Ikiwa unapanga safari kwenda Afrika Mashariki, fikiria kujifunza maneno ya kiswahili ili kuweza kuzungumza na watu unaokutana nao kwa lugha yao wenyewe huenda mbali kuziba pengo la kitamaduni. Ukiwa na tajriba inayofaa, utapata kuwa watu ni marafiki zaidi na wanasaidia sana kila uendako.
Nani Anazungumza Kiswahili?
Kiswahili ni lugha inayozungumzwa sana katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, na hufanya kama lugha ya kawaida kwa watu wengi wa Afrika Mashariki (ingawa sio lazima kuwa ndio lugha yao ya kwanza). Nchini Kenya na Tanzania, Kiswahili ni lugha rasmi pamoja na Kiingereza, na watoto wa shule za msingi kawaida hufundishwa kwa Kiswahili. Waganda wengi wanaelewa Kiswahili tena kwa sasa kimewekwa kama somo la lazima kwenye mtaala mpya wa madarasa ya chini ya sekondari yaani kidato cha kwanza na cha pili, ingawa ni nadra kuzungumzwa nje ya mji mkuu, Kampala. lakini wengine husema wanyankore waishio magharibi mwa nchi uganda ndio wamekibeba kiswahili hadi hapa kilipo. Lugha rasmi ya Visiwa vya Comoro mara nyingi huainishwa kama lahaja ya Kiswahili.
HISTORIA FUPI YA KISWAHILI NCHINI UGANDA Kiswahili ni lugha ya asili iliyotokea katika pwani ya Kenya. Katika karne ya 20 kiswahili kilikuwa kimeishaimarika na kukubariwa nchini Kenya na Tanzania lakini Uganda kilikuwa bado hakijaenea. Kiswahili kilifanya majukumu mengi katika ya nchi hizo mbili Kenya na Tanzania.
Kifursa, kutumika kwa lugha ya Kiswahili katika vita vya guerrilla kati ya wanajeshi wa NRA Walioongozwa na Museveni na wale wa rais Obote ndicho kilichokipa Kiswahili fadhila katika macho ya viongozi wa NRM. Hatimaye kikapewa kipaumbele kutumika katika makundi ya wanajeshi baada ya rais Museveni kupata uongozi. (tafsiri yangu) Whiteley (1969) anaripoti kuwa Kiswahili kiliendelea kutumiwa na polisi, sehemu za Kaskazini kuwasiliana na watu ambao hawajui Kiingereza na Luganda. Vilevile Wanilotiki wa Uganda walitumia sana Kiswahili kuwasiliana na makabila mengine. Kiswahili kilitumika pia kwenye mipira, na sehemu nyingine ambazo Kiingereza na Luganda havikuhitajika au havikuwezekana kutumika. Kulingana na Mukama (1995) kabaka mutesa 1 ambaye alikuwa anaongoza wakati huo alikuwa anapenda lugha. Kama ndilolililokuwa la muhimu siku hizo Kiswahili kilikuwa kimeishaenea katika maeneo mengi ya afrika mashariki pamoja na Afrika Ya kati juu ya biashara. Wakati wamisionari walipofika Uganda kama H.m stanely (1864) Kiswahili kilianza kuenea juu ya kusambazwa kwa injili lakini baada yao kujifunza lugha nyingiine Kiswahili kikabaki nyuma.
Whiteley (1969) anaripoti kuwa Kiswahili kiliendelea kutumiwa na polisi, sehemu za Kaskazini kuwasiliana na watu ambao hawajui Kiingereza na Luganda. Vilevile Wanilotiki wa Uganda walitumia sana Kiswahili kuwasiliana na makabila mengine. Kiswahili kilitumika pia kwenye mipira, na sehemu nyingine ambazo Kiingereza na Luganda havikuhitajika au havikuwezekana kutumika. Kingine, kuja kwa wote wasome ya shule za msingi (UPE), serikali inalaumiwa kwamba wote wanaoacha kusoma shuleni ni kwa ajili ya kutojua kingereza katika shule za misingi (1981, December 2oo4).Hata hivyo, kwa urahisi wanaweza wakazungmza katika Kiswahili. Kiswahili ni lugha inayotumiwa katika vyombo vya habari. Sasa hizi televiseni ambazo zinakuja zinaendelea kutumia Kiswahili kamaRadio FM OPG, Mbale FM,Uganda Radio zinachangia katika kukuza Kiswahili katika nchi nzima ya Uganda. Hata hivyo Uganda inakaribia kuanzisha magazeti yanayotumia Kiswahili. Hivi vyote vitasaidia katika kuelimisha watu na kuwaangazia kuhusu masuala yanayowakabili. Mfano thabiti ni kwamba wakati ugonjwa wa ebola ilipokuwa inasambaa katika Uganda ya kaskazini, wakati huo Kiswahili kilikuwa kinatumika kuelimisha watu kuhusu jinsi ya kujiokoa na kuelewa usafi wa watu binafsi.
