RIWAYA YA KISWAHILI NA SIFA ZAKE


RIWAYA YA KISWAHILI NA SIFA ZAKE
MAANA YA RIWAYA NA AINA ZA RIWAYA:
Riwaya imefasiliwa na wataalamu mbalimbali miongoni mwao nikama vile, Encyclopedia Americana (EA), Jz. 20 (1982:510f) wakinukuliwa naMulokozi (1996) wanasema, riwaya kuwa ni hadithi ya kubuni inayotosha kuwa kitabu.
Udhaifu; Maelezo haya yanaibua utata kwani hayafafanui kitabu kinapaswa kuwa na urefu kiasi
gani.
Mathalani kwa mujibu wa UNESCO katika Mulokozi (1996) kitabu ni chapisho lolote lenye kurasa 48 au zaidi. Ama urefu wa kitabu hautegemei idadi ya kurasa tu pia unategemea ukubwa wa kurasa (upana na kina) ukubwa wa maandishi na mpangilio wake.
Encyclopedia Britanica EB, Jz.8, (1985:810) wakinukuliwa naMulokozi (1996) wanaeleza kuwa,
riwaya ni masimulizi marefu ya kinathari yaliyochangamana kiasi, yenye kuzungumzia tajriba ya
maisha ya binadamu kwa ubunifu.


Udhaifu: Udhaifu wa hoja hii ni kwamba wamejikita katika kigezo cha urefu, lakini hatujui urefu huo wapaswa kuwa kiasi gani.
Wamitila (2002) Senkoro(2011) na hawakubaliani na kigezo cha kufasili riwaya kwa kutumia
kigezo cha urefu. Mfano Senkoro anaeleza kuwa ,“Ikiwa tutakichukua kipimo cha jumla ya
maneno (75,000) kuwa kielelezo cha riwaya basi itaonekana kuwa tuna riwaya chache mno katika
fasihi kwa hali hii nadhani sifa ya mchangamano ni nzuri zaidi kuelezea maana ya riwaya” (uk.
56)

Naye Wamitila anendelea kuelezea kuhusiana na suala la urefu kuwa,“Kigezo hiki cha urefu hakifai tunapoziangalia kazi za fasihi ya Kiswahili…Mfano kazi mbili za E. Kezilahabi,“Nagona
na Mizingile” hazina idadi kubwa ya maneno lakini ni riwaya”.
Wamitila (2002) na Senkoro (2011) wanasema riwaya nikisa mchangamano ambacho huweza
kuchambuliwa kupimwa kwamapana na marefu kifani na kimaudhui.

Riwaya ni kisa au mkusanyiko wa visa, vyenye urefu unaoviruhusu vitambe na kutambaa mahali
pengi na kuambaa vizingiti vingi vya maisha kama apendavyo mwandishi wake.
Riwaya basi ni hadithi ndefu ya kubuni,yenye visa vingi, wahusika zaidi ya mmoja, na yenye
mazungumzona maelezo yanayozingatia kwa undani na upana, maisha ya jamii.Riwaya hutoa
picha ya jumla ya maisha ya mtu toka nyumbani hadikatika kiwango cha taifa na dunia nzima.
Madumula (2009), Riwaya ni masimulizi marefu ya kubuni yaliyo katika mtindo wa kubuni
yakisawili mtindo maalumu na madhumuni maalumu. Mhusika katika Riwaya anakuwa ni
kipaza sauti cha mwandishi.
Hivyobasi; Riwaya ni masimulizi ya kubuni yenye msuko au mpangilio fulani wa matukio au ploti inayofungamana na wakati au kusawiri wakati na yenye visa vingi vivavyotendeka katika wakati fulani na yenye mawanda mapana yenye mchangamano wa dhamira, visa na wahusika.


MAANA YA RIWAYA KISWAHILI:
Riwaya ya Kiswahili ni ile ambayo inafungamana na utamaduni wa jamii ya waswahili katika lugha ya Kiswahili ambao hupatikana katika nchi ya Afrika Mashariki. Pia ni ile riwaya ambayo inawahusu waswahili wenyewe.


VIPENGELE VYA MSINGI KATIKA RIWAYA;
Ili kujua maana ya riwaya ni vyema kuzingatia mambo kadhaa ambayo ndiyo ya msingi, na mambo hayo ni;
1) Lazima riwaya iwe na lugha ya kinathari,
2) Isawiri maisha ya jamii,
3) Iwe na masimulizi ya kubuni na visa virefu,
4) Wahusika zaidi ya mmoja,
5) Iwe na mpangilio na msuko wa matukio,
6) Lazima na maneno kuanzia elfu thelathini na tano na kuendelea, na
7) Riwaya ni lazima ifungamane na wakati yaani visa na matukio ni lazima viendane na matukio.


