MWONGOZO WA RIWAYA YA KIU: Arigumaho Johnpaul na Simon T Kawaida.

MWANDISHI: MOHAMED S. MOHAMED
RIWAYA: KIU
MWAKA: 1970


UTANGULIZI


Riwaya hii iliandikwa na Mohamed S. Mohamed mnamo mwaka 1970. Riwaya hii ilijipatia zawadi ya kwanza katika mashindano ya uandishi wa hadithi za kubuni katika lugha ya Kiswahili, ambayo yaliandaliwa mnamo mwaka 1970.


Mwandishi huyu, ametumia nadharia ya uhalisia katika utunzi wake wa kazi hii yaani, anazungumzia mambo yanayojitokeza katika jamii nyingi za dunia hasa za Afrika, kwamfano, anazungumzia juu ya usaliti wa namna yake kama Idi anavyomsaliti mzee mwinyi ambaye ni mwajiri wake lakini mwishowe anamsaliti kwa kumwoa Bahati ambaye mzee mwinyi anatamani sana na kumtuma Idi lakini yeye anasema kivyake.

Isitoshe, mwandishi ametumiamandhari mbali mbali ili kujenga maudhui fulani fulani. Mandhari mingi yake hujikita sana Kwa Afrika kwa kuonyesha mienendo ya utamaduni, ndoa, Imani au itikadi ya miungu, maisha ya kawaida nk.

Na haya yote huonyeshwa kutokana na uchoraji wa wahusika wake na mandhari na pia mbinu fulani fulani alizotumia.


Fauku ya hayo, mwandishi huzungumzia juu ya suala la mapenzi na athari yake, namna watu wanavyochukiana kwa ajili ya mapenzi na hasa mapenzi yasiyo ya dhati.


Dhamira kuu:

Mwandishi ananuia kuonyesha athari za mapenzi yasiyo na msingi yaani mapenzi yasiyo ya dhati, kwamfano, mwandishi anamwonyesha Idi kama mlaghai wa mapenzi anayemlaghai Bahati ya kuwa yeye anampenda lakini yeye Idi hampendi ila tu anamtumia kama chombo cha starehe anataka kuitimiza shauku zake za kilimwengu.


Bahati anamwona Idi kama anayempenda bila kujua ya kuwa Idi ni chui anayejifunika kwa ngozi ya mbuzi.

Baada ya miaka mitano kwa ndoa, Idi anaonyesha rangi yake kamili au kama vilivyo kuwa dhahiri shahiri yeye hampendi Bahati, sasa Bahati huanza kujuta kwani alijikuta ameishanaswa na kamba ya mapenzi lakini kamba isiyo ya ukweli labda ya ulaghai.


Vile vile mwandishi analenga kuonyesha usaliti ambao umejenga ghorofa kwa mioyo ya wanajamii husika. Mfano mzuri ni Idi ambaye anamsaliti mzee Mwinyi ambaye ni mwajiri wake anayemchukuwa kama ndugu yake, mtoto wake ingawa yeye ni mwajiriwa wake yaani ni dereva yake.
Mwinyi anamwamini sana Idi ndiyo sababu akimtuma kwa Bahati ili amwelezee ya kuwa anampenda lakini Idi anasema mambo yake na baadaye anamwoa yeye mwenyewe.

Isitoshe, baada ya miaka mitano anatengana na Bahati na kuingia mapenzini na Rehema bintiye marehemu mzee Mwinyi.

Yaendelea……. Johnpaul Arigumaho (+256757223817 )na Simon T Kawaida (+256 788 586176)

6 thoughts on “MWONGOZO WA RIWAYA YA KIU: Arigumaho Johnpaul na Simon T Kawaida.

Leave a comment