RIWAYA YA BARAKA ZA MAMA
Riwaya ya Baraka za Mama ni riwaya ilioandikwa na Vicent M. Tweyambe mnamo mwaka wa 2018 nchini Uganda. Riwaya hii inazungumzia juu ya maisha ya kijana mmoja Baraka ambaye anafiwa wazazi wake na kuachwa chini ya ulezi na Ami yake Aitwaye Baguma. Riwaya hii Ina wahusika kadha kama vile Mariamu,Baguma ,Mandela,Twese na Madikizela.
MAUDHUI KATIKA RIWAYA YA BARAKA ZA MAMA
BARAKA
Baraka ni hali ya mtu kupata nafasi au maisha mazuri katika maisha yake .Tunaona Baraka Fulani katika riwaya ya Baraka za mama.
- Mhusika Baraka baada ya kufiwa na mama yake ami yake Baguma anamhadi kumlipia karo kutoka shule la msingi mpaka chuo kikuu. Hatimaya ahadi hiyo ilitimika na Baraka akasoma kozi ya uanasheria.Jambo hili linadhihirisha maudhui ya Baraka.
- Wakati Baraka akiwa basini akielekea kwa ami yake Entebbe wanafika sanga na police wakiwa wasimamisha kwa ajili ya ekisesi [kuwa wengi garini] baada ya kushuka basi hiyo, gari jingine likaja na kuwachukua jambo hili linaonesha Baraka wa husika Fulani waliyopata.
- Katika riwaya ya Baraka za mama, mhusika Baraka anatuelezea namna alivyonusurika miongoni mwa wale wote waliokufa kwa kupata ajali katika barabara ya lami ya Masaka. Hili ilikuwa Baraka ya mhusika Baraka kwa kutokufa miongoni mwa wale wengi.
- Baraka anapata baraka wakati alivyobahatika kupata kazi kwa kampuri ya mhindi Ruviraj group of canpanies.Alikuwa miongoni mwa wale wachache waliopate kazi .hili nayo ni Baraka
- Baraka akiwa kwa nyumba ya mandeta akaishi maisha mayuma lakini siku moja wakasoma gazeti la daily monitor wakapata kazi katika uwanja wa ndege Entebbe. Jambo hili linaonesha Baraka Mandela na Baraka waliyopata katika maisha yao.
- Baraka akiwa anafanya kazi katika uwanja wa ndege wa taifa alisingiziwa kuwa ndiye aliva mlinzi katika kituo cha ndege akatiwa jelani na kushtakiwa lakini kwa bahati nzuri ushahidi ukagunduliwa kuwaami yake ndiye alipanga njema ya kumwua. Rafiki yake madikizela ndiye alimsaidia kulate ushahidi,mwishoni Baraka akaachiwa uhuru
- Baraka baada ya kuachiwana uhuru kutoka jela akapata bahati nzuri na kuolewana na msichana madikizela aliyekuwa anatamani kwa muda mrefu ,wakazaa watoto watatu yaani, makeba , kimathi, na kambarage. Jambo hili linaonyesha Baraka ali yopatamhisika Baraka.
- Katika riwaya hii tunaona kabla mamake Baraka kufa,anamtakia mtoto wake Baraka za mama. Tunamwona akiwa hospitali mulago anamwambia mtoto wake kujitegemea. Maneno hayo mamake Baraka aliyomwambia yanaonyesha maudhui na Baraka alizompatia mwana wake na mwishowe akazipata . Mandelea naye akapata Baraka wakati anapopata kazi katika uwanja wa ndege Entebbe .alikuwa katika wachache waliopata kazi baada ya muda mrefu bila kuwa kazi.
- Watoto wa Baguma nao ni wenye Baraka kwa mfano baada ya kusoma wote wakapata kazi nzuri. Mfano Tom ali kuwa anafanyia benki kuu ya taifa, Nobel ali kuwa rubani wa kampuni ya ndege nchini Rwanda.
UVUMILIVU
- Baraka anavumilia maisha magumu ya chuo kikuu wakati alipokuwa akisoma. Hata hivyo, anavumilia hali ngumu ya kazi katika kampuni ya mhindi.