HISTORIA FUPI YA RIWAYA:
Riwaya ilizuka kutokana na maendeleo ya mageuzi ya kiutamaduni. Suala la ukoloni na uvumbuzi pia liliumba hali ambazo zilihitaji kuelezwa kwa mawanda zaidi ya yale ya ngano na hadithi fupi. Hapo hapo kuzuka kwa miji na viwanda pamoja na maendeleo ya wasomaji yalifanya riwaya nyingi ziandikwe.
Uchangamano wa maisha ya jamii kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni wenyewe ulizusha haja ya kuwa na utanzu wa fasihi ulio na uchangamano kifani na kimaudhui.
Kupanuka kwa usomaji, hasa wakati wa mapinduzi ya viwanda huko Ulaya, kuliwafanya waandishi waandike waandiko marefu kwani sasa walikuwapo wasomaji hasa wanawake waliobaki majumbani wakati waume zao walipokwenda viwandani, wasomaji ambao muda wao
uliwaruhusu kusoma maandiko marefu marefu ijapokuwa hii lilikuwa jambo la baadaye sana
wakati wa kina Charles Dickens. Hii historia fupi ya chimbuko. Senkoro (2011:55).

CHIMBUKO YA RIWAYA YA KISWAHILI;
Tanzu za asili zinaonyesha kuwa ndio zilichangia kwa kiasi kikubwa sana katika kuibua riwaya
za Kiswahili. Na yafuatayo ni mawazo ya wataalamu mbalimbali juu ya chimbuko la riwaya ya
Kiswahili.
Madumulla (2009), ameeleza kuwa riwaya ilitokana na nathari bunifu simulizi kama vile hadithi,
hekaya, na ngano inayosimuliwa kwa mdomo. Anaendelea kusema kuwa fasihi ilitokana na maandiko ya fani ya ushairi hususan ni tendi za Kiswahili katika hati za kiarabu kwa sababu
ndiyo maandishi yaliyotamba katika pwani ya Afrika Mashariki. Wazungu na waarabu
hawakubadilishana maarifa kwa urahisi na hivyo pakapelekea kuwa na majilio ya taratibu za
maandiko ya kinathari. Mwanzoni riwaya zilitafsiriwa kwa Kiswahili toka katika lugha za ulaya
na kufanya riwaya za Kiswahili kutokea. Mfano wa riwaya hizo ni kama vile; Habari za mlima
iliyoandikwa na Sheikh Ali Bin Hemed (1980).
Senkoro (2011) anaeleza kuwa riwaya zilizuka kutokana na maendeleo na mageuzi ya
kiutamaduni, uchangamano wa maisha ya kijamii, kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni
yaliyopelekea haja ya kimaudhui zaidi ya ngano na hadithi fupi. Anaendelea kusema kuwa
riwaya za kwanza zilitafsiriwa toka riwaya za kizungu mpaka za Kiswahili, Anasema riwaya mojawapo ni ile ya James Mbotela ya Uhuru wa Watumwa. Ndiyo riwaya ya kwanza kutafsiriwa
kwa Kiswahili. Pia anaeleza kuwa riwaya ni utanzu uliozuka kutokana na hali mahususi za
kijamii. Riwaya kama ile ya kiingereza ya Robinson Crusoe iliyoandikwa na Daniel Defoe ni miongoni mwa riwaya za mwanzo.

Mulokozi (1996) anaeleza kuwa chimbuko la riwaya ya Kiswahililipo katika mambo makuu
mawili ambayo; nifani za kijadi za fasihipamoja na mazingira ya kijamii. Fani za kijadi za fasihi,
Mulokozi anaeleza kuwa riwaya haikuzukahivihivi tu bali ilitokana na fani za masimulizi yaani
hadithi, na ndipozikapatwa kuigwa na watunzi wa riwaya wa mwanzo. Fani hizozilizopata
kuchipuza riwaya za mwanzo ni kama vile; riwaya zakingano, tendi, hekaya, visakale, historia,
sira, masimulizi ya wasafiri,insha na tafsiri.
Ngano, Mulokozi anasema, kuwa ni hadithi fupi simulizi pia huwa nihadithi za kubuni na nyingi
hasa zinawahusu wanyama wakali, piazinahusu malaika, binadamu, mazimwi na majini.
Anasema kuwamara nyingi ngano huwa na msuko sahihi na wahusika wake ni bapana wahusika
hao ni mchanganyiko wa wanyama, mazimwi nabinadamu. Anatolea mfano wa ngano zilizo
chukua visa vya kinganokuwa ni kama vile riwaya ya Adili na Nduguze ya Shaaban Robert (1952), Lila na Fila ya Kiimbila (1966), Kusadikika ya Shaaban Robart(1951).
Hekaya,ni hadithi za kusisimua kuhusu masaibu na matukio ya ajabuyaani yasiyokuwa ya
kawaida. Mara nyingi masaibu hayohufungamanishwa na mapenzi. Hekaya hizo zimepelekea
riwaya zaKiswahili kama vile; Hekaya ya Adili na Nduguze ya Sharban Robart(1952), hekaya ya
Ubeberu Utashindwa ya Kiimbila (1971), na Hekayaya A.J.Amiri, ya Nahodha Fikirini, (1972).
Tendi (utendi), ni hadithi ya kishairi kuhusu mashujaa wa kihistoria na wa kubuni, ambao
waweza kuwa ni wa kijamii au kitaifa. Kwa kawaida baadhi ya tendi zina sifa za kiriwaya ila tu
badala ya kuwa na umbo la kinathari zenyewe zina umbo la kishairi. Kuna tendi za aina mbili
ambazo ni tendi andishi na tendi simulizi. Riwaya pevu kama tendi husawiri mawanda mapana
ya kijamii na kihistoria. Huwa na wahusika wababe yaani mashujaa wenye kuwakilisha pande
zinazopingana. Mfano wa tendi ni kama vile; Utendi wa Vita vya Wadachi Kutamalaki Mlima ya
Hemedi Abdallah, (1895), Utendi war as (Ghuli), utenzi wa Fumo liyongo wa Mohamed
Kijumwa K.(1913).Tendi katika riwaya za Kiswahili imetumia wahusika wawili tuambao ni
wahusika wa kubuni na wale wa kijadi wa kiafrika.

