hauzingatii sarufi bali muktadha au wakati mwingine tungo au misemo inayopinduliwa kwa mfano, Mganga haagizi mchicha/tembele (Kiendacho kwa mganga hakirudi), Tembea kobe wengi (Taratibu ndio mwendo) n.k.

(iv) Nadhariatete Ingizo.

Kwa mujibu wa nadhariatete hii, binadamu uamilia lugha ya pili anapopokea ingizo la lugha ya pili ambalo liko juu ya maarifa ya awali (anaingiza kitu kidogo cha ziada).

Kwa mfano, mjifunzaji yupo katika hatua ‘i’ uamiliaji utakamilika pale atakapata ingizo kamili na kumpeleka katika hatua ‘i’+’1’. Ingawa Krashen anaitambua i+1 kuwa ni data muhimu, nadharia Elekezi haijaeleza ni kitu gani hicho na kwa vipi i itabainishwa.

Jambo linalosisitizwa ni kuwa mawasiliano kutokana na ingizo asilia yanayozingatia maana ndiyo yawe msingi wa uamiliaji kuliko muundo.

Kwa mfano, kama mjifunzaji ana maarifa ya awali ya kuunda sentensi, “Mama anampiga mototo”. Akiweza kusema, “Mtoto anapigwa na mama” basi kuunda tungo ya utendwa ni ingizo nyongeza.

Tatizo linabaki katika kujua ni kiasi gani cha maarifa ya awali alichonacho mwanafunzi.

v. Nadhariatete Mchujo Athari.

Krashen anadai kuwa kuna mambo mengi yanayochangia katika mchakato wa uamiliaji lugha ya pili. Mambo hayo ni kama vile kwamfano, utulivu, mtazamo chanya kuhusu kujifunza lugha n.k.

Mchujo wa chini, hauruhusu vipingamizi katika ingizo la maana. Kinyume na hayo, mazingira ya mfadhaiko au msongo utokanao na mjifunzaji labda kwa mfano, kulazimishwa kuongea kabla hajajisikia kuwa tayari kuongea huweka vizuizi katika kuchakata ingizo.

Nadharia hii husaidia kueleza tokeo geugeu la UALU2 kwa wanaojifunza L2 ambayo ni pamoja na tofauti za umri wa wanaojifunza na hali ya darasani.

Athari chanya zina nafasi kubwa ya kumwezesha mjifunzaji kuamili lugha ya pili kuliko mwanafunzi mwenye athari hasi.

Kwa namna gani nadharia hueleza mambo yaliyojidhihirisha katika uchunguaji wakati wa UALU2

  1. Ingizo la vipengele vya lugha kwa misingi ya kujua maana katika UALU2 ni muhimu. Jukumu la ingizo hasa ingizo la maana katika nadharia hii ni wazi na linaeleweka. Ingizo ndiyo nguvu ya msukumo katika UALU2.

Nadharia inadai kuwa mjifunzaji wa lugha ya L2 hutumia kifaa cha uamiliaji lugha (KIULU) katika ubongo sawa na mjifunzaji wa L1.

  • Vipengele vingine katika UALU2 mtu hujifunza bila kujua wakati mjifunzaji akilenga kwenye maana.

Siyo lazima kwa mjifunzaji kudhamiria kujifunza ndo uamiliaji ufanyike.

  • Tokeo kwa mjifunzaji mara nyingi hufuata njia tabirifu pamoja na hatua tabirifu katika UALU2 katika miundo husika.

 Huu ni msingi mkuu wa nadharia Elekezi kwa sababu ujifunzaji wa lugha zote huongozwa na michakato majumui ya ndani. Hivyo nadharia haiwezi kueleza mpangilio halisi.

