Mwongozo wa mfalme Edipode-Sofokile:

Johnpaul Arigumaho na Simon T Kawaida @2022

TAMTHILIA: MFALME EDIPODE
MWANDISHI: SOFOKILE
MWAKA: 1969
MFASIRI: SAMUEL S. MUSHI

Utangulizi:


Mchezo huu wa mfalme edipode uliandikwa na sofokile na kuchapishwa mara ya kwanza mwakani (1969).

Lakini imekisiwa kuwa ulitungwa kati ya mwaka 429 na mwaka 420 kabla kristo, na ni mopjawapo wa mfululizo wa hadithi zinazohusiana na ufalme wa Thebe huko Ugiriki.
Mchezo huu ulitafsiriwa katika lugha ya Kiswahili na Samuel S. Mushi na umetoa mchango mkubwa katika fasihi ya Kiswahili.

Ni mchezo wa aina yake wenye muundo wa kishairi na ambao haupangwi kwa maonyesho na vitendo kama ilivyo katika michezo mingine.

Yote yaliyomo hutendeka maskani mwa mfalme Edipode.
Uchambuzi wa kichwa cha mchezo:
Kichwa cha mchezo huu ni “Mfalme Edipode”. Mfalme maana yake ni mtawala mwanamume aliyepata nguvu za utawala kwa njia ya urithi au uwezo mwingine kama vile ushujaa.

Edipode kulingana na mchezo huu, humaanisha ‘miguu iliyovimba’. Kwa hivyo, mchezo huu ukapewa kichwa hicho kulingana na yaliyo mtukia Edipode kwanzia pale anapofungwa miguu mpaka ikapata uvimbe, kupelekwa koronto na kurudi kwake ugiriki.

Kwa kifupi, unayazunguka maisha yake Edipode tangu utotoni mpaka laana yake inapomfika na kufunuliwa kwake mpaka ikasababisha utoboaji wa macho yake kwa mikono yake mwenyewe.


Uchambuzi wa picha ya jalada:
Jalada la mchezo huu wa mfalme Edipode huonyesha kichwa cha mfalme ambacho kimechorwa kwa rangi nyekundu.

Kichwa chenyewe kimetobolewa macho. Kulingana na yaliyomo, picha hii ya jalada huelezea giza analoliishi mfalme edipode kwa kufurahia ndoa na mwili wa mamake bila kujua, kitendo ambacho kinamfanya yeye kujitoboa macho yote mawili kwa kutumia vifungo vya vazi lake dhahabu, ili macho yake yasione tena aibu yake baada ya ukweli kufunuliwa kuwa ndiye najisi muuaji wa Laio babake mfalme wa Thebe na mwoaji wa mama mzazi kama ilivyotabiriwa na Apolo huko Delfi.


Dhamira ya mwandishi/Mtunzi:
Sofokile alidhamiria kuonyesha kuwa la mungu ni la mungu, haliwezi kuepukanwa.

Kupitia tamthilia hii, anaonyesha utabiri kuwa mtoto atazaliwa katika nyimba ya mfalme na kuwa mtoto huyo huyo, atamuua babake na amwoe mamake mzazi. Lakini wazazi wa kitoto hicho baada ya kukizaa, wakahofu kukiua kwa mikono yao na kukipa mchunga wanyama akipeleke msituni huko kitaroni na akitupe huko.

Kwa nguvu za mungu, mchunga wanyama naye vile akakihurumia kitoto na kukipa mchunga mwenzie akipeleke ugaibuni kikulie huko kisije kikarudi ugiriki. Huko alikopelekwa, katiwa kwenye ufalme wa korinto, nguvu ya mungu bado ingali. Mtoto kakuzwa kama mfalme mpaka anaposikia habari kutoka kwa mpita njia mlevi kuwa polibo na merope hawakuwa wazazi wake edipode.

Kwa wasiwasi, edipode kawaendea polibo na merope kuwauliza juu ya yale aliyoyasikia na wao wakamdanganya kuwa ndio wazazi wake halisi. Edipode kaenda kuuliza kwa miungu, na habari alizopata zikamshutua.

Habari zenyewe zikawa zinasema kuwa alizaliwa na laana ya kumuua babake na kumwoa mamake. Kwa hofu nyingi, akakimbia kwao ili aje aepukane na msiba huo huo. Na kukimbilia ugiriki akidhani amekimbia nyumbani bila kujua alikokimbilia ndiko palikuwa nyumbani.

Na mwishowe akamua babake na kumwoa mamake na kuzaa naye wana wawili na mabinti wawili. Kama ilivyotabiriwa, vikatukia na mji wa Thebe kuanza kuambukizwa na maradhi ya tauni na majonzi yakajaa ufalme wote…………

Yanaendelea..,…………. Wafikie wahakiki Arigumaho Johnpaul (+256778514179) na Simon T Kawaida ( +256703 573917)

Johnpaul Arigumaho amefunza katika Shule ya Upili Nyabuhikye, shule ya Upili Bright-Seeta, shule ya Upili-Seeta na kwa Sasa Ni mwalimu wa kiswahili shule ya Upili Uganda martyrs-Namugongo Jijini Kampala.

Simon T Kawaida Ni mwalimu na mbobezi wa lugha na fasihi ya kiswahili nchini Uganda. Amefundisha Kiswahili katika shule kadhaa na Taasisi za kielimu nchini Uganda. Kwa Sasa Ni mwalimu wa shule ya Upili St Lawrence-Kyengera mjini Kampala.

26 thoughts on “Mwongozo wa mfalme Edipode-Sofokile:

  1. Kwa ukweri na uhakiki, unastahili kuwa Mwalimu. Nashukhuru kwa Kazi yako bora. Waswahili ninawahidi kuendeleza kiswahili na kuwavutia wenzetu ili lugha yetu ienezwe nchini kwote. Umoja ni nguvu, utengano no udhaifu.

    Like

  2. Mwongozo húu no sawa kabisa kwa mwanafunzi na mwalimu ambaye hakuielewa kitabu vizuri. Ninakushukuru kwa kazi nzuri

    Like

Leave a reply to Mugisha joseph Cancel reply