- Mamake Baraka mariam alivumilia maisha maguma aliishi baada ya kufukuzwa kutoka kwa nyumba ya mama Baraka alifukuzwa nyumbani akiwa mjamzito. Alihamia katika kibandakatika kituo cha biashara Rutoma maisha yalikuwa maguma kabisa.
- Baraka alivumilia maisha ya bila kazi katika nyumba ya ami wake Baguma akifanyau kazi za nyumbani kwa muda mrefu kabla aliumua kuhamia kwa rafiki yake Mandela.
- Jack anaonasha uvumilivu wakati aliposubiri Rose aliyeonda ngambo hadi akarudi nyumbani baada ya Rose kurudi nyumbani , akapendana na Jack na mwishoni wakaolewanau” mvumilivu hula mbivu”
Elimu
- Madikizela alisomea chuo kikuu cha makerere alisoma kazi ya uwekili
- Baraka alisoma hadi Chuo Kikuu .
- Katika riwaya kuna mhusika Daktari msomali ambaye anadhihirisha elimu
- Watoto wake Baguma ami yake Baraka wanakizungumza kingereza kwe upesi wa samaki kuogelea majini kuchanganya ndime me playa football good [uk 6] baraka anafunga sentensi ya kingereza alikuwa na binamu zake.
MABADILIKO
- Baguma aliyekuwa waziri wa biashara na Mbunge aligeuka kuwa mnyonge baada ya kugunduliwa kuwa ndiye mlizi wa kituo cha ndege. Alishatikuwa kufungwa maisha hata na mali yake yote ikichukuliwa na serikali
- Baraka anabadilika kutoka kwa umaskini na kuwa tajiri baada ya kupata kazi katika kituo cha ndege Entebbe, alimaliza muda mrefu akiwa maskini
HAKI Vs MAOVU
- Katika sura ya kwanza, tunamuona dereva wa basi anafanya maovu kwa kujariba kumpa afande wa polisi kitu kidogo baada ya kukamatwa na ekisesi barabarani
- Pia afande wa polisi alifanya haki wakati alipokutaa bahasha ya kitu kidogo kutoka kwa derevu
- Katika sura ya pili tunaona majambazi wananyakuo bidhaa za wafanya biashara lakini tunaona askari polisi walikuwa tuu hapo wakikodolea macho sinema hiyo .hawakufanya lolote kuwasaidia wafanya biashara waliopokonywa mali yao
UMASKINI
- Tunamwona mzee basini alieleza kwamba hajapona kikohozi kwa kukosa pesa za matibabu
- Baada ya mamake Baraka kufukuzwa katika jumba lake, aliisha maisha mabaya ya umaskini . Tunafahamishwa kuwa aliisha katika kibanda kilichoezekwa na nyansi na hata alikuwa anafanya kazi za salubu kwa shemeji yake baguma,
- Pia tunaona shule ambaya Baraka alikopelekwa ilikuwa ya maskini kwasababu tunaambiwa kuwa majengo yaliyoezekwa kwa nyasi na hata ndani. vumbi lilijaa tele
- Pia tunaona Baraka akivaa viatu vya plastiki shuleni vilivyojulikana kama bagagawale. Hata na sare yake ilikuwa mararuraru ya rangi takasiri kama tausi. Mararuraru yalikuwa ni vipande vya nguo za gomesi ya mamake alizowahi kumiliki .huu unaoyesha umaskini kabisa.
UTAJIRI
- Watoto wa ami Baguma wana vaa jozi za viatukwakila shughuli.
- Watoto wa baguma wanakula vyakula vizuri kama soseji na gorilozi
- Ami yake Baraka aitwaye Baguma ni mtajiri yaani ana aina mbalimbali za gari kama tax ,BMW na Benz.
- Pia na mzee Omoro babake madikizela ni mtajiri kwani ni mbunge wa jimbo Fulani
KUKATAA TAMAA
- Mzee basini aliyekuwa na ugonjwa wa kikohozi alikataa tamaa kwa kutembelea hospitali za umaa na kuambiwa nenda rudi .