  • Ujifunzaji wa lugha ya pili ni geugeu katika tokeo. Nadharia hii inaweza kueleza utofauti wa matokeo baina ya wajifunzaji wa lugha kulingana na maana ya ingizo.  Wakati mwingine inawezekana ni matokeo ya mazingira tofauti ya athari mchujo ambazo zinaweza kumwekea mjifunzaji vizuizi katika maana ya ingizo.
  •  Athari za lugha ya kwanza katika UALU2. Kwa kuwa uamiliaji wote uongozwa na michakato majumui ya ndani, kwa mujibu wa nadharia hii Elekezi, athari za L1 ni ndogo sana.

Wajifunzaji wote hutumia mbinu sawa katika kujifunza L2 kama inavyoonyeshwa na kasoro zinazofanana za wanafunzi wenye usuli wa aina tofautitofauti wa lugha.

  •  Athari za ufundishaji katika UALU2.

Kwa mujibu wa nadharia hii, uamiliaji hutokea kiasili katika uwepo wa maana ya ingizo ambalo ni aina pekee ya data muhimu kwa ajili ya vichakata vya ndani vinavyohusika na uamiliaji wa lugha. Ufundishaji kwa mujibu wa nadharia hii huchangia kidogo katika maana ya ingizo.

  • Athari za tokeo katika UALU2.

Kwa mujibu wa nadharia Elekezi, utendaji lugha ni tokeo la uamiliaji.

Vichakata vya ndani vinavyosukuma uamiliaji, huweza kutumia muundo mmoja tu wa data ya isimu ambayo ni maana ya ingizo.

Kwa mfano, wajifunzaji wanapoongea au kuandika, kwa ujumla huwa wanatumia lugha ambayo wamekwisha amilia.

Mjadala wa ama kujifunza kwa kujua au kutokujua

Nadharia Elekezi inafafanua wazi tofauti za kujifunza kwa kujua na kujifunza bila kujua kama unajifunza na maarifa yanayoambatana na ujifunzaji huo.

Uamiliaji unapofanyika kwa ingizo sahihi katika mazingira rafiki, matokeo ya uamiliaji ni maarifa ndani (maarifa yanayopatikana bila kujua) ambapo maarifa nje matumizi yake ni kidogo tofauti na maarifa ndani ambayo ni chanzo cha utumizi wa lugha kimawasiliano.

Uhakiki wa nadharia Elekezi

Nadharia hii Elekezi imekuwa ikipingwa kwa miaka mingi. Kila nadhariatete yake inaonekana kuwa na tatizo kwa namna fulani.

Pamekuwepo na tafiti jaribizi mbalimbali kujaribu kila kipengele cha nadharia hii. Sababu mojawapo ni kuwa kulikuwa na tatizo ambalo watafti waliliita „utendeshaji wa mihimili‟. (operationalization of the constructs) ambapo fasili zake zina uvulivuli na kufanya ujaribizikuwa mgumu.

Kwa mfano, hapakuwepo na njia inayojitegemea yakuthibitisha ni chanzo kipi cha maarifa kinaamiliwa au kujifunzamjifunzaji hutumia kama msingi au maarifa ya awali katika matumizi.

Aidha, mipangilio tabirifu ya uamiliaji kwa pamoja huelezwa kwa ushahidi wa kiuamiliaji lugha.

Nadharia haikutoa ufafanuzi kuhusu dai la mipangilio ya uamiliaji, tokeo la mwingiliano wa ingizo pamoja na mbinu za ndani za uamiliaj.

Mambo mengine ambayo hayakuungwa mkono ni pamoja na: Athari mchujo na mchango wa viingizo kama vile kutoka kiwango cha awali i kwenda katika kiwango cha juu yaani i+1, kwa kuwa haiwezi kuwekwa kwenye uhalisi wa matumizi.

Kwa kiasi kikubwa inaonyesha kuwa ushahidi wenye nguvu katika nadharia hii Elekezi ni uzoefu wao binafsi.

