MWONGOZO WA KUFA KUZIKANA

MWONGOZO MKAMILIFU
WA
KUFA KUZIKANA












Simon T Kawaida
na
Johnpaul Arigumaho






@2022






RIWAYA: KUFA KUZIKANA
MWANDISHI: KEN WALIBORA
MWAKA: 2006


Utangulizi:

Riwaya hii iliandikwa na Ken walibora mwaka wa 2003 na kuchapishwa mara ya kwanza 2006.
Kufa Kuzikana ni hadithi ya urafiki kati ya vijana wawili, Akida na Tim, wanaotoka kwenye makabila yenye uadui. Ni hadithi ya migogoro, mingongano, vikwazo na vizingiti katika uhusiano wao. Je, urafiki wao huo unaweza kuvistahimili vishindo hivyo? Je ni urafiki wa kinafiki au una nguvu ambazo hazishindiki?
Riwaya yenyewe huzungumzia maswala ya kiuhalisia yaani;
Ukabila na utamaduni, maadili na mapenzi, usawa wa kijinsia na uhuru wa mtu binafsi. Hayo yote hujidhihirishwa na hulka/tawasifu au namna mwandishi alivyochora wahusika wake na kuwapa majukumu mbali mbali.


Dhamira ya mtunzi: Mtunzi katika Riwaya hii analenga kuonyesha athari mbaya wa ukabila yaani anaonesha ukabila kati ya makundi mawili yaani wakanju na wakorosho wanavyo chukiana, wanavyouana, wanavyotusiana kwamfano katika Uk 26 ambapo Akida na Tim wanapo mtembelea mjombake Tim na kusema eti Hakuna mkanju ana mke mmoja, wakanju wanapenda matanga sijui matanga ya mjomba, sijui matanga ya binamu ……… wataanzahata kuenda matanga ya mbwa na paka…
Hayo yote yajitokeza wakati mjombake Tim anapomwuliza kuwa babake ana wanawake wangapi?
Kweli kweli, ukabila katika nchi ya kiwachema umejenga ghorofa katika mioyo ya wananchi hii na wengi wao waameathiriwa vibaya kama kupoteza nafasi serikali, kupoteza maisha na kuongeza chuki nchini nzima.
Vile vile ; mwandishi yataka kuonyesha urafiki wa dhati au kufa kuzikana ingawa ni wa kabila tofauti tofauti yaani Akida ni mkanju na Tim ni mkorosho lakini wanakutania shuleni na wapendana, nyumbani wanachukiana wanauna katika vita vya kikabila na kwa hivyo, mwandishi anataka kuonyesha dhima ya urafiki hata urafiki wa dhati au wa ukweli ambao unakumbwa na vizingiti au vikwazo mbali mbali lakini wao wakendelea daima dawamu.


Mandhari: Riwaya hii mandhari yake ni kiafrika hasa hasa nchini Kenya kwani mahali mengi yanayozungumziwa yanahusiana sana kama:- kiwachema, sangura. Vile vile mandhari yake ni ya kiafrika kwani maudhui mengi yanayojengwa yanahusu sana mambo yanayokumba nchi za kiafrika kama;- ukoloni mamboleo, usaliti, ukabila nk.
Pengine: Riwaya hii, kiwakati ni ya kisasa kwani inazungumzia mambo ya kisasa ; elimu, urafiki wa kisasa na mitazamo mipya kuhusu ukabila kulingana na uchoraji na maudhui husika na utendaji wake.


Jalada: Mwandishi ametumia picha mbali mbali yaani wahukika wawili wanonyesha nyuso zenye huzuni na machozi yakitiririka, ishara kuwa kuna mambo ambayo hayaendi vizuri.
Pengine, Jina lake “Ken Walibora” limeandikwa kwa rangi nyekundu ishara kuwa kuna matatizo mengi yanayosheheni riwaya nzima.
Isitoshe, Kwa jalada/gamba lenyewe kuna vibanda ambavyo vimechomeka na moto na kuna mbwa ambaye anatafuna kitu Fulani labda yaweza kuwa mifupa ya watu ambao wananauawa kwa vita vya kikabila.

UCHAMBUZI WA RIWAYA YENYEWE KWA UJUMLA (PLOTI)


Riwaya yenyewe huanza na mhusika Akida akienda mjini- kiwachema ili aweze kuzawadiwa na wizara ya elimu baada ya kuwa miongoni mwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa yaani akawa mtu wa tatu nchini Kiwachema.
Uk01, Akida wanapofika, Tungule anakumbuka kifo cha mamake aliyefariki katika ajali walipokuwa wakienda huko mjini.
Vile vile, Akida anaenda mjini ili apate kujua mswada wa babake umefika wapi yaani babake yu mgonjwa na ana matumaini mingi kuona mswada wake ukichapishwa.
Akida anakumbuka mwalimu wake Alex aliyekuwa mkorosho kama Tim mtegemezi wake jijini ingawa wakorosho wengi hawakumpenda kwasababu alikuwa na ushirikiano mkubwa na wakanju.
Anakumbuka manemo ya mbunge Jonhstone mabende katika kituo cha biashara cha Baraki akiwatusi wakanju akisema “ Hatutaki madoadoa, wakanju wahame waende kwao kanju……… Uk 02.
Akida na wenzake kwenda kwa mzee mangala ambaye ni mmoja wao watu wachache wenye redio kijijini ili waweze kusikiliza matangazo ya mpira ….Uk 03. Kwani Timu ya taifa ya Kiwachema ilikuwa inashindana na Timu ya Kenya na mambo ya ukabila yakaibuka sana wakisema wale wachezaji ni wakorosho yaani Timu ya Taifa haiwezi kukamulika bila wao……. Uk 04
Kuuawa kwa mwalimu Alex, na wakorosho kudai kuwa wakanju ndio waliomuua na kudai kuwa wahamie kwao kanju na ishara ya vita vya kikabila zikaonekana sana…….uk 6


