MWENENDO FASAHA WA TAALUMA YA UALIMU.
(TEACHER’S PROFESSIONAL CODE OF CONDUCT)
ILANI YA KISHERIA (2012)
LEGAL NOTICE (2012)
SHERIA YA HUDUMA YA ELIMU (2002)
MWENENDO FASAHA WA TAALUMA YA UALIMU.
MPANGILIO WA AYA.
Aya.
SEHEMU YA KWANZA-KURASA ZA AWALI.
Kichwa.
Matumizi.
Ufahamu/ufasiri/uelewa.
SEHEMU YA PILI-WALIMU.
Uanachama wa taaluma ya ualimu.
SEHEMU YA TATU-MWANAFUNZI
Uhusiano na mwanafunzi.
MWENENDO FASAHA NA JUKUMU.
Mwenendo fasaha wa taaluma.
Jukumu la kitaaluma.
SEHEMU YA TANO-MWENENDO WAWALIMU.
Majukumu ya kibinafsi.
Uhusiano na marafiki/workmates.
Uhusiano na wazazi.
Mwalimu na mwajiri.
Mwalimu na jamii.
HUDUMA YA ELIMU (MWENENDO FASAHA WA TAALUMA YA UALIMU)
(Rejelea kifungu 29 cha sheria ya huduma ya elimu 2002)
Kwa mamlaka inayopewa kwa tume ya huduma ya elimu na kifungu 29(1) cha sheria ya huduma ya elimu (2002) taarifa ya kisheria hii imetolewa leo 21 agosti 2012.
SEHEMU YA KWANZA-KURASA ZA AWALI.
Kichwa.
Notisi/ilani hii inaweza ikarejelwa kama mwenendo fasaha wa walimu 2012.
Matumizi.
Taarifa ya kisheria ya ualimu inawalenga wote binadamu katika huduma ya elimu.
Ufahamu.
SEHEMU YA PILI-WALIMU.
Uanachama katika taaluma ya ualimu.
Uanachama katika taaluma ya ualimu utakuwa wazi kwa;
Yeyote ambaye amemaliza kozi ya ualimu inayotambulika na ametunikiwa cheti cha ualimu , yule ambaye jina lake limesajilishwa katika sajili ya walimukwamujibu wa masharti wa sharia ya elimu.
Yeyote ambaye amepewa cheti cha usajili na mkurugenzi wa masomo kama mwalimu.
Yeyote ambaye hatimizi matakwa ya kifungu 1(a) hapo juu yaweza kujiunga na huduma ya elimu ikiwa ametimiza mahitaji ya kupewa kauli ya uhakika na leseni ya kufundisha kwamujibu wa masharti ya sharia ya elimu.
SEHEMU YA TATU-MWANAFUNZI.
Uhusiano na mwanafunzi.
Jukumu kubwa la mwalimu kwa mwanafunzi ni kumhudumia.
Mwalimu anafaa kuelekeza mwanafunzi ili amsaidie kimwili, kiakili, kinafsi/kimoyo, kitabia na kiutu.
Mwalimu anatalajiwa;
Kutoweka ujumbe alioupata kuhusu mwanafunzi unaopokelewa pitia majukumu yake ya daima/kila siku wazi isipokuwa sheria kukiweka wazi au maamuzi ya mwalimu kutegemea maslahi ya mwanafunzi.
Kutambua uhusiano wa kuheshimiana kati ya mwalimu na mwanafunzi na atajiepusha kuuvunja kwa utovu wa nidhamu.
Kutojiingiza na masuala ya kujamiiana, kumuudhi, au kumnyanyasa kimapenzi mwanafunzi wake.
Kumtetea mwanafunzi dhidi ya vikwazo vinavyomkumba katika shughuli zake za kusoma au maadhara kwa afya na usalaama wake.
Kumpa mwanafunzi fursa ya kujipima uwezo wake kwa kumwaangalia kwa makini udhaifu wake.
Kudumisha mzingira mazuri ya kusoma kwa mwanafunzi.
Kujiepusha na kutumia nguvu za wanafunzi kufanya kazi kwa faida ya mwalimu binafsi na;
Kutompa adhabu ya viboko kali au tendo lolote linalompa mwanafunzi maumivu ya kimwili au kusababisha maadhara ya kimwili.
