MWONGOZO WA UHASAMA KILIMANI

UHASAMA KILIMANI

UTANGULIZI

Uhasama kilimani ni riwaya iliyoandikwa na Masereka George Black mnamo mwaka wa 2017 nchini Uganda. Riwaya hii inazungumzia juu ya ukatili na uongozi mbaya wa kiuhasama  wa viongozi wa ufalme wa Bunyangabo uliongozwa na mfalme Kamanzi akisaidiwa na Sambara Kibelu, Mwanzira na Wengine.

Sambara Kibelu ni wakala na liwali mkuu wa mfalme Kamanzi anayeongoza vibaya wanajamii wa Jimbo la Bwera huko Bunyangabo kwa hali ya kiuhasama yaani kikatili. Jambo hili halikufurahisha kila mtu katika jamii ya Bunyangabo. Wanajamii wakawa wakilalamika kimoyomoyo huku wengi wakijutia maisha yao duniani.

KUHUSU MWANDISHI

Mwandishi ni Masereka George Black ambaye ni mzaliwa wa wilayani Kasese magharibi mwa   Uganda. Ni mtunzi ambaye amebobea sana katika lugha na fasihi ya Kiswahili.Ana shahada na stashahada ya Elimu katika Lugha ya Kiswahili. Amefundisha Kiswahili kwa muda mrefu sana hadi leo. Sasa hivi ni mwanajeshi katika jeshi la ulinzi wa wananchi wa Uganda.

                                             KUHUSU JALADA/GAMBA LA RIWAYA

Juu sana  kabisa ya riwaya kuna michoro inayoandamana hadi kuonekana kama mlima fulani ambao sasa mwandishi akadhania. Juu pia kuna maandishi yaani UHASAMA KILIMANI. Mwandishi ametumia rangi tatu katika maandishi haya yaani rangi ya Nyekundu na ya Njano katika neno UHASAMA. Maana hapo ni kudhihirisha tumaini dhidi ya watu kufa na kunyanyashwa vibaya. Yaani anayekutesa leo naye atateshwa kesho. Hakuna lisilo mwisho.

Neno KILIMANI limeandikwa kwa kutumia rangi nyeupe mara nyingi ranji hii hutumiwa kudhihirisha Heri na ushindi. Maanake hapo ni kwamba ingawa watu wa kilimani watanyanyashwa kiukatili, kuna imani na tumaini kwamba kutakuwa na ushindi baada ya ukweli kutambuliwa.

Katikati mwa riwaya kuna watu wanne ambao mwandishi amepamba kwa kuwavalisha mavazi ya rangi tofauti ambazo maranyingi huwa na ujumbe fulani kwa mchambuzi kitaswira. Lakini mbali na hayo, watu hawa wanaonekana kuwa wapo juu kabisa ya  kilima wote wan’ne wakishikana mikono kuonyesha kwamba umoja ni nguvu, na nikupitia umoja huu ambapo watakomesha na kutupilia mbali ukatili na unyanyasaji kilimani.

Chini kabisa ya riwaya hii kuna mchoro tena wa kilima ambacho kimepambwa kwa rangi ya nyekundu kuonyesha ukatili na umwagikaji wa damu katika kilima hicho jambo hili linadhihirisha kabisa uhasama kilimani. Mnamo kilima hicho, kuna watu watano, watatu wao wameshika mikuki na karibu  waue wenzao. Jambo hili lina jenga taswira ya jamii mbili kilimani ambazo zilipingana na kusababisha vifo vya watu maskini wengi.

            UHAKIKI WA JINA LA KITABU YAANI UHASAMA KILIMANI

Jina la kitabu ni UHASAMA KILIMANI. Uhasama ni vitendo vya kikatili na kiunyama vinavyotendwa na binadamu dhidi ya binadamu.  

UHASAMA KILIMANI ni vile vitendo/visa vya kiunyama/kikatili/unyanyasaji ambavyo viliwaandamana watu kilimani katika ufalme wa Bunyangabo katika kilima cha Rwenzori.

Ni ukweli kwamba kuna uhasama kilimani katika riwaya uhasama kilimani. (Ukweli kuhusu jina la kitabu)

  • Wenyeji wa jimbo la Bwera kunyimwa haki za kuvuna, kuchimba na kula kwa rasilimali iliyokuwa kwenye jimbo lao kama vile Chumvi, samaki. Sambara kibelu anaweka ulinzi wa kikatili dhidi ya rasilimali katika jimbo hilo la Bwera. Mwajamii angeuwawa Ikijulikana kuwa amekutwa na chumvi bila idhini au ruhusa.
  • Wenyeji wa jimbo la Bwera na mnomno zaidi wanaume wanashurutishwa na kulazimishwa kubeba kilo nzito za chumvi na kuzisafirisha sehemu za mbali kabisa bila malipo yoyote, na hata kutembezwa kwa mwendo wa haraka wengi wakipigwa na manyapara. Uk 9
  • Wanawake wawili katika jimbo la bwera wanatendewa visa vya unyanyasaji na hata hivyo bwana wao wanajulikana kuwa waliuwawa na hata hivyo miili yao ilikuwa imekonda ikakondeka kwa sababu ya ukosefu wa mahitaji ya kimaisha kama tunavyoambiwa na mhusika Kibwana riwayani.
  • Mzee Makali anatendewa uhasama kwa kuuliwa na liwali ambaye ni Mwanzira. Mzee huyu anatiwa Kitanzi  eti kwasababu amezungumzia juu ya uongozi wa ufalme wa Bunyangabo.
  • Wenyeji wa Bunyangabo wanatozwa kodi kwa hali mbaya ya kuwatusi, kuwapiga vibaya na hata kuuwawa. Kwamfano, mzee Kitholhu anauliwa na Mwanzira na baadaye wanalazimisha bibiye kuendelea kulipa kodi hiyo ingawa baada ya kuuwa bwanake.
  • Usaliti pia ni kitendo cha uhasama
  • Kujiuwa kikatili kwa Kujitia kitanzi pia ni kisa cha uhasama
  • Kifo cha Paluku ni kwasababu ya uhasama

                            DHAMIRA KUU YA MWANDISHI

Mwandishi anadhamiria kutuonyesha kwamba Ukatili na Uongozi mbaya ni Vitendo vyo uovu katika jamii ambavyo pia husababisha majuto kwa watendaji baada ya mda fulani. kwamfano mwandishi anatuonyesha viongozi akina Sambara Kibelu, Mwanzira na Sombe Ekamukumbi ambao wananyanyasa wanajamii katika ufalme wa Bunyangabo. Lakini mwishowe nao wanahukumiwa vibaya baada ya ukweli kujitetea na baadaye wanafariki kwa kujutia.

                        MTAZAMO WA MWANDISHI

Mtazamo huwa ni hali ya kuyaona mambo katika hali halisi au katika maisha kwa kuzingatia mazingira aliomo msanii au mwandishi.

Masereka George Black ana mtazamo wa kiakinifu.kwa mfano yale yote yanayotendeka katika Riwaya ya Uhasama kilimani huwa yametendeka na yanatendeka katika jamii zetu za kiafrika.