Kwa mfano, Kitu kinachofundishwa mwanafunzi si mara zote ajifunze, na kile ambacho amekimudu kwa kujifunza kwa kurudiarudia na mazoezi mengine yanayoratibiwa huonekana kupotea katika shughuli zinazohusisha matumizi ya lugha kwa hiari.

Tathmini na hitimisho.

Kwa ujumla mwandishi amejitahidi kueleza kwa kina nadharia zilizotumika mwanzoni katika UALU2 kabla ya nadharia za sasa.

Ameonyesha hatua kwa hatua asili ya nadharia, mafanikio na mapungufu yake na hoja zilizojitokeza kuipinga kutokana na tafiti jaribizi za kisayansi. Kwa kila nadharia ameonyesha mihimili yake na mambo yanayoelezwa kutokana na uchunguaji katika matumizi ya nadharia.

Tunaweza kusema kuwa, nadharia hizi za Utabia na Elekezi pamoja na udhaifu uliobainishwa ndizo zilizoweka misingi ya nadharia za sasa na tafiti mbalimbali kuhusu UALU2. Nadharia za sasa kwa kiasi kikubwa zinaboresha au kuongeza vipengele katika nadharia za awali. Izingatiwe kuwa hakuna nadharia inayotoka katika ombwe.

Nadharia zote katika taaluma zinajenga misingi kutokana na uwepo wa jambo fulani lililokuwepo hapo awali. Jambo lingine katika kazi hii ni kwamba mwandishi amebainisha mkabala wa isimu- muundo mwanzoni lakini maelezo yake hayakuendelezwa.

Hii inatokana na ukweli kuwa mkabala huu ulifungamanishwa na nadharia ya utabia na utabia ulichomoza zaidi katika UALU2.

Mkabala wa Isimu muundo unafungamanishwa moja kwa moja na ufundishaji wa lugha na mbinu zake.

Pamoja na hayo, kazi hii imetupa mwanga wa uelewa kwa kiasi kikubwa kuhusu masuala UALU2.

Imeibua hoja nzito ambazo zinashughulikiwa katika nadharia nyingine.

Kazi hizi zinahitaji uelewa wa hali ya juu kwa sababu katika kuonyesha udhaifu wa nadharia kama vile utabia au elekezi unauonyesha kwa misingi ya nadharia na tafiti ambazo tayari zimeishafanyika.

Hivyo kama mtu hana uelewa wa nadharia nyingine au tafiti zinasemaje ni vigumu kuunganisha mawazo. Mawazo ya wanautabia na Uelekezi bado yana nafasi kubwa katika mchakato wa uamiliaji na ujifunzaji lugha ya pili

kwani kuna vipengele vya kiutamaduni ambayo ni sehemu muhimu ya lugha yoyote ile.

NADHARIA YA UHALISIA

Nadharia hii katika upana wake, humaanisha uwakilishi wa uhalisi wa mambo katika maisha ya binadamu.

Nadharia hii ilizuka katika karne ya kumi na tisa hususa kwa sababu za kupinga mkondo wa ulimbwende.

Mhalisia huamini katika matokeo ya mambo na ukweli anaouzingatia ni ule unaoweza kuonekana na kuthibitishwa kwa tajiriba.

Vilevile, wahalisia huiamini demokrasia kama hali ya maisha, na malighafi anayochagua kueleza maisha ni yale ya kawaida, ya kadiri na ya kila siku.

Hivyo basi uhalisia hujikita katika mambo yaliyopo, tukio mahsusi na matokeo yanayoweza kuthibitika.

Imani ya mhalisia ni kwamba kazi yeyote yapaswa kuwaweka wanajamii husika katika ulimwengu wao wa kawaida, wa kweli, na halisi.

Hivyo basi hata picha za ulimwengu atakazoumba msanii, zapaswa kudhihirisa hali hiyo. Kama tulivyotaja hapo juu, uhalisia ulizuka ili kupinga ulimbwende ambao ulizingatia mambo ya kihisia na yasiyo halisi maishani.

