Kidato Cha kwanza

WATU WA NYUMBANI.
1.  Baba-Father.
2. Mama-Mother
3. Mjomba-Uncle.
4. Dada-Sister.
5. Kaka- Brother.

Kutunga sentensi kwa kumtumia msamiati wa watu was nyumbani.(Construction of Sentences Using Vocabulary of Home people.)

i,. Baba yangu ni dereva wa basi.
(My father is a bus driver)

ii. Mama yangu ni mwalimu wa Kiswahili.
(My mother is a kiswahili teacher.)

iii. Dada yake Peter anafundisha katika Chuo Kikuu cha Kyambogo.
(Peter’s sister teaches at Kyambogo University.)

iv.  Kaka yangu anasomea katika Chuo cha walimu cha Kabale. (My brother studies at National teacher’s college Kabale)

v. Tafadhali niitie yule kaka yangu.
(Please, call me my brother)

vi.Dada yako anaitwa nani?
(What’s the name of your sister?)

arigumaho810@gmail.com
Jifunzekiswahiliart.wordpress.com
Arigumahop5.(Twitter)
0778514179(WhatsApp)

Hisabati na Tarakimu
Msamiati wa hesabu/hisabati unaangazia: majina mbalimbali ya tarakimu/nambari; kuandika tarakimu kwa herufi.maneno; tarakimu za kiarabu; akisami (fractions) na asilimia (percentages).

Tumekuandalia:
Nambari za Kimsingi (0-9) Kiswahili na Kiarabu
Kumi na (11-19) Kiswahili na Kiarabu
Makumi/Ukumi (10-90)
Akisami (fractions)
Mifano Kadhaa
NAMBARI ZA KIMSINGI
Haya ni majina ya tarakimu mbalimbali zinapoandikwa kwa herufi (badala ya nambari) yenye asili ya Kiswahili/Kibantu na pia yale yenye asili ya Kiarabu. Pia, tumeongezea majina ya makumi mbalimbali (10-90)
TARAKIMU KISWAHILI KIARABU
0 sufuri sufuri
1 moja wahed
2 mbili thenini
3 tatu thelatha
4 nne aroba
5 tano hamsa
6 sita sita
7 saba saba
8 nane themania
9 tisa tisa
KUMI NA
Majina ya ya tarakimu kutoka (11-19) kwa Kiswahili na kwa Kiarabu.
10+ KISWAHILI KIARABU
11 kumi na moja edatashara
12 kumi na mbili thenashara
13 kumi na tatu thelathashara
14 kumi na nne arobatashara
15 kumi na tano hamsatashara
16 kumi na sita sitatashara
17 kumi na saba sabatashara
18 kumi na nane themantashara
19 kumi na tisa tisatashara
MAKUMI
Kuandika tarakimu mbalimbali katika hali ya ukumi. (11-99).
*10 JINA MFANO
# KISWAHILI KIARABU
10 kumi 12 kumi na mbili thenashara
20 ishirini 27 ishirini na saba saba wa ishirini
30 thelathini 32 thelathini na mbili thenini wa thelathini
40 arobaini 42 arobaini na mbili thenini wa arobaini
50 hamsini 52 hamsini na mbili thenini wa hamsini
60 sitini 61 sitini na moja wahed wa sitini
70 sabini 76 sabini na sita sita wa sabini
80 themanini 89 themanini na tisa tisa wa themanini
90 tisini 93 tisini na tatu thelatha wa tisini
AKISAMI
Akisami hutumiwa kuonyesha sehemu ya kitu kizima. Kwa mfano, ukigawa kilo moja kwa visehemu vinne vinavyotoshana, kila kisehemu kitakuwa na uzani wa robo kilo ( sehemu ya nne au moja kwa nne ) ya kilo.
1/# JINA MFANO
1/2 nusu 1/2 nusu moja kwa mbili
1/3 thuluthi 2/3 thuluthi mbili mbili kwa tatu
1/4 robo 2/4 robo mbili mbili kwa nne
1/5 humusi 3/5 humusi tatu tatu kwa tano
1/6 sudusi 4/6 sudusi nne nne kwa sita
1/7 subui 6/7 subui sita sita kwa saba
1/8 thumuni 7/8 thumuni saba saba kwa nane
1/9 tusui 3/9 tusui tatu tatu kwa tisa
1/10 ushuri 6/10 ushuri sita sita kwa kumi
1/100 asilimia 72/100 asilimia sabini na mbili sabini na mbili kwa mia moja
MIFANO ZAIDI
Andika nambari zifuatazo kwa maneno/herufi:
3 – tatu
952 – mia tisa hamsini na mbili
680 – mia sita themanini
4521903 – milioni nne, na mia tano ishirini na moja elfu, na mia tisa na tatu
556100016 – mia tano hamsini na sita milioni, na mia moja elfu, na kumi na sita
Andika tarakimu zifuatazo kwa nambari
sufuri – 0
mia tatu ishirini na mbili – 322
sabini na tatu elfu, na mia nane hamsini na tano – 73855
mia tano sabini na nane elfu, na mia tatu hamsini na tisa – 578359
mia sita tisini na sita milioni, na mia tisa tisini na nane elfu, na mia saba ishirini na tatu – 696998723
Andika akisami zifuatazo kwa maneno

Leave a comment