Kwa mujibu wa watalaamu mbalimbali una maana ya; Kimani Njogu na Rocha Chimera (1999) wanasema kwamba udhanaishi ni nadharia inayoshughulikia zaidi na “dhana ya maisha “Swali la kimsingi katika nadharia hii ni maisha ni nini? Wadhanaishi huchunguza kwa undani nafasi ya mwanadamu ulimwenguni, pia wanajishughulisha na uchunguzi kuhusu uhusiano uliopo kati ya binadamu na mungu.
Wamitila K.W (2003) katika kamusi ya fasihi na nadharia amefanunua udhanaishi kama dhana inayotumia kuelezea maono au mtazamo inayohusiana na hali ya maisha ya binadamu, nafasi na jukumu la binadamu ulimwenguni, na uhusiano wake na Mungu au kutokuwepo na uhusiano na Mungu.
Wanjala Simiyu (2012) katika kitabu Kitovu cha Fasihi Simulizi Udhainishi ni falsafa au mtazamo wa maisha ulio na kitovu chake katika swala kuwa, maisha ni nini na yana maana gani kwa binadamu? Ni kwa njia gani mwanadamu anaweza kuyabadilisha maisha yake yaliyojaa na dhiki, mashaka na huzuni?
Kimani Njogu na Wafula L M katika Nadharia za Uhakiki wa Fasihi (2007) wanasema, Udhanaishi ni falsafa kuhusu dhana ya maisha. Ni falsafa inayo husiana na utamaushi kutokana na neno “kutamauka”. Kutamauka ni kutokuwa na furaha au kutokuwa na tamaa kwa kuhisi kutokuwa na matumaini katika maisha.
Naye Camus (1984) Udhanaishi ni falsafa inayoshugulikia maswala kuhusu maisha; ni mtazamo unaokagua kwa upembuzi hali ya nafasi ya mtu katika ulimwengu anamoishi na pia ni falsafa inayo zungumzia uhusianao uliomo kati ya mtu na Mungu na iwapo mtu anapaswa kuamini kuwepo kwa Mungu.
Nadharia hii inatusaidia kuhakiki maisha ya mwanadamu anayeishi katika ulimwengu uliojaa shida na matatizo mengi ambayo yanayosababishwa na binadamu mwenyewe. Matatizo anayoyapitia ni kama vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa misingi ya kidini, njaa na uchumi kuharibika, kukosa kazi, ajali barabarani. Matatizo haya yanafanya mwanadamu kukata tamaa na kushuku iwapo kweli mungu yuko.
WAASISI WA NADHARIA YA UDHANAISHI
Wasisi wa nadharia hii wamewekwa kwenye vitengo tofauti.
Wanaoamini kuwepo kwa Mungu
Soren Kierkegerd ni mwanathiolojia wa Kidenimaki aliyekuwapo kati ya mwaka wa 1813 hadi 1855 na aliweza kuandika makala mbali mbali hasa;
The concept of dread
Fear and trembling
The sickness unto death. Wafula R.M na Kimani Njogu (2007) na Wamitila. W (2003)
Wasiomini kuwepo kwa Mungu
Wanafalsafa wakijerumani wakiongozwa na FRIDRICK NIETZSCHE,MARTIN HEIDEGGER,
GABRIEL MARCEL na KARL JASPERS walitokea katika karne ya ishirini. (Wamitila K.W 2003)
Wasio na uhakika wa kuwepo kwa mungu.
JEAN PAUL SATRE aliyetokea baada ya vita vikuu vya dunia na alikuwa mwanafalsafa wa kifaransa. Kimani Njogu na Rocha chimera (1999)
HISTORIA FUPI
Udhanaishi unaouhusishwa kwa kiasi kikubwa na mwanathiololojia wa Kidenimaki kwa jina Soren
Kierkegaard (1813-1855) katika maandishi yake mbalimbali
Soren kieregaard (1844), The concept of dread
Soren kieregaard (1843), Fear and trembling
Soren kieregaard (1849), The sickness unto death.
Kierkegaard anaeleza kuwa mtu haishi kwa nguvu zake mwenyewe kuna nguvu zinazomtawala ambazo
ni za Mungu. Binadamu anapoishi hutenda dhambi na ili apate utulivu wa kiroho inambidi atubu dhambi hizo. Wanaamini kuwepo kwa Mungu kwa binadamu wote.
Anaeleza kuwa binadamu ni kikaragosi cha nguvu zilizomuumba ni katika kuzicha mtu huyu hupata utulivu wa kiroho.
Anaendelea kusema kwamba udhanaishi ni dhana ya hofu pale ambapo binadamu huogopa adhabu kutoka kwa Mungu kwa hivyo, amefunikwa na wasiwasi hataki kumkosea Mungu.
Anasisitiza binadamu ni mtu binafsi (hali ya
kujijali).
Binadamu hupata kimbilio kutoka kwa mivutano ya maisha kupitia kwa Mungu. Imani hii ilishika nguvu sana kwenye ukristo, huu ukawa mwanzo wa udhanaishi wa ukristo. (Christian Existentialism)
Kwa mujibu wa Wamitila .K.W (2003) kamusi ya fasihi, istilahi na nadharia, anasema kuwa katika karne ya ishirini, Udhanaishi ulipata msukumo mpya kutoka kwa mwanafalsafa wa kijerumani Friedrich Nietzsche na wengine kama Martin Heidegger, Gabriel Marcel na Karl Jaspers.