Visasili, hizi ni hadithi zinazohusu asili na hatima ya watu, vitu,viumbe, ulimwengu na mataifa,
na pia huangalia uhusiano wawanadamu na mizimwi pamoja na miungu. Hadithi za visasili zinapoonyeswa huaminika kuwa yakweli tupu hasa kwa kusimuliamatukio mengi ya kiulimwengu.Mfano wa visasili; Lila na Fila ya Kiimbila (1966) ambayo imekopamotifu ya asili
ya ziwa ikimba huko Bukoba. Hadithi ya Mungu waKikuyu huko Kenya. Roza Mistika ya Kezilahabi (1971), Nagona(1987) na Mzingile (1991), Siku ya Watenzi Wote ya Sharban Robert.
Visakale, ni hadithi ya kale kuhusu mashujaa wa taifa,kabila au dini. Mara nyingi visa kale
huchanganya historia na masimulizi ya kubuni, na hadithi hizi hupatikana karibu katika kila
kabila kila lugha.Baadhi ya visakale vya Kiswahili masimulizi huhusu chimbuko la miji ya
pwani, mijikenda, mwinyi mkuu huko Zanzibar.Visa kama hivi ndivyo vinavyopelekea
kuandikwa kwa riwaya za kiswahili. Mfano wake ni riwaya ya Abdalla Bin Hemed bin Ali
Ajjemy (1972) katika kitabu cha Habari za Wakilindi, Kisima cha na Giningi ya M.S.Abdulla
(1968) na ile Hadithi ya Myombekela na Bibi Bugonoka na Ntulanalwo naBuhliwali (1980) ya A. Kitereza.
Masimulizi ya kihistoria, haya ni masimulizi ya matendo ya, mwanadamu katika muktadha wa
wakati, na ni fani muhimu sana katika jamii yeyote ile. Masimulizi halisi ya kihistoria yaweza
kuwa ni ya mdomo au hata maandishi na yote huwa ni chemichemi nzuri ya riwaya. Mfano wa
riwaya hizo ni; Habari za pate za Fumo Omari Nabhany (1913) ambayo yalikuwa ni maandishi
ya masimulizi na uchambuzi. Riwaya zingine zilizoathiriwa na matukio ya kihistoria ni;Uhuru
wa Watumwa ya J. Mbotela (1934), Kifo cha Ugenini ya O. Msewa (1977), Kwa Heri
Iselamagazi ya B. Mapalala (1992) na Miradi Bubu ya Wazalendo ya G. Ruhumbika (1992).
Sira, ni masimulizi ya kweli kuhusu maisha ya mtu au watu. Sira iliathirikuchipuka kwa riwaya
hasa kwa kuonyesha masilimulizi ya maishaya mtu toka utotoni mpaka uzeeni. Masimuliza ya
riwaya hiziyalikuwa katika masimulizi na hata katika maandishi pia kwa maanakabla ya ukoloni
yalikuwepo maandishi yaliyohusu maisha ya mitumena masahaba.Mifano ya hadithi hizi ni;
Kurwa na Doto ya M. S.Farsy (1960),Rosa Mistika ya Kezilahabi (1971), Kichwa Maji ya
Kezilahabi (1974) pamoja na Dunia Uwanja wa Fujo (1975), Mzimu wa Baba waKale ya Nkwera
(1967),na riwaya ya Maisha Yangu baada ya MiakaHamsini ya Sharban Robart (1951).