SEHEMU YA NNE-MATENDO HALALI YA KITAALUMA NA MAJUKUMU.
Matendo halali ya kitaaluma.
Mwalimu anatalajiwa;
Kutojitenda kwa namna inayosababisha taaluma na huduma ya elimu kupokea jina baya.
Kuonyesha umahiri wa msingi na ujuzi katika mbinu za kielimu.
Kufundisha kwa uangalifu na bidii, waaminifu na kwa utaratibu.
Kufundisha kwa kufuatia malengo.
Kutotumia fursa ya cheo chake kufundisha nje na matalajio kwa mwanafunzi au kwa malengo yake mahususi au mafundisho ya sharti.
Kuandaa maazimmio ya kazi, mipango ya somo, na vifaa vya kufundishia vingine vile kuendeleza kuhakikisha ufanisi wa kufundisha na kusoma, tena mwalimu atavikabidhi mwalimu mkuu au mkrurugenzi na kwa mkuu wa idara kwa ukaguzi wakati wowote vikihitajika.
Kuweka na kuanda kazi/zoezi za maandiko na vitendo kwa ufanisi wa kufundisha na kusoma , maramoja kusahihisha kazi au zoezi hilo na kueleza maoni na majibu sahihi ya kutosha kwa mwanafunzi.
Kufanya mafundisho ya ziada akiombwa kutimiza.
Kuangalia kwa makini udhibiti na malekezo kuhusu mafundisho ya ziada na maelekezo ya kibinafsi yanayopewa muda kwa muda na mamlaka unaofaa.
Kutojiingiza na shughuli zinazochafusha ubora wa kufundisha kama taaluma.
Kutofundisha kwa kuathiriwa na pombe, au madawa ya kulevya na kutokuja shuleni akiwa amelevya au amepinduliwa na pombe.
Kuandaa mitihani yote ya ndani na nje kwamujibu wa udhibiti unaotakiwa.
Kutojiingiza na vitendo vichafu vya kuiba mitihani kwa wanafunzi.
Kufuatia mpango unaokubaliwa na kupitishwa na mkuu wa idara na atalazimishwa kushirikiana na mkuu wa idara pamoja na walimu wengine kutimiza mpango huo.
Kukubali ukaguzi unaofanywa na mamlaka unaofaa wakati wa kufundisha.
Kutumia mbinu zinzofaa za mawasiliano wakati wa kufundisha kuhakikisha utoaji wa ujumbe.
Kudumisha na kupeleka rekodi za wanafunzi za utendaji kwa uangalifu wa mitihani, shughuli za co-curicula, kumwezesha mwalimu kuripoti kwa usahihi na kishabaha katika kila maendeleo ya mwanafunzi.
Kutumia nafasi ya fursa zote za maendeleo ya kitaaluma kufundisha na mbinu za kisasa za ufundishaji.
Kuhakikisha kuonyesha kiwangogezi chake cha taaluma lakini haruhusiwi kufanya hivyo kwa gharama ya wanafunzi.
Kufundisha mbinu za uraia uzuri maadili mazuri, Amani na jukumu la kijamii.
Kuonyesha akili inayohitajika kama huduma ya kwanza, hatua za usalaama na tahadhari, huduma ya afya ya msingi mazingira na ufahamu wa jinsia na;
Kufanya utafiti wa kimaadili kujulisha na kuboresha taaluma.
Jukumu la kitaaluma;
Mwalimu anatalajiwa;
Kutoa muda wa kutosha kwa majukumu yake kama yanayohitajika na tabia za taaluma yake.
Kutojiingiza na shughuli zake za kibinafsi akiwa anatalajiwa kufundisha, kusimamia kusoma na shughuli nyingine za mitaala.
Kutokuwa rashidi kwa shughuli yeyote ile au kulenga kusababisha usumbufu au uasi shuleni.
Kutodai hongo kutoka kwa wanafunzi au kwa umma ili kutimiza jukumu lake.
Kuandaa na kufundisha masomo yake bila ubaguzi au upendeleo dhidi ya mwanafunzi yeyote yule katika darasa lake kwa kutojali rangi yake, dini, kabila, mahali anapotoka au jinsia na;
Kudumisha na kuhifadhi vizuri rekodi za mali ya shule ndani ya utunzaji wake na anafaa kuelezea jinsi vinavyotumiwa akiombwa na mkuu wa idara, mwalimu mkuu au mkurugenzi.