FALSAFA YA MWANDISHI

Falsafa ni mwelekeo wa Imani ya msanii.George Black Masereka anaendelea kuamini kuwa hakuna jambo na mpango unaoshindwa na utakao shindwa ikiwa kuna umoja na ushirikiano.

Pia Ana amini kuwa Mtenda Maovu au mabaya pia hulipwa mabaya mda wake ukifika.Kwa mfano Sambara Kibelu akatendea na kuongoza watu vibaya  lakini mwishowe  naye akahukumiliuliwa kuuliwa bila shaka.

                            ORODHA YA WAHUSIKA, UFASILI WAO NA SIFA ZAO

  • Kamanzi.

Ni mfalme na kiongozi wa ufalme wa Bunyangabo

  • Sambara Kibelu; Ni mhusika mkuu katika riwaya ya uhasama kilimani ambaye ni wakala na Liwali mkuu wa mfalme Kamanzi katika jimbo la Bwera la ufalme wa Bunyangabo.
  • Mwanzira; Ni mfuasi wa mfalme Kamanzi. Pia, ni mtumishi mwali wa Kibelu na askari muuaji katika ufalme wa Bunyangabo.
  • Sombe Ekamakumbi; Ni mwaasi na pia mpiganaji wa ufalme wa Kamanzi.
  • Makuha; Ni jemadari na kamanda wa Kibelu katika kambi ya huko Kisinga katika ufalme wa Bunyangabo. Ni mtoto wake Mukalu
  • Mbokoli; Ni mfuaasi wake mfalme Kamanzi.
  • Kapamba; Ni mfuasi wa mfalme Kamanzi na jemadari mkuu wa vikosi vya jimbo la Bwera katika ufalme wa Bunyangabo.
  • Singasinga; Ni mfuasi wa mfalme Kamanzi ambaye ni Diwani katika kijiji cha Kitswamba katika ufalme wa Bunyangabo.
  • Mubala; Ni mfuasi wa mfalme Kamanzi na ni Diwani wa kijiji cha Karambi katika ufalme wa Bunyangabo.
  • Machozi; Ni mfuasi wa mfalme Kamanzi na ni Diwani wa kijiji cha Hima katika ufalme wa Bunyangabo.
  • Mutera; Ni mfuasi wa mfalme Kamanzi na ni Diwani wa kijiji cha Kisinga katika ufalme wa Bunyangabo.
  • Mboka; Ni mfuasi wa Sambara Kibelu katika Kambi ya Kisinga.
  • Mukalu; ni babake Makuha.
  • Mbaka Lututu; Ni kiongozi msimamizi na mwenyekiti wa kundi la wapinzani lililokuwa likinyanyaswa (Abasukali) na ufalme na uongozi mbaya wa mfalme Kamanzi na wakala wake Sambara Kibelu.
  • Mabiraki; Ni mwanamke mjane na shujaa ambaye ni mfuasi wa Mbaka Lututu.
  • Kibwana;Ni mfuasi wa Mbaka lututu na kwa hivyo ni mpinzani wa uongozi  wa mfalme Kamanzi na maliwali wake kama vile Kibelu na Mwanzira.Sifa zake ni kama zifuatazo;
  • Ni mpelelezi mwenye umakini na mwangalifu sana.kwamfano tunamuona akinyamazisha ndugu yake Lukanga ili wapate kutambua wapi sauti za watu zitokapo.kibwana anasema”Hebu tega sikio. sikiliza kwa makini, nyamaza!”
  • Lukanga ; Ni mfuasi wa Mbaka Lututu.
  • Wanawake wa wili; Ni wafuasi wa mbaka lututu na kwa hivyo ni mpinzani wa uongozi  wa mfalme kamanzi kisirsiri na maliwali wake kama vile Kibelu na Mwanzira.Wanawake hawa wakafiwa wanaume wao na kwahivyo hali ikawawia vibaya na kuwafanya wawe wamekonda na kukondoka kwa sababu ya ukosefu wa mahitaji.
  • Mzee Makali; Ni mwenyeji wa jimbo la bwera ambaye anauwawa na Mwanzira kwa kukutwa akizungumza na wazee wengine kuhusu uhasama wa ufalme wa Bunyangabo.
  • Turudo; Ni mfuasi wa mbaka lututu na kwa hivyo ni mpinzani wa uongozi  wa mfalme kamanzi na maliwali wake kama vile Kibelu na Mwanzira.Ni mwenyeji wa jimbo la Bwera.
  • Kithasamba; Ni mungu mdogo anaye aminiwa kuwa anamiliki vilima vya mwezi vilivyokuwa jimboni mwao wenyeji wa Bunyangabo.
  • Kibuthi; Ni mwanamme wa sehemu ya  nyakahya ambaye pia ni mzee mfuasi wa mbaka Lututu ambaye ndiye aliye mhoji makuha.Kibuthi  ni msawishi bora.
  • Kambalu wa Ngotho; Ni mfuasi wa mbaka lututu na kwa hivyo ni mpinzani wa uongozi  wa mfalme kamanzi na maliwali wake kama vile Kibelu na Mwanzira.
  • Bitire; Ni mtoto wake wa kike Kibuthi.
  • Musoki; Ni mkewe makuha
  • Mrengu; Mwanamke jirani wa makuha aliyekuwa wa kwanza kumuona makuha ambaye walikuwa wamedhani akafariki.Makuha alitekwa nyara na wafuasi wa Mbaka Lututu.
  • Musabuli;Ni mwanamke rafikiye Mwanziri kimapenzi ambaye anamuokoa mvulana Kambale dhidi ya kifo.
  • Kambale ; Ni kijana  mfuasi wa mbaka lututu na kwa hivyo ni mpinzani wa uongozi  wa mfalme kamanzi na maliwali wake kama vile Kibelu na Mwanzira. Kambale siku moja akajitolea kisujaa na kumwendea Mwanzira mtu anaye ogopwa, na hatimaye akamchokoza kwa kumtobolea maovu yake dhidi ya watu wa Bunyangabo.Akamwambia kwamba asiendelee kusababisha vifo vya watu masikini.
  • Mzee Kitholhu; Ni babake mrehemu Paluku ambaye pia nauwawa kikatili na Mwanziri ambaye mfuasi wa mfalme kamanzi na kibelu. Mzee Kitholhu anauliwa na Mwanzira na baadaye wanalazimisha bibiye kuendelea kulipa kodi hiyo ingawa baada ya kuuwa bwanake.
  • Paluku ;Ni mtoto wake wa kiume wa kwanza wa mzee Kitholhu ambaye anafia msituni wakati wa kusafirisha chumvi ya ufalme.kapalu anajaribu kusaidia Mzee Sibitha kwa kupunguza kwa mzigo wake wa chumvi na kuongezea kwa wake mziko.Hii ni kwasababu mzee Sibitha alianza kulemewa.Na kwasababu ya huruma nautu,paluku akasaidia.Paluku akabeba mzigo mkubwa huo na kwasababu safari ilikuwa ndefu sana,Paluku anaanza kulemewa na miguu yake ikashindwa kuendelea.Hapo akabaki nyuma na wanyama wakali wenye njaa kama Simba wakamla.
  • Mzee Sururu; Ni mmoja wa wenyeji wa Bunyangabo ambaye ana lalamika zaidi juu ya  mungu wao mdogo Kithasamba ambaye anawaangalia tuu wakiwa wanateseka na kunyanyaswa.Anapendekeza kuwa wanafaa mungu mwengine ambaye anafaa na kudhania watu wake wakati wa dhiki.
  • Bi-Kyabilo; Ni nyanyake Mbaka Lututu ambaye anamtobolea mengi kuhusu jina lake la Lututu na maisha yake ya utoto.
  • Mzee Baminya; Ni babake Mbaka Lututu
  • Kambalu wa Ngoto; Ni mfuasi wa mbaka lututu
  • Karoli wa Kibuti; Ni mfuasi wa mbaka lututu
  • Kapota/Mwenda;Ni mhunzi aliyempa Mbaka Lututu mikuki  ya kumsaidia kupambana na wafuasi wa ufalme wa kamanzi.
  • Bi-Kizee; Ni bibi anayemsaidia Mbaka Lututu kumpata mhunzi yaani Kapota/Mwenda baada ya kumtafuta kwa mda mrefu sana bila kumpata.
  • Mzee Twata Munyangabo Kalonge; Ni babake mzazi wa mfalme kamanzi.
  • Kasuka;
  • Amiri;
  • Ithungu;