Wahalisia wanaona kwamba kazi ya fasihi yapaswa kuwa sahihi, iliyo wazi na inayozingatia maswala halisi moja kwa moja bila kupiga chuku.

Maswala ya kati maishani huhusu maadili na hivyo basi msanii hana budi kuyazingatia kwa kiwango fulani cha uteuzi.

Wahalisia wanashikilia kwamba msanii anapaswa kuteua

lakini akiwa na nia ya kuendeleza maswala yake kama yanavyowahusu watu katika hali halisi za maisha.

Mwelekeo huu wa uhalisi katika ujifunzaji lugha unamfanya mhalisia kumwona mjifunzaji kama kiungo muhimu sana katika Maisha.

Hivyo basi anazingatia saikolojia ya wajifunzaji lugha katika kufunza.

Nadharia pia hupembua namna mfunzaji anavyodhihirisha uhalisi wa mambo kupitia maudhui aliyoyazingatia na wahusika

aliowasawiri.

Kwa muhtasari basi msanii anatarajiwa kusawiri wahusika, matukio na mandhari yanayokubalika na kuaminika katika jamii ya wakati wake.

Ufahamu wa mazingira na maisha anayoyalenga mtunzi ni nguzo muhimu kwa mhakiki wa kihalisia. Shida inayoletwa na nadharia hii ni kuchukulia kwamba uhalisi na maana yake hauna utata wowote katika jamii yoyote, ni kwamba unachukulia kuwa watu wote katika jamii hiyo waona uhalisi mmoja na kuwa na

fasili sawa kuhusu maisha yao.

NADHARIA YA UCHANGANUZI MAKOSA.

Wanafunzi wanaojifunza lugha ya pili hufanya makosa mengi yakiwemo matamshi mabaya ya maneno.

Kutokana na hali hiyo, wanaisimu wamekuwa katika mstari wa mbele kubaini chanzo cha makosa na vilevile kubuni mbinu faafu zinazochangia katika kutatua matatizo hayo.

Uchanganuzi Makosa Mtazamo wa Uchanganuzi Makosa uliasisiwa na Corder na wenzake miaka ya 1960.

Mtazamo huu uliibuka kukidhi upungufu wa uchanganuzi linganuzi uliotumiwa na wanaisimu kutofautisha lugha ya kwanza na ya pili ya mwanafunzi ili kukisia makosa.

 Uchanganuzi makosa ni mbinu itumiwayo kuthibitisha makosa yanayopatikana katika lugha ya mwanafunzi.

Walimu wa lugha wanaowasikiliza wanafunzi wao wakizungumza hutambua makosa. Ukweli ni kuwa kila mtu hufanya makosa anapoongea hata walimu na wazawa wa lugha hufanya makosa.

Wazawa wa lugha hawafuati kanuni za sarufi zilizoandikwa vitabuni.

Uchanganuzi makosa, huchunguza aina ya makosa na visababishi vya makosa hayo. Kulingana na mwanaisimu Corder, mtafiti hufuata hatua zifuatazo katika uchanganuzi makosa:

1. Kukusanya sampuli ya kazi ya wanaojifunza lugha 11

2. Kutambua makosa

3. Kueleza makosa.

Makosa yanawekwa katika makundi na kuelezwa kisarufi.

Hivyo makosa yenyewe ndiyo hutumiwa katika kuainisha kategoria za kisarufi.

 4. Kufafanua chanzo cha makosa haya.

5. Kutathmini / kuyasahihisha makosa haya ili kujua jinsi ya kukabiliana nayo.

Tunapowasikiza wanafunzi wakizungumza tunafahamu makosa wayafanyayo. Kwa sababu hii ni vyema kujiuliza kile mzungumzaji alikusudia kukisema na angekisema vipi. Kusahihisha makosa haya sio jambo rahisi kwa sababu kuna zaidi ya njia moja ya kufanya hivyo.