Sura ya Pili
Akida kufika jijini Tandika uk 07, mara yake ya kwanza na kwa mshangao mkubwa.
Anamtegemea sana Tim, mkorosho biniye mzee Zablon, aliyemsasidia kutokana na wachokozi shuleni….. Uk 08, kutokana na hayo wakaanza kuitana “shemeji” ingawa ni jambo la nadra sana mkanju kumwoa mkorosho….. Jambo jingine Akida hakubahatika nadada yeyote ………Uk 8.
Tim akawa Rafiki yake wa kufa kuzikana nap engine alioea sana kuja kwao kusuhudia kipawa cha babake mzee sululu mwenye kipawa cha utunzi nyimbo na ala hizo…. Uk 08.
TIM akawa Rafiki yake wa kufa kuzikana na pengine alizoea sana kuja kwao kusuhudia kipawa cha babake mzee sululu mwenye kipawa cha utunzi nyimbo na ola hizo……….Uk08
Isitoshe, anapenda sana kutokan na siku ile alipomponya kutokana na janga la kuumwa na nyoka alipokuwa bado mtoto mdogo………Uk 09
Jambo la kwenda Jijini Tandika ni jambo ambao linahusiana sana na watu wanaokwenda kwa mahakama kwa ajili ya keshi zao au labda kwenda kwa hospitali kuu ya Rufaa Jijini..Uk09
Babake Akida kumwambia ili aende kwa Bwana Gembo apate kujua madai ya malipo ya bima ya hayati mamake. Pengine aende kwa hatubagui publishers…………….uk 11
Uk 11, kwa ukunjufu na Bashasha, tim anampokea shemeji yake…… wakaenda mkahawani wakala na wakanywa na Akida akashangaa kwa chakula walichowaletea kwani yeye alizoea na vyakula vya kijiji siyo chips na sauages………………….
Uk 13, wanaulizana habari tofauti tofauti kuhusu nyumbani, ndipo Akida kamwelezea kufeli kwa Tamari mitihani, Tim akamwambia eti” kila mwaka nyie mwapata mazo bora kuliko wazee wangu..
Uk 14, anaona friji mara yake ya kwanza ingawa alikuwa akisoma vitabuni. Pengine, David kwenda ghafla anapoonana na Tim mkahawani kwani alikuwa na deni lake la muda.
Uk 15, Tim anamfurahia Akida na kumwambia eti atasoma na kuwa profesa kwa maporofesa..
Uk 16, Akida alipoona wanawake waliokuwa nusu uchi…………. Wakati wanapokwenda kwa Tim shauri moyo………….


Sura ya Tatu
Tim alikuwa anafanya kazi ya ukarani kwenye kiwanda cha kusindika mafuta baada ya kufeli mitihani…. Uk18
Uk 18, Akida kutumia Taulo na kuoga maji ya bafu la manyunyu mara yake ya kwanza na akashangaa sana Uk 20, Akida anamuuliza nani pichani? Naye Tim akamwambia eti ni dadake wa kirohoni….pamela kutoka sangura.
Uk 20-23, Akida kumtembeza jijini kokote baada ya kumwomba ruhusa mjombake kazini……….
Uk 23, kumtembelea mjombake Tim na kumkuta msichana mdogo akisoma kitabu “war and peace” na Akida akama viatu vyake ambavyo vilikuwa na mnuko kama mayai yaliyooza waliokuwa wakitazama filamu walidai…………………… Uk 24.
Uk 28, mjombake Tim kuja na kawasalimu—Tim kumjulisha kwa mjombake na akasema Akida kwa ni mkanju mjombake akakasizika akasema “Hakuna mjinga kama mkanju…… mimi sifihi kitu …. Babako ana wanawake wangapi? Akamuuliza naye akasema Akida mmoja ……… uk 26 akaendelea hana number two?” mkani wa aina gani? Wakanju wanapenda mazishi……….”
Uk 27, Tim na Akida kufanya mradi na mipango ya kutembelea ofisi ya Bwana Gembo, Hatubagui publishers…..
Uk 28, 29, 30 , Habari ikatolewa kuwa vita vya kikabila vimeendelea wilayani korosho hasa eneo la Baraki na watu kunawa, Tim akakanusha habari hiyo…….. na kulikuwa na propanganda kwani sauti ya kiwachema husema hakuna vita na BBC, husema vita vimepanda moto….. uk 29.



Sura ya Nne
Tim kwenda kazini na Akida kwenda jijini kutafuta gazeti lakini kwa bahati mbaya hakupata kitu, polisi ikawafukuza wauzaji wa magazeti………. Uk 31, na Akida kupotelea njiani kuelekea shauri moyo- wa Tim. Vilevile, Akida kuona vigoli vikichizea mtaroni na kuambiwa eti, usivione vidogo hivyo….. mazee usiku vina kwenda na wenye pajero na mabenz…. Uk 33
Uk 33, Akida kumpumzika kidogo baada ya kuchoka kwa matembezi na viatu vyake alivyomwazima shemejiye – Tim kuibiwa ndipo akasema “chaka la simbahalilali nguvuwe”. Baadaye akakutana na binti mrembo aliyemsaidia kwa kumwonyesha barasbara kuelekea shauri moyo,,,,,… Uk 34.


Sura ya Tano
Tim na Akida kukutana nyumbani na kujitia kwa utani “Nilidhani mambo ni yamkono kumbe ni ya upembo……. Uk 35 Akida akifanya mzaha kwa Tim.
Uk 35-36, pam kipenziche Tim kamtembelea na kukumbatana kwa mapenzi sana “uchumba piani wakati wakufumbia macho makosa ya mchumba. Wakati wa kujikiri mtu ni maasumu. Hukumbuki Kasisi John alivyotahadharisha kwenye mahubiriye mara nyingi ? Kuwa wakristo wanaochumbiana waweza kupoteza udhibiti wa utashi wao- wakijikuta wamefanya dhambi kama vile Daudi alivyofanya na mkewe uriah …….uk 36
Uk 38, Akida kuwaimbia ubeti mmoja wapo wa wimbo wababake; na wote wakzana mapenzine.
Uk 40, kwenda kwa bwana Gembo, Akida na wenzake kuuliza malipo ya bima ya mamake aliyekufa ajalini lakini sekretari hakuwapatia ufadhili wowote labda akaendelea na kazi yake ndipo Akida akakumbuka shairi la babake alilomtungia kuhusu hasira kwani alikuwa karibu afanye jambo la ajabu………. Uk42
Watu wote wakasema, tumechoka mpaka tuonane na bwana Gembo atulipe pesa zetu…….. mzee matuko.


