Stephen Pit Corder (6 Oktoba 1918 – 27 Januari 1990) alikuwa profesa wa isimu tumizi katika Chuo Kikuu cha Edinburgh aliyejulikana sana kwa mchango wake katika uchunguzi wa Nadharia ya uchanganuzi makosa. Alikuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha Uingereza cha Isimu tumizi 1967-70 na alisaidia sana katika kuendeleza taaluma ya isimu-tumizi nchini Uingereza.
Pit Corder alizaliwa Bootham Terrace York, katika familia ya Quaker. Baba yake, Philip Corder (Alizaliwa. 1885), alikuwa mwalimu wa shule mwenye asili ya Uingereza, na mama yake Johanna Adriana van der Mersch (Alizaliwa. 1887), alikuwa Mholanzi.
Pit alisomea katika Shule ya Bootham, shule ya bweni ya Quaker karibu na New York, ambapo babake alikuwa mwalimu. Aliendelea kusoma lugha za kisasa katika Chuo cha Merton, Oxford kuanzia 1936 hadi 1939.
Baada ya Oxford, Corder alifundisha katika Shule ya Great Ayton Friends' hadi akahudumu katika Kitengo cha Magari ya Wagonjwa (Friends ambulance) wakati wa Vita vya Pili vya Ulimwengu nchini Ufini na Misri.
Mnamo 1946 alimwoa Nancy Procter (b. 1916), binamu yake wa pili, ambaye alizaa naye wana wawili wa kiume na wa kike.
Baada ya vita, Corder alifanya kazi katika Baraza la Uingereza huko Austria, Uturuki, Jamaika na Kolombia. Wakati huo pia alikuwa anafundisha. akifanya kazi ya kutengeneza silabasi pia na kuandaa nyenzo mpya za kufundishia lugha.
Mnamo 1957 Corder alijiunga na shule ya isimu tumizi katika Chuo Kikuu cha Edinburgh ingawa aliendelea kuajiriwa na Baraza la Uingereza. Baraza la Uingereza lilihitaji wataalamu wa isimu tumizi kwa ajili ya upanuzi wake duniani kote. Corder alisomea stashahada ya isimu tumizi ili kutimiza hitaji hilo. Baada ya mwaka wa masomo, Baraza la Uingereza lilimtuma Nigeria ambako alisaidia kutengeneza vifaa vya kufundishia kwa lugha ya Kiingereza kwa ajili ya mafunzo ya televisheni.
Corder aliondoka kwenye Baraza la Uingereza (British council) baada ya hili, ingawa haliko wazi juu ya lini haswa. Kulingana na taarifa kuhusu kifo chake kutokana na Chama Cha Uingereza cha Isimu tumizi (British Association for Applied Linguistics), aliacha Baraza la Uingereza mwaka wa 1961, alipoanza kufundisha katika Chuo Kikuu cha Leeds.
Hata hivyo, kulingana na wasifu wake katika Kamusi ya Oxford, alipendekezwa kwenda kufanyia Chuo Kikuu Cha Leeds na Baraza la Uingereza. Aliacha tu shirika hilo mnamo 1964 alipokuwa mkurugenzi wa shule ya isimu tumizi katika Chuo Kikuu cha Edinburgh.
Corder alikaa katika Chuo Kikuu cha Edinburgh kwa maisha yake yote ya kitaaluma. Corder alianzisha Mihadhara na Idara ya Isimu tumizi huko Edinburgh mnamo 1964.
Katika Uchanganuzi Makosa na Lugha Nyingine, Corder alianzisha wazo kwamba ujifunzaji wa lugha ya pili au ya kigeni ni maendeleo na unaweza kuchunguzwa kwa kuchanganua makosa ambayo wanafunzi wanafanya. Makosa haya yanapaswa kutazamwa kama ishara za maendeleo chanya ya lugha badala ya mapungufu. Hoja ya Corder ilikuwa kwamba lugha ya mwanafunzi, ambayo baadaye iliitwa 'interlanguage' na Larry Selinker (1972), ni lugha yenyewe sasa inakubalika kwa jumla.
