Namna Tanzu za Sarufi Zinavyokamilishana
Umewahi kujuliuliza namna Tanzu tofauti za Sarufi zinavyosaidiana na kukamilishana?
Fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki ni Tanzu ambazo mmoja hauwezi kuwa na maana bila msaada wa utanzu mwingine.
Kwa hivyo, hizi Tanzu Tanzu zinafanya kazi pamoja ili tamko, neno, sentensi yeyote iweze kuwa na maana.
Kwa upande wa mofolojia, maneno huundwa na mofimu na mofimu huundwa na na sauti. Uundaji wa mofimu hufauata taratibu maalum za mfuatano wa sauti za lugha husika. Kwa hiyo basi kutokana na uhusiano mkubwa uliopo kati ya fonolojia na mofolojia ya Kiswahili, vitu hivi viwili haviwezi kujadiliwa katik upeke wake bali lazima vifuatane kwani vinategemeana sana. Huwezi ukajifunza mofolojia kabla hujapata kuelewa kwa kutosha kuhusiana na fonolojia ambayo inajadili lugha katika kiwango cha sauti halafu mofolojia inafuatia ambayo huzungumzia lugha katika kiwango cha maneno.
Kwa ujumla uhisiano wa tanzu za isimu unaweza kuelezwa kama ifuatavyo:
Ili kujifunza lugha yoyote ile inabidi kuanza na sauti uchunguzi wa sauti za lugha hiyo ambazo huchunguzwa chini ya mchakato wa kifonolojia. Ukishafahamu sauti za lugha husika inabidi uchunguze mchakato unaotumika katika kuunda maneno ya lugha husika ambao hujulikana kama mofolojia.
Ukishafahamu mchakato wa uundaji wa maneno katika lugha inabidi ujue mpangilio wa maneno hayo katika tungo zenye maana. Mchakato unaoshughulikia mpangilio wa maneno katika tungo na kazi za maneno hayo katika lugha husika hujulikana kama sintaksia. Baada ya kujua mpangilio wa maneno katika tungo na kazi za maneno hayo inabidi kujua maana za maneno katika tungo hizo. Kwa hiyo basi mchakato unaohusiana na maana katika lugha hujulikana kama semantiki. Katika suala la maana ya maneno na tungo mbalimbali kunahitajika kujua maana mbalimbali za maneno kulingana na muktadha, kwa hiyo tanzu ya sarufi inayoshughulikia maana kulingana na muktadha inajulikana kama pragmatiki, lakini tawi hili ni sehemu ya semantiki kwa sababu yote mawili yanashughulikia maana katika lugha na si miongoni mwa tanzu kuu za isimu au sarufi.