Sura ya Sita
Akida na Pam kuenda kwa afisi ya waziri wa elimu kuzawadiwa. Akida alikuwa watatu nchini, Donald Kitenge ndiye aliyekuwa wa pili na msichana Regina ndiye aliyebwaga wote mtihani waTaifa…….Uk 50.
Uk 51, vilevile, wanaongozana hadi ofisi ya hatubagui publishers na kukuta mswada wa babake ulikuwa umetumwa kwake kwa njia ya posta….Uk 52.
Uk 57 Akida kupoteza zawadi yake garini

Sura ya Saba
Asubuhi na mapema, Akida yuko nyumbani kwa Tim, akawaza nakuwazua matendo. Yaliyofanyika kumkamata mikononi waziri wa elimu yeye mwenyewe na kupoteza zawadi yake garini…….uk 58
Anasoma kitabu cha babake, kero za mkiwa, mawazo juu ya kijiji cha Baraki na kiwachema yakazidi kwani Tom biniye mzee mangala akawelezea habari kuhusu kwao… Tom akaoa mzungu…… uk 59.
Wote waamezama kwa mawazo tele baada ya kusikia habar ikuhusu vita vya kikabila na kudai kuwa wadadisi wa mambo wanasema. Ingawa makabila hayo mawili yamekuwa na chuki baina yao, huenda vita hivyo vimechochewa na watu wenye usawishi mkubwa wa siasa…… uk 61.
Uk 62, kifo cha matuko aliyejitupa kutoka ghorofa (22) ya Tembo House baada ya wakili wake Bwana Tony Gembo kukataa kuonana naye juu ya malipo ya bima yake.
Sasa, Akida yajiuliza iwapo ataweza kuwa na bahati ya kwenda kwa shule ya taifa,…… Uk 65, nipande ghorofa nijitupe kama mzee Yusufu Matuko?……………. Akida akaanza. kujiuliza.


Sura ya Nane
Pam anamkaribisha Akida na kumjulisha kuwa Tamari yu mgonjwa …… Uk 67, kuleta habari kuwa kwao Baraki wilayani korosho vita vimepamba moto.
Habari ya kifo cha mzee sululu kuwa maiti yake imelazwa kwa mochware na Akida kwenda kwa hospitali nakukagua maiti hiyo nakusema kuwa si babake…… Uk 70-71


Sura ya Tisa
Wakaaenda hospitali ya Rufaa ya Tandika iliyojengwa wakati ule giza la ukoloni na wakakuta wagonjwa wengi kutoka korosho wamelezwa papo hapo kwamfano mzee uledi ambaye bintiye Regina alisoma naye Akida darasa moja huko Baraki, wanafunzi wangemwiita Regina “mtawa” kwa jinsi alivyojitenga kabisa na mambo ya kimapenzi……uk 74. Na mzee uledi akielezea namna alivyomsawisha mzee sululu ili waepuke vitisho na vita vya wakorosho lakini mzee sululu hakuweza…..uk 78.

Sura ya Kumi.
Tim na Akida kumtembelea Tom mtotowe mangala mwenye, bibiye mzungu….. Jenelle, wakati wanapotoka kwa Rufaa ya hospitali.
Vilevile , kifo cha kighafla cha mzee mangala……. Uk 85 mwili wa mzee Mangala ulikuwa katika hospitali ya nduchi ……..Uk 86 -. Uk 90, wakidai kuwa watupilie mbali majina kama sululu au mangala kwani yatambulisha sana kikabila.
Uk 91, Tom kufanya mradi wakumzika babake- mzee mangala na polisi ili waweze kuwasindikiza mpaka Baraki ili wamzike mzee mangala kwa heshima.


Sura ya Kumi na Moja
Tom, Akida kwenda kwa mazishi ya Mzee mangala na watu wengine wakisaidiwa na polisi.
Vilevile: kuona namna watu walivyoUawa huko Baraki. Akida akiona mabadiliko ya kwao.
Uk 99, Tom kusema “Baba kama ungalikuwa umesoma” ungalikuwa umewahi kumsikia Antonio. Antonio ndiye aliyesema juu ya mwili wa Juliasi kaizairi “ nimekuja kumzika sio kumsifu kaizairi….”
Tom, kumwahidi Akida kuwa angemfanyia mpango wakwendaCanadaa iliasomee huko kwani ni mtu mwenye vipawa…… Uk 101, na kumwahidi kuwa akitaka kumwoa mzungu ni hiari yake. Naye akasema “ nioe muzungu, nizae wazungu hata wakiitwa chotara, eeh!! Kuoa mzungu! Nitakuwa wa kupigiwamfano kamaTom.
Vile vile wanapotoka mazishini kunazuka ubishi wa ukabila garini wakimtusi dereva kuwa yeye ni mchungwachungwa…..


Sura ya Kumi na Mbili
Akida kumkomboa Tom wakati anapolala chini ya mwembe na kumtia kwa Toroli wakati wakorosho wanaotaka kuwaua na kulikuwemo mzee Zablon ambaye ndiye Rafiki wa kufa kuzikana – Tim….. Uk 107 kwani Tom alikuwa amepigwa mshale.
Uk 108, mwenye gari kumsaidia Akida na kumchukuwa kwa korosho hospitalini na wenye gari hao ni wafanyikazi wa shirika la “Action men” linaloshughulikia kwa kutoa msaada kama; chakula kwa wakimbizi……… Uk 108. Na katika mwendo huo ndipo wanapoona vipande vya watu vikitafunwa na mbwa kando kando ya barabarani……………….


Sura ya Kumi na Tatu
Akida kwenda mtaa wa Falkland, maarufu kwa jina la kambi mchafu kwa simon mwenye duka liitwalo Mla chake ili aweze kumwelekeza kwa Tim aliye kuwa akiishi huko baada ya kufukuzwa kazini na mjombake kwa kuwa na uhusiano mkubwa na Akida- mkanju..
Akida anampa habari Tim kuhusu kupigwa mshale na kulazwa hospitali ya korosho.
Sasa Akida akitafuta kazi ya aina yeyote ndiyo maana akisema “mshoni hachaguinguo yakhe……’ Akida kupatanatena naTamari aliyekuwa anamchukia sana mwanzoni. Tamari akasema “ nisamehe kwa ufedhuli wangu majuzi yale. Amina hebu tuseme uhamasa wangu kwako tangu tukiwa shuleni… Uk 17 Tamari naye vilevile anamwibia Akida et
Nakupenda bila kiasi
Mpenzi ondoea wasiwasi
Hayafi mapenzi yetu sisi
Hayaji ijapo kwa risasi…. Uk 118


Sura ya kumi na nne
Akida kuzoea mtaani Falkland kama mwenyeji na kuishi na Tim kama ndugu yake wa ukweli … Tamari naye vile vile angekwenda kuwafulia nguo matajiri ile waweze kupata riziki ……. Uk 119.
Akida kukumbuka mahuburi ya kasisi John, kuhusu yale maneno yake ya uhalisia na hata ya ukweli kuhusiana biblia kuhusu uesherati, Daudi na Bathsheba, mkwe uri……Uk 121
Akida akiendelea kupatana na Tim kwa hali ngumu sana kwani bidhaa kama sukari, maziwa namkate wakaviondoa kwa orodha yao ya mahitaji, hivyo vikawa vitu vya starehe isiyokuwa lazima …uk 127.


