BARAZA LA KISWAHILI LA TAIFA UGANDA:WILL KISWAHILI FINALLY BE EMBRACED IN UGANDA?

Baraza la Kiswahili la Taifa la Uganda.

Mnamo 2010 , serikali ya Uganda ilifichua mipango ya kuanzisha Baraza la Kiswahili ili kuimarisha ufundishaji wa lugha ya Kiswahili nchini humo. Ilikuwa hadi Septemba 9, 2019 ambapo baraza la mawaziri lilipitisha azimio la kuunda Baraza la Kitaifa la Kishwahili. ( URN. “Ugandans must prepare to learn, speak Kiswahili – Ofwono”. The Observer – Uganda. Retrieved 2020-06-12)

Baraza la Kiswahili la Taifa linakusudiwa kuongoza mchakato wa kupanga, utekelezaji wa afua na ugawaji wa rasilimali kwa matumizi na maendeleo ya Kiswahili kama Lingua franca -lugha ambayo inachukuliwa kuwa lugha ya kawaida kati ya wazungumzaji ambao lugha zao za asili ni tofauti.

Wakati wa utawala wa Idi Amin Kiswahili kilipewa nafasi. 
Mnamo 1973 Idi Amin
alianzisha mjadala kuhusu lugha ya taifa nchini kote uliohusisha chaguo kati ya
Kiswahili na Luganda.
Wilaya kumi na mbili zilipigia kura na kuunga mkono kiswahili.

Wilaya nane ziliipigia kura Luganda Jambo ambalo  lilionyesha mgawanyiko uliokuwa kati makambi hayo kuhusu kiswahili.
Kambi  lililopendelea Luganda lilikuwa
Likiongozwa na Buganda na kuungwa mkono na vibaraka wake wanne wa kihistoria Busoga, Bugisu
na Bukedi katika eneo la Mashariki na Ankole katika eneo la Magharibi.
Baada ya wiki za mashauriano, tarehe 7 Agosti 1973 Kiswahili kilitangazwa kuwa lugha ya taifa ya Uganda kwa amri. 
Amri hiyo, hata hivyo, haikutekelezwa kamwe
Kimazoezi, ingawa haijawahi kufutwa na serikali zilizofuata.
PAWLIKOVÁ-VILHANOV' (1996) ASIAN AND AFRICAN STUDIES.*

Mnamo 1992 , Kiswahili kipipitishwa na serikali ya Uganda Kama lugha ya pili rasmi nchini Uganda.

Ni upi utofauti uliopo Kati ya lugha ya taifa na lugha rasmi? 🤷‍♂️

Hivi, Tumezoea Sera kubaki tu vitabuni?

Hivi, ni kina Nani wanaopaswa kutekeleza.

Hivi, Ni siasa ili tupiganie tupigiwe ili kura?

*Hivi, umuhimu wa lugha ya kiswahili unatambulika au vipi?🤷‍♂️

Hivi, Baraza la mwawaziri/Serikali likipitisha Sera Ni kina Nani wanaopaswa kutekeleza?

Maswali yangu pengine najiuliza kwa uelewa tu🤷‍♂️*

@la tafakari ✍️

Uganda National Kiswahili Council *.

In * 2010 *, the Ugandan government unveiled plans for a Kiswahili Council to strengthen the teaching of Kiswahili in the country.
It was not until September 9, 2019 that the The cabinet passed a resolution to form the Swahili National Council. (URN. "Ugandans must be prepared to learn, speak Kiswahili - Ofwono". The Observer - Uganda. Retrieved 2020-06-12 *)

The Kiswahili National Council is intended to carry out the process of planning, implementing interventions and allocating resources for the use and development of Kiswahili as a Lingua franca - a language that is considered to be the common language among those whose native languages are different.

In 1992 , Kiswahili was adopted by the Ugandan government as the second official language in Uganda.