HURUMA
- Tunamwona Afande Karimu alimhurumia Baraka wakati alikuwa katika kituo cha polisi kwa ajili ya kukosa njia . Afande Karimu alimsaidia kumtoa kwa utata wa Afande matata na hata akamsaidia kwa kumpigia simu ami yake Baguma ili amuelekeze .Anamsindikiza mpaka kituo cha teksi za kuelekea Entebbe ami yake Baguma anapoishi.
- Baada ya Baraka kuibiwa pesa zake,kondakta anamhurumia na kumsamehe kutolipa pesa za teksi au nauli .
- Daktari msamari anahurumia mamake Baraka kwa kumhudumia na kumwosha vindonda wakati alipokuwa akilazwa hospitalini mulago .
WIZI
- Tunaona majambazi wakinyankua mali ya wafanya biashara .
- Pesa za Baraka kuibwa lakini hajui ni nani aliyeziiba.
KIFO/MAUTI
- Mamake Baraka anakufa baada ya kuugua na ugonjwa wa saratani wakati Baraka alipokuwa na miaka kumi.
- Tweshe mke wa Baguma alijitia kitanza baada ya maisha kumwendea kombo.
- Hata mlinzi wa kituo cha ndege aliuawa na walinzi wenziwe wakiamrishwa na Baguma ili wamsingizie Baraka kuwa ndiye muaji.lakini baadaye ukweli mtupu ukajitokeza.
MAPENZI
- Baraka anapendana na mamake baada na hata kabla ya kufariki dunia. Baraka anasema hivi riwayani“ingawa uko huko kusikofikika wala kuonekana najua wanipenda mama—-
- Kuna mapenzi ya Jack kwa Rose.
- Kuna mapenzi ya Baraka kwa madikizela.
DINI
- Kuna dini ya uisilamu, kwamfano tunaambiwa kuwa shelk mstafa anaongoza waisilamu katika msikiti
UNYAKUZI
- Familia ikiongozwa na Baguma wakanyakua kila kitu cha mamake baraka baada ya mke huyu maimuna kufiwa mumewe.
UNYANYASAJI
- Wafanyakazi wa kampuni ya Ruviraj group of company wananyanyaswa na wanyapara wa mhindi vibaya kwa kutowalipa pesa zao yaani mishahara na hata baadaye wakafukuzwa kazini.
- Bamtindi mumewe Kinaya na akanyanyaswa na shangazi yake Baraka kwa kupigwa vibaya na hata baadaye kumvunja mkono.
- Afande matata anamnyanyasa Baraka kwa kumuliza maswali magumu na hata kumtishatisha kwa maneno ya ukali.Hata hivyo hakumsaidai kama baraka alivyotarajia badala akamufumanisha.
MIGOMO
- Tunaona madaktari wa hospitali wakigoma kwa kutofanya kazi kwa sababu ya serikali kutolipa mishahara yao.
MILA NA DESTURI
- Baraka anatuambia kwamba katika ukoo wa babake, kumzaa mtoto wa kiume ilikuwa nyota ya Jaha. Mtoto wa kiume alithaminiwa sana, hata hivyo mwanamke angezaa watoto wa kike tuu, alionekana kama mtu aliyelaaniwa.
UFISADI
- Sekritari mmoja wa kampuni ya Umma alimuomba baraka atoe rushwa ya shilingi milioni moja ili amsaidie kuajiriwa na kampuni hiyo.uk84
USHIRIKINA
- Babu wa Baraka mzee kalekezi alikuwa mshirikina aliyemwamini mungu wake nyabingi.Huyu alikuwa kifaruzimwizimwi aliyeaminiwa sana na babu yake kuwa mkuu wa miungu yake yote
- Tunamwona Tweshe mkewe Baguma anauza nyumba ili apate pesa kuwaendea miungu kwa ajiri ya kumwokoa mumewe aliyefungwa maishani.
UNAFIKI
- Baguma ami yake Baraka alimpangia njama mpwa wake [Baraka] kuwa aliva mlinzi wa kituo cha ndege . Baraka akafungwa kuwa jelani lakini baada ya ukweli. Ukafichuliwa kuwa Baguma mwengewe ndiyo alikuwa muaji.