Sura ya Kumi na Tano
Tamari kumsawisha Akida ili waingie mapenzini…… na kukumbuka mahubiri ya Juma pili moja pale mhubiri John alipowahubiri kuwa Yusufu alikuwa nzi aliyenaswa kwenye utandabui alipoaniwa na mke wa potifa………… Uk 128, Daudi na mke wa ruiah…. Navile akakumbuka maneno ya Tim “ mimi nakuamini wewe, ten asana najua huwezi kufanya lolote kunidhuru…… uk 129.
Tamari kusema eti Akida ni mbakaji – Uk 130, bada ya kutaka kuingia naye Akida mapenzini na kukataa na kni mbwa tu” Akida yataka kutoka kwa Tim lakini Tim anakataa akasema hawezi kumwaacha ……….Uk 131
Uk 132, ndipo Akida akamziba kibao mzee Tito Tembo akidhani ni mzee Zablon aliyekuwa akijisifu kuwa ameua watu wengi huko Baraki………..uk 133

Sura ya Kumi na Sita
Akida kutorekea sangura baada ya kumpiga kibao mzee Tito Tembo akidhani kuwa ni mzee Zablon. Na njiani anakuta wanafunzi wa chuo kikuu cha Tandika barabarani baada ya kufanya mgomo na kuteketeza magari matatu….. uk 138.
Wanafunzi wanadai kuwa wahadhiri wa kume wanawaangusha wanafunzi wakiume kwa kuwa hawana chakuwapa uk 138


Sura ya Kumi na Saba
Akida kufika kituo cha Biashara cha binge na kukuta watu wakipiga foleni kwa duka moja asubuhi na mapema na akataka kuvuka foleni na wakamwambia eti “ wewe wacha kuruka foleni, wadhari sisi ni viatu..uk 144.
Akida kwenda kwa uchochoro kwa haja ndogo ………uk 144.
Uk 146, Akida kwenda kutafuta kazi kwa mzee muyaka nakusikia sauti ya lugha asiyo jua akiimba yaani mtotowe mzee muyaka – Johnstone Jerumani ambaye ni zumbukuku.
Uk 147, Bi.Tina kupinga suala la tohara ya wanawake akidai kuwa wengi wao wanaanga dumia kwa mzungu huo.
Uk 149, muyaka, mzee aliyepigana katika vita vya dunia, kali sana akampatia kazi ya kufunga wanyama. Na ndipo msichana yuyule aliyemkuta uchochoroni akijisaidia anaporudi nyumbani na kumkuta kwao ….. Cynthia bintiye mzee muyaka kufanya “home work”
Sura ya Kumi na Nane
Akida kujigeza jina ili wasimtambue akajibandika jina la “Kipande madodo” ili wasimtambue hasa kabila lake… uk 152. Jerumani kupenda sana kandanda..
Jerumani kumwelezea kilichotokea na kufungwa jela na serikali ya ujerumani ndiyo ilikuwa inamlipia ufadhili masomo yake lakini ikaondoa baadaye kwani alikuwa amepewa nafasi kwa kuwa “best student”
Mzee muyaka kugombana na mtotowe jerimani kwa kumwita kichaa.


Sura ya Kumi na Tisa
Habari kutolewa kwa jarida mojawapo la shirika moja la kutetea haki za kibinadamu yakionyesha athari ya vita vya kikabila wilayani korosho …. Uk 160 –161. Katika habari hiyo kulikuwa John Kasisi aliyekuwa akishtakiwa kwa kufadhili mapigano.
Uk 163, Bi. Tina kwenda kwa mkutano wa kundi la wanawake linalopinga ukeketaji wa sehemu za siri za wasichana na wanawake …..uk 164
Jonhson Jerumani kutoroka nyumbani baada ya kumpiga babake na Akida kumpa msaada ….. uk 167
Uk 168, mzee muyaka kuibiwa na bunduki yake na kwenda akilia, na polisi wenye landrova wakaja nyumbani kwake na kumhoji na baadaye wakmchukua na Bi. Tina naCynthia wakalia sana lakini baadaye mama anauza ngo’mbe na kwenda kuwahonga polisi nakurudi jioni na mmewe wakishikana mikono …. Uk168.


Sura ya Ishirini
Kipande madodo –Akida kutaka kuingia mapenzini na Cynthia lakini akakumbuka maneno ya mzee muyaka ili ajitahadhari na bintiye cynthia- lakini baadaye akajingiza mapenzi na Susana rafikiye wa karibu Cynthia — uk 169. Ingawa Susana baadaye akakataa kusoma na kuolewa na Joseph mwenye biaskeli..
Akida kumtorosha Cynthia kisu cha ngariba mpaka mjini sangura kwa biaskeli ya joseph ….. kwani anahofu sana kuwa angeweza kufariki kwa tohara kama vilivyo kwa watu wengi siku hizo..
Akida kusahau kila kitu na hasa kila mtu na vile Tim Rafikiye wa kufa kuzikana baada ya miaka miwili kutoka Tandika – Uk 173 vilevile, Akida kusikia kifo cha waziri Johnstone mabende aliyenawa, wakati anapokikiliza kwa redio yam zeemuyaka……..Uk 173.