PLOTI YA RIWAYA

Riwaya inaanza na Kibwana ambaye ni mfuasi wa Mbaka Lututu akiwasiliana na rafiki yake Lukanga ambaye pia ni mmoja wapo wa wafuasi wa Mbaka Lututu Kibwana na Lukanga wakawa wamejificha kichakani karibu na barabara inayoelekea katika uwanja mkuu ambapo kungekuwa na mkutano siku hiyo.

Kibwana na Lukanga wakapitiwa na wanawake wawili ambao wamo safarini kwa kasi ya kuelekea kwenye mkutano.Kibwana anaamua kutoka kichakani na moja kwa moja anawafuata wanawake hao lakini kwa mwendo wa kunyatia.Kibwana anawafikia na jambo linalomhudhunisha ni kwamba wanawake hawa walikuwa wamekonda na wakakondeka ingawa warembo. Hii ni kwasababu hali nyumbani ilikuwa mbaya sana. Na sababu za hali kuwa mbaya ni;

  • Sambara Kibelu kuwakandamisha na kuwanyanyasa wenyeji wa Bunyangabo
  • Kuawawa kwa wanaume na wake wengi kubaki wajane na watoto yatima.
  • Kubebeshwa chumvi na kuisafirisha sehemu mbali kwa safari ndefu
  • Watu kutozwa na kulazimishwa kulipa kodi kiwango cha Thulusi kwa kila mvuno. Kwa Mfano mzee Kitholhu anauwawa kwa kujaribu kujificha wakati wa kulipazwa kodi.
  • Paluku  na mzee makali kuawawa ovyo ovyo.Jambo lililo wakera sana wenyeji.

Kibwana anawafikia wanawake na anatumia mbinu tofauti za kuzungumza nao na kuwasawishi ili apate kujua sababu ya Sambara Kibelu kuitisha mkutano.Wanawake wakaogopa sana kumtobolea sababu kwani makachero(wapelelezi) wa kibelu  siku hizo walikuwa wengi sana.Ingawa hivyo,kibwana akawasawishi na wakazungumza naye. Kibwana anaamua kuita rafikiye Lukanga ili kufatana na wanawake hao na kuhudhuria mkutano.

Inajulikana kwamba kibwana na lukanga wote ni wafuasi wa Mbaka Lututu,na kwa hivyo waikuwa wamemaliza siku saba wakiwa wanalala nje kwa ajili ya kufanya upeleleza,utafiti na uchunguzi juu ya uongozi, viongozi na makachero wa mfalme kamanzi mfalme wa ufalme wa Bunyangabo. Kibwana na lukanga wangetafuta habari tofauti kutoka jimbo moja hadi jingine .Na kwa hivyo, kwa ajili ya kupata habari zaidi wakalazimishwa kujiunga katika mkutano huo ulioandaliwa na Sambara kibelu.Wakajiunga katika mkutano kiholelaholela huko wakijificha sana kutotambulika na kibelu pamoja na wafuasi wake.

Kupitia mazungumzo ya wazee Njiani ambayo Kibwana na lukanga wakapata kuyafatilia,tunagundua ya kwamba Mbaka lututu ambaye ni mpinzani wa uongozi wa mfalme kamanzi,akadai kuwa alipokuwa kwenye Ndoto,Mungu kithasmba akamwambia kwamba anzishe kundi la wapinzani ili kujiokoa dhidi ya uhasma na unyanyasaji.Kithasamba akamuahidi ushindi.kwasababu hii,Mbaka Lututu siku moja akamuandikia barua mfalme kamanzi kwamba Jimbo la Bwera asilihesabu tena katika majimbo ya ufalme wake yaani yeye atakuwa mfalme wa jimbo hio.

Mfalme kamanzi anapopokea barua/nyaraka hii, anaanza kubabaika na kusema matusi mengi sana akijaribu kumchafusha na hata hivyo kumkejeli Mbaka Lututu.moja kwa moja, Mfalme Kamanzi anawaza na kuwazua na badaye anaamurisha Wakala na liwali wake mkuu Sambara Kibelu kuenda katika jimbo la bwera na kuitisha mkutano wa dharura.Pia anaamru Sambara kibelu kumtafuta Mjinga na masking Mbaka Lututu na kumleta akiwa hai.

Papo hapo,kibelu akaitisha mkutano uliohudhuriwa na wenyeji wengi wa jimbo la bwera na hata ikiwemo na makachero wengi wa Mbaka Lututu ambao walihudhuria kisirisiri ili kupata habari kuhusu mkutano.kibwana na lukanga wakawa watulivu sana mkutano ulipoanza ili kunasa na kuhefadhi yote yatakayojadiliwa na Sambara kibelu.

Sambara Kibelu akaanza mkutano kwa kutambulisha tena madiwani na wawakilishi wake wapya wan’ne ambao ni;  Kapamba ambaye ni Jemadari wa jimbo la bwera,Singasina jemadari wa Kitswamba,Mubala diwani/jemadari wa Karambi, na Machozi kuwa Jemadari wa Hima. Jambo hili la kuwaletea madiwani hawa ambalo wenyeji wakachukua kuwa mizigo tena halikufurahisha wengi hata kamwe na watu wote wakanungunika zaidi.Lakini baada ya hayo yote,Sambara Kibelu akawaonya wenyeji wa jimbo la Bwera na hata wa majimbo mengine kujitenga na jambo la Upinzani.Kibelu anatuma wanaojiita wafuasi wa Mbaka Lututu ambaye akamuita kiroboto kwamba wamuambie kuwa mfalme kamanzi atabaki mfalme wao milele na milele.Atakaye jaribu kupinga ataonyeshwa chamtemakuni.mkutano ukamalizika wenyeji wakiwa wananungunika.