UTABIRI
- Kwa mfano mama baraka yaani maimuna kumuita mtoto wake baraka na badaye tunaona akipata baraka maishani
URAFIKI
- Baraka ni rafikiye Okocha.Wakapendana wakati wanapokuwa chuo kikuu wakisoma.
- Pia baraka na Mandela ni marafiki , wanafanya kazi pamoja kwa kampuni ya mhindi ya ruviraji group of companies .
- Pia baraka na kiplimo masool wana urafiki wa dhati. Walisoma pamoja wakiwa shule ya msingi baraka anampelekea kipade cha mkate kila asubuhi
- Baraka anapelekea na madikizela. Hawa wawili walianza kuwa marafiki wa dhati kabla ya kuolewana.
SIFA ZA WAHUSIKA
- Afande karimu.
- Ni mwenye huruma alihumia Baraka kwa kumsaidia katika kitou cha polisi ,Alipiga simu ami yake Baguma na baadaye akamelekeza Entebbe
Baraka
- Ni mhusika mkuu
- Ni mwenye mapenzi ya dhati .Alipendana na marafiki wake kama madiiikizela / mke wake kiplimo masool okocho Mandela .
- Ni mvumilivu . Alivumilia maisha magumu katika chuo kikuu na hati alivumilia hali ngumu kazini kwa kampuni ya mhindi mwaka nzima .
- Ni msomi .Alisoma kutoka shule ya msingi hadi chuo kikuu na kusoma kozi ya uanasheria .
Magezi
- Ni mbumbumbu masomoni. Tunaambiwa kuwa hakuwezi kupata sita na kuigawi mbilina kupata jibu hata katika milihani angoweza kunakili kazi za wengine na hata jina.
Okocha
- Ni mjanja na mwenge akili darasa.
- Hata tunaambiwa namna alivyokuwa wembemasomoni.
- Ni Malaya/msherati.Alipenda marinda kiasi kwamba hata rinda lingefungwa mtini angeukimbilia mti huo .Anaenda kuwapeleka violosho vilabuni kunywa Pomb ya kienyeji ilioywewana wanywaji huko wakizingira chombo chenye kinywaji huko waki kifyonza kwa miriji mirefu .
- Nimpenda michezo ya sulubu kama vile mchezo kamari .anap0teza pesangingi sana hata na pesa za kara .shilingi million tatu za karo
- Ni mwenye maradhi kwamfano ni mgonjwa wa ukimwi .Aligundua baada ya kupimwa damu hospitalini,
Baguma
- Ni muaji kwani anapanga njama ya kuwua mlinzi wa kituo cha ndege huko akisinzia ya kwamba baraka ndiye muaji.
- Ni mnafiki kwani anageukia mupwa wake baraka baada ya kushi naye muda mrefu .
- Ni mdanganyifu Alimdanganya Baraka kwamba atamtafutilia kazi na baadaye akamsaliti.
- Ni mtenda maovu kwamfano kula rushwa,kuangamiza Baraka na kuua mlinzi wa kampuni.
- Ni mtajiri yaani ana magari,Zaidi ya moja na hatan alikuwa waziri wa biashara
Madikizela
- Ni mwenye mapenzi wadhati .Anapendana na Baraka na wakaona na kuzaa watoto.
- Ni mwanasheria.
- Ni mwenye huruma . Alionyesha huruma wakati alipopigania Baraka alipofungwa jelani.
- Ni mpenda haki wa chuo kikuu wakati waliodhulumiwa na baada ya wahadhiri wa kiume waliowataka kimapenzi ili wapiti mitihani ya kozi zao.
- Ni shujaa. Madikizela aliwashinda wavulana wote katika kampeni na kuwa kiranja mkuu wa shule yake Alikwangura ushindi dhidi ya mafahari alioshinolana nao.
KINAYA
- Baraka alikuwa anafikiri kwamba kila kitu jijini ni cha bure kama kijijini kwao lakini hiki ni kinyume na vile anavyofikiri kwasababu kila kitu jijini kinategomoa pesa uk.
KONDAKTA
- Ni mwenye huruma . Alihurumia baraka kwa kumsamehe kulipa pesa za teksi baada ya kugundua kuwa ameibiwa pesa zake.