SEHEMU YA TANO- MWENENDO WA KIBINAFSI WA MWALIMU.
JUKUMU LA KIBINAFSI.
Mwalimu anatalajiwa;
Kuvaa ipasavyo kwa heshima na kuwa maridadi akiwa kwenye jukumu.
Kujitilia mkazo jinsi anavyoonekana kuhakikisha nadhifu na mtazamo mzuri wa kufanya jukumu hata katika jamii.
Kutoandika au kulazimishwa kuandikwa kwa barua yeyote bila utambulisho au nyaraka yeyote ile kwa dhamira ya uhabithi/kuvunja.
Kuwa mfano mwema wa kuigwa shuleni na katika jamii nzima na;
Kuheshimu utawala wa sheria na kuwa mfano chanya /mwema katika utekelezaji wa majukumu ya kiraia kama vile elimu ya kingono, ndoa na uzazi.
UHUSIANO NA WENZAKE.
Mwalimu anatalajiwa;
Kuheshimu wengine na hisani, kuthamini nguvu za wenzake, kugawana utaalamu na akili kwa kufanya pamoja.
Kutolawama au kudharau walimu wengine au kazi yao kati ya wanafunzi na;
Kutofanya ripoti mbaya kuhusu kazi au matendo ya mwalimu mwengine bila kumjulisha mwalimu huyo namna ulivyoandaa hayo yote.
UHUSIANO NA WAZAZI.
Mwalimu anatalajiwa;
Kuheshimu na kuwa na adabu kwa wazazi.
Kujali mitazamo ya wazazi wakati wa kufanya maamuzi yenye athari juu ya elimu au ustawi wa mwanafunzi.
Kuwasiliana na kushauriana na wazazi kwa namna nzuri na;
Kuamua kufanya tendo sahihi wakati wa kujibu masuala ya wazazi.
MWALIMU NA MWAJIRI.
Mwalimu anatalajiwa;
Kuelewa masharti ya ajira yake na kuziheshimu vilivyo.
Kuomba kazi popote pale penye nafasi wazi ambapo pametangaziwa na tume kupitia njia rasmi za kawaida na hatasawishiwa au turubaiwa kwa uteuzi na;
Kuwajibika kwa mafanikio ya utekelezaji wa mipango na mageuzi ya kielimu.
MWALIMU NA JAMII(JUMUIYA)
Mwalimu anatalajiwa;
Kutetea picha nzuri ya jamii anamotoka kwa kujihusisha na shughuli tofauti za jamii hiyo.
Kuheshimu sheria.
Kuhudhuria kibinafsi iwezekanavyo shughuli za kidini anazozipenda na kuheshimu dini nyingine zinazotambulika wazi shuleni anapofundisha.
Kuwa mfano mzuri kwa jamii na shule kwa ujumla .
Kuhamasisha /tia moyo wazazi na kufanya pamoja na jamii kuhakikisha kuwezesha watoto katika jamii kupata kuhusika na kumaliza masomo na;
Kujihusisha/kuhusika katika mitandao na ushirikiano wote rasmi na yasiyo rasmi ambayo inalenga kwa kutimiza mtaala na ustawi wa wanafunzi.
SEHEMU YA SITA-MWALIMU MKUU AU MKURUGENZI.
Mwalimu mkuu au mkurugenzi.
Mwalimu mkuu au mkurugenzi anafaa kufanya matendo yanayofaa na atakuwa mfano mzuri katika maadhimisho makali ya matakwaya code hii.
Mwalimu mkuu au mkurugenzi atalazimishwa kuheshimu maadhimisho ya mwenendo wa walimu unaofaa na walimu wote kwamujibu wa udhibiti na masharti kwa kurejelea huduma ya elimu na ataadhibiwa maramoja na ukiukaji wa mwenendo huo.
Mwalimu mkuu au mkurugenzi anatalajiwa;
Kuwa mlinzi wa kiwango kikubwa cha elimu katika shule lake na atadhamiria kiwango kikubwa cha elimu.
