FASIHI YA KISWAHILI.

Fasihi ni sanaa inayotumia lugha. Fasihi hutumia lugha kutoa sanaa mbalimbali katika jamii.

Tanzu za Fasihi

Kuna tanzu mbili kuu za fasihi, na kila utanzu una vipera vyake: Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi: Fasihi Simulizi ni kama vile Hadithi (Ngano) – hekaya, mighani, visasili, Nyimbo – za jandoni, za ndoa, za kazi, Maigizo – michezo ya kuigiza, ngomezi, Tungo Fupi – methali, vitendawili n.k

Fasihi Andishi huwa ni fasihi inayoelezwa na kuhifadhiwa kimaandishi.kv

1) Hadithi Fupi – hadithi isiyokuwa ndefu iliyochapishwa katika mkusanyiko wa hadithi nyingine

2) Riwaya – Hadithi ndefu iliyochapishwa katika kitabu chake pekee

3) Tamthilia – Mchezo wa kuigiza uliowekwa kwa maandishi

4) Ushairi* – Mashairi yaliyoandikwa.

Tofauti kuu kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi ni kwamba, fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo au matendo ilhali fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi.

Tanbihi:Ushairi ni kipera cha nyimbo lakini pia mashairi yanaweza kuwa chini ya fasihi andishi, ikiwa yamechapishwa.

Tofauti kati ya Fasihi Andishi na Fasihi Simulizi

Fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo na/au matendo ilihali fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi

2. FS ni mali ya jamii lakini FA huweza kuwa Kazi na mali ya mwandishi (na mchapishaji)

3. Msimulizi anaweza kubadilisha sehemu fulani lakini Kitabu kilichoandikwa hakiwezi kubadilishwa

4. FS huhifadhiwa akilini ilihali FA huhifadhiwa vitabuni

5. Kazi simulizi hubadilika na wakati lakini kazi andishi haibadiliki na wakati.

6. FS huhitaji msimulizi au fanani na hadhira yake wawe mahali pamoja wakati wa masimulizi lakini Msomaji anaweza kusoma kitabu cha hadithi peke yake, mahali popote, wakati wowote.

7. Katika FS, Mtu yeyote anaweza kutunga na kusimulia lakini FA Ni lazima mwandishi na msomaji wawe na uwezo wa kusoma.

8. FS hutumia wahusika changamano (wanyama, watu, mazimwi nakadhalika lakini FA hutumia wahusika wanadamu.

Umuhimu wa Fasihi Katika Jamii

  1. Kuburudisha jamii. Takribani vipera vyote vya fasihi huwa na kusudi la kufurahisha, kutumbuiza na kusisimua hadhira.

2. Kuelimisha. Fasihi hukusudia kuelimisha hadhira kuhusu jamii, mazingira n.k Kudumisha maadili katika jamii kwa kuelekeza, kuonya na kunasihi hadhira jinsi ya kufuata mwelekeo unaokubalika katika jamii.

3. Kuunganisha jamii. Fasihi huleta pamoja watu katika jamii. Kwa mfano, katika nyimbo, miviga, vichekesho.

4. Kukuza lugha. Aghalabu tungo zote za fasihi hutumia lugha. Isitoshe, fasihi hutumia mbinu nyingi za lugha. Wasimulizi na waandishi wa fasihi huhitaji kuwa na ukwasi wa lugha.

5. Huhifadhi mila, tamaduni na itikadi za jamii. Aghalabu kazi za fasihi (hasahasa Fasihi Simulizi) huambatanishwa na desturi mbalimbali za jamii husika.

6. Hukuza uwezo wa kufikiri. Vipera vingi vya fasihi huwachochea hadhira kufikiri sana ili kupata suluhisho. k.m vitendawili, ngano za mtanziko nakadhalika…

arigumaho810@gmail.com.

4 thoughts on “FASIHI YA KISWAHILI.

Leave a reply to Ismael Cancel reply