
KUHUSU KITABU – KISWAHILI DARASANI (S1 & S2)
Kufuatia mafanikio makubwa na mapokezi ya kupendeza ya Kiswahili Darasani (S3 & S4) kote nchini Uganda, tunajivunia kutambulisha Kiswahili Darasani kwa Kidato cha Kwanza na cha Pili (S1 & S2). Hiki Kitabu ni rasilimali iliyoboreshwa, inayomlenga mwanafunzi na inayolenga kukuza ujuzi wake huku ikiandaliwa kwa ustadi ili kuimarisha msingi wa lugha ya Kiswahili katika shule za upili nchini Uganda
Kitabu hiki kimeandaliwa na Idara ya Kiswahili ya Shule ya upili Uganda Martyrs Namugongo na kinaendana kikamilifu na Mtaala wa msingi wa umilisi (CBC). Kitabu hiki kimeandaliwa mahususi kurahisisha ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili huku kikimpa mwanafunzi stadi muhimu zinazohitajika ili kufanya vizuri na kupata milisi zinazohitajika kuanzia Kidato cha Kwanza hadi cha Nne (O-Level).
KWA NINI KITABU HIKI NI MUHIMU?
Mara nyingi Kiswahili kimeonekana kuwa somo gumu hasa kutokana na mahitaji ya mitihani ya kitaifa. Kiswahili Darasani (S1 & S2) kimekusudia kubadili mtazamo huo kwa kuwaandaa wanafunzi mapema, kujenga kujiamini na kukuza hatua kwa hatua uwezo unaohitajika kumudu Lugha na Fasihi kwa urahisi wafikapo Kidato cha Nne.
SIFA ZA KIPEKEE ZA KISWAHILI DARASANI (S1 & S2)
✅ Muhtasari rahisi na uliopangwa vizuri kulingana na mahitaji ya CBC.
✅ Shughuli jumuishi (AOI) za kukuza ujuzi ili kuimarisha ujifunzaji binafsi.
✅ Mashairi mafupi na hadithi fupi ili kuimarisha ufahamu na stadi za kifasihi.
✅ Mazoezi yaliyosanifiwa kwa makini ili kuwaandaa wanafunzi kwa Karatasi ya Kwanza na ya Pili katika kidato cha tatu na nne.
✅ Tafsiri za Kiingereza za msamiati mgumu wa Kiswahili kwa uelewa bora.
✅ Kinafaa kwa shughuli za darasani na tathmini endelevu.
✅ Nyenzo madhubuti za msingi zinazowaandaa wanafunzi kufanya vizuri katika S3 na S4.
MAONO YETU
Ingawa kila juhudi ya kitaalamu inastahili kuungwa mkono au kulipiwa, nguvu inayotusukuma kuandaa kitabu hiki ni zaidi ya biashara. Dhamira yetu ni kuona Kiswahili kikiwa somo rahisi, la kufurahisha na linalopendwa katika shule zote za upili nchini Uganda. Tunaamini kuwa wanafunzi wakiongozwa vyema kuanzia ngazi ya chini, wengi watakichagua Kiswahili kama somo lao la hiari hata kabla halijafanywa la lazima katika ngazi ya O-Level.
Kupitia nyenzo rahisi za ujifunzaji zinazolenga ujuzi kama Kiswahili Darasani, tunaendelea kupigania ukuaji, uthamini na maendeleo ya lugha ya Kiswahili nchini Uganda.
📍 JIPATIE NAKALA YAKO LEO!
Inapatikana WALIMU BOOKSHOP UGANDA, Kyaliwajjala (Opposite market).
📞 Wasiliana nasi:
- Johnpaul Arigumaho: +256 778 514 179
- Crispus Mukama: +256 702 745 415 / +256 772 611 379
- Joseph Bikorwomuhangi: +256 784 590 576
- Peter Nuwajuna: +256 785 372 409
📘 KISWAHILI LEO, KISWAHILI KESHO – NYUMA HATURUDI!

Kazi bora lazima
LikeLike
ASANTE CHUMA
LikeLike