FUNZO LA MAISHA

Kila Jambo Lina malipo yake baadaye..
Picha ilipigwa na KEVIN CARTER, kama sehemu ya mradi wake ambao alikwenda kuufanyia huko huko Sudan. Picha inatuonesha ndege (Vulture) akiwa pembeni anavizia mtoto afe ili aende kula mzoga.

Hadithi ilikuwa hivi mwaka 1993 Kevin Calter alisafiri kwenda Sudan. Karibu na kijiji cha Ayod. Alipokuwa njiani, alimuona mtoto akiwa amepumzika baada ya kutembea safari ndefu sana kuelekea Kambi ya chakula ya Umoja wa Mataifa (United Nations feeding centre).

Kabla hajapiga picha alimuona huyo ndege, Kevin akajificha sehemu fulani kwa takribani dakika ishirini (20) ili ndege asishtuke akaruka akaikosa picha. Lengo la kujificha muda wote huo alikuwa akisubiria ndege asogee karibu kabisa na Mtoto ili aweze kunasa picha yake. Baadaye alifanikiwa kupiga picha yake, akaendelea na safari yake.

Picha ilisambaa ikaanza kupata maoni tofauti na vile yeye alivyokuwa akifikiria. Gazeti la PETERSBURG TIMES huko FLORIDA liliandika kwamba, “Aliyepiga picha hii naye pia ana roho ya unyama kwa sababu badala amfukuze ndege yeye yuko bize kupiga picha”. Kevin alifafanua kwamba, wakati alipoagizwa kwenda kufanya mradi huo, alipewa maelekezo kwamba asishikeshike kila kitu akutanacho njiani ili asije akaambukizwa magonjwa. Japo baadaye alionesha hali ya kujutia kwa kutochukua hatua yoyote kumwokoa yule mtoto.

Mwaka 1994 Kevin Calter alipata tuzo katika mashindano ya picha ambazo zinatisha/zinahuzunisha kwa kupitia picha hii. Hata hivyo mwaka huohuo Kevin Calter akiwa na miaka 33 alijiua kutokana na msongo wa mawazo.

Inasemekana hii haikua mara yake ya kwanza kupiga picha za aina hii. Huko nyuma alikuwa amepiga picha kadhaa za matukio ya watu wakiuawa, wakiumizwa na hata kupiga picha za Maiti ikiwa kama sehemu yake ya kazi kama Mwandishi wa habari/Mpiga picha.

Baada ya kujiua walikuta alikuwa ameacha maandishi akieleza jinsi kumbukumbu za picha hizo zilivyopoteza furaha katika maisha yake kila alipokuwa akizikumbuka na ndipo akaamua kujiua.

Hadithi hii inatufunza na kutuonyesha vile watu siku hizi wameanza kutenda matendo ambayo siku hizi ni ya kiunyama. Badala ya mtu kumwokoa mwenzake siku hizi anashika simu yake yake na kuanza kunasa picha ili awe na kumbukumbu katika simu au kompyuta yake.

Hivi juzi sehemu za Entebbe ufukoni Nabnoonya, wenye hela zao walikuwa wameenda kula raha katika eneo hilo. Ghafla mtoto wa miaka kama kumi na mmoja akaonekana akipiga kelele akizama majini. Watu wengine ambao walikuwa na uwezo wa kumwokoa hawakusita bali walianza kunasa picha moja kwa moja na mtoto akazama na kufa.

Unajifunza nini? Saidia mwenzako kwa sababu maisha hayana maana na haya matendo ya kunyama.

Asanteni sana,

@Johnpaul Arigumaho-Kamapala

Leave a comment