Maafisi wa Trafiki
- Ni mkweli na haki alionyasha ukweli na haki baada ya kukataa bahasha ya pesa aliyopewa na dereva wa basi kwa kupakia ekisesi.
Afande Matata
- Ni mwenye matata kama jina lake, Alionyeshaukali na matatizo kwa Baraka alipokuwa kwa kituo cha polisi .Alimwuliza maswali makali.
Daktari Msamari.
- Ni mwenye huruma, Alimhurumia mamake Baraka alipokuwa akilazwa hospitalini mulago.
- Alimhurumia mamake Baraka kama mtoto wake
- Aliviosha vidonda vyake bila kuona karahe.
Mwalimu Mpamire
- Ni mkali sana, Alimpiga mwanafunzi magezi kwa kuuliza swali la kibwege.
Sheik Mustafa
- Ni mkali na mnyanyasaji. Alimuharaza mtoto wake kiplimo masool kwa baraka thelathini tumboni na kuogiza anyimwe chakula kwa siku nne nyongeza kila asubuhi aliamshwa kwa nyongeza ya mikwaju sita ya sheria ya baraka
- Ni mjukumu.Alipiga marufuku ungwaji wa pombe kijijini akitumia korofindo yake aliyopewa na serikali kama chifu wa usalama wa kijijini aliwafunga pingu wachapa maji wote.
Ni mdini. Tunamwona alikuwa anaongozawatu katika msikiti.
Ni mwenye urafiki Alikuwa rafiki ya mamake Baraka anamtembelea nyumbani na hata hospitali akiwa mgonjwa.
MBINU ZA LUGHA
Nahau.
- Tandika viboko uk 3 mwalimu mpamire alimtandika viboko sita , kuangua kichako. Uk 5 , kufa moyo (25) ana kwa ana (uk 32), kukaza kisabuni (uk 32).
Utohozi
- Krismasi ekisesi (uk10) mkuu wa polisi aligoka baada ya kuangalia basini ,sitetiment (uk10) anko sista (uk18) Baraka anaeleza namna mwanamke mfanya biashara aliwashawisha wateja kununua mikoba, oparesheni (uk44),Hapo ndipo Daktari alimwambia baraka kuwa mamake anahitaji oparesheni.
Maswali ya Balagha
- Huo ni ukweli? (uk7) Baraka anajuiliza baada ya kuambiwa kwamba mamna ya saseji nigina ya gari.
- Nao hawa kifo uhawaogofuga kweli? Wao hawaonaje maskini? (uk15)
- Sasa nifanyeje? Baraka anajiuliza baada ya kukosa anwani ya kumelekea kwa ami yake baguma
- Tangu lini kula chamcha kuchukua muda huu wote? (45) Sheik Mustafa akijiuliza baada mkurungezi wa hospitali kutoa ripoti kuwa daktari alienda kupata chamcha
Jazanda
- Hii ni mbinu ya kuficha maneno yenye aibu na kutumia maneno yasio na aibu ktk jamii kmf kwenda uani kusukuma jiwe , kuchimba dawa , piga risaasi baada ya kuisema kuenda chooni kunya .
Methali
- Majuto ni majukuu( uk22) ,jogoo wa shamba hawiki mjini (uk7) mungu ni mwenye kudra (uk28) kuishi kwingi ni kuona mengi (uk29) ahambo chema ni baraka ya mvuvi (uk32), Ahadi ni deni (uk54) mvumilivu hula mbivu (uk56), mwenye macho haambiwi tazama (uk70) Tamaa mbele, mauti nyuma (uk82), penye nia pana njia (uk121).
Tashibihi
- Watoto wakiporomosha kingereza mithilia ya wazungumzaji wazaliwa (uk7)
- Kubanana basini kama magunia ya mafaka yaliyo kuwa yakisafirishwa sokoni
- Uvundo uliomtoka kinywani ulikuwa mithilia ya yai viza.
- Wafanya biashara wote walitawanyika kamawa kundi la panya lililongiliwa na paka
- Nilingia huku nikutetemeka kama mgonjwa wa homa ya matumbo (uk23)
- Mkali kama pilipili (uk35).