Baada ya mkutano, wafuasi wake Mbaka Lututu wakaenda moja kwa moja na kumupasa habari kuhusu yalioajiri katika mkutano dharura.Na mambo muhimu yakawa ni kibelu kuwatambulisha madiwani wapya tena katika kila jimbo la ufalme ili kuongezea kwa ulinzi zaidi.Jambo la pili ikawa ni kuwaonya wenyeji wa jimbo la Bwera kujitenga na jambo la upinzani dhidi ya ufalme.Na jambo mhimu la tatu ikawa ni kumtafuta kamanda wa wapinzani Mbaka Lututu popote alipo.

Mbaka Lututu anaposikia kwamba anasakwa na Kibelu ,anajipanga vilivyo na kuwashauri wafuasi wake kupinga moyo konde kwasababu yupo tayari kupata ushindi.Mbaka lututu wakati huu wa kuwaza na kuwazua, kitaswira anamkumbuka mrehemu shujaa mwenzake kijana Paluku ambaye angekuwa mpiganaji bora na hivyo mtu wa muhimu kwake.lakini ampate wapi?

Ingawa hivyo, Mbaka Lututu anasawishi wafuasi wengi kujiunga naye.mfano ni mwanamke kwa jina la Mabiraki ambaye ni mjane na hata ambaye anasifiwa sana kwa ushujaa wake wa kuwa mwanamke pekee wa kwanza kukabiliana na Fisi na baadaye akamuua katika ufalme wa Bunyangabo.mwanamke huyu akawa anasifiwa na kuogopwa sana kivita.Mwanamke huyu Mabiraki kwa bahati nzuri anakubali kujiunga na kuwa mufuasi bora wa Mbaka Lututu.moja kwa moja shughuli zikaanza.

Mbaka lututu sasa anaanzisha kambi huku porini katika kijiji cha Mbata huko kilimani.Hata hivyo anamwendea mhunzi kwa jina la Mwenda au Kapota ili amutengenezee mikuki kama mia moja.Akampata mhunzi huyu kwa usaidizi wa bi-kizee.Mbaka lutut akazungumza na mhunzi na kumsawishi sna.Mhunzi kapota baada ya kuvutiwa na kutaamashishwa na maelezo ya Lututu, akakubali kumpa Lututu mikuki mia moja ya bure na mingine ataendelea kutengeneza kwa mda usiombali.

Mbaka Lututu akaanza matayarisho ya vita na akaongezea kufungua kambi zaidi huko kilimani.wafuasi wake mbaka lututu wakaanza kuonyesha ushujaa wao.kwamfao,Mwanamke aitwaye Mabiraki akamteka nyara makuha ambaye ni kamanda jemadari wa Sambara Kibelu.Mabiraki anatumia hadhi ya jinsia na urembo wake na akampoteza fikra jemadri wa Kibelu yaani Makuha na kumshika na badaye kumsafirisha safari ndefu huko kilimani hadi katika kambi ya mwisho katika sehemu ya Kangaluma ya bundibujo ambapo anafungiwa kwa siku saba.Mzee kibuthi ndiye aliye mhoji makuha na kupata habari yote kuhusu mipango ya Sambara kibelu kivita na hata aina ya silahi walizo nazo.

Habari za kutekwa nyara kwa kamanda wake sambara kibelu zikamfikia.kibelu hakuamini na hata hakujiamini.akendelea kuwa na wasiwasi  na fikra zikamjaa.kibelu pia akaripoti kwa mkuu wake mfalme Kamanzi.Mfalme kamanzi pia akaishiwa nguvu na baadaye akaanza shughuli za kufikiria tena kuhusu ile Barua alioandikiwa na Mbaka Lututu akiomba na kumfahamisha kwamba jimbo la Bwera si lake tena.

Kwake Kibelu, akaamua kuitisha mkutano wa wapiganaji wake wote kutoka kila jimbo.katika mkutano,Kibelu akawapa habari hiyo ya huzuni ya kutekwa nyara kwa kamanda wao Makuha.Hata hivyo akwaonya kwa waangalifu sana yaani ukiona kichwa cha mwenzako kikinyolewa jitie maji pia chako.Kibelu akawashauri kuongezea bidii zaidi katika kazi za ulinzi wa ufalme ,na pia akawahidi kuwa atawapa mafunzo ya silah yao mpya ya SAR ambayo Makuha alikuwa amejifunza vilivyo.

Huko mwituni, waasi wa lututu walikuwa wamegubikwa furaha tele. Furaha za kumshika kamanda wake kibelu yaani makuha,furaha za kuwaokoa wachawi walioshikwa nakibelu,furaha za kumpenda zaidi mwanamke shujaa yaani Mabiraki na shughuli zake na hata zaidi furaha za kuwa na shujaa jasiri Mbaka lututu na juhudi zake za kuwasawishi waasi wengi kujiunga naye.waasi wengi wakati hapo wakaanza kuimba nyimbo za kumsifu Shujaa wao Mabiraki pamoja na shujaa mkuu Mbaka Lututu.

Siku moja mbaka lututu akaitisha mkutano wa waasi wak huko mwituni ili kuwapa tumaini na mawaidha waasi wake. Akawaambia kwamba vita na mapambano yao dhidi ya mfalme Kamanzi si kusababisha vifo bali ni kuleta amani.Anawaarifu kwamba wamejitayarisha vilivyo kupambana na mfalme kamanzi ili kuokoa maisha ya Binadamu wengi na hata kupata ufalme wao mpya ambao utapewa jina la “UFALME WA KILIMA CHEMA”. Akawaambia kuwa wamemuachilia huru Makuha ambaye ni kamanda wa mfalme kamanzi na sambara Kibelu.Lututu anawaarifu kuwa hili litakuwa funzo kwake mfalme kamanzi kwamba sisi si wauaji na bali wataka amani,uhuru na umoja.

Mwituni pia, baada ya kibuti kukusanya habari yote aliokusudia kwake makuha,anafungwa tambara usoni na kusafirishwa hadi alipotekewa nyara.wakamufungua mikono na kumuachilia huru.wakamuaga kwa kumuambia afike salama, na amsalimu sambara Kibelu na mfalme Kamanzi na watu wake.pia wakamtuma kumwambia sambara kibelu kuwa Mbaka Lututu amesema arudi kule alipotoka na aache huru wana jamii.Makuha hakuamini kuwa ameachiliwa lakini ndivyo ilivyo kuwa.

Huko nyumbani kwake makuha, wenyeji wakakubali kuwa makuha aliuwawa na nilazima wamfanyie matanga.wanafamilia wakaanda siku ya sherehe hiyo na wakaanda.wakati wa sherehe hi, Sambara Kibelu akahudhuria.Akawaonya wenyeji kujitenga na vitendo vya kiuchawi.Kibelu akamsifu marehemu Makuha kwa ujuzi wake wa kuchapa kazi vilivyo.Kibelu pia anawarifu kuwa mfalme kamanzi amesema kuwa kuanzia leo, kodi ndogo wanowatoza ikome.