Maandishi kuhusu dhima ya ukuzaji na uendelezaji wa Kiswahili Nchini uganda


(Mulokozi, 2000) anatambua kwamba lugha ni nyenzo kuu ya utambulisho. (Nsibambi, 2000). Hii na kwa maana kwamba, nchi nyingi za Afrika ambazo zinatumia lugha za kigeni hazijihisi vizuri katika kujitambua kiutamaduni na badaaye wako tayari kupokea lugha asili ambayo inaweza ikawatatua kutoka misha hayo.
Whiteley (1969) anaripoti kuwa Kiswahili kiliendelea kutumiwa na polisi, sehemu za Kaskazini kuwasiliana na watu ambao hawajui Kiingereza na Luganda. Vilevile Wanilotiki wa Uganda walitumia sana Kiswahili kuwasiliana na makabila mengine. Kiswahili kilitumika pia kwenye mipira, na sehemu nyingine ambazo Kiingereza na Luganda havikuhitajika au havikuwezekana kutumika.
Kingine, kuja kwa wote wasome ya shule za msingi (UPE), serikali inalaumiwa kwamba wote wanaoacha kusoma shuleni ni kwa ajili ya kutojua kingereza katika shule za misingi (1981, December 2oo4).Hata hivyo, kwa urahisi wanaweza wakazungmza katika Kiswahili.
Kiswahili ni lugha inayotumiwa katika vyombo vya habari. Sasa hizi televiseni ambazo zinakuja zinaendelea kutumia Kiswahili kamaRadio FM OPG, Mbale FM,Uganda Radio zinachangia katika kukuza Kiswahili katika nchi nzima ya Uganda. Hata hivyo Uganda inakaribia kuanzisha magazeti yanayotumia Kiswahili. Hivi vyote vitasaidia katika kuelimisha watu na kuwaangazia kuhusu masuala yanayowakabili. Mfano thabiti ni kwamba wakati ugonjwa wa ebola ilipokuwa inasambaa katika Uganda ya kaskazini, wakati huo Kiswahili kilikuwa kinatumika kuelimisha watu kuhusu jinsi ya kujiokoa na kuelewa usafi wa watu binafsi.
Katika siasa, wanajeshi wanatumia Kiswahili kuendeleza umoja na kukomesha ukabila. Katika Uganda ya kaskazini, Kiswahili ndiyo lugha inayotumiwa kupigania uhalifu na ukosefu wa usalama inayoletwa na uasi. Kupitia njia hiyo, Kiswahili ni kifaa cha kuleta umoja wa makabila inayotamaniwa leo.
Sasa, wanasiasa wanaowakilisha Uganda katika bunge la afrika masahriki wanatumia lugha ya Kiswahili. Hata nyumbani, wagombea viti vya ubunge kutoka kaskazini, mashariki, na magharibi wanatumia lugha ya Kiswahili katika kampeni zao. Juu ya yote, mbio uraisi haiwezi ikakamilika bila wagombezi kutumia Kiswahili. Hii ni maanakwamba hivi karibuni lugha ya Kiswahili itachukua jukumu la kuleta demokrasia kati ya wanaUganda na hatimaye itachukuliwa kiraia kutumika katika elimu kama ilivyo Kenya na Tanzania.
Katika biashara, jukumu la Kiswahili la Kiswahili linaweza kukaguliwa. Inabidi kieleweke kwamba lugha hii iliingia Uganda hasa juu ya Biashara na imechangia sana kitaifa na kimataifa. Juu ya hayo yote, lugha hii ni lugha muhimu katika kuleta umoja. Inatumiwa katika thieta na barabarani na wakomedia kubrudisha watu.(Johnpaul 2019)

WILL KISWAHILI FINALLY BE EMBRACED IN UGANDA.?
During Idi Amin's rule Swahili was given a perspective.
In 1973 Idi Amin
initiated a countrywide national language debate involving the choice between
Swahili and Luganda .
Twelve districts voted then in favour of Swahili while
eight districts voted for Luganda which testified to a persisting cleavage between two ethnic blocs with regard to Swahili.
The bloc favouring Luganda was
led by Buganda and supported by four of her historical vassals Busoga, Bugisu
and Bukedi* in the Eastern region and Ankole in the Western region.
After
weeks of deliberations, on 7 August 1973 Tuesday, Swahili was declared the national language of Uganda by decree .
The decree was, however, never implemented in
practice, although it has never been repealed by successive governments.
VIERA PAWLIKOVÁ-VILHANOV' (1996) ASIAN AND AFRICAN STUDIES.
 
My unanswered questions?

What is the difference between * national language * and * official language? * 🤷‍♂️

So, Are we used just policy staying in the books?
Also, who are the ones who have to act?

So, Is it political so that we fight for a vote?
Not forgetting Is the significance of Swahili language recognized in Uganda  or what? 🤷‍♂️
Vile vile, when the Cabinet / Government approves the Policy Who are the ones to implement?

My questions are probably with no answers🤷‍♂️

@mwalimu Johnpaul Arigumaho.

@la tafakari ✍️

Leave a comment