WALIMU BOOKSHOP UGANDA (WABU)

*HAMJAMBO NDUGU WADAU WA KISWAHILI!

UZINDUZI WA “WALIMU BOOKSHOP UGANDA* ”

Miongoni mwa watetezi wa Kiswahili Uganda waliothubutu kusimama kidete kuendeleza lugha hii nchini Uganda, sasa wamejitokeza na mchango mkubwa wa vitendo kwa kufungua WALIMU BOOKSHOP — duka maalum la vitabu vya Kiswahili lililoko Kyaliwajjala, mkabala na soko la Kyaliwajjala.

Katika duka hili, tunayo vitabu vya Kiswahili Darasani kwa wingi, hata ukihitaji kwa idadi kubwa kwa matumizi ya shule au taasisi. Tunahakikisha kila mwalimu, mwanafunzi na taasisi za elimu zinapata nakala stahiki kwa wakati.

Zaidi ya hayo, tunahifadhi na kuuza vitabu vya Kiswahili vya aina mbalimbali vikiwemo: kamusi za Kiswahili, Biblia za Kiswahili kwa ajili ya maelekezo ya misa, hadithi fupi kwa wanafunzi wachanga, novela ndogo ndogo, tamthilia rahisi kwa shule za sekondari na msingi, pamoja na vitabu vyote vya mtaala mpya wa msingi wa umilisi wa kiwango cha chini (lower secondary Competency-Based Curriculum).

Tunajivunia pia kuwa na vitabu vya Kiswahili kwa kila kundi la jamii, vikiwemo kwa:

  1. Wanaoanza kujifunza Kiswahili (beginners)
  2. Watumishi wa uhamiaji na mipakani (immigration professionals)
  3. Wafanyakazi wa shirika la ndege la Uganda Airlines
  4. Wawakilishi wa kanda ya Afrika Mashariki wasioelewa Kiswahili — kwa ajili ya mafunzo ya kitaalamu
  5. Wabunge na Mawaziri wa Uganda wanaohitaji Kiswahili cha kazi na mawasiliano rasmi
  6. Wafanyabiashara nchini Uganda wanaotaka kutumia Kiswahili katika soko la Afrika Mashariki.

Aidha, WALIMU BOOKSHOP imezinduliwa kama kitovu cha kukuza Kiswahili nchini Uganda kwa kuhakikisha kuwa vitabu vyote vya waandishi wa Kiswahili kutoka Uganda vinapatikana hapa — ni jukwaa la kuwainua waandishi wetu wazalendo na kuunga mkono kazi zao.

Vilevile, tutakuwa tunauza kazi bora za waandishi mashuhuri wa Kiswahili barani Afrika kama Marehemu Prof. Ken Walibora, Prof Penina Muhando, Alamin Mazrui, Prof Mutembei, Prof Ponera na wengine walioweka msingi thabiti wa lugha na fasihi ya Kiswahili.

Tunaalika shule, walimu, wanafunzi, wazazi, taasisi za elimu, taasisi za serikali na zile za kibinafsi pamoja na wapenzi wa Kiswahili kufika WALIMU BOOKSHOP ili kujipatia vifaa bora vya kujifunzia na kufundishia Kiswahili kwa kwa ajili ya kukuza na kuendeleza Kiswahili nchini Uganda.

📞 Kwa mawasiliano:
‪+256 778 514179‬ ‪+256 702 745415‬
arigumaho810@gmail.com

#KiswahiliLeoKiswahiliKesho

#UgandanyumaHaturudi

#WALIMUBookshop

#Kiswahiliuganda

Leave a comment