Baada ya siku, habari ikaenea kote kuhusu kupatikana kwa makuha ambaye walikuwa wamebatiza jina la marehemu.mwanamke mrengu ndiye aliye kuwa wa kwanza kumuona wakati anapoenda kuchota maji asubuhi.Habari hii inapomfikia kibelu,anachanganyikiwa kidogo na fikira zikawa nyingi sana jambo lililommaliza nguvu.

Makuha anachukuliwa kwa mfalme kamanzi ili kutoboa yote alioyaona,yasikia,aliyofanyiwa na alioambiwa na waliomteka nyara.Makuha akamtobolea yote na baada ya mazungumzo haya,mfalme kamanzi akajiwa na fikra nyingine kwani mambo yakamchanganya na kumzidi.Mfalme kamanzi akauitisha mkutano wa maliwali na mawakala wake wote katika kila jimbo.Akaalika hata wenyeji wa ufalme wa Bunyangabo wote.mkutano ukatayarishwa kwa siku kumi na n’ne.wakati wa siku hizo kabla wakiwa wanangojea mkutano,mfalme ana waachisha masambulizi wapiganaji wake dhidi ya waasi wa Mbaka Lututu,akamwambia kibelu kutowasaka waasi wa lututu na wakati huu akatambua kwamba Mbaka Lututu huenda akwa Rafiki mwema.

Baada ya siku kumi na n’ne kutimizwa, siku ambazo wenyeji walikuwa wanahesabu moja baada ya nyingine,siku yenyewe iliokuwa ikingojewa ikafika na watu wote ikiwemo na hata makachero wa mbaka lututu,wakafika uwanjani wa mkutano kwa hamu ya kutaka kujua yatakayo semwa na mfalme kamanzi.wenyeji siku hiyo wakawa wana taswira nyingi sana moyoni.hata hivyo maliwali na waasi wake kamanzi katika kila jimbo wakawa wamefika ikiwemo hata Sambara kibelu ambaye ni liwali mkuu.

Mfalme Kamanzi akafika uwanjani alipokuwa akingojewa kwa hamu.moja kwa moja akaanza hotuba yake kwa kuomba msamaha kwa wenyeji wa Bunyangabo na mno zaidi wa jimbo la Bwera kwa uhasama na ukatili uliowafanyiwa na makachero wake.Mfalme kamanzi anamlauma Sambara kibelu ambaye maranyingi angetenda ukatili na uhasama kwa watu bila idhini ya mfalme.Anawafahamisha kuwa kuwe muungano wa Abasukali na Abaswagha.Pia akawrifu waasi wa lututu kuwa wamuambie popote alipo kuwa Ombi lake la kuanzisha ufalme wa Bwera limekubaliwa na kutiliwa mhuri.watu wakashangilia na kufurahia sana na hat asana zaidi.

Sambara kibelu ambaye ako pembena mwa mfalme akaanza kutetema na kujisahau,akawaza na kuwazua.akaanza kujuta na kufikiria lile na lile.akaanza kuangalia kule na pale na badaye macho akayaweka chini.na hata makachero wengine wenzake.Hata hivyo,Sambara Kibelu anahukumiwa kifo kama ishara ya kuonyesha kuwa mfalme kamanzi alijutia vitendo vyake  alivyovitendo bila hata idhini yake. Sombe Ekamakumbi akatimua mbio na hakuonekana tena kijijini na ufalmeni kwa sababu ya vitendo vyake vya kiuhasama.Mwanzira naye akapatikana huko mtini mwili wake ukininginia huko.Alikuwa amejitia kitanzi kwasababu akafikiria kuwa ana vitendo vingi vya kiovu na kiuhasama.

Mbaka lututu anatoka kichakani na anasherekea na anakuwa mwenyekiti wa baraza la UFALME WA KILIMA CHEMA huko mwanamke Mabiraki akiwa makamu wa mwenyekiti.mwisho kabisa mfalme kamanzi anaungana na Mbaka Lututu na wanasaidiana katika shughuli kadhaa za kufukuza njaa,kujenga amani na ushirikiano na kuendeleza maendeleo ya jamii. 

  MAUDHUI/VISA VILIVYOMO KATIKA RIWAYA YA UHASAMA KILIMANI

Kuna maudhui ya umasikini/unyonge

  • Mfano,mwandishi anasema kijiji cha Bwera kilikuwa kimejengwa kwa vijumba na vibanda vidogo vidogo vya kikale aina ya manyata.uk2
  • Wenyeji wa bwera kuwinda na kula wanyama wa porini ni kisa cha kukosa mahitaji ya nyumbani kama vyakula.
  • Wanawake wawili kukonda na kukondoka ilikuwa ni kwasababu ya ukosefu wa mahitaji maishani jambo lililowafanya kuonekana vibaya sana

Kuna maudhui ya uongozi wa kiufalme

  • Mfalme kamanzi ni kiongozi na mfalme wa ufalme wa Bunyangabo na wana jamii wa ufalme huu.
  • Sambara Kibelu naye ni kiongozi mbaya ambaye ni liwali mkuu wa mfalme kamanzi katika Jimbo la Bwera
  • Mbaka lututu anatoka kichakani na anakuwa mwenyekiti wa baraza la UFALME WA KILIMA CHEMA katika sehemu ya Bwera.
  • Mwanamke Mabiraki naye ni kiongozi bora.akamsaidia mbaka lututu na hata watu wa jimbo la bwera kwa kuwaongoza viru ili kupinga ufalme na uongozi mbaya wa mfalme kamanzi.Mabiraki baada ya ushindi dhidi ya uhasama wa sambara kibelu, anapewa cheo cha  makamu wa mwenyekiti wa Baraza la Ufalme wa Kilima Chema.

Kuna maudhui ya majuto

  • kwamfano wengi wa wanajamii wa jimbo la Bwera walikuwa wanajutia maisha yaliokuwa yana badilika vibaya kila kukicha.kwa hivyo wengi wakajutia eti kwa nini wakazaliwa

Kuna maudhui ya utumwa

  • Huko Bwera wenyeji wengi waliishi kwa hali na maisha ya kitumwa.kwamfano wanaume kubebeshwa chumvi na kuisafirisha mbali zaidi bila malipo ila tuu malipo yangekuwa kuwapiga na kuwaua.kwamfano Mvulana paluku anakufa kupitia njia hii ya utumwa.

Kuna maudhui ya ukame

  • katika uk.5,mwandishi anasema kwamba baada ya Istiwai kupitia katikati mwa jimbo la bwera,sehemu hizo zikawa kame sana na kavu zaidi.kwasababu hii,kukawa na njaa iliyosababishwa na ukaukaji wa memea na rotuba

Kuna maudhui ya baraka/ubaraka

  • wenyeji wa jimbo la Bwera miongoni mwa majimbo mengine huko Bunyangabo,wakabarikiwa na vitu vingi vya thamani kama vile vijiwa vya chumvi,samaki na mito tele
  • Pia wana barikiwa na washujaa kama Mbaka Lututu na Mwanamke Mabiraki ambao wanapigania haki za wanajamii na kuwaokoa katika uongozi wa kiuhasama uliokuwa umewalalamisha wengi na hata kusababisha vifo vya watu tele bila hata kosa watendalo.
  • Pia wanabarikiwa na mungu wao mdogo kithasamba ambaye wengi wakamwamini na hata viongozi kama mbaka lututu ikiwemo na wazee jimboni wakamwaninia na hata hivyo kithasamba akawasaidia kupata uhuru

Kuna maudhui ya ulalamikaji

  • wenyeji wa jimbo la bwera wakaishi kwa kulalamika sana,na mnomno wakalalamikia majira ya Liwali Kibelu aliyekuwa ameshikilia ndindi utekelezaji wa sheria mbaya zilizokuwa zimewekwa.