Kusahihisha makosa kunategemea kile msikilizaji anafikiri mzungumzaji alikusudia kukisema na kosa lenyewe.

Ni vyema kufikiri namna nyingi tofauti za kusahihisha makosa. Kwa sababu huna uhakika wa kilichokusudiwa, mwache mwanafunzi akusaidie kuamua sahihisho sahihi.

Kufafanua makosa haya, kwataka kujua kisababishi. Makosa yanaweza kutokana na kuhamisha kanuni au ruwaza za lugha ya kwanza.

Makosa mengine yanaweza kusababishwa na jinsi mwalimu au vitabu vya kaida vinavyoeleza kanuni fulani.

Au inaweza kuwa mikakati ya mawasiliano anayotumia mwanafunzi hata kama anajua kanuni anazotumia sio sahihi. Utafiti huu si linganishi kwa sababu hatujalinganisha lugha mbili ili kutambua makosa.

NADHARIA YA UAKILI (Ubunifu wa Lugha)

Hii nadharia inadai kwamba kila mtumiaji wa lugha ana uwezo wa kuzalisha sentensi nyingi na mpya kabisa zilizo sahihi kisarufi na ambazo hajawahi kuunda hapoawali.

Vilevile, anaweza kuelewa ujumbe uliomo katika sentensi nyingi tena mpya kabisa ambazo hajawahi kusikia hapo awali.

Hii inamaanisha kwamba, sio jambo la kawaida watu kuiga semi ambazo wamewahi kuzisikia zikisemwa bali wao hubuni semi zao mpya huku wakiongozwa na kanuni za Kifunza-Lugha.

Ukweli huu umewapelekea baadhi ya watafiti kudai kwamba ni kiasi kidogo sana cha sintaksia ya lugha ambacho mtu anaweza kufunzwa, kwani ni mambo mengi sana ambayo yeye mwenyewe hujigundulia.

UHAKIKI WA NADHARIA YA UAKILI.

Nadharia ya Uakili inatupa mwangaza zaidi kuhusu nafasi ya akili katika kumwezesha mtu kujifunza lugha.

Hata hivyo, bado haijulikani kikamilifu jinsi Kifunza-Lugha hufanya kazi. Pia sifa nyingi za sarufi bia bado hazijagunduliwa.

Isitoshe, ingawa nadharia ya Uakili imeelezea kwa kirefu jinsi watu hujifunza sarufi ya lugha, haijaelezea waziwazi jinsi watu hao hujifunza maana za maneno na sentensi katika lugha.

 Nadharia hii pia ina udhaifu kwa sababu inafafanua matumizi ya lugha pasipo kuzingatia muktadha wa kijamii.

Wanaisimu-jamii wamedai kwamba matumizi ya lugha hayaathiriwi tu na akili ya mwanafunzi bali huathiriwa pia na sababu mbalimbali za kijamii.

Sababu hizi nipamoja na mielekeo, mazingira, jinsia, athari za kimakundi na utamaduni.

NADHARIA YA UHALISIA-NAFSI (THATHMINI-SAIKOLOJIA)

Kiini cha nadharia hii ni tabia ya ndani ya mtunzi ambapo nia, azma, motisha na fikra za mtunzi ndizo huchukuliwa kama nguzo ya utunzi.

Mwitifaki mkuu wa mkondo huu ni mtaalamu wa elimu ya nafsi Sigmund Freud ambaye mbali na kueleza vitendo vinavyozuliwa na nguvu za ndani za mtunzi alieleza kwanini vitendo hivyo hutokea.

Kimsingi, Freud alielemea maana ya kuwa utamaduni hutumiwa kufinya na kuondoa hisia na hamu zetu za kinyama tulizonazo ili kutustaarabisha na kutuwezesha kuisha na

wengine. Lakini huwa hisia na hamu hizi hazitoweki bali hutokea katika sura mbali

mbali za maisha yetu kama vile katika ndoto, matamanio, na michezo yetu.

