HADITHI YA BABU MAMLAKA NCHINI UGANDA-MAJONZI😭😭

Eweee! Mshutuko wa sauti kama za mfalme wa shambani zikasikika eneo la kamwokya karibu kitante mjini kampala.

Furaha tele kama ya wachinjaji kondoo ikawafikia wanafunzi wa shule ya upili Kitante baada ya kujuzwa kuwepo kwa babu mamlaka. Maaskari milango yote ikafunguka. Huku na kule ikawa ni mchezo wa kumtega ili kumnasa wasimsitishe.

Viongozi wa eneo wakawa macho wazi na densi zikachezwa za muziki wa kisasa wakimungoja babu mamlaka na mzigo aliouleta kutoka miongo ya kitambo.

Basi mazingira yakatulia tulii Kama maji mtungini.

Hakuna ndege aliyekuwa akiruka mara babu mamlaka alipoanza msafara.
Mara msafara wa babu mamlaka ukiongozwa na gari la polisi ukakaribia mwendo wa kasi huku wanajeshi wa UPDF na polisi wakikimbilia karibu na gari la Babu mamlaka mwendo dhidi wa duma.

Baada ya muda, babu mamlaka mgeni kabambe kawasili huku akiongozwa na wanahabari wa NBS, NTV-Uganda, BBS-TELEFAYINA, BABA TV-OBUSOGA BURAIRE pamoja na vyombo vingiine ili kushika habari ya siku ya kimataifa juu ya usimulizi wa Babu mamlaka.

Babu mamlaka mara alipoingia shuleni, alikaribishwa na mvua kidogo ukinyesha huku kipara kikiwasha kama dhahabu nywele za kati zikiendelea kunyooshwa na mvua. Ilikuwa siku yangu ya kwanza kumuona Babu mamlaka akitembea mbele ya uma bila kofia yake inayomzunguka kichwa kizima.

Kofia niliyoambiwa na Babu wa Babu yangu kwamba alipewa na Kemikyenkye ili asiondolewe madarakani hadi kifo chake.

Mara nilipomwona Babu mamlaka bila kofia nikafikiri ndoto yangu imetimizwa na furaha zikanijia matumaini yakawa tu kama muda kuondolewa. Kumbe kilikuwa kinyume chake bila shaka baada ya mvua kunyesha, Babu mamlaka hakusahau kofia yake, Bali Ilikuwa karibu na gari lake.


Bila shaka alitembea mwendo wa kinyonga mwanzo kuelekea jukwani lakini miishio mwendo ukawa kama wa Duma ukiashiria masambulizi ya mji wa Luwero miaka ya 1986.
Jukwani akajitupa basi akawasitisha kuongea kwa kuashiria kidole kinywani huku wengine wakiingia ukumbini.

Kuingia ukumbini ilikuwa dalili kwamba aliyeingia ni mfalme wa nchi kwa vile usalaama ulioshika sehemu zote za jiji la Kampala kuanzia sehemu za Kyengera hadi Mukono ili babu mamlaka asi shambuliwe na maadui wa vyama vya upinzani.

Kuingia ukumbini asiye na pua ndefu alitupiliwa mbali na kuwasili Ilikuwa safari ndefu ya kukaguliwa mwili mzima ili usiingie na milipusho kumwangamiza mfalme wa Uganda Babu mamlaka.


Punde si punde, Safari yake kutoka Ikulu Nakasero ilizimisha mji mzima umeme, magari yakasitishwa kutembea, Askari polisi wakiongozwa na mkubwa Ochola wakajitwanga mji mzima kama siafu.

Jeshi la UPDF la taifa pamoja na kiongozi wao pia wakawa macho wazi bila kusita ili babu mamlaka awasili sehemu za Kamwokya kwa usalaama.


Magari yaliyokuwa yakitoka sehemu za Hoima yakasimamishwa sehemu za Mattugga, yaliyotoka Mbarara hawakupita Mpigi, yaliyotoka Jinja mara walipofika Mukono wakasimamishwa na waliokuwa wanatoka Fortportal hawakuruhusiwa kupita Mityana kwa vile babu mamlaka ana mkutano sehemu za Kamwokya.