Sura ya Ishirini na Moja
Bi.mkubwa yaani mamake muyaka akafa tena kwa mwanawe baada ya mwezi kupita baada ya kuwa na hitilafu kubwa kwa kutotahiriwa wajukuu wake.
Matayarisho ya kupokea wageni wanaoletaposa ya nanayakoyanafanywa juuchini nambuzi kunawa …. Uk 175
Barua ikaletwa kutoka kwa mzee muyaka na Bi.Tina kuichukua mpaka kwa mkewe Joseph – Susana ili amsomee lakini akashindwa …. Uk 178, ndipo Akida akawasomea.
Kwa wazazi wangu,
Hayawi hayawi huwa, Tangu kufanya uchumba na mchumba wangu wangu sikuwahi kufikiria kuwa mtego ungeweza kujiri. Alikuwa wangu mandhia Matamanio na mapendezi yake yalikuwa sawa na yangu. Itakadi na faja zake zilikuwa zafanana na zangu. Nilipomtazama mbele niliona mustakabali mzuri katika ndoa isiyo na doa. Ila sasa mbele hakwendeki. Pamepita hitilafu kubwa kati yangu na mchumba wangu. Nakutumai mmeipokea barua hii mapema ilimuradi kuepuka kuingia gharama ya bure kwa maana hatutakuja nyumbani kwa shughuli ya posa kama tulivyo kuwa temepanga. Niobee mungu anipe moyo wa subira wakati huu wenye utata.
Binti yenu mpendwa
Nana
Akida kutoka sangura kwelekea mjini Tandika baada ya miaka mitatu bila kuaga kwani wote wamepigwa biwi la simanzi kwa habari kutoka kwa nana binti yao.


Sura ya Ishirini na Mbili
Akida kurudi Tandika na kujipeleka kwa kituo cha polisi na kujiripoti kuwa aliua mzee zablon na kushindikwa kwa jela.
Vilevile akawakuta wafungwa mbali mbali na wenye mashtaka Fulani Fulani. Na hakupata bughadha kali na askari poli kurani wakampa ufadhili …. Uk 190
Akida kua chiliwa uhuru kwa kesi alizokuwa nazo kwani mzee zablon alijina mwenyewe na hata mzee Titi Tembo ai akamsamehe kwa kumziba kibao badala yam zee Zablon………
Tim kukutana naye baada ya kartini miaka mitatu ilikuwa imeishatoroka tokea wakati Akida alipokwenda sangara.

Sura ya Ishirini na Tatu
Tim kuandamana na Akida mpaka mtaa wa Falkland.
Tim vilevile kumwelezea kwa mapenzi yake na Pam yakapata kisogo,
Tim kumwelezea kifo chababake mzee Zablon kwa kusitia kitanzi miezi michache iliyopita. Pia vifo vya ndugu zake na mamake katika vita vya ukabila.
Tamari na Tim kumficha Akida wakati watoto wa mzee Tito Tembo wanapowa wavamia kwao na kumvalisha gauni ya wasichana na baadaye kumpeleka mpaka kwa mtaa wa mama nasambu kwa shangazi ya Pam.


Sura ya Ishirini na Nne
Akida kufika kwa mtaa wa mama Nasambu ili kujisalamisha, Tamari kutoka baada ya kumfikisha huko. mara kwa mara Tim, Tamari wengekuja na kumtembelea huko.
Akida kumwelezea Pam, kuwa alifanya kazi ya kwa mzee muyaka ambaye alipigana kwa vita vya dunia na habari chungu nzima iliyomfikia kwa miaka hiyo mitatu.
Akamwelezea kuhusu kuvunjika kwa mapenzi ya Nana na mchumbake.
Isitoshe, Akida akifanya kama daraja la kuwaunganisha tena Tim na Pam tena.


Sura ya Ishirini na Tano
Shangazi yake kumfukuza Akida yaani hamtaki na baadaye anaomba mzee Toili ambaye ni mlinzi wa kwake shangazi-Pam ili ampeleke kwao aweze kujificha vilivyo.
Pam angempa pesa ya matumizi huko kwa mzee Toili na baada ye kabisha habari ikaja Tom kukumbkuka ahadi yake ya kumpeleka ulaya ili- kusoma kwa kuwa ameichukia nchi yake ya kiwachema.
Vilevile, Akida anashangaa sana kuona Regina mtawa bintiye ya maheremu mzee uledi akisiuza kimasomaso … uk 220.
Uk 221, Pam na Tim, wameshikana mikono na kumpungia naye vile vile Akida anawapungia anapopanda ndege mara yake ya kwanza na kusema “Niache nendeuzunguni nisome nioe mzungu ikibidi………….Uk 221)
Uk 222, Akida analia, akisema mbona nalia? Naiacha nchi yangu ambapo mimi ni mwananchi kindakindaki. Nichukie kiwachema ? ……… Akisema kiwachema kwa heri kwa sasa usilie nisubirinitarudi………

WAHUSIKA NA UTAMBULIZI
WAHUSIKA WAKUU.


Akida sululu (Mkanju)
Ni mvulana wa Mzee sululu na Joan sululu. Ni mkanju kwa kabila na rafikiye wa dhati waTim. Alikuwa wa tatu katika mtihani wa kitaifa na akazawadiwa na waziri Bwana Kato wa elimu.
Sifa/tawasifu /tabia/hulka