Nietzche(1927) “” anadai kuwa Mungu amekufa.
Tamko hili lake pamoja na misimamo ya wenzake vinakuwa misingi muhimu ya kuzuka kwa udhanaishi wa ukanaji Mungu (atheistic existentialism)
Kwa mujibu wa tovuti, Martin Heidegger, mwanafalsafa wa Kijerumani na mwanafunzi wa Husserl aliamini kuwa neno ‘nitakufa’ si katika dunia ya ukweli.
Kwa mujibu wa kimani Njogu na Rocha Chimera (1999) wanaelezea kuhusu mwanafalsafa wa Kifaransa Jean Paul Satre ambaye ndiye mwasisi mkuu wa udhanaishi. Baada ya vita vikuu vya dunia anadai kuwa mtu huzaliwa au hujipata ametumbukia katika ombwe la aina fulani.
Vilevile mtu yuko huru kuishi tu na kukabiliana vilivyo na ulimwengu unaomzunguka. Isitoshe, kwa vile
binadamu hana uwezo kwa yale anayoyapitia maumivu na mateso, anaweza kukata tamaa. Katika mhadhara alioutoa Jean Paul Satre, (1946) “Existentialism and Humanilism”alisisitiza kuwa “kuzimu ni za watu wengine” Hii ni ishara kuwa ana uwezo wa kuchagua na uhuru wa kila mtu anaweza kuathiriwa na watu wengine.
Alisisitiza pia, dini haiwezi kutatua shida za binadamu.
Ishitoshe, aliegemea katika suala
la ubinafsi wa mtu.
MIHIMILI YA UDHANAISHI
Waandishi mbalimbali wameweza kutoa mihimili ya udhanaishi, kwa kuwarejelea Wafula .R.M na
Kimani Njogu (2007) wao wameainisha mihimili hiyo kama ifuatavyo;
a. wanatilia mkazo matatizo halisi yanayomsibu mwanadamu na kuwa anakwepa imani ya kijozi juu ya imani ya kuishi.
b. Hawaamini uwepo wa mungu na uumbaji wake wa ulimwengu.
c. Juhudi za mtu binafsi kujisaka au kupambana na maisha huishia katika mauti.
d. maudhui yanayotajwa na wadhanaishi ni kama vile uhuru wa mtu binafsi, uwezo wake wa kujifikilia na kujiamlia.
e. Hujadili hali kama vile mashaka na uchovu wa mambo mbalimbali yanayotutatiza maishani na jinsi
yanavyoathiri maisha ya binadamu.
f. Hujadili maudhui ya ukengeushi (hali ya kukata tamaa au kutokuwa na uhakika)
g. Mtindo wanaotumia wa udhanaishi ni taswira wanayochorea msomaji picha mbalimbali za maisha ya
kuteseka anayopitia mwanadamu ulimwenguni.
HITIMISHO
Ufaafu
a) Nadharia ya udhanaishi inaweza kuhakiki wahusika katika kazi ya fasihi mfano wahusika waliokata
tamaa, walio na matatizo, walijawa na uchovu.
b) Kuhakiki maudhui katika kazi za fasihi kama vile ukengeushi, ubinafsi, kukata tamaa.
Udhaifu
Nadharia hii haiwezi kuhakiki vitabu ambavyo havijatumia nadharia ya udhanaishi.
UHAKIKI WANADHARIA YA UDHANAISHI KWA KUZINGATIA RIWAYA YA DUNIA UWANJA WA FUJO-E. KEZILAHABI.
Mwandishi Euphrase Kezilahabi ni miongoni mwa wadhanaishi wa fasihi ya Kiswahili.
Kwa kutumia riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo tunapata Nadharia ya udhanaishi.
MAREJEREO
a.Kimani, N na Chimera, R.(1999). Ufundishaji wa fasihi,Nadharia na mbinu. Nairobi, Jomo kenyatta
foundation.
b.Wafula, R na Kimani, N (2007) Nadharia za uhakiki wa fasihi. Nairobi. Jomo Kenyatta Foundation.
c.Wamitila, K.N (2002) Uhakiki wa fasihi, misingi na vipengele vyake, Nairobi: Phoenix publishers ltd.d.Wamitila,K.N (2003): Kamusi ya fasihi, Istilahi na Nadharia, Nairobi: Focus publications ltd.

Kazi nzuri,ila nataka nipate uhakiki wa Riwaya ya Rosa Mistika kwa misingi ya nadharia hii ya utamaushi
LikeLike
Sawa, tuwasiliane
LikeLike
Hongera Mwalimu na kazi unazozifanya
LikeLike
Asante sana mwenzangu
LikeLike
Nimependa sanaa maandiko haya ahsante sanaaa
LikeLike
Nashukuru sana ndugu yangu. Twendelee kushabikiana
LikeLike
perfect
LikeLike
Asante ndugu
LikeLike
Ni kwa namna gani mchango wa E. Kezilahabi katika nathari umeathiriwa na kuainishwa na nadharia ya Udhanaishi ?
LikeLike
Nifikie kikashani. au kupitia anwani pepe, arigumaho810@gmail.com 0778514179
LikeLike