Kelele zikapunguka mara moja kwa moja babu Baraka akawasili jukwani huku wote macho kama ya paka usiku wa manane wakitazama bila kusita.


Maswali ya balagha yakimjaza Kijana mwerevu moja huku akijiuliza je, Fulani akikutendea mazuri mabaya yanakusahau?
Wahenga hushikilia kwamba. “ Bora kurekebisha kabla hujakosea” nikisoma vitabuni zamani wakati wa ukoloni mnamo 1894-1962, kijana mwenye balehe aliyetambulika kama Ahmad Bin Ibrahim alimshauri mfalme wa Buganda kuhusu umuhimu wa biashara za nje ya taifa, upatikanaji wa nguo, bunduki na Baruti. Ibrahim pia alianzisha dini ya Uislamu lakini mfalme alitega sana bunduki, Kijana kanena.

Machache tuliyoyatambua kumbe athari za biashara hizo ingekuwa utumwa na kuuza nchi yetu. Mawazo yakamwongoza Mfalme kulenga tu bunduki bila hata kuelewa jinsi ya kuzitumia.

Sasa Bei ya vitu Kama vile sabuni, mafuta, sukari na vinginevyo kupata kimoja unauza ardhi….ukimwona Babu mamlaka hela zote akiweka katika Mambo ya usalama ni kutojali raia Wake. Na unamwona akiongozwa na walioshiba wakati wa uchaguzi wakirusha miamoja miamoja kwa kila mganda ili awapigie kura. Mawazo haya yalimshika Kijana mwerevu lakini hakuwa na ziada isipokuwa kuonja utamu wa pilipili akitabasamu bila kujali ulimi.


Bila shaka yeye Babu mamlaka alitembea mwendo wa kinyonga mwanzo kuelekea jukwani lakini miishio mwendo ukawa kama wa Duma ukiashiria masambulizi ya mji wa Luwero miaka ya 1986.


Jukwani akajitupa basi akawasistisha kuongea kwa kuashiria kidole kinywani huku wengine wakiingia ukumbini. Kuinngia ukumbini ilikuwa dalili kwamba aliyeingia ni mfalme wa nchi kwa vile usalaama ulioshika sehemu zote za jiji la kampala kuanzia sehemu za kyengera hadi Mukono ili babu mamlaka asi shambuliwe na maadui wa vyama vya upinzani.


Safari yake kutoka Ikulu Nakasero ilizimisha mji mzima umeme, magari yakasitishwa kutembea, Askari polisi wakiongozwa na mkubwa Ochola wakajitwanga mji mzima kama siafu. Jeshi la UPDF la taifa pamoja na kiongozi wao pia wakawa macho wazi bila kusita ili babu mamlaka awasili sehemu za kamwokya na usalaama.


Kwa utulivu tuio nao Zaidi ya kupigwa na kufanyishwa kazi za sulubu bila kujali malipo ilimradi chakula tushike.


Sera za kikoloni zililazimisha kuangamia kwa sekta za Kiafrika kwa ujumla na kujenga utegemezi wa bidhaa zilizoagizwa kutoka ulaya.
Kuteswa, kunyanyaswa na kutoridhika kwa Waganda kukazidi lakini tulikuwa watulivu tuli kama maji mtungini.
Mateso ya aina moja au nyngine yaliwachochea raia wa Uganda wakiongozwa na wachache walio na mamlaka mnamo 1962, ili tujitegemee. Lahaula! Ni matope kwenye njia ya malkia hata baada ya uhuru, Uganda ikashikwa na madikteta hadi leo hii.
Hatahivyo, upole na ustamaha wa waganda umekua Zaidi ya kunyakuliwa chakula ulichojitafutia tangu 1986.



Adui mwerevu huanzia ndani.

arigumaho810@gmail.com

8 thoughts on “HADITHI YA BABU MAMLAKA NCHINI UGANDA-MAJONZI😭😭

  1. Hiyo ndiyo Uganda wetu na viongozi wasio jali wapigakura. Hakuna cha kufanya bali utulivu nakumiombea kupumua kwa vipande wala si usalama

    Like

Leave a reply to Quraish nsamba Cancel reply