Katika siasa, wanajeshi wanatumia Kiswahili kuendeleza umoja na kukomesha ukabila. Katika Uganda ya kaskazini, Kiswahili ndiyo lugha inayotumiwa kupigania uhalifu na ukosefu wa usalama inayoletwa na uasi. Kupitia njia hiyo, Kiswahili ni kifaa cha kuleta umoja wa makabila inayotamaniwa leo. Sasa, wanasiasa wanaowakilisha Uganda katika bunge la afrika masahriki wanatumia lugha ya Kiswahili. Hata nyumbani, wagombea viti vya ubunge kutoka kaskazini, mashariki, na magharibi wanatumia lugha ya Kiswahili katika kampeni zao. Juu ya yote, mbio uraisi haiwezi ikakamilika bila wagombezi kutumia Kiswahili. Hii ni maanakwamba hivi karibuni lugha ya Kiswahili itachukua jukumu la kuleta demokrasia kati ya wanaUganda na hatimaye itachukuliwa kiraia kutumika katika elimu kama ilivyo Kenya na Tanzania. Katika biashara, jukumu la Kiswahili la Kiswahili linaweza kukaguliwa. Inabidi kieleweke kwamba lugha hii iliingia Uganda hasa juu ya Biashara na imechangia sana kitaifa na kimataifa. Juu ya hayo yote, lugha hii ni lugha muhimu katika kuleta umoja. Inatumiwa katika thieta na barabarani na wakomedia kubrudisha watu. Nordic Journal of African Studies 15(2): 154–165 (2006) Kiswahili and Its Expanding Roles of Development in East African Cooperation: A Case of Uganda MWENDA MUKUTHURIA Egerton University, Kenya.
MATATIZO YALIKIKUMBA KISWAHILI NCHINI NCHINI UGANDA.
Upotwashwaji wa Kiswahili NCHINI UGANDA hutokea kwa namna kadhaa kwamfano,) MAGANGA anatufahamisha kwamba lugha ya maandishi ya Kiswahili chini uganda ilianza kutumika katika Baraza la Kifalme la Buganda na Bunyoro, hata kabla ya ukoloni (1862). Nchini Uganda Kiswahili kilitumika katika shughuli za biashara, dini na mila. Wakoloni walipofika walikuta lugha hii inatumika, ingawa sio kwa kiwango kikubwa. Wakoloni walikitumia katika maswala ya kiserikali na kidini. Lakini maendeleo ya Kiswahili nchini Uganda yalikuwa duni sana ukilinganisha na Tanganyika na Kenya. Maganga, (1997) anaeleza kuwa Sababu zilizokifanya Kiswahili nchini Uganda kuwa duni sana ukilinganisha na Tanganyika na Kenya ni kama ifuatavyo: (a) Waganda walikiona Kiswahili kwamba ni lugha ya ki-Islamu, na Waislamu ni maadui wa dini ya Kikristo, na kwa hiyo, Waislamu ni maadui wa Wakristo. Hivi ndivyo ilivyoaminika wakati ule huko Uganda.Kwa mantiki hiyo, kukipenda Kiswahili waliona ni kuwakaribisha Waislamu ambao ni maadui wakubwa wa Wakristo, kwani Kiswahili kilimaanisha Uislamu. (b) Katika kufundishia elimu, mkazo zaidi ulikuwa katika matumizi ya Kiingereza na lugha ya Bunganda. Kiswahili kilitumika katika sehemu chache tu kwa upande wa Elimu, kama vile Jimbo la Mashariki (isipokuwa Busoga), sehemu za Kaskazini na Magharibi ya Nile.Kwa msingi huo, Bunyoro, Toro, Ankole na Buganda hazikufundishwa lugha ya Kiswahili. (c) Watawala na viongozi pia walipinga kuenezwa kwa Kiswahili nchini Uganda. Kabaka Daudi na Maaskofu wa Uganda walipinga kuenezwa kwa Kiswahili nchini