1. Kaweto => Mwanamke anayeolewa na mwanamke mwingine ili amzalie katika ndoa yake.
2. Mkembe => Kijana aliyebaleghe na hajaoa.
3. Mlungizi => Ndugu anayezaliwa baada yako.
4. Mtawa => Mwanamke anayewekwa ndani kwa ndani na kuangaliwa asitoke ovyo.
5. Mziwanda => Mwana wa mwisho.
6. Mhavile => Mume wa Shangazi.
7. Mhale => Mume wa Halati.
8. Mkwerima => Jina ambalo wazazi wa mke humwita mume wa binti.
9. Ahali => Jina jingine la mke.
10. Kirimale => Mke aliyepewa talaka. Pia huitwa Mtalaka.
11. Mwamu => Kaka wa mke wako.
12. Suriama => Mtoto wa suria
13.Mjukuu-Mtoto wa mtoto wa nyanya
13.Kitukuu-Moto wa mjukuu
14.Kilembwe-Mwana wa kitukuu
15.Kilembwekeza-Mwana wa kilembwekeza
16.Amu-Kaka wa baba
17.Bavyaa-Mzazi wa kiume wa mume wako
18.Mavyaa-Mzazi wa kike wa mume wako
19.Binamu-Mwana wa kiume wa amu
20.Bintiamu-Mwana wa kike wa amu
21.Mkoi-Mwana wa mjomba/shangazi
22.Shemeji-Ndugu wa mume/mke
23.Wifi-Mke wa kaka
24.Mwamu-Kaka wa mke
25.Mnuna-Ndugu anayekufuata