Kuna maudhui ya vifo na tanzia

  • uk.17, kuna mzee Makali ambaye anauwawa na mwanzira kwa kujaribu kuzungumzia juu ya uongozi wa kamanzi.mzee makali anauwawa kwa kutiwa kitanzi.
  • Vifo vya wanaume wa wanawake wawili kama tunavyo ambiwa na Kibwana. wanawake hawa wakawa wamekonda na kukondeka kwa sababu ya ukosefu wa mahitaji maishani.
  • Kuna pia kifo cha Sambara kibelu ambaye akauwawa baada ya kuhukumiwa kifo na mfalme kamanzi kwa ajili ya kutenda visa vya kiuhasama na kusababisha vifo vya wenyeji bila idhini ya mfalme
  • Mwanzira ambaye ni mwaasi wa mfalme kamanzi naye anajitia kitanza baada ya kujua kwamba mfalme kamanzi amemuhukumia kifo mkuu wake sambara kibelu.mwanzira anajiua kwasababu ya vitendo vingi vya uawaji alivyovihusika
  • Mzee Makali anauliwa na liwali ambaye ni Mwanzira.Mzee huyu anatiwa kitanzi  eti kwasababu amezungumzia juu ya uongozi wa ufalme wa bunyangabo.
  • Mzee Kitholhu anauliwa na Mwanzira kwasababu ya kujaribu kujificha wakati wa kutozwa kodi. Hata baada ya kumuua, wanalazimisha bibiye kulipa kodi hiyo ingawa baada ya kuuwa bwanake.
  • Kuna kifo cha paluku ambaye anakufa kwa sababu ya kubebeshwa mzigo mzito.paluku anakufa baada ya kuachwa nyuma na wabeba mizigo wengine kwani akalemewa na kushindwa kuendelea na safari.Simba wenye njaa wakamua na wakamla.

Kuna maudhui ya usaliti

  • Mzee Torudo anasaliti mzee mwenzake mzee Makali baada ya Mwanzira kuwakuta wakizungumzia vibaya juu ya uongozi uliopo.Torudo anasema”sasa makali umeona?Nilikuambia kama ninavyokuambia kila siku.sasa tazama mambo yako ya kijinga!.Nimekuonya mara ngapi kwamba usithubutu kumpiga mfalme?
  • Mbokoli anasaliti watu wa kabila na aila yake kwa kujiunga na wafuasi wa Kibelu na mfalme kamanzi na kunyanyasa watu hao kiuhasama.
  • Mfalme anasaliti maliwali wake akina sambara Kibelu kwa kumhukumia kifo.
  • Mwanzira na Sambara kibelu wanasaliti mfalme kwa kutenda vitendo vya kiovu kupitia jina la mfalme lakini bila idhini yake.

Kuna maudhui ya upinzani

  • Mbaka lututu anapinga uongozi wa mfalme kamanzi pamoja uongozi mbaya wa maliwali wa mfalme kama mwanzira na sambara kibelu ambao wanatenda vitendo vya kiukatili dhidi ya wana jamii wa jimbo la bwera.
  • Wana jamii wengi pia wanauwawa kwa kujaribu kupinga uongozi mbaya wa sambara kibelu na mwanzira .kwa mfano mzee makali.
  • Wenyeji wengi wa jimbo tofauti huko bunyangabo wakapanga kupinga uongozi wa mfalme Kamanzi na wakaanza kujiunga na shujaa Mbaka lututu ili waanzishe ufalme wao wa jamii ya Abasukali na kuacha kutumikia kamwe jamii ya Abaswagha.

Kuna maudhui ya ukombozi

  • Kuna ukombozi wa Abasukali kutoka utumwani wa uongozi mbaya wa mfalme kamanzi kupitia maliwali wake kama sambara kibelu.

Kuna maudhui ya ukatili/uhasama

  • Wenyeji wa jimbo la bwera kunyimwa haki za kuvuna,kuchimba na kula kwa rasilimali iliokuwa kwenye jimbo lao kama vile Chumvi,samaki.Sambara kibelu anaweka ulinzi wa kikatili dhidi ya risilimali katika jimbo hilo la Bwera. Mwajamii angeuwawa Ikijulikana kuwa amekutwa na chumvi bila idhini au ruhusa.
  • Wenyeji wa jimbo la Bwera na mnomno zaidi wanaume wanashurutishwa na kulazimishwa kubeba kilo nzito za chumvi na kuisafirisha sehemu za mbali kabisa bila malipo yoyote,na hata kutembezwa kwa mwendo wa haraka wengi wakipigwa na manyapara.Uk 9
  • Wanawake wawili katika jimbo la bwera wanatendewa visa vya unyanyasaji na hata hivyo bwana wao wanajulikana kuwa waliuwawa na hata hivyo miili yao ilikuwa imekonda ikakondeka kwa sababu ya ukosefu wa mahitaji ya kimaishi kama tunavyoambiwa na mhusika kibwana riwayani.
  • Mzee Makali anatendewa uhasama kwa kuuliwa na liwali ambaye ni Mwanzira.Mzee huyu anatiwa kitanzi eti kwasababu amezungumzia juu ya uongozi wa ufalme wa bunyangabo.
  • Wenyeji wa Bunyangabo wanatozwa kodi kwa hali mbaya ya kuwatusi kuwapiga vibaya na hata kuuwawa.kwamfano,mzee Kitholhu anauliwa na Mwanzira na baadaye wanalazimisha bibiye kuendelea kulipa kodi hiyo ingawa baada ya kuuwa bwanake.
  • Usaliti pia ni kitendo cha uhasama
  • Kujiuwa kikatili kwa kujitea kitanzi pia ni kisa cha uhasama
  • Kifo cha paluku ni kwasababu ya uhasama

Kuna maudhui ya imani ya miungu

  • wenyeji wengi wa bunyangabo wakaamini mungu mdogo aitwaye”Kithasamba”kwa kilugha choa.hata kupitia hadithi ya wazee wa jimbo la bwera,wanatuambia vizuri kuwa kithasamba ni mungu wakuamini
  • Mbaka Lututu anasema kwamba watakwaruzana na mfalme kamanzi pamoja na kibelu…..anasema” Naapa kwa jina la Kithasamba na mlima huu ambao daima umekuwa nikimbilio letu Abasukali”

Kuna maudhui ya Ndoto

  • Mzee kitholhu anaota akiwa na mtoto wake Kapalu ambaye alikufa zamani
  • Mbaka lututu anaota kithasamba ambaye ni mungu mdogo akimuambia kwamba aupinge ufalme wa kamanzi na anzishi kundi la wapinzani.
  • Mbokoli anaota watu wakikamata na kuchukua mfuasi mwenzake makuha.