Kusajilisha na kukubali wanafunzi kuingia shule bila ubaguzi na kwamujibu wa udhibiti na masharti ya sharia zinzoongoza Uganda.
Kukusanya na kupokea madai ya shule, zawadi, michango na tunu (majaaliwa)
Kupangia hela zote na mali zinazokusanywa kwa niaba ya shule.
Kutekeleza sera zinazotolewa muda kwa muda na mamlaka husika inayoaminiwa.
Kuweka rekodi za shule zote chini ya ulinzi wake katika hali ya usalaama na kuhakikisha kuwa rekodi zote zinabeba ujumbe sahihi.
Kukataa mahusiano na waajiriwa wengine yanayoletea mtu kutenda kinyume na sharia au tendo lolote ambalo laweza likachafusha taaluma ndani nan je ya shule.
Kutokubali hongo ili kutimiza wajibu au majukumu yake.
Kuhakikisha kwa uhalisia na usahihi unaheshimiwa na walimu wote pamoja na wanafunzi.
Kuripoti kwa usahihi na kwa kufuatia malengo rasmi waajiriwa wengine kuhusu masuala yahusuyo utendaji wa kila mwaka, ripoti za tathimini au wakati wa kupima uwezo wa mwalimu katika kazi aliyoiomba au wakati wa kuripoti uvunjaji kanuni wowote au udhibiti unaotolewa muda kwa muda na mamlaka inayofaa.
Kuripoti wa usahihi na kwa kufuatilia malengo kuhusu masuala ya wanafunzi bila kuogopa, upendeleo/fadhila,, upendeleo au ubaguzi.
Kutoshughulikia biashara yeyote ya kibinafsi ndani au nje ya shule wakati wa muda rasmi wa jukumu.
Kutoadhibu mwalimu anayehusika katika uvunjaji/ukiukaji kanuni kwa kutumia nguvu.
Kuhudhuria shuleni kwa kiasi kikubwa iwezekanavyo, na wakati wowote akiwa nje ya shule ataacha nyuma ujumbe kuhusu kutokuwepo kwake na naibu wake au mtu mwingine yeyote anaye kwa mamlaka anafanyia katika nafasi yake.
Kuhakikisha kuwa walimu na wanafunzi wawepo na fursa ya kuwasiliana na mwalimu mkuu au mkurugenzi na wamfikie ili kusikilizwa malalamiko yao.
Kushabika maendeleo na ushiriki wa wanafunzi katika shughuli za mtaala za ziada zinazofaa.
Kuhakikisha kwamba mageuzi ya serikali na mipango yanatekelezwa.
SEHEMU YA SABA-UTEKELEZAJI WA MWENENDO UAOFAA WA TAALUMA YA UALIMU.
Mwenendo unaofaa wa taaluma ya ualimu.
Ni jukumu la kila mwalimu kuheshimu na kutilia mkazo sheria na kanuni za mwenendo wa taaluma ya ualimu hii; na kuripoti ukiukaji wowote kwa mamlaka unaofaa.
Masuala yote yahusuyo ukiukaji wa kanuni hii yataripotiwa kwenye tume na yataangaliwa kwamujibu wa sheria ya huduma ya elimu (2012)
Masuala yote yanayoangaliwa na mamlaka inayofaa yatapelekwa kwa uagalifu na hayatatambuliwa kwa uwazi kwa watu wasio na mamlaka.
Walimu wanaokiuka kanuni/sheria watatozwa kimaalum katika Uganda public service standing orders na adhibu za wakiukaji nidhama katika udhibiti wa tume ya huduma ya elimu na maelekezo ya utawala yanayotolewa muda kwa muda muda.
Adhabu zifuatazo zitaadhibiwa na mkiukaji kanuni hii;
Maonyo au kukemewa(reprimanded)
Kusimamishwa kuongezewa mshahara kwa muda Fulani.
Kuzuiwa uongezo au kukomeshwa kwa muda Fulani.
Kukomeshwa maongezo.
Kubebeshwa au kufidia.
Kupunguziwa cheo au daraja.
Kufukuzwa kutoka huduma kwa maslahi ya umma.
Kufukuzwa kirasmi.

Reblogged this on Jifunze kiswahili na mwalimu Johnpaul Arigumaho and commented:
Good
LikeLike