Ni mwenye hasira alimjeruhi mzee Tito akidhanii ni mzee Zablon kwa madai kuwa alikuwa akijivunia kwa kuwa amewauwa wakanju wengi.
Ni mvumilivu – alivumilia wakati Tamari alimsingizia kuwa ni mbakaji.
Ni mwongo: (a) Anamdanganya mzee uledi ya kuwa Tim ni msangura.
Anamdanganya B.Tina ya kuwa yeye ni mchungwachungwa.
Ni msiri: Hakumwambia Tamari ya kuwa babake ndiye aliyekuwa akiwaua wakanju huko wilayani korosho.
Ni msomi/mwerevu: Ni yeye aliyekuwa wa tatu kitaifa mitihanini kwa shule ya msingi.
Ni mwenye bidii: Akida alifanya vizuri katika mitihani ya mwisho wa shule ya msingi na kizawadiwa na waziri wa elimu.
Ni mwenye utu: Akida anapomsaidia Tom baada ya kupigwa mshale na kulala chini ya mwembe na kumpeleka hospitalini Korosho. Akida anamwokoa mzee Muyaka anapoumwa na nyoka kwa matibabu zahanati na kliniki za sangura zilikuwa mbali tena zilikuwa na uhaba wa madaktari na dawa.
Ni mtulivu: (a) Tamari anaposema kuwa Akida ni mbakaji alituliza hasira yake na kutoka nje.
Anapoona ofisi ya stesheni ya sauti ya kiwachema anashikwa na hasira na kutaka kuvunja kioo cha ghorofa hiyo lakini anaacha na kuenda zake.
Ni mcha mungu: (a) Akida alikuwa akienda kanisani kila juma pili na Tamari na Tim.
(b) Akida anafuatia maneno ya kasisi John anavyowahotubia kanisani kama kuhusu umalaya.
Ni mwimbaji: Akida anawaiimbia Pam na Tim wanapomsihi awaimbie.
Ni msamehevu: Akida anamsamehe mzee Zablon kwa kumuua Mzee sululu ambaye ni babake.
Ni mzalendo: Anasema ya kwamba akienda ulaya atasoma atatue shida za ukabila huko kiwachema.
Mwenye mapenzi: Aliamua kumpeleka Tom hospitalini isapokuwa amejeruhiwa namshale na akabaki hapo bila. Kusita mpaka wakati alipompeleka hospitalini.
Ni mkatili: Akida alimpiga mzee mmoja aliyefanana na mzee Zablon mapisi ambaye alikuwa akidaiwa kwa kuua wakanju.
Ni mwenye wivu: (a) Alipoona vile Tim ameendelea akamwonea wivu. Alionyesha pia wivu wakati anapomwona.
Mpatanishi: Anajaribu kupatanisha Pam na Tim wanapokosana.
TIM MAPISI (MKOROSHO)
Mtoto wa mzee Zablon mapishi, ni mkorosho na ni ndugu yake Tamari na hata mpenzi wa Pam.
Ni mchezaji bora wa kandanda. Alikuwa anacheza sana mpira huko shuleni.
Ni mwenye mapenzi
Anapendanana Pam ambaye ni mpenziwe.
Alimpenda Akida sana na kumsaidia wakati wa shida.
Anampenda dadake Tamari aliporudishwa shuleni kusoma.
Ni mwenye utu: (a) Tim alimsaidia Akida na viatu alipoona kuwa ana miguu mitupu?.. Alionyesha utu anapomlipa mchungaji wa mortuary nduchi ili waweze kutafuta maiti ya babake Akida.
Ni mtilivu (a) Hata baada ya kupigwa kalamu kazini aliendelea kuwa rafiki na Akida. Anamtuliza Akida baada ya mjombake sasmson Tangu kumtukana.
Ni mcheshi . Anacheka anapokutana na Akida akirudi nyumbani miguu yake mitupu bila viatu.
Ni mwenye bidii. Anaonyesha bidii yake wakati hana kitu ya kujikimu maisha na anaamua kuuza viatu vyake ili kujikimu maisha.
Ananunua vitu vipya baada ya kupita kazi ndogo ndogo.
Ni mlinzi : anamlinda Akida shuleni ili wanafunzi tundu wasimchokoze. Vilevile, anamlinda Akida wakati watoto wa Tembo wanapokuwa wakimsaka.
Ni mwenye matumaini: Hata baada ya kufutwa kazini anaendelea kujikimu maisha.
Ni mwenye hasira: ananyesha hasira yake baada ya shetesheni ya sauti ya kiwachema kueneza habari yenye uwongo.
Ni mvumilivu: anavumilia maishani mwake hata kama haendi anavyohitaji.
Ni mwenye wivu: (a) wivu wake unabainishwa anapoona Pam anamkumbatia Akida baada ya kupewa zawadi na waziri wa elimu Bwana kato. Vilevile Akida anapofika mjini Tandika mara yake ya kwanza na Tim kumwelezea kuwa shamba lao hutoa mazao mengi kuliko yao kila msimu na hata ng”ombe wao hutoa maziwa mengi kuliko yao.
Ni mkarimu: Anamsaidia Akida na viatu bada ya kuona kuwa viatu alivyo navyo vimeharibika. Anampeleka Akida hotelini aweze kula chakula.
Ni mwazi: anamwambia mjombake Samson Tangu kuwa Akida ni mkanju bila kumdanganya.
Ni mjasiri: anampeleka Akida kwa mjombake Samson Tangu na kumwambia eti ni mkanju bado anaendelea kuishi naye hata akijua atachukiwa.
Ni mwaminifu: anamwamini Akida kwa kila kitu asemacho.
Tom mangala: Ni mtoto wa mzee Mangala ambaye ni bwanake Jenelle. Akasoma hadi akafika ulaya na kisha akafanya kazi na kampuni ya Anken
Ni msomi: Inaonyeshwa wakati Tom anasemekana alisoma ulaya na kisha kufanya na kampuni ya Anken.
Ni mwenye mapenzi: Yaani anapendana na Jenelle na hatamzungu na kumwoa akida na Tom wana mapenzi ndiyo maana Akida anafanikiwa kwenda ulaya kusomea huku.
Ni mvumilivu: Hata baada ya kuambiwa eti babake ameuawa vitani korosho yeye hakulia bali alivumilia
Ni mkarimu: Anakubali kusafiri na Akida na Tim kwa kutafuta baba zao.
Ni jasiri: Anaenda kumzika babake huko katika eneo la vita bila uoga wowote.
Ni mtu mwenye bidi
Ni mwenye utu.
Ni mwasi (Rebellious)
Ni mwaminifu.
Ni mnyamavu.
Mzalendo


MZEE MUYAKA: Babake Johnstone na Cynthia na mkewe ni Bi.Tina. Aliwahi kushiriki katika vita vya dunia vya pili na hutoka sangura.
Ni mjeuri: Akida anapokuwa akitafuta kazi hamjibu wakati anapo msalimu. Hakujali kuhusu maisha ya mwanawe Johnstone Jerumani.
Ni mwoga: Anaposikia kitu kimeanguka anajificha chini ya meza…………
Ni shujaa: Kwa kuwa alipigana kwa vita vya dunia.
Ni mnyonge wa afya.
Ni mnyamavu: Anamnyamavu wakati Akida anakuja kutafuta kazi.
Anaongea vibaya kuhusu mtotowe Johnstone Jerumani kwa kkuwa ni mwkenda wazimu.
PAMELA Ni mpenzi wa Tim na alikuwa akiishi na shangazi yake eneo la mama Nasambu
Ni mpatanishi Anajaribu kupatanisha Akida na Tamari baada ya Tamari kusema kuwa mzee sululu amena babake.
Ni mcheshi
Ni mwenye utu: Akida alipoletwa kwao na Tamari yeye alikubali ku mchunga.. Alipowaona watu wenye silaha nje ya nyumba yao anakuja na kumwambia mpenziwe Tim.
Ni msaliti /mhafidiana: Anasaliti mapenzi kati yake na Tim.
Ni mcha mungu: Anaenda kanisani kwa ajili ya ibada kilaJuma pili.

