Taifa la Wenyewe
Nchi yetu itaishi vipi, Rushwa siku baada nyingine,
Ukabila hutawala uongozi, umbali gani tunakwenda?
Rasilimali kachukuliwa zote, raia umaskini shingoni,
Maswali kupewa kazi serikalini, wewe ni mtoto wa nani?
Taifa ikiwa kuna wenyewe, gawanyeni tugawane vipande.
Mikono na mbavu zavunjika, kuokota vipande tumeshindwa
Kiongozi baada ya mwingine , kuahidi kufanya dunia nzima
Madarakani macho hufumbwa, Vitendo so watu wa kawaida
Hata elimu kwa kila mtu, imebaki kwa baadhi yao
Taifa ikiwa kuna wenyewe, gawanyeni tugawane vipande.
Kuahidi ardhi na dunia, ulafi ndo unatanguliza
Waumiao uchaguzini, wakumbukwa tu uchaguzini,
Awamu yote miaka mitano, kushibisha tu matumbo yao,
Jeshini twatamani wengi, ila vyeo kwa waliopigana,
Taifa ikiwa kuna wenyewe, gawanyeni tugawane vipande.
Kumbukeni walowachagua, waliona mwanga ndani yenu
Kubadilika muda bado tayari, tupeni matumaini na amani
Mema ndo tunatalaji toka kwenu, nija ya mwongo ni fupi.
Sikieni sauti za wanyonge, taifa letu mbele lisonge
Taifa ikiwa kuna wenyewe, gawanyeni tugawane vipande.
Ahadi ni deni kakosa maana, maneno hayaashirii vitendo,
Ada ya mja hunena zaidi, mwungwana yaonwa kivitendo.
Kizazi chetu huruma zenu chalilia, yote yatendwe mola yu hai,
Maskini wananchi twajifunza, kutoa ni moyo so utajiri.
Taifa ikiwa kuna wenyewe, gawanyeni tugawane vipande.
Atim Cloe Enanga: Kidato cha nne. (2024)
Shule ya Upili Uganda Martyrs Namugongo
MASWALI
- Taifa ikiwa kuna wenyewe, gawanyeni tugawane vipande” ni mstari unaojirudia. Mwandishi anamaanisha nini anaposema hivyo?
2. Taja mambo mawili ambayo yanaumiza taifa letu kulingana na shairi hili. Eleza kwa maneno yako.
3. Eleza jinsi viongozi wanavyoahidi mema lakini hawatendi, kama inavyoelezwa kwenye shairi.
4. Mwandishi anasema elimu na kazi ni kwa wachache. Kwa nini anasema hivyo? Toa mfano kutoka shairini.
5. Shairi hili lina huzuni na hasira. Ni wapi unahisi hisia hizo na kwa nini?
6. Shairi linaonyesha kuwa wananchi wana matumaini. Taja mstari mmoja unaonyesha tumaini na ueleze maana yake.
7. Kwa maoni yako, mwandishi anatufundisha nini kuhusu taifa letu na viongozi wake?