Kuchanganya Ndimi
- Stop police chauk (uk9)under a rrest please (uk10) afija wa polisi alitoa amii This is terrible my friend (uk10) Afanda wa polisi akalalamika kwa ekisesi , city Authority (uk19) watu walinyankua bidhaa za mwanamke walikwa wanavaa ngowo za manjano zilizokuwa zimeandikwa city Authourity mgongoni , city boys (uk27) jina la teksi Baraka alisafiria kuelekea Entebbe , Radio therapy , break down (uk44) please my friend don’t dare (uk76).
Tamathali za Sauti
- Tulia tuli (uk29) nyeupe pepepe kama theluji (uk10) sare za maafisa wapolisi zilikuwa ujeupe, kiza totoro (uk 23) wakwti Baraka alipoingia kituo cha polisi.
Kuboroga Sarufi
- Huyu basi inaruhusiwa kubeba wantu Baraka hasmini lakini wewe maweka wantu mingi sana (uk10)
- Sarufi iliborogwa katika barua Mandela aliyoandikia Baraka (uk72)
Kinaya
- Afisa wa polisi kukataa bahasha aliyopewa na dereva ili asunurike lakini afisa polisi alikataa .Alisemahivi “my friend mimi ni afande wa gavumenti”
- Baraka anasema wengi walidhani mamake.hakuwa na pesa za kuyakimu maisha yao wawili lakini ilikuwa tofauti kwake kwa vile alisitahidi kuyamudu mahitaji yake yote (uk32)
Wimbo
- Kuna wale wale walishabarikiwana mungu wale——-(uk15)
- Kutia chumvi macho mekundu zaidi ya damu (uk50)
Takriri
- Mikoba. Mikoba mikoba (uk18) liponi liponi liponi (uk27) .
Kuweka chumvi
- Maneno ya kumtua nyoka pangoni (uk17) chumvi, macho mekundu zaidi ya dama (uk50)
Ulinganishaji
- Baraka alipofika ktk kituo cha polisi alimsalimu afande wakati alipokuwa na hafu akitetemeka kama mwanafunzi mbele ya mwalimu.
- Mwandishi analinganisha Okocha na Sungura kwa ujanja wake na akili.
- Okocha alikuwa wembe masomoni (uk79) mwandishi alinganisha okocha na wembe kwa ukali wake na akili ktk masomo
Mbinu Rejeshi
- Baraka anakumbuka siku mamake alimwaga hospitalini mulago anadeza hali yote yalikuwa ktk hospitalini (uk30)
Kimajazi
- Afande Matata .Alipewa jina matata kwa kuwa na matata kmf alimtatiza Baraka ktk kituo cha polisi .
- Afande Karimu alipewa jina karimu kwa ukurimu wate kwani alimsaidia Baraka ktk kituo cha polisi (uk25)
- Mhusika mashamba anaitwa jina la mashamba kwaungwa, matikitimaji
Barua.
- Kuna barua ambazo Jack alikuwa amandika Rose Barua zilikuwa za mapenzi
- Mandela aliandikia Baraka barua alipokuwa shuleni (uk71).
Tanbihi: Ikumbukwe kwamba mwongozo huu haubebi yote namna inavyojitokeza katika mchezo, kwahivyo inakubidi wewe kama mtumiaji kusoma mchezo kwanza na kasha ukasome mwongozo kukusaidia kuelewa vipengele mbalimbali vinavyopatikana na ambavyo vimeangaliwa hapa ndani. Asante!!!

kazi unayofanyia ulimwengu, Mwenyezi Mungu-mwumbaji wa dunia, ataikufanyia hata na mbinguni.
Fikiri kwamba, Mtenda jamala, hulipwa jamala.
LikeLike
Asante kaka
LikeLike
Asante kaka yangu
LikeLike
Mwalimu kabambe ndivyo apashwavyo kufanya. Endelea na kazi hiyo bora.
LikeLiked by 1 person
Asante mwenazangu . Tuendelee Kuomba Mungu atuwezeshe
LikeLike
Safi
LikeLike