Ni mwenye utu: Anamlurumia Akida anapomwona kuwa ana wasiwasi na Tim , anapendana na Tamari na hata Akida .
Ni king’ang’anzini.
Mzee sululu: Babake Akida na ni mume wa Joan sululu. Alizaa watoto wengine lakini wote walifariki kabla ya Akida kuzaliwa.
Nimwenye utu: Anamponya Tim anapoumwa na nyoka.
Ni mwimbaji hodari: Kwani ni mtunzi wa nyimbo na hataanataka kukchapisha mswaada wake .
Ni mjasiri.
Ni mwenye muamananawatu: Anamfundisha Akida jinsi ya kumtibu mtu anapokuwa mgonjwa.
Ni mwenye bidii
Ni mpweke
Ni mhariri
Ni mpenda amani
Ni msomi: kwani anajulikanasana kwakuandika vitabu vya ushairi.


JOAN SULULU: Mke wa mzee sululu mama yake Akida. Aliangaa dunia miaka lo, iliopita baada ya basi la abiria kupata ajali na lori Tungule kilimani . Alikuwa anauza samaki, matunda nk kiduka cha Baraki huko Korosho


MZEE ULEDI: Ni mkanju aliyenusurika kifo na kukimbilia Tandika baada ya vita kuzuka , baba yake Regina
Ni mlevi: Wakati Akida na Tim walipokuwa wanamuliza kamayeye ni mzee Uledi mwanamume mmoja akamwambia kuwa alikuwa ametindi.
Ni mwenye hasira
Ni mkatili
Ni mwenye bidii
Anapenda ukabila: Ilibainika wazi wakati alipouliza Tim ni kabila gai na Akida akamdanganya na kuanza kupayukapayuka.
Ni mcheza marimba na gitaa, yaani anawaambia Akida natim eti wakati waliporamiwa na wakorosho alikuwa akipiga gitaa yake.
Ni mwenye taasubu ya kiume
Ni omba omba


REGINA ULEDI: Mtoto wa mzee Uledi na alikuwa akisoma darasa moja na Akida.
Ni msomi
Alikuwa mtawa – Hakupenda mambo ya mapenzi.
Kahaba
Mhafidina/msaliti


TAMARI: Mtoto wa mzee Zablon, na mdogo wake Tim, alimusurika kifo kwenye vita baina ya wakerosho na wakanju.
Ni mwongo: Anadanganya ndugu yake Tim kuwa Akida alikuwa anataka kumbaka . anadanganya kwamba Babake Akida ameua Babake-mzee Zablon.
Ni ujinga.
Ni mwenye bidii
Ni usomi
Ni mtafutaji- Anafulia watu nguo kwenye maeneo ya uatajiri ili apate riziki.


MLINZI TOILI: Mlinzi kwa shangaziye Pamela – mtaa wa mama Nasambu.
ROSE NA TIM: Ni wanachuo kikuu cha kiwachema ambao walifukuzwa kutokana na migogoro ya cheshi na walipendana.
MZEE KIJOKA: mzee anayeelewa kabla ya kwenda kwa mzee muyaka. Ni mkali.
JOSEPH: aliyemoa susan rafikiye Cynthia
SAMSON TUNGU: Mjombake Tim. Ni mkabila, mkarimu, ni mwazi nk.








MAUDHUI KATIKA RIWAYA YA KUFA KUZIKANA.


Ndoa, Ni wakati watu wawili wanaishi Pamoja wakishaoana na mapenzi. Ni mahusiano ya kikaribu kati ya watu wawili.
Mapenzi: Mapenzi kati ya Akida naTim nak walikuwa watu wa kabilatofauti (mapenzi ya kufa kuzikana)
Mapenzi kati ya Akida na Tom (Kufa kuzikana )
Mapenzi kati ya Pam na Tim (mapenzi ya kawaida )
Mapenzi kati ya Tim na babake Mzee Zablon mapishi.
Mapenzi kati ya Pam naTamari.
Mapenzi katiya susan na kipande madodo.
Mapenzi kati ya Johnstonenakipande madodo.
Mapenzi kati ya nananamchumbake.
Mapenzi kati ya Bi. Tina na biniye Jerumani
Ndoa:
Ndoa kati ya Joan Sululu na mzee Sululu
Ndoa kati yam zee Zablon na mkewe.
Ndoa kati Ya Joseph na Susan.
Ndoa kati ya Bi. Tina na mzee muyaka
Ndoa kati ya Jenelle na Tom.
Ukabila: Ni mapendeleo ya mtu Fulani kwa kabila lake. Kabila zinazopatikana kwenye kitabuni wakorosho nawakanju wachungwachungwa, wasangura nk.
Askari alipokuwa mwandamani wa Akida aliposema “nakwambia hakuna watu zumbukuku kama wakanju.
Mjombake Tim- Samson tungu anapomtu si Akida akisema waknju wapenda mazishi sijui mazishi ya shangazi mjomba ….. nk hata wataanza kwanda mazishi ya mbwa.
Vilevile, Tamari akionyesha ukabila anaposema Babake Akida ndiye aliyeua babake.
Mazingira: Akida anapoenda Tandika mara yake ya kwanza, anapoenda Sangura kwa mzee muyaka.
Ugonjwa: Mwalimu Alex na Jerumani.
Utamaduni: Kupashwa tohara.
Umri wa kuoa
Malenzi: Mwanamke alikuwa na jukumu la kuwalea wanawe.
Elimu: Wanawake hawakupewa nafasi ya kupata elimu.
Swali
“Migogoro ni chanzo cha maangamizi katika Jamii” Jadili
Kuna mifano mwafaka katika riwaya.
Kati ya wakanju na wakorosho
Kati ya Akida na Tamari
Kati yam zee Muyaka na Bi.Tina mkewe.
Kati ya Akida na Tito Tembo.
Kati ya Tim namjombake – Samson Tungu
Kati ya Pam na mpenziwe – Tim
Kati ya mzee Matuko na sekretari
Kati ya mzee Sululu na mzee Zablon
Kati ya mwalimu Alex na mheshimiwa Johnstone Mabende.
Kati ya serikali na vyombo vya habari.
Swali
“Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu” Jadili methali hii ukirejelea Riwaya hii;
Maana ya methali, Akida alipata nafasi ya kwenda ulaya kwasababu ya Rafikiye Tim aliyemfanta ajuane na Tom-
Regina na babake mzee uledi.
Mzee Zablon mapisi na tim.
Mzee muyaka na Johnstone Jerumani
Mzee Sululu na Akida.
Mzee mangalana Tom.
Tom nanchi yake kiwachema.
Mzee Sululu na mkewe Joan Sululu
Kipande madodo na mzee muyaka.
Swali: “Hakuna chuki katika riwaya ya Kufa Kuzikana ila ni mapaendeleo katika kabila” Jadili?
Chuki ni kuwa na hisia mbaya kwa mtu.
Wakorosho na wakanju.
Mbunge Jonstone mabende na wakanju.
Mwalimu Alex na wakorosho wenzake .
Tamari na Akida
Mzee matuko na watu waliokwenda kwa Bwana Gembo kudai bima ya malipo yao na sekretari.
Tito Tembo na Akida .
Mjomba Samson Tungu na Tim.
Mjomba SamsonTungu na Akida.
Swali: “Ni nini nafasi ya Elimu katika Riwaya ya kufa kuzikana.
Elimu ni maarifa yanayo patikana ndani nanje ya shule.
Mwalimu Alex alitumia elimu yake kutoleta vita wilayani korosho.
Tom
Akida
Tamari
Jerumani
Mzee Sululu na mzee Zablon mapisi
Tim
Swali: “umaskini”
“Kukosa vitu vya maana muhimu maishani
Akida alikuwa masikini karasababu anapomfika Tim nampa nguo….
Tim aliposhi mtaa wa Falkland
Tajiri na masikini waishi hahali tofauti tofauti.
Watu wanaishi kwenye nyumba ya nyasi wilayani korosho.