SIFA ZA RIWAYA;
Kwa mujibu wa Wamitila (2002) sifa hizo ni kama zifuatazo;
Uwazi na uangavu,
 Kazi husika ya fasihi isiwasumbue na kuwatatiza wasomaji kuzielewa,
 Muwala na muumano,
 Kazi yariwaya lazima iwe na mshikamano au mtiririko mzuri wa visa aumatukio kuijenga
kazi ya kifasihi,
 Uchangamano wa visa yaani kutokea kisa zaidi kimoja,
 Wingi wa maana kuhusiana na sifa ya uchangamano na ukamilifu ni kule kuwako kwa
elemeti zotemuhumiu na za kimsingi katika kazi ya fasihi.
 Riwaya haifungwi na sheria wala kanuni.
 Riwaya ina matumizi ya lugha ya kinathari. Ni lugha ya mjazo wa maneno na mtiririko
wa mawazo.
 Riwaya ina urefu na upana wa kutosha,,,,,, urefu na upana wa kimaudhui unapelekea
kubeba vijitanzu vingine vidogovidogo ndani ya Riwaya.
 Riwaya zao la kibepari: Riwaya ilizuka katika mfumo wa kibepari huko Ulaya , Riwaya
ina sifa ya ubinafsi, ina uhitaji mkubwa wa viwanda nah ii ilianza ktk kipindi cha
mapinduzi ya viwanda hivyo inahitji uchumi madhubuti kama vile uandishi na uchapaji.
 Riwaya iko karibu na uhalisia, inahusisha masimulizi ambayo yalikuwepo,,,,, yapo,,,,,au
yanatazamiwa yatokee na whusika hujengwa katika mazingira hayo.
 Riwa inahitaji ujuzi wa kusoma na kuandika.
 Riwaya inahitaji maisha tulivu,,,,, maisha anbayo yatamfanya mtunzi awe katika hali ya
kutunga Riwaya.


AINA ZA RIWAYA:
Riwaya zinagawanyika katika makundi makuu mawili ambayo ni;
RIWAYA DHATI; Hizi ni Riwaya ambazo zina mambo dhati, wasaha na mambo ambayo
ni adili kwa binadamu. Hutumia lugha fasaha, nyofu na hakuna matusi. Mfano ‘Kosa la
Bwana Mussa’, ‘Mzimu wa Watu wa Kale’, ‘Utengano’ na ‘Almasi za Bandia’.
RIWAYA PENDWA; Hizi huzungumzia maswala ya upelelezi, mapenzi na mambo
mengine ambayo ni pendwa. Riwaya pendwa huchomaza zaidi vipengele vya fani kuliko
maudhui. Mara nyingi hutumia methali, misemo na mbinu nyingine ambazo humfanya
msomaji asitafakari zaidi maudhui. Mfano: Pendo la Kifo, Njama, Kikosi cha Kisasi,
Nyuma ya Pazia na Mfadhili.


AINA ZA RIWAYA KWA KUZINGATIA VIGEZO
 KIGEZO CHA FANI:
Riwaya sahili; Hii ni aina ya riwaya ambayo ina muundo rahisi na
inaweza kueleweka kwa urahisi. Kwa mfano; riwaya ya “Mkwamo-Masereka Levi Kahaika”.
Riwaya changamano; Ni riwaya ambayo ina muundo mgumu na inayohitaji umakini kuielewa.
Kwa kawaida msuko wa riwaya hii huwatata. Inawezekana pakawepo na matumizi mapana ya
mbinu rejeshi,upana mkubwa wa wahusika na mandhari, matumizi mengi ya lugha ya kitamathali, mfano; “Mzingile” ya E. kezilahabi, “Zirail na Zirani” ya W.E Mkufya.
Riwaya ya majaribio, Ni riwaya inayojadili mkondo wa nafasi na riwaya kweli. Riwaya ya mjadala nafsi hutungwa bila kuzingatia kanuni za kawaida za uandishi wa riwaya, watunzi wa
riwaya hii hudai kuwa kumbo la kawaida ya riwaya hii haitoshelezi mahitaji ya karne hii huwakilisha ukweli wa maisha. Riwaya hizi hutumia nafsi ya pili na wakati mwingine hutumia
nafsi mimi kiasi kwa mwandishi ndiye mhusika. nafsi ya pili humfanya msomaji kuonekana
kuwa ndiye katenda jambo. Mfano, “Mtunzi wa Hukumu” ya Kasri na “Bina-Adamu” na Musaleo” za Wamitila vilevile Nagona na Mzingire zake E, Kezilahabi.