Kuna maudhui ya mila na Desturi/utamaduni

  • wenyeji wa jimbo la Bwera yaani wanaume wa Abasukali hutahiriwa.kwamfano kibwana anamdharau Kapamba kwa kusema kwamba alikimbia kisu cha ngariba.
  • Hakuna mwanamke ambaye angekubaliwa kuolewa na mwanamme ambaye bado hajatahiriwa.
  • Wenyeji wa bunyangabo kuamini kuwa mwana/mtoto wa kiume pekee ndiye anastahili kurithi mali ya babake na hata mzazi wake.
  • Watoto wakike hawachukuliwa kama watoto na wanaume wengi wa ufalme wa bunyangabo.kwamfano Kibuti anajutia kwa kutozaa mtoto wa kiume.
  • Mwanamme ambaye hajazaa mtoto wa kiume hapewi nafasi hata kamwe ya kuzungumzia katika mkutano wa jamii.

Kuna maudhui ya uzalendo

  • Mbaka lututu ni mzalendo kwani anapigania utu na haki za wananchi kwa kudai uhuru wa wenyeji wa jimbo la Bwera.
  • Mbaka lututu anaonyesha uzalendo wake kwa kumuandikia barua ya upinzani wa ufalme wa kamanzi, mfalme alioogopwa sana na wenyeji.
  • Mbaka lututu anaandaa mikutano ya wazalendo ili Wapange jinsi ya  kujikomboa dhidi ya unyanyasaji wa mfalme kamanzi na viongozi wake.
  • Mwanamke Mabiraki ni mzalendo kwa anajiunga na mbaka lututu ili kuokoa watu wengi dhidi ya uhasama.
  • Mabiraki kumteka nyara mnyanyasaji wa mfalme kamanzi yaani Makuha ni moyo wa uzalendo.
  • Kibwana na Lukanga ni wazalendo kwani nao wakawa na nia kuu ya kuokoa watu wa bunyangabo dhidi ya uhasama.wakaamua hata kulala vichakani juu ya kutaka uhuru.
  • Mhunzi Kapota/mwenda naye ni mzalendo kwasababu akajitolea kumtengenezea mikuki kadha mbaka lututu ili afukuze wanyanyasaji katika jimbo lao.
  • Kambale naye ni mzalendo, kwani anajitolea kumwendea mwanzira ambaye ni muuaji na kumuuliza sababu za kumfanya kuwauwa watu maskini.

Kuna maudhui ya ushujaa

  • mwanamke Mabiraki ni shujaa kamili,kwa mfano akawa mwanamke wa kwanza katika jimbo la Bwera na hat ufalme wa bunyangabo kumua fisi ambaye ni mnyama anayeogopwa.
  • Mwanamke mabiraki ni shujaa kwani hakuogopa kumteka nyara kamanda Jemadari wa mfalme kamanzi yaani makuha.
  • Mbaka lututu kumwandikia barua ya upinzani wa ufalme wa kamanzi ni jambo la ushujaa.
  • Kambale naye ni mzalendo,kwani anajitolea kumwendea mwanzira ambaye ni muuaji na kumuuliza sababu za kumfanya kuwauwa watu maskini.
  • Kibwana na lukanga ni shujaa.kwamfano wanafanya upelelezi kwa kuhudhuria mkutano ulioandaliwa na kibelu.wanafanya juu chini kuhudhuria mkutano huu ingawa kwa uerevu.

Kuna maudhui ya uhunzi

  • kwamfano kapota/mwenda ni mtengeneza mikuki na anamsaidia lututu kupata vifaa vya vita.

Kuna maudhui ya umoja na ushirikiano

  • Mbaka lututu anaugwa na wakereketwa wengine ili kujiondoa katika hali mbaya dhiki ya amri za kibelu
  • Kibwana na lukanga ni wenye nia mja ya kuleta umoja kupitia ushirikiano wao
  • Mabiraki ni mwenye ushirikiano wa kusababisha umoja.kwamfano anajiunga na mbaka lututu ili kujiokoa dhidi ya uhasama
  • wenyeji wa jimbo la bwera ni wenye ushirikiano

Kuna maudhui ya mapenzi

Kuna maudhui ya mabadiliko

  • mfalme kamanzi anasabisha mabadiliko.kwamfano baada yake kufika ufalmini,kukawa na mabadiliko katika utamaduni wa kutahiriwa.sherehe za kutahiriwa zikaachwa.
  • Kuna mabadiliko ya utamaduni kwa mfano wanawake kuolewa bila kuchunguza ikiwa mwanamme ametahiriwa au la.jambo la kuolewa na mwanamme ambaye hajatahiriwa lilikuwa nadra
  • Kuna mabadiliko ya uongozi
  • Kuna mabadiliko ya fikra au kimawazo

Kuna maudhui ya usawishaji

  • Mbaka lututu ni msawishi,kwamfano anawasawishi wenyeji wengi wa ufalme wa Bunyangabo kujiunga naye ili kukomboa watu dhidi ya uhasama.kwamfano mabiraki,kapota,kambale,kibuti na wengine wanajiunga naye.
  • Mbaka lututu anasawishi kapota kumtengenezea vifaa vya vita,na ndipo kapota akaamua kutengeneza mikuki zaidi ya mia moja kwa bure
  • Pia Kibwana ni msawishi .kwa mfano anasawishi wanawake wawili ili kumpasha habari kuhusu mkutano ulioitiwa na kibelu
  • Kibuthi naye msawishi.kwamfano anamsawishi makuha ili kumtobolea kila siri kuhusu mipango ya mfalme kamanzi na liwali wake Kibelu
  • Mwanamke Mabiraki ni msawishi.Anamsawishi makuha na hadi kutekwa nyara na kuchukuliwa hadi kambi za mbaka lututu huko mbali ya kilima.
  • Msabuli ni msawishi.Anamsawishi mwanzira ambaye karibu amuue mvulana kambale anaye mchokoza kwa kumtobolea wazi ukweli.lakini msabuli anapunguza hasira zake mwanzira kwa kumsawishi kwamba kambale ni mtoto.

Kuna maudhui ya Tumaini

  • Mbaka lututu anatumaini kwamba watapata ushindi siku moja.kwa mfano anamuahidi mhunzi kapota kuwa”malipo yako utapewa madaraka katika Baraza la uongozi wa ufalme tutakaouanzisha baada ya kumshinda mfalme na watu wake.
  • Makuha akawa na tumaine ya kuishi tena baada ya kujikuta ameachiliwa huru

Kuna maudhui ya Utengano

  • kuna utengano baina ya Mbokoli na mkewe
  • Mbaka lututu anajitenga na mfalme kamanzi
  • Kibelu anatengana na mfalme na hata jamii nzima
  • Mwanzira anatengana na jamii ya bunyangabo
  • Makuha anatengana na wafuasi wenzake

Kuna maudhui ya Vita

Kuna maudhui ya Migogoro

Kuna maudhui ya usawiri/nafasi/hadhi ya mwanamke.

