*Kabila na ufalme wa ankole magharibi mwa Uganda*
*Bagyendanwa* , ilikuwa Ngoma ya Kifalme ya ufalme wa Ankole.
Wasomi wengine wanaamini kuwa Ankole mwanzoni ilikuwa ikichukuliwa na *Bairu* ambao walijulikana sana kwa *kilimo* wenye asili ya Kibantu. Baadaye, Bairu walikubali wafugaji waliohama kutoka *Ethiopia* kusini kuingia eneo lao. Wafugaji hawa badaaye walishinda Bairu na kujitangaza kuwa *watawala* wa nchi.
Kulingana na wataalam wengine, Bairu wengi walikuwa watumishi na Bahima walikuwa tabaka kubwa la watawala. Kwa sehemu kubwa makabila hayo mawili yalishirikiana kwa amani.
Wakati Waingereza walipoiweka Uganda chini ya utawala na mamlaka yao mnamo 1888, ufalme wa Ankole ulikuwa ufalme mdogo sana uliotawaliwa na mfalme *(Mugabe)* aliyekuwa na nguvu nyingi kabisa.
Mnamo 1901 Waingereza walipanua ufalme kwa kuunganisha na falme ndogo kama hizo za *Mpororo, Igara, Buhweju, *na Busongora.*
Nguvu za Omugabe zilipunguzwa sana mara tu ufalme wake ulipodhibitiwa kisheria na kikatiba.
Lakini, kama Omugabe wa Ankole, alikuwa bado na haki ya vyeo vyote, hadhi, na ukuu ambao uliambatanishwa na ofisi yake chini ya sheria na mila za Ankole.
Uhusiano wa kisiasa uliohusisha utumwa na utunzaji haukuwepo chini ya utawala wa Briteni ingawa Bairu *walikejeliwa* na *kudharauliwa* .
Kufikia 1752 *Omukama Kamurari* II alikuwa kwenye kiti cha enzi cha Mpororo hata hivyo alinyakuliwa na kaka yake *Kahaya Rutindangyezi* , ambaye alichukua kiti na katika enzi zake kugeuza macho tu kuona ufalme unasambaratika baadaye na kugawanyika katika majimbo sita.
Kwa kweli uongozi wa machifu ulitawaliwa na wanawe. ; moja ambayo ilikuwa *Igara* (kitambo Ufalme wa Igara uliotawaliwa na Omukama; “mfalme”), ambapo Ntungamo inapatikana sasa. Ilifanikiwa zaidi kuliko baadhi ya machifu wengine watano kufuatia kusambaratika kwa ufalme wa Mpororo na ikabaki imara katika karne ya 18, sio kwa sababu tishio lake kuu bali ufalme wa Ankole (Nkore), ulikuwa umeshikwa na wasiwasi wa ndani ukiacha pengo kidogo au uwezo wa upanuzi wa nje.
Pamoja na hayo, viongozi machifu wa Mpororo waliobaki hawakutambuliwa na Waingereza kwasababu illizingatiwa kuwa ndogo sana, dhaifu na isiyo na maana kuidhinisha masilahi yoyote ya kiutawala au nyingine.
Kwa hivyo uongozi wa machifu sita ambao hapo awali walikuwa wa ufalme wa Mpororo baadaye walipokelewa na kupitishwa katika Ufalme wa Ankole mnamo 1901.
Mnamo 1878 Omukama wa Igara aliyekuwa anatawala wakati huo aliambiwa na Waingereza kusafiri kwenda Mbarara kusalimiana na mfalme wa Ankole.
Hata hivyo badala ya kukabiliwa na aibu za kufanya hivyo alijiua kwa *kujichoma kisu* tumboni.
Lakini, kama “Omugabe wa Ankole” (mfalme wa Ankole) alikuwa na haki , mamlaka, hadhi, na ukuu ambao uliambatanishwa na ofisi yake chini ya sheria na mila za Ankole.
jifunzekiswahiliart.wordpress.com