USIMULIZI:
Riwaya barua ni riwaya ambayo huwa na muundo wa barua kuanzia mwanzo hadi mwisho, au
ni majibizano ya barua. mfano “Pamela” ya S.Richardson na “ Barua Ndefu kama Hii.
Riwaya ya kimonolojia ni riwaya ambayo sauti inayotawala ni moja. Sauti hiyo ni ya
mwandishi. Wahusika wanaopatikana katika riwaya hii hudhibitiwa kwa kiasi kikubwa na sauti
ya mwandishi. Mfano “Walenesi” na “Mafula” za Katama Mkangi.
UPEO WA KIJIOGRAFIA:
Riwaya ya kiambo; ni riwaya ambayo inatilia mkazo kwenye mandhari, usemi au muundo wa
kijamii na desturi za mahali maalumu. Mandhari na mahali huathiri njia mbalimbali za kuhisi na
kuwaza kwa wahusika wanaopatikana kazi ya aina hii. Huelezea mambo ya tamaduni mfano,
‘Bwana Myombokera na Bi Bugonoka’, watu wa Ukerewe na ‘Kisiwa Cha Giningi’.
Riwaya ya kidastopia hii husawili jamii isiyokuwa ya kawaida na isiyokuako kwa wakati
maalumu bali inafikirika tu. Katika jamii hiyo sheria za kawaida za kijamii zimebadilishwa kwa
namna inayowafanya watu wengi waishie kutaabika na kuteseka sana. Mfano wa riwaya hizi ni
kama vile “ Kusadikika” ya Shabani Robert na “Walenisi” ya Katama Mkangi.
Riwaya Kitaifa; hizi hujikita katika upeo wa kijiografia ambapo haivuki mipaka ya nchi.
Maudhui na mawanda huwa ni yamambo yanayojiri katika taifa husika,
Riwaya za Kimataifa; Hi ni Riwaya ambazo ni kinyume cha zile za kitaifa kwa hujadili mambo
ya nchi zaidi ya moja, mfano wan chi zinazoendelea na zilizoendelea.


MAUDHUI:
Riwaya historia ni aina ya riwaya ambayo msingi wake kuhusu matukio fulani katika jamii ya
mwandishi, tukio hili huwa ni kubwa na la muhimu kijamii, laweza kuwa la kikabila au la kitaifa
mfano “Uhuru wa Watumwa” ya J. Mbotela, “Miradi Bubu ya Wazalendo” ya Luhumbika na
“Zawadi ya Ushindi” ya B. Mtombwa.

Riwaya ya kimaadili ni riwaya ambayo ina nia ya kufundisha maadili fulani mfano “Kufikirika”
ya S Robert. Ni riwaya inayotoa maadili kwa jamii. Riwaya hizi huelezea mambo ya dini,
mafunzo na maonyo ya maisha. Hujengwa katika nguzo tatu ambazo
a. Mathema (kosa): Kosa analolifanya mhusika mkuu linafanya jamii ipate shida. Kosa hilo
humfanya mhusika ajifunze na jamii ijifunze.
b. Pathema (Funzo):Mafunzo anayoyapata mhusika juu ya kosa alilolifanya,
c. Cathersis (utakaso): Utakaso unapatikana baada ya funzo na kubadilika.
Riwaya ya kimapinduzi ni riwaya ambayo inajadili migogoro namaisha ya binadamu kwa
kutafakari kwa mantiki na kina kuhusumambo ambayo urazini wake hauonekani kwa
urahisi.Hudodosa mapambano, mikinzano na matabaka katika jamii Mfano“Umleavyo” ya Haji
na Kichwa Maji” ya E.Kezilahabi, vilevile na Dunia mti mkavu na Kusadikika.
Riwaya ya kisosholojia au jamii ni riwaya ambayo inasawiri maisha ya kawaida ya jamii kwa
kuchunguza matatizo yake, yawe kifamilia kitabaka, kiuchumi, kisiasa au hata kiutamaduni
mfano “Titi la Mkwe” ya A. Banzi, “Kurwa na Doto” ya M.S. Farsi na “Rosa Mistika” ya E.
Kezilahabi.
Riwaya saikolojia ni aina ya riwaya inayododosa nafsi ya mhusika, fikra, hisia mawazo, imani,
hofu, mashaka, matumaini na athari ya mambo hayo kwake binafsi na labda kwa jamii mfano
“Kichwa Maji” ya E.Kezilahabi, “Kipimo cha Mianzi” ya Feud na “Kiu” ya M.S. Mohammed.
Riwaya ya kifalsafa, ni riwaya ambayo inashughulikia masuala ya kifalsafa. Mada ya kifalsafa
huchukua sehemu muhimu katika riwaya ya aina hii kuliko wahusika, mandhari, msuko au
mtukio.Mtunzi hutaka wasomaji wafikirie kifalsafa mambo Kama vile kuwepo au kutokuwepo
kwa MUNGU, Baadhi ya viumbe, kufa na kuishi ni nini? Utu na mtu nini? Mfano, “Nagona na
Mzingile” ya E kezilahabi na “Umleavyo” ya Haji Gorra Haji.
Riwaya ya mapenzi ni riwaya yenye kusawiri uhusiano wa kimapenzi kati mvulana na
msichana. Huchomoza zaidi fani kuliko maudhui, Mfano “Kweli Unanipenda” “Mwisho wa
Mapenzi” za Simbamwene.

