Ualimu nimechoka: vipi nitambulike

*Ualimu nimechoka*

*Vipi Nitambulike?*

Nashika kalamu yangu, yalo kitwani nandika
Kwenye huu ulimwengu, lini nije tambulika
Tena mujue jina langu, lisije sahaulika
Ni vipi Nitambulike, walimwengu munijue?

Ama ni hii siasa, ndio mutanitambua
Niishi kua anasa, ila mukinichagua
Bali marufu nakosa, Je vipi tanitambua?
Ni vipi Nitambulike, walimwengu munijue?

Na nikijita pasta, miujiza kuzitunga
Tena wana wa munguwe, mnifuate ja kupinga
La inahitaji bidii, hata kanisa kujenga
Ni vipi Nitambulike, walimwengu munijue

Nikiwa mkubwa Gaidi, Redioni tasikika
Taliban na Alikaidi, Alshabab Nitambulike
Bali mimi si Lokech, Mogadishu wanizike
Ni vipi Nitambulike, walimwengu munijue?

Muziki pia Jameni, umarufu upo sana
Ni muige Bobiwine, nikamfikie Akon
Ila sipendi usani, shabiki takosekana
Ni vipi Nitambulike, walimwengu munijue.

Ukomedia nishike, Ila mpamire nishinda.
Nimuige mariachi, Matusi kwa kike Sina.
Nimfate Madrat,  chiko njama tiyari.
Ni vipi nitambulike walimwengu munijue.

arigumaho810@gmail.com.

@ni hayo路‍♂️

Leave a comment