NADHARIA YA UCHANGANUZI MAKOSA.
Wanafunzi wanaojifunza lugha ya pili hufanya makosa mengi yakiwemo matamshi mabaya ya maneno.
Kutokana na hali hiyo, wanaisimu wamekuwa katika mstari wa mbele kubaini chanzo cha makosa na vilevile kubuni mbinu faafu zinazochangia katika kutatua matatizo hayo.
Uchanganuzi Makosa Mtazamo wa Uchanganuzi Makosa uliasisiwa na Corder na wenzake miaka ya 1960.
Mtazamo huu uliibuka kukidhi upungufu wa uchanganuzi linganuzi uliotumiwa na wanaisimu kutofautisha lugha ya kwanza na ya pili ya mwanafunzi ili kukisia makosa.
Uchanganuzi makosa ni mbinu itumiwayo kuthibitisha makosa yanayopatikana katika lugha ya mwanafunzi.
Walimu wa lugha wanaowasikiliza wanafunzi wao wakizungumza hutambua makosa. Ukweli ni kuwa kila mtu hufanya makosa anapoongea hata walimu na wazawa wa lugha hufanya makosa.
Wazawa wa lugha hawafuati kanuni za sarufi zilizoandikwa vitabuni.
Uchanganuzi makosa, huchunguza aina ya makosa na visababishi vya makosa hayo. Kulingana na mwanaisimu Corder, mtafiti hufuata hatua zifuatazo katika uchanganuzi makosa:
1. Kukusanya sampuli ya kazi ya wanaojifunza lugha ya pili
2. Kutambua makosa
3. Kueleza makosa.
4. Makosa yanawekwa katika makundi na kuelezwa kisarufi.
5. Hivyo makosa yenyewe ndiyo hutumiwa katika kuainisha kategoria za kisarufi.
6. Kufafanua chanzo cha makosa haya.
7. Kutathmini / kuyasahihisha makosa haya ili kujua jinsi ya kukabiliana nayo.
Tunapowasikiza wanafunzi wakizungumza tunafahamu makosa wayafanyayo. Kwa sababu hii ni vyema kujiuliza kile mzungumzaji alikusudia kukisema na angekisema vipi. Kusahihisha makosa haya sio jambo rahisi kwa sababu kuna zaidi ya njia moja ya kufanya hivyo.
Kusahihisha makosa kunategemea kile msikilizaji anafikiri mzungumzaji alikusudia kukisema na kosa lenyewe.
Ni vyema kufikiri namna nyingi tofauti za kusahihisha makosa. Kwa sababu huna uhakika wa kilichokusudiwa, mwache mwanafunzi akusaidie kuamua sahihisho sahihi.
Kufafanua makosa haya, kwataka kujua kisababishi. Makosa yanaweza kutokana na kuhamisha kanuni au ruwaza za lugha ya kwanza.
Makosa mengine yanaweza kusababishwa na jinsi mwalimu au vitabu vya kaida vinavyoeleza kanuni fulani.
Au inaweza kuwa mikakati ya mawasiliano anayotumia mwanafunzi hata kama anajua kanuni anazotumia sio sahihi. Utafiti huu si linganishi kwa sababu hatujalinganisha lugha mbili ili kutambua makosa.
Kulingana na ndharia yake Corder, kila mjifunzaji lugha ya pili huunda lugha kadirifu. Lugha kadirifu - Ni lugha inayojitokeza wakati mwanafunzi anapojifunza lugha ya pili. Lugha hii huwa imekiuka kanuni za lugha lengwa hivi kwamba hujitokeza kama lugha kamili yenye mfumo wake wa kiisimu. Pia huitwa lugha kati.
Johnpaul Arigumaho is a Kiswahili educator and researcher from Ibanda, Uganda. He holds a Bachelor’s in Arts with Education (Kiswahili) from Bishop Stuart University and a Master’s in Kiswahili (FCH) from the Islamic University in Uganda.
Johnpaul is an Assistant Lecturer at Uganda Martyrs University and Bugema University and also teaches at Uganda Martyrs SS Namugongo – Kampala.
View all posts by Mwalimu Johnpaul Arigumaho