MWONGOZO WA TAMTHILIA YA KIJIBA CHA MOYO-TIMOTHY .M. AREGE.
Mwalimu Johnpaul Arigumaho 2022.
Utangulizi.
“Moyo hupenda, moyo huchukia, moyo hukinai, moyo huhurumia, lakini moyo unapopatwa na dhiki ni rahisi kujua unaponzwa na nini.”
Tamthilia ya kijiba cha moyo ni tamthilia inayoangazia maisha ya Sele kudhaniwa kuwa mgonjwa, kunyimwa haki zake, na kutotetewa kwa namna yeyote anapopambana na waiotaka kuiba moyo wake halafu akabaki na kijiba.
Sele ni kijana ambaye amebadilika kitabia katika familia, moyo wake umepatwa na kutu, familia yake imekosa kupata utulivu kwa kughasiwa na ugonjwa wake. Sele kila tendo analiona kuwa ni uonevu , sele ana kijiba cha moyo. Je mawaidha ya bibi yatautibu ugonjwa wa Sele?
Dhamira ya mwandishi..
Timothy ananuia kutuonyesha uongozi wa kiimla uliotapakaa katika nchi nyingi za bara la Afrika na kukita mizizi pale.
Tamthilia hii ni miongoni mwa kazi za kifasihi zinazo chunguza uhusiano uliopo baina ya ubepari wa mataifa na hali duni ya kiuchumi iliyojiri mataifa ya ulimwengu wa tatu kwa mtindo wa kinaya.
Mwandishi anatalii maudhui ya kiuchumi na mfumo wa kibepari ambao licha ya kuwakandamiza wakazi wa mabara ya Afrika unapunguza nafsi za wafanyikazi na kuwafanya kujihisi kuwa duni. Mahusiano haya yameendelezwa kwenye misingi ya udhalimu.
Mwandishi ameelezea maonevu haya kwa kinaya akitumia sitiari pevu ili kukejeli mfumo mzima wa uelewaji wa dhana ya uhuru katika uzalishaji mali.
Katika tamthilia hii mwandishi pia analenga kutuonyesha kuwa uongozi uliopata mashiko yake kwenye mfumo wa kibepari, umemiliki nyenzo za kimsingi za uzalishaji mali kupitia kwa ufisadi, uongo na zaidi katika kuwakandamiza wale waliopata mwangaza wa kuona njama hii ya kunyanyaswa.
Hili hutekelezwa ili kuzuia juhudi za wale waliopata mwamko mpya kisiasa dhidi ya kuwazindua wanyonge wengine katika jamii. Mwandishi kupitia kwa mhusika nguli (Sele), anasawiri uhusiano uliopo baina ya mataifa ya ulimwengu wa kwanza ambayo huyapa misaada na kuyamiliki mataifa ya ulimwengu wa tatu kwa kuyafanya yakose kujitegemea.
Mwandishi anasawiri kwa kina misaada inayotolewa kwa mataifa machanga na kuonyesha kuwa misaada hii haiwafai Waafrika ila tu ni chombo kinachotumiwa ili kuweza kupata fursa ya kuwanyonya Waafrika rasilimali zao.
Hii ni kinaya kwa kuwa Waafrika wenyewe hawaelewi hali hii.
Arege analenga kutuonyesha kuwa hali ya uhitaji katika mataifa mengi ya bara la Afrika imesababishwa na unyonyaji wa nguvu za wakazi wake kwa malipo duni.
Anaeleza kuwa mipango ya kuyasukuma mbele kimaendeleo mataifa machanga barani Afrika ambayo inaamuliwa na kuwekwa na mataifa yanayodai kujitegemea ni chanzo cha kudorora kwa maendeleo yanayotarajiwa. Hii inatokana na ukweli kwamba walioshikilia (wakoloni)
nguzo za mfumo huu wa kibepari waliwafumba macho wakazi wa nchi changa kwa kuwapa misaada isiyowafaa.
Falsafa ya mwandishi.
Mwandishi ameongozwa na falsafa ya “UJinga ni Ugonjwa”Nchi zenye nguvu zinatumia aina zote za kutoa misaada ili kumiliki rasilimali za mataifa aina ya tatu juu ya ujinga na kutoelewa kinachofaa kufanywa. Hili linachorwa vizuri na mhusika sele alipojitoa kupigania haki wengine wakafikiri ni mgonjwa(ujinga).
Mtazamo wa mwandishi.
Mwandishi ameegemea Mtazamo wa kisiasa yaani kiyakinifu; Kuungana, kujitahidi na kujikomboa kimawazo ni suala liwezalo kusaidia waafrika
kujiendeleza kwa misingi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Hiki kinabainika baada ya kutamatisha kusoma tamthilia hii ambapo inabainika kuwa ugonjwa wa Sele si ule wa kawaida kama ulivyochukuliwa na wahusika tamthiliani bali kuzinduka kutokana na mwamko mpya wa kisiasa na kijamii.
Msimamo wa mwandishi.
katika tamthilia ya kijiba cha moyo mwandishi anamsimamo wa kimapinduzi kwani amejadili matatizo yanayochangia kukwama kwa ujenzi wa jamii mpya.
Msimamo wake umebainishwa kutokana na jinsi alivyochora mhusika Sele, akijaribu kujiokoa na kujikomboa kimawazo wengine wakifikiri ni mgonjwa lakini akakosa kupata washabiki werevu. (kijiba)
arigumaho810@gmail.com. +256778514179/757223817.

Asante
LikeLike
Nashukuru sana ndugu yangu 🙏
LikeLike
Habari bwana kakangu,ningependa kupata miongozo hiyo iliotajwa hapo juu.sasa najiuliza niyipateje?
LikeLiked by 1 person
Fuata tovuti…nifikie kwa Whatsapp 0778524279.
Asante kufuatilia
LikeLike
Ndugu Asante Sana kuelimisha Wana Uganda!
LikeLiked by 1 person
Nashukuru sana. Asante kufuatilia Ndugu yangu 🙏
LikeLike