MWONGOZO WA RIWAYA YA KUFA KUZIKANA.

RIWAYA: KUFA KUZIKANA
MWANDISHI: KEN WALIBORA
MWAKA: 2006


Utangulizi:

Riwaya hii iliandikwa na Ken walibora mwaka wa 2003 na kuchapishwa mara ya kwanza 2006.
Kufa Kuzikana ni hadithi ya urafiki kati ya vijana wawili , Akida na Tim, wanaotoka kwenye makabila yenye uadui. Ni hadithi ya migogoro, mingongano, vikwazo na vizingiti katika uhusiano wao. Je, urafiki wao huo unaweza kuvistahimili vishindo hivyo? Je ni urafiki wa kinafiki au una nguvu ambazo hazishindiki?


Riwaya yenyewe huzungumzia maswala ya kiuhalisia yaani;
Ukabila na utamaduni, maadili na mapenzi, usawa wa kijinsia na uhuru wa mtu binafsi.

Hayo yote hujidhihirishwa na hulka/tawasifu au namna mwandishi alivyochora wahusika wake na kuwapa majukumu mbali mbali.


Dhamira ya mtunzi:

Mtunzi katika Riwaya hii analenga kuonyesha athari mbaya wa ukabila yaani anaonesha ukabila kati ya makundi mawili yaani wakanju na wakorosho wanavyo chukiana, wanavyouana, wanavyotusiana kwamfano katika Uk 26 ambapo Akida na Tim wanapo mtembelea mjombake Tim na kusema eti Hakuna mkanju ana mke mmoja, wakanju wanapenda matanga sijui matanga ya mjomba, sijui matanga ya binamu ……… wataanzahata kuenda matanga ya mbwa na paka…


Hayo yote yajitokeza wakati mjombake Tim anapomwuliza kuwa babake ana wanawake wangapi?
Kweli kweli, ukabila katika nchi ya kiwachema umejenga ghorofa katika mioyo ya wananchi hii na wengi wao waameathiriwa vibaya kama kupoteza nafasi serikali, kupoteza maisha na kuongeza chuki nchini nzima.


Vile vile ; mwandishi yataka kuonyesha urafiki wa dhati au kufa kuzikana ingawa ni wa kabila tofauti tofauti yaani Akida ni mkanju na Tim ni mkorosho lakini wanakutania shuleni na wapendana, nyumbani wanachukiana wanauna katika vita vya kikabila na kwa hivyo, mwandishi anataka kuonyesha dhima ya urafiki hata urafiki wa dhati au wa ukweli ambao unakumbwa na vizingiti au vikwazo mbali mbali lakini wao wakendelea daima dawamu.


Mandhari:

Riwaya hii mandhari yake ni kiafrika hasa hasa nchini Kenya kwani mahali mengi yanayozungumziwa yanahusiana sana kama:- kiwachema, sangura. Vile vile mandhari yake ni ya kiafrika kwani maudhui mengi yanayojengwa yanahusu sana mambo yanayokumba nchi za kiafrika kama;- ukoloni mamboleo, usaliti, ukabila nk.


Pengine: Riwaya hii, kiwakati ni ya kisasa kwani inazungumzia mambo ya kisasa ; elimu, urafiki wa kisasa na mitazamo mipya kuhusu ukabila kulingana na uchoraji na maudhui husika na utendaji wake.
Jalada: Mwandishi ametumia picha mbali mbali yaani wahukika wawili wanonyesha nyuso zenye huzuni na machozi yakitiririka, ishara kuwa kuna mambo ambayo hayaendi vizuri.


Pengine, Jina lake “Ken Walibora” limeandikwa kwa rangi nyekundu ishara kuwa kuna matatizo mengi yanayosheheni riwaya nzima.


Isitoshe, Kwa jalada/gamba lenyewe kuna vibanda ambavyo vimechomeka na moto na kuna mbwa ambaye anatafuna kitu Fulani labda yaweza kuwa mifupa ya watu ambao wananauawa kwa vita vya kikabila.

Yanaendelea…..

10 thoughts on “MWONGOZO WA RIWAYA YA KUFA KUZIKANA.

    1. Riwaya ya Kufa Kuzikana inaweza kuchambuliwa kwa kutumia nadharia kadhaa za fasihi, lakini mojawapo inayoweza kuwa dhahiri ni Nadharia ya Uhalisia (Realism).

      Hii ni kwa sababu mwandishi anaangazia maisha halisi ya jamii, migogoro ya kijamii, na uhalisia wa maisha ya watu wake.

      Pia, Nadharia ya Umaksi inaweza kutumika ikiwa riwaya inachunguza mgawanyiko wa kitabaka na ukandamizaji wa kijamii. Ikiwa una maswali zaidi kuhusu uchambuzi wa nadharia, nieleze!

      Like

  1. Ahsante kabisa mwalimu Kwa kutupatia kazi nzuri hii…Nimependa namna ulivyoiunda pia na kuifupisha. Kama una masomo Kwenye U-tube hebu tafadhali nijulishe.

    Like

Leave a reply to Shillah Nteyera Cancel reply