Riwaya ya kitawasifu, ni riwaya ambayo ina muundo unafanana na muundo wa tawasifu kwa
kuyachunguza maisha ya mtu fulani na kwa nafsi ya kwanza. Mfano riwaya ya “Uhuru wa
watumwa” J. Mbotela na “Maisha Yangu baada ya Miaka Hamsini” ya S.Robert.
Riwaya ya wasifu, ni riwaya ambayo mwandishi huandika kwa lengo la kumhusu mtu fulani,
mfano “Wasifu wa Siti Binti Saad” ya S. Robert.
Riwaya ya ujasusi ni wa upelelezi wa kimataifa. Majasusi ni wapelelezi wanaotumwa na; nchi,
serikali au waajiri wao kwenda katika nchi nyingine kuchunguza siri zao hasa siri za kijeshi,
kiuchumi na kisayansi ili taarifa hizo ziwanufaishe wale waliotumwa mfano “The thirty nine
steps” ya E. Msiba. “Mzimu wa Watu wa Kale”.
Riwaya ya kisayansi ni riwaya inayotumia taaluma ya sayansi kama msingi wa matukio,
masahibu na maudhui, mathalani riwaya hii hubashiri namna sayansi itakavyoathiri maendeeo ya
mwanadamu katika karne zijazo. Mfano “Safari Kiini cha Dunia” ya Jules Vernes.
Riwaya tendi ni riwaya yenye mawanda mapana kama tendi aghalabu riwaya hii husawiri
matendo ya ushujaa na masuala mazitoya kijamii yenye kuathiri historia ya taifa husika. Mfano
“Vita naAmani” ya Leo Tolstoi na “Chaka Mtemi wa Wazuru” ya Thomas M.
Riwaya istiara ni riwaya mafumbo ambayo umbo lake la nje niishara au kiwakilishi tu cha
jambo jingine. Mfano “Kusadikika” yaS.Robert ambayo inasawili utwala wa mabavu na
“Shamba la Wanyama” ya Kawegere
Riwaya chuku ni riwaya ambayo hueleza vituko na masahibu yasiyo kuwa ya kawaida, ni riwaya
ambayo haizingatii uhalisia namara nyingi masahibu yake huambatanana mapenzi.Mfano “Alfu
lela Ulela” ya G. Bocci ccio na “Kusadikika” ya S.Robert”

Riwaya ya kingano, ni riwaya yenye umbo na mtindo wa ngano mathalani huweza kuwa na
wahusika wanyama,visa vyenye kutendeka nje ya wakati wa kihistoria. Mfano “Lila na Fila” ya
Longman na “Adili na Nduguze” ya S. Robert
Riwaya kinzani ni riwaya inayotumiwa kuelezea ambayo imekwenda kinyume na matarajio au
kaida za uandishi wa riwaya. Mfano, kuwana muundo wa kimajaribio wahusika kukosa motisha,
kuwako kwamatendo yasiyoweza kuungwa kimantiki.
Riwaya ya utetezi hii hutumiwa kuielezea riwaya ambayo inahusu matatizo ya kijami, kiuchumi
pamoja na dhuluma inayowapatawanyonge au wasiokuwa na uwezo katika jamii fulani. Hivyo
riwayahii hukusudia kurekebisha hali iliyopo katika jamii. Mfano “Uhasama Kilimani-Masereka George Black” ambayo inazungumzia usambalatishi wa mfalme Kamanzi na ukombozi wa watu na “Kuli’ na “Vuta n’kuvute” za Shafi A.Shafi.
Riwaya ya kipolifoni; ni riwaya ambayo inahusishwa na urejeleaji ambapo kila wahusika
wanapozungumza au kuongea sauti zao mbalimbali zinawakilisha mikabala mbalimbali kiitikadi.
Mfano “Duniamti mkavu” ya S.A Mohamed.
Riwaya ya kisiasa; ni riwaya inayohusu wanasiasa na maisha yaowanasiasa. Hudhamiria
kuyafichua mambo yanayotendeka kinyumena picha inayoonekakana waziwazi. Mfano; “Nyota
ya Huzuni” ya George Liwenga na “Njozi Iliyopotea” ya C.G. Mng’ong’o.
Riwaya ya kitarihi ni riwaya ambayo inajihusisha na mawanda makubwa ya kiwakati na
kimandhari.Wahusika wengi walioteuliwakuakisi hali mbalimbali za kijamii na kiuchumi za
wakati maalumu.Mfano;Riwaya ya “Habari za Wakilindi”
Riwaya ya kiutopia hii ni riwaya ambayo inasawiri jamii anayoiona mwandishi kama jamii
kielelezo na aghalabu huhusisha sifa zaKifantasia au kinjozi. Mfano wa riwaya hii ni kama,
“Siku ya Watenzi Wote” ya Shaaban Robert.
Riwaya ya kiurejelevu hii ni riwaya inayojirejelea. Aghalabu katika usimulizi wake, riwaya ya
aina hii huishia kutoa maoni kuhusu usimulizi wake na njia za kubuni na kutunga riwaya. Tunawezakusema hii ni riwaya inayofichua mbinu zake za kiutunzi. Mfano“Musaleo” ya
K.W.Wamitila.
Riwaya tatizo; ni riwaya ambayo inajishughulisha na tatizo aumgogoro fulani katika jamii.
Huweza pia kuelezea aina ya riwayaambayo inachunguza tasnifu au swala fulani la kisaikolojia.
Mfano;“Kuli” ya Shafi A.shafi na “Mafuta” ya K. Mkangi.
Riwaya kampasi; ni riwaya ambayo mandhari yake ni chuo kikuu. Hata hivyo hii imepanuliwa
nakuhusishwa na kazi za kuchekesha auzenye mwelemeo wa kitashititi. Kazi za aina hii
hukusudia kufichuaudhaifu uliopo katika tabia za wanachuo.Mfano; “Small world” yaDavid
Lorge.