TAMTHALI ZA USEMI KATIKA RIWAYA YA UHASAMA KILIMANI

Fani ni jumla ya mbinu za kisanaa/lugha ambazo mwandishi anazitumia kuwasilisha ujumbe wake kwa hadhira.

Takriri/mrudio/sauti na milio.

  • Hii ni mbinu ya kurudiarudia neno, kirari, kishazi, au  sentensi kwa ajili ya kusisitiza ujumbe. Kwa mfano.

 Kejeli

  • Ni mbinu ya matumizi ya maneno yenye dharau. Pia, maneno yanayotumiwa yanakera.

      Utohozi.

  • Ni mbinu ya kuswahilisha maneno yasiyo ya Kiswahili yatamkike kama ya Kiswahili, mathalani, mwandishi ametumia mbinu ya utohozi katika UK

      Methali.

  • Ni mbinu ya Sanaa/kifasihi inayotumia mafumbo. Kwa ufupi, methali ni kifungu cha maneno ya hekima yenye maana fiche. Ubora wa hekima hiyo hutegemea muktadha ambako methali hiyo imetumika.

Tanakali sauti

  • Ni tamathali ya semi ambayo ambayo mhusika anauliza swali huku akijua jibu lake . Kwa mfano,

Mseto/ kuchanganya ndimi

  • Ni mbinu ambayo lugha za kigeni zinatumika katika maneno au sentensi za Kiswahili.

       Ushairi.

  • Shairi ni maandishi/wimbo unaoelea wazo/ mawazo au hisia juu ya maisha.
  • Pia, ushairi ni tukio, hali au wazo ambalo linaonyeshwa kwa upangaji mzuri wa maneno. Kwa mfano, kuna matumizi ya shairi yaani,

Nidaa.                                                                         

Ni tamathali ya semi ambayo inaonyesha kushangaa au kushangazwa na jambo fulani.Alama za mshangao zinatumika. Kwa mfano;

  • “Hebu sikiliza! Sikiliza,Kibwana anamwambia kwa sauti ya chini ndugu yake Lukanga.uk1

Taswira/ jazanda

  • Ni mkusanyiko wa picha zinazoundwa na maelezo ya msanii katika kazi yake ya ubunifu.Taswira hujengwa kutokana na matumizi ya tamathali za semi hasa sitiari, na tashbihi.

 Tasfida.

  • Ni tamathali ya semi ambayo kwayo maneno yatumikayo yanapunguza ukali, aibu na kero za msemaji. Pengine, mbinu hii inajumuisha maneno yatoayo heshima. Kwa mfano,

 Tashbihi/ Mishabaha.

  • Ni tamathali ya semi ambayo vitu viwili au zaidi vyenye sifa tofauti hulinganishwa kwa kutumia viunganishi kama vile, mithili ya, kama, kama kwambia ‘mfano wa , fanana na nk..  

Uzungumizi nafsia / uzungumzaji nafsi

  • Ni matumizi ya lugha ambayo mhusika anazungumza peke yake. Kwa mfano,

 Nahau/Semi

  • Ni mafungu ya maneno yenye maana fiche au isiyo wazi ambayo hutumiwa na mwandishi ili kuweka maadili katika matamshi

 Sitiari /istiara

  • Ni mbinu ya kulinganisha vitu viwili au zaidi bila kutumia viunganishi.

 Chuku/udamisi.

  • Ni fani ambayo inatumiwa na mwandishi kutia chumvi katika mazungumzo. 

      Tashihishi/uhaishaji.

  • Ni mbinu ya lugha ambayo kitu kisichokuwa na uhai hupewa sifa za kiumbe mwenye hai.

      Maswali ya balagha.

  • Haya ni maswali yasiyohitaji majibu. Hapa mbusika anaweza kuwa anasema peke yake huku akijiuliza maswali kwa vile hakuna mhusika wa kumjibu.

Alama za dukuduku/mdokezo

  • Ni mbinu ya kifani au kisanaa ambayo kwayo mtu husema baadhi ya maneno na kuacha mengine Hali hii inasababishwa na, kilio, hasira, kicheko, furaha, mchanganyiko na mazungumzo ya simu, hofu, au mtu kukatisha maneno kwa mfano.

 Nyimbo.

  • Ni matumizi ya sauti zenye toni ya mahadhi ama ya juu au chini

 Majazi/ Majina ya Lakabu.

  • Ni upaji wa mhusika jina kulingana na kazi yake, tabia yake, maneno yake, umri wake, mavazi yake pamoja na matendo yake,
  • Jina Bwera lina maana ya umasikini yaani lilitokana na hali dhiki ya umasikini ya maisha ya wenyeji.kwa kilugha cha mandhari ya mwandishi neno bwera hutoka kwa neno ‘Obwera’ yaani umasikini.
  • Jina kapota kwa kilugha cha abasukali ni mtu anayefanya kazi ya uhunzi.
  • Jina kabafu ni mahali walikozikwa waliokuwa na ugonjwa wa ukoma, yaani hawazikwe karibu na watu wengine kulingana na sheria za utamaduni.
  • Jina nyabugando ni sehemu palipo na miti yenye miba iitwayo”emighenge au amaghando”kwa kilugha cha mwandishi.
  • Jina nyakahya, lilitokana na uwindaji wa wanyama kwa mbinu ya kuchimba shimo waliloita”obuhya”kwa kilugha cha wenyeji wa ufalme wa bunyangabo.
  • Jina mwanzira ni mtu aliyezaliwa njiani kulingana na utamaduni wa ufame wa Bunyangabo.
  • Jina musabuli ni mtu anayeokoa kulingana na kilugha cha utamaduni wa Bunyangabo kwamfano msichana mwanzira ndiye aliyeokoa kambale wakati alipozuiwa na muuaji mwanzira.
  • Kapamba ni mtu aliyezaliwa wakati wa mvuno ya pamba.
  • Mukalhu ni jina linalotokana na nyama iliokaushwa ikakauka.mukalhu alikuwa anapenda nyama aina hiyo na jina lake likatokana na tabia hiyo.
  • Makuha ni mtu  mgumu kama mfupa.
  • Mbaka ni mtu mwenye ubishi yaani anaye bishana sana,na hata hakubali kushindwa.

Dhihaka.

  • Ni tamathali ambayo kwayo mtu kwa makusudi husema maneno kumbeza mtu mwingine. Dhihaka ni tofauti kidogo na kejeli kwa sababu maneno ya dhihaka yanasemwa kimzaha.

Taharuki .

  • Ni mbinu ya kumwacha msomaji na hamu au mvuto ya kuendelea kusoma ili ane yanayofuata.

Tanbihi: Ikumbukwe kwamba mwongozo huu haubebi yote namna inavyojitokeza katika mchezo, kwa hivyo inakubidi wewe kama mtumiaji kusoma mchezo kwanza na kasha ukasome mwongozo kukusaidia kuelewa vipengele mbalimbali vinavyopatikana na ambavyo vimeangaliwa hapa ndani. Asante!!!.

9 thoughts on “MWONGOZO WA UHASAMA KILIMANI

Leave a reply to Mwalimu Arigumaho Johnpaul Cancel reply