Uganda; badala yake walipendelea lugha ya Buganda iwe lugha rasmi ya Uganda.Kutokana na hatua hii, Kiswahili kilitengwa kuhusishwa katika shughuli au mipango ya maendeleo ya Uganda. Kiswahili kilididimizwa zaidi na Tume ya Kifalme ya Afrika Mashariki ambayo ilizuia kutumika kwa Kiswahili na Vyombo vya Serikali, Kiingereza peke yake ndicho kilichopewa kipaumbele badala ya Kiswahili (d) Nchini Uganda Kiswahili kilifikiriwa kwamba ni lugha ya watumwa. Na kwa kuwa Kiswahili kilitumiwa zaidi na Polisi na Wanajeshi ambao, kwa bahati mbaya mara nyingi walikosa nidhamu, wananchi wengi waliichukia lugha hii kwa kuinasibisha na utumwa.Kwa msingi huo, Waganda kwa ujumla wao hawakuwa tayari kukipokea Kiswahili. (e) (Mnamo, 1960)na(Maganga, 1997) Serikali ya Uganda iliporuhusu na kulazimisha Kiswahili kitumike nchini Uganda; Kiingereza na lugha za kikabila zilikuwa tayari zinatawala mawasiliano Uganda nzima. (f) Kwa ujumla wakati wa ukoloni, matumizi ya Kiswahili nchini Uganda yalibakia sehemu za Kaskazini tu, tena mapolisi, wanajeshi na madereva wa taksi tu, ndio waliotumia Kiswahili; na watumishi hotelini waliongea Kiswahili cha kibiashara. Uchanganyaji wa Kiswahili na kingereza na pia kutumia Kiswahili kwa maneno yasio sanifu na pia utumizi wa Kiswahili ulioathiriwa na sarufi ya lugha za kikabila hususan kimatamshi na kimuundo.
Ikiwa unasafiri nchini Rwanda au Burundi, Kifaransa labda itakufikisha mbali kuliko Kiswahili, lakini maneno machache hapa na pale yanapaswa kueleweka na juhudi zitathaminiwa. Kiswahili pia huzungumzwa katika sehemu za Malawi, Zambia, DRC, Somalia, na Msumbiji. Toleo la mwaka wa 2019 la chapisho la kumbukumbu Ethnologue linakadiria kuwa lahaja za Kiswahili huzungumzwa kama lugha ya kwanza na watu takriban milioni 16, na kwamba zaidi ya watu milioni 82 huizungumza kama lugha ya pili. Hii inafanya Kiswahili kuwa lugha ya 14 inayozungumzwa zaidi ulimwenguni.
Johnpaul Arigumaho is a Kiswahili educator and researcher from Ibanda, Uganda. He holds a Bachelor’s in Arts with Education (Kiswahili) from Bishop Stuart University and a Master’s in Kiswahili (FCH) from the Islamic University in Uganda.
Johnpaul is an Assistant Lecturer at Uganda Martyrs University and Bugema University and also teaches at Uganda Martyrs SS Namugongo – Kampala.
View all posts by Mwalimu Johnpaul Arigumaho
Ahsante sana kwa kupenda na kudumusha lugha yetu nchini uganda na Afrika yote.
Ni lazima tushabikiane ktk shughuri tofautitofauti ili tuiendeleze lugha yetu duniani yote.
Kiswahili leo, kiswahili kesho.👏👏👏👏
Asante sana Kwa kazi nzuri
LikeLiked by 1 person
you are welcome. karibu sana ndugu yangu
LikeLike
Ahsante sana kwa kupenda na kudumusha lugha yetu nchini uganda na Afrika yote.
Ni lazima tushabikiane ktk shughuri tofautitofauti ili tuiendeleze lugha yetu duniani yote.
Kiswahili leo, kiswahili kesho.👏👏👏👏
LikeLiked by 1 person
asante sana Agnes. sambaza tovuti basi
LikeLiked by 1 person