NADHARIA ZA UCHAMBUZI WA FASIHI
Wataalamu mbalimbali wameainisha nadharia mbalimbali za uchambuzi wa kazi yoyote ya
fasihi. Miongoni mwa nadharia hizo ni pamoja na;
(i) Nadharia ya umuundo (structuralism)
Umuundo ni nadharia inayojibainisha kwa kuangalia Ujumla wa uhusiano wa sehemu moja kwa
nyingine katika kufanya kitu kizima. Kwa mfano muungano wa maneno hufanya sentensi na
sentensi zikiungana zinaunda aya au onesho na onesho kuunda tamthiliya. Ntarangwi (2004)
anasema kuwa umuundo waweza kuelezwa kama mtizamo wa kitathimini ambao huzingatia
zaidi miundo inayojenga kazi binafsi.
Mwasisi anayetajwa sana katika nadharia hii ni Ferdinard De saussure aliyependekeza mtizamo
mpya kuhusu lugha. Kinyume na wataalamu wengine walioshughulikia historia na sura maalumu za lugha fulani, Saussure alivutiwa na miundo inayohimili lugha zote, huku akijaribu kuonyesha
kwamba lugha zote za ulimwengu zaweza kutathiminiwa kwa kaida maalum za umuundo.
Alizua istilahi parole' na langue’ kueleza maoni yake: `Parole’ au uzungumzi ni lugha katika
matumizi na hiki ndicho walichokizingatia wanaisimu wa awali,
Mkondo huu wa mawazo ya umuundo kuhusu sayansi za jamii ulianzia ulaya na kuathiri
mtazamo wa elimu mbalimbali (duniani) kama vile: Falsafa, Anthropolojia, Historia, Uhakiki wa
kifasihi na Sasiolojia. Kwa hivyo twaweza kuangalia jamii katika muundo wake wa kijuu juu na
kuielewa lakini tukitaka kupata maana mwafaka lazima tuchunguze muundo wake wa ndani
ambao hupatikana katika kila jamii ya wanadamu. Kwa hiyo hata katika kuielewa fasihi lazima
tuifahamu lugha yake.


UMUUNDO NA FASIHI
Kama vile muundo wa lugha ulivyo mfumo, muundo wa fasihi pia una vipengele
vinavyotegemeana na vinavyoelezwa katika muktadha wa vipengele vingine. Katika kazi ya
fasihi kuna kitengo cha kisanaa kama vile maudhui, ploti, wahusika, muktadha na lugha. Hakuna
kipengele cha fasihi kati ya hivi kitakachoelezwa katika upekee wake. Lazima kielezwe kwa
kuzingatia kuwepo kwa jukumu la vipengele vingine. Kwa mfano katika kueleza au
kuzungumzia ploti, wahusika watashirikishwa na lugha yao kuzingatiwa. Kwa hiyo nadharia ya
umuundo husisitiza vipengele vya kazi ya sanaa, jinsi vinavyohusiana hadi kuikamilisha kazi
hiyo. Huangalia namna sehemu mbalimbali za kazi za sanaa zilivyofungamana. Yaani Neno
halihitaji urejelezi ili lipate maana, na Kazi yenyewe ilivyoundwa ndivyo hutoa maana. Yaani
maana inavyoumbwa ina dhima kubwa kuliko maana yenyewe.