MBINU ZA LUGHA:
Ni njia ambazo mwandishi ametumia lugha ili kuwasilisha ujumbe wake;
Mbinu rejeshi (Kisengele nyuma /Dambini) mbinu ya kurejelea mambo yaliyopita.
Akida anaporejelea kifo cha mamake katika ajali miaka 10 iliyopita kwa ajali. Vilimani Tungule.
Akida akiwa stesheni ya polisi alivyofista. Ki kuwa alimwua mzee Tito Tembo akidhani kuwa ni mzee Zablon.
Mjini Tandika Akida anakumbuka maisha shuleni na Tim. Anasema akisema kuwa Tim alikuwa Mchezaji bora wa soka na wasichana walikuwa wanampanda
Mzee matuko anurejelea jinsi ahivyokuwa kwenye ajali iliyotokea huko Tungule vilimani.
Tim alivyoumwa na nyoka.
Akida anarejelea kuhusu mwalimu Alex
Barua yam zee Zablon inarejelea majuto kwake kwa kumuua mzee Sululu ambaye kwa hakuna nakosa lolote.
Akida na Pam wanarejelea mambo yaliyokuwa huko sangura.
Akida anarejelea mambo yalivyokuwa Baraki na maneno ya Johnstone Mabende.
Akida anarejelea mahali mamake alipokuwa akiuza bidhaa zake kama; samaki wakati walipokuwa watoto.
Taswira, ujenzi wa picha akilini mwa msomaji.
Akida alivyoleza vile mwalimu Alex akirukwa na kichwa.
Akida alipokuwa akienda mjini Tandika anajengapicha kwa masomaji jinsi mamake alivyo kufa kwa ajali.
Mbwa alivyokuwa akila kichwa cha mtu huko Baraki wakati wa vita.
Akida alipomwiimbia Tima na Pam.
Akida alivyozawadiwa nawaziri wa elimu Bwana Kato.
Akida alipompiga mzee Tito Tembo akifikiria kuwa mzee Zablon
Ch) Uzungumzaji nafsi: ni mbinu ya lugha ambayo mhusika huonyeshwa kimoyomoyo Tim kusahau zawadi yake kwenye gari alisema “huyu Tim kumbe limbukeni hivi? Vipi anaachia zawadi yangu kupotea vivi hivi tu? Na zawadi yenye nilikuwa hata sijafungua.
Jiji hili silijui wala nyuma yake nitafanyeje? … Akida anapofika Tandika.
Akida akiwa kwenye mkahawa naTim alisema “Tahau ola ladha nzuri ajabu” watu wamashambani yanatupita mambo mazuri hayo? Au ni upya wa mambo?”
Akida alipokuwa kwa mjombake Tim, alizungumzia nafsia akasema….. ama alitakakuonyesha mali na amuali zao?
Sadfa: Vitu viwili kutokea wakati mmoja bila kutorajiwa.
Tim kuenda mahakamani. Akida akisubiri kusomewa mashtaka.
Akida na tim wakienda kwa tom. Tom naye akapata habari ya msiba.
Akida anapoenda klabuni.
Tito Tembo anapokuwa klabuni akinywa.
Akida kuzaliwa na kupata vitabu mzee Sululu.
Akida kwenda ofisini ya Bw. Tembo na mzee Matuko kuwepo.
Akida kupanga kurudi nyumbani, habari ya mipango kutambaa.
Habari kusambaa, Tamari kufika kwa Tim.
Tim na Akida kwenda hospitalini, mzee uledi akiwa anatibiwa.
Akida kujisalamisha polisi, Kasisi John akiwa jela.
Akida na tom kurudi Baraki, vita vikiwa bado havijamalizika.
Vile vile Ken Walibora ametumia mbinu nyingine kama:
Tashbihi
Kinaya
Barua
Dhihaka /tabaini nk, ili kuwasilisha ujumbe wake.

HITIMISHO:


Tanbihi: Ikumbukwe kwamba mwongozo huu haubebi yote namna yanavyojitokeza katika riwaya nzima, kwa hivyo inakubidi wewe kama mtumiaji kusoma riwaya kwanza na kisha ukasome mwongozo kukusaidia kuelewa vipengele mbalimbali vinavyopatikana na ambavyo vimeangaliwa hapa ndani. Asante!!!

3 thoughts on “MWONGOZO WA KUFA KUZIKANA

Leave a comment