Mpendwa rafiki yangu, Hakuna sehemu ambayo ni salama kwa kila kitu. Kila mmoja wetu kuna changamoto fulani anayopitia kwenye maisha yake. Unapojikuta uko katika hali fulani ya changamoto ndiyo sehemu ya maisha hivyo unatakiwa tu kujifunza namna ya kuikabili hiyo hali. Unajua vitu vyote vitapita na kuisha lakini changamoto hazitokuja kuisha ila vitaisha kwako tu pale tu utakapokufa lakini kama uko hai, maisha ni changamoto na pambana ili uishi vile unavyotaka wewe. Huwa kuna watu wanatabia ya kuchukua mambo ya kazini na kuyaleta nyumbani, na wengine na kuchukua ya nyumbani na kuyapelekea kazini. Vitu kama hivi vinakuwa vinaathiri utendaji wa kazi wa sehemu zote mbili kwa kiasi kikubwa sana. Acha kila sehemu ijitegemee yenyewe, kama ni mambo ya nyumbani yaache yaende nyumbani na kama ni ya kazini yaachie huko kazini. Kumbuka mafahari wawili hawakai zizi moja kama wasemavyo waswahili.
arigumaho810@gmail.com
