
Je, unajuta kwenda shuleni ?
Jibu : Kabisa. Sikuhitaji kuzungumza Kiingereza ili kufanikiwa; Wachina hawazungumzi Kiingereza, lakini ndio wanaongoza uchumi zaidi duniani, wakati Amerika inayozungumza Kiingereza ndio wanaodaiwa zaidi duniani.
Nikikumbuka miaka yote niliyopoteza kukaa shuleni, najuta kabisa ningebaki nyumbani na kupanda mahindi, kufuga ng’ombe na kujifunza kutengeneza juisi kutoka kwa ndizi na kuiuza kote ulimwenguni. Ningekuwa mtaalam kabisa.
Je, unaweza kutambua kwenda shuleni kama hatua yako ya kugeuka/kubadilika kimaisha?
Jibu : Ilikuwa . Kabla ya hapo, nilikuwa Mwafrika wa akili pevu ambaye ungetamani kukutana naye.
Nilidhani kwamba watu wazungu walikuwa miungu na miungu ya kike na kwamba Yesu alikuwa mzungu.
Nilikuwa nakunywa pombe, soda na kula chakula cha mikebe (tinned food) na kuku.
Nilikuwa nikitazama mpira wa miguu uliotengenezewa Ujerumani, nikivaa fulana, suti na tai zilizotengenezewa Ulaya.
Nilienda Uingereza kwa sababu mazoezi niliyopata shuleni yalinipa hamu ya kwenda Ulaya.
Ilikuwa imenifanya nipendezwe na maisha pamoja na historia ya Ujerumani, Italia na kila kitu kuhusu Ulaya, lakini nilipofika Uingereza, jambo la kwanza nililoona ni jinsi watu maskini walivyoishi huko.
Na nilipoanza kusoma kuhusu watu weusi, nilitambua kwamba sikuwa na elimu kama nilivyodhani.
Nilianza kujitambulisha kuwa mtu mweusi mwenye historia. Nilikua na hamu kubwa ya Uafrika na utambulisho wangu kama Mwafrika.

Leo, nina mzio wa nguo zilizotengenezwa Uropa na ninakula tu chakula kinacholimwa huku Afrika katika udongo wetu.
Dr Kihura Nkuba.