(ii) Nadharia ya umarx (marxism)
Kwa maana rahisi kabisa, tunapoongelea kuhusu nadharia ya UMarx tuna maana ya kurejelea
mikabala mbalimbali ambayo misingi yake mikuu ni mawazo yanayohusishwa na Carl Marx na
Friedrich Engels. Katika kitabu cha The Germany Ideology, Marx na Engels walisema kuwa kitu
cha msingi katika maisha ya binadamu ni kula na kunywa, kupata malazi na mavazi na mambo
mengine. Tendo la kwanza la kihistoria kwa hiyo ni kutafuta njia ya kuyakidhi mahitaji haya ya
msingi. Ili kufanikiwa katika lengo hilo, binadamu hulazimika kujiunga pamoja au kuunda umoja
ili kuimarisha umoja na wepesi wakuizalisha mali ya kukidhi mahitaji hayo. Muungano huo
huwa na ugawaji wa majukumu au kazi ambayo ndiyo msingi wa kuundwakwa matabaka katika
jamii.


Umarx katika Fasihi
a. Usanii ni uumbaji wa Ukweli katika maisha.
b. Ukweli unaooneshwa katika kazi za fasihi hiyo ni usahihi wa mambo katika jamii? Kama
ni Riwaya, Tamthilia, Ushairi na kadhalika
c. inawakilishaje ukweli?
d. Kazi za kisanaa zinatakiwa kuonesha mivutano iliyopo katika jamii hasa kati ya
wanyonyaji na wanyonywaji.


(iii) Nadharia ya urasimi
Kwa mujibu wa Njogu na Wafula (2007) Urasimi ni wakati maalumu ambapo misingi ya kazi za
sanaa huwekwa na kukubalika kuwa vipimo bora kwa kazi nyingine. Hii ina maana kwamba kila
jamii ina urasimi wake. Urasimi katika Kiswahili ulikuwepo kati ya karne ya 18 na karne ya 18.
Nao urasimi wa Kigiriki ulikuwepo baina ya karne ya nne (KK) na takriban karne ya nne (BK).


Sifa za urasimi kwa ujumla
Pamoja na kwamba imeshatajwa hapo mwanzo kuwa kila jamii ina urasimi wake, lakini bado
tunaweza kutoa sifa za jumla za urasimi mahali popote ulipo. Kwa mfano:


a. Kazi ya kirasimi huwasilishwa katika lugha inayoeleweka kwa urahisi. Hii ina maana
kuwa wazo linaelezwa moja kwa moja. Mitindo ya Kinjozi (mf.Nagona, Mzingile, Bina-
Adamu, Walenisi) haitumiwi.Uhalisia unasisitizwa.


b. Kazi nyingi za kirasimi hazichoshi kusoma. Hii ni kwa sababu kazi hizi ni kazi bora.
Husomwa mara nyingi na watu wengi na kila unapoisoma wazo jipya hupatikana.


c. Fani na maudhui katika kazi za kirasimi ni mambo yaliyofinyangwa kwa kutumia mbinu
kamilifu na teule. Daima kuna ufungamano uliokamilika kati ya kinachoelezwa na jinsi
kinachoelezwa.

Marejeleo.

omukabe-2019

24 thoughts on “RIWAYA YA KISWAHILI NA SIFA ZAKE

    1. RIWAYA DHATI; Hizi ni Riwaya ambazo zina mambo dhati, wasaha na mambo ambayo
      ni adili kwa binadamu. Hutumia lugha fasaha, nyofu na hakuna matusi. Mfano ‘Kosa la
      Bwana Mussa’, ‘Mzimu wa Watu wa Kale’, ‘Utengano’ na ‘Almasi za Bandia.

      Riwaya dhati hukusudia kuchora tajriba ya mwanadamu kwa kutumia mambo halisi yanayomzunguka yaani inajishughulisha moja kwa moja na uhalisia wa maswala ya kila siku ya jamii, maswala yanayotambuliwa kuwa “halali” kushughulikiwa na fasihi. Inaweka maudhui mazito ambayo yanatokana na kutathmini na kuchunguza maisha ya mwanadamu. Riwaya dhati imepewa dhima ya kuziangalia nyanja zote za maisha na kuzingatia tafsiri tofauti za kimaadili. Katika riwaya dhati, dhima ya kuburudisha imepewa mipaka yake kisanii kwa kiasi ambacho nafasi kubwa huchukuliwa na dhima ya kufunza na kuelimisha jamii. Maswali yanayorejelewa sana na riwaya hizi ni kama vile ukombozi, uongozi, ukoloni mkongwe na ukoloni mamboleo, malezi, utamaduni, elimu na kadhalika.

      Like

Leave a comment