Wahakiki walioegemea mkondo huu waliingiza maoni ya Freud katika fasihi huku wakiiona kazi ya mtunzi kama kielelezo cha hamu na hisia hizo.

Katika kueleza nguzo ya nadharia hii, Freud anamlinganisha mtunzi na motto anayecheza. Anasema kuwa kwa mtoto, jambo au kazi anayoipenda sana inayomridhisha, ni kucheza.

Twaweza kusema kwamba mtoto awapo mchezoni, hufanana na mtunzi kwa ambavyo yeye (mtoto) huumba ulimwengu wake, au kwa maneno mengine yeye huvipanga upya vitu katika ulimwengu wake ili vimpendeze.

Ni kosa kuchukulia kwamba mtoto huyu hatilii maanani huu ulimwengu wake; kinyume na

hivyo, ni kwamba yeye huutilia maanani sana kiasi cha kwamba huhusisha kiwango kikubwa cha hisia zake.

Ama kwa hakika, kinyume cha mchezo ni uhalisi.

Ni katikaulimwengu huu wa mtoto ambapo anapata uhuru wa kutenda atakacho bila kukanywa na watu wazima.

Hata ingawa kiwango kikubwa cha hisia zake huhusishwa katika huu ulimwengu wa mchezo, ifahamike kwamba huyo mtoto huubainisha ulimwengu wake wa mchezo na maisha halisi na hupenda kuvioanisha vitu vyake bunia na vile avipatavyo katika ulimwengu halisi.

Ndoa hii ndiyo inayotofautisha kule kucheza na kuota

(Phantasyzing).

Kulingana na nadharia hii, mtunzi hufanya kazi yake sawa na mtoto anayecheza.

Yeye huumba ulimwengu wake bunia ambao anautilia maanani sana – yaani anahusisha kiasi kikubwa cha hisia zake pale – huku akiutengamisha na uhalisia.

Jambo hili la kubuni hufaidi mtunzi kwa vile kazi yake huwa ya kuvutia kwa hadhira yake.

Mara nyingi mtunzi hutumia visa halisi vya maisha na kuunda huu ulimwengu bunia wake ambapo mambo anayoyazingatia huwa ni yanayoweza kutokea.

Pana jambo lingine linalozingatiwa na nadharia hii. Baada ya mtoto kukua na kuacha kucheza na baada ya kupambana kwa miaka mingi kuhimili maisha katika uhalisia wake, huenda siku moja akajipata fikirani mwake amefikwa na ile hali ya

kutenga mchezo na uhalisia. Jinsi watu wanavyokua ndivyo wanavyoacha kucheza na huonekana kana kwamba wamesahau raha waliokuwa wanapata mchezoni.

Lakini yeyote anayemwelewa mwanadamu, hufahamu kwamba hakuna kitu kigumu kwake kama kusahau raha aliyowahi kupata.

Ama kwa hakika hatuachi lolote, bali hulibadilisha na

lingine, tukapata kitu chengine cha kuchukua nafasi ya shibe au utoshelezi uliyoletwa na mchezo. Yaani nafasi ya jambo moja huchukuliwa na lingine ili kuonekana kana kwamba la kwanza limetoweka. Hivyo basi wakati mtoto akuapo na kuacha kucheza, anachotengana nacho ni vifaa halisi, na badala ya kucheza yeye hushiriki ndoto.

Hizi ndoto, kulingana na nadharia hii, ndizo nguzo katika utunzi.

Hii ni kwa sababu ni vigumu kuona ndoto za watu wazima ikilinganishwa na michezo ya watoto. Mtu mzima huona aibu kuwa na ndoto hizi kama amali za nafsi yake na kwa kawaida ataona ikiwa rahisi kukiri makosa yake kuliko kutoa kiini cha ndoto zake kwa yeyote.

Mchezo wa mtoto huongozwa na matamanio yake. Aghalabu yeye hucheza akiwa `mtu mzima’ na katika michezo yake, yeye hushirikisha yale anayoyafahamu kuhusu watu wazima.

Hana sababu yoyote ya kusetiri matamanio haya. Kwa upande ule mwingine, mtu mzima anafahamu kuwa hatarajiwi kuendelea kucheza au kuota, bali hupaswa kutenda mambo kihalisia, kiutu uzima; hivyo basi anongozwa na kufungwa na

matarajio ya kijamii kwake.

Isitoshe, baadhi ya matamanio yanayozua ndoto zake huwa ni yale yanayohitaji kusetiriwa yasijulikane kwa wengine kwani huwa ni kinyume na matarajio ya jamii.

Hivyo basi hawezi kuyatoa hadharani lau yatachukuliwa kuwa ya kitoto na yasiyokubalika. Lakini ni lazima yatoke ili atue.

Hapo ndipo anapata utulivu katika utunzi: anayatoa katika utunzi.

Kwa kawaida, chanzo na msukumo wa ndoto ni matamanio yasiyotimizwa, na kila ndoto hutokea kutimiza kila tamanio ili kuchukua nafasi ya uhalisia usioridhisha.

Hivyo basi kazi ya fasihi, kulingana na mtizamo huo, huwa ni jaribio la kutimizan matamanio ya mtunzi ambayo hayakutimizwa katika ulimwengu halisi.

Uhusiano kati ya ndoto na wakati, kwa kawaida huwa muhimu sana na huchukuana na vipindi vitatu – – navyo ni vipindi vinavyohusika katika ujenzi wa dhana katika binadamu. Kazi ya fikra huanzishwa na jambo linalotokea wakati uliopo na linalosisimua matamanio ya mhusika.

Kutoka hapo linarejelea tajiriba ya awali ambapo tamaa hiyo ilitimizwa; kisha inajenga hali inayohusisha wakati ujao inayowakilisha kutimizwa kwa tamaa hiyo. Kile kinachotokea ni ndoto inayobeba chembe chembe za asili yake kutokana na hali iliyoizaa hiyo ndoto pamoja na ukumbufu (memory). Hivyo basi wakati uliopita, uliopo, na utakaokuja huunganishwa pamoja na uzi wa matamanio na kudhihirika katika utunzi.

Tunachokipata tangu michezo ya utotoni hadi ndoto na hadi kazi za sanaa ni kwamba Freud anataka kuonyesha jambo moja kuu; kwamba binadamu kwa kawaida huwa na hamu ya kubadili kilichopo na hasa kile kisichoridhisha au kisichotosha katika

ulimwengu halisi.

Kwa hivyo fikra zinaendelezwa katika kubuni hali ambapo matamanio ambayo hayajaridhishwa hutimizwa. Hapo ndipo twaona kazi ya fasihi ikielezwa kama zao la ndoto na matamanio ya mtunzi anayehusika.

Mhakiki anayezingatia nadharia hii ataichukulia kazi ya fasihi kama kielezo cha matamanio ya mtunzi na juhudi zake za kuyatimiza katika ulimwengu wa sanaa.

Hapoinahitajika wahakiki kwa kiwango fulani wazingatie maisha halisi ya mtunzi husika ili kuielewa kazi yake ipasavyo.

Nadharia hii yaweza kutumiwa kueleza sanaa kama vile ya sinema, muziki, na drama ambazo maudhui yake huenda yakadhihiri mambo ambayo hayatendeki kwa ulimwengu halisi lakini ambayo yanasisimua na kuvutia hadhira kwa ambavyo yanatoa picha ya mambo ambayo yapaswa kutokea.

5 thoughts on “NADHARIA NA MBINU ZA UJIFUNZAJI NA UAMILIAJI LUGHA YA PILI

Leave a reply to Mwalimu Arigumaho